Simba ikikosa ubingwa wa CAF Shirikisho ni kwa sababu mbili kuu

Simba ikikosa ubingwa wa CAF Shirikisho ni kwa sababu mbili kuu

Akicheza Che Malone simba anapigwa si chini ya goli 3, cha pili matumizi ya nafasi kwa simba ni janga kubwa sana
 
Kama unaitakia mema simba sc ingewasiliana na uongozi wa simba au ata ahmed ally kuliko kulileta uku

Hujataja sababu, basi hizi ni porojo tu

We ulisikia wapi

Huu ni mwaka wa Lissu hivyo ni mwaka wa Simba

We ni mbabaishaji tu hauna tofauti na kaka yako Manara, ungekuwa mzalendo kweli ungesema hilo jambo ili watu waliongelee lifanyiwe marekebisho mapema.

Kama huyasemi haikuwa na maana ya kuanzisha uzi, unavizia matokeo then useme?

Ungetaja sababu kabla ya mechi ingesaidia zaidi.katika mechi za kimataifa kama hii ushindi ni sifa kwa taiga zima la Tanzania pia Lakini wakishindwa laumu tunawachia simba hii si haki.Kwa maoni yangu simba itatwaa kombe kwa sababu za kisakolijia wapinzani watacheza kwa hofu kubwa kwa sababu wameiona na kuisikia simba!;na hofu inamfanya adui ashindwe.Pili simba ina nguvu inapokuwa uwanjani

Sasa boss, kusema baada ya kuukosa ubingwa inakufaidisha nini? Sema tu wasipofanyia kazi ulishafanya sehemu yako. And ukisema baada ya kuukosa ubingwa hakuna namna ya kuthibitisha kuwa ndicho ulichokiona kabla ya mechi, udhaifu wowote unaweza utumia.

Simba ikilikosa hili kombe itakuwa haijajifunza kwa makosa iliyofanya mwaka 1993. Mimi nadhani kwa watu wenye akili timamu ukikosea mara moja, hutakiwi ukosee mara ya pili.

Huna tofauti na Genta ..kabla ya mechi mnaweka post kimitego ili likitokea la kutokea mdai kuwa nyie ni critical thinkers...Shame on you

Ndugu yangu hapa umepiga porojo,ni zaidi ya Lamri chonganishi.
Sasa ulianzisha uzi kwa sababu gani?

Naona umekua mnajimu siku hizi kaka angu...

Mshaanza kutafuta chaka la kujificha mkiukosa ubingwa.

Hapo ushajiweka safe kwa upande wako hapa jf, kwamba mkikosa useme "nilijua tu, si nilisema, makosana ni ....., mi najua mpira, nilishaona hilo, huu ubingwa nilijua tu tutaukosa, tulishakosea nk"

Halafu mkishinda uje na " simba ni kubwa, hakuna wa kutuzuia, kwa nkapa hatoki ntu" 😀😀😀

Nafikiri hujamwelewa.
Ameamua kutotaja sababu kwa sababu za kiusalama.
Kutotaja sababu pengine ni kuficha ili udhaifu huo usiende kwa maadui.
Ana hoja.

Ushauri wangu.
Usizitaje hizo sababu hapa.
Fanya juu chini umpate kiongozi wa Simba alie karibu na timu umuambie.
Wasipofanyia kazi wewe utakua huna kosa.

Acha ramli chonganishi

Anapoweza kusema.

Anataka aje aonekane wa maana baada ya 51mba kufungwa...!!
Nimefanya tafakuri juu ya hizi sababu nimeona ni vyema nikakaa kimya. Ikitokea tukakwama itatusaidia mbele ya safari kutorudia haya makosa.

Naombea sababu hizi zisiwe kikwazo kwa Simba kutwaa ubingwa wa CAF msimu huu.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Nimefanya tafakuri juu ya hizi sababu nimeona ni vyema nikakaa kimya. Ikitokea tukakwama itatusaidia mbele ya safari kutorudia haya makosa.

Naombea sababu hizi zisiwe kikwazo kwa Simba kutwaa ubingwa wa CAF msimu huu.
Mhhh huna lolote... 😆 😆 😆 😆 huu ni ubashiri tuu kama ubashiri mwingine
 
Nimefanya tafakuri juu ya hizi sababu nimeona ni vyema nikakaa kimya. Ikitokea tukakwama itatusaidia mbele ya safari kutorudia haya makosa.

Naombea sababu hizi zisiwe kikwazo kwa Simba kutwaa ubingwa wa CAF msimu huu.
Ambao hawajawahi kusoma threads zako zilizopita hawawezi kukuelewa.

Shida hapa JF kila mtu ni mjuaji, ila mtu alisema jambo na likaja kutokea exactly ndo unaona thread inafufuliwa na mtoa Uzi anaanza kupongezwa "Aisee we jamaa noma, hivi ulijuiaje?".
 
Ni sawa unasema iwapo mvua kesho haitanyesha basi kua litatoka au kutakuwa na mawingu...

Self Fulfilling Prophecy
 
Ambao hawajawahi kusoma threads zako zilizopita hawawezi kukuelewa.

Shida hapa JF kila mtu ni mjuaji, ila mtu alisema jambo na likaja kutokea exactly ndo unaona thread inafufuliwa na mtoa Uzi anaanza kupongezwa "Aisee we jamaa noma, hivi ulijuiaje?".
Sasa kasema nini?? Ww umeona alichokisema...angekua ametoa sbb tungesubiri hizo sbb zikitokea kweli tutafufua uzi ila yy kabaki na nadharia...
 
Aziseme hadharani ili maadui wazitumie. Hajazitaja pengine kwa kuhofia hilo.
Tumemwambia kama anaipenda Simba amwambie meneja wa Simba sc Patric Rweyemamu...ila kama anaona akae kimya basi akae tuu mwisho wa siku simba ikifeli hakuna kuleta humu porojo...Patric ndo anahusika na benchi zima la ufundi na wachezaji....
Aende tuu inbox au amfikishie Ahmed Ally ampe meneja taarifa
 
Mimi ni mmoja wa watu wachache sana ambao tuliitabiria makubwa Simba kabla hata msimu huu haujaanza. Kwa maana hiyo mimi ni mmoja wa watu wachache ambao tuna kibali cha kuona na kutafsiri kwa usahihi sehemu ambapo klabu au timu imeteleza.

Wakati timu ikijiandaa kwenda Morocco kwa ajili ya mechi ya kwanza ya fainali ya CAFCC, wapenzi na mashabiki wa Simba tuna matarajio makubwa katika fainali hii ili kombe hili libaki Tanzania.

Bila kusema mengi, pamoja na kwamba hata mchezo mmoja wa fainali bado haujachezwa ila kuna makosa mawili makubwa ya kiufundi yamefanyika ambayo kuna uwezekano yakaenda kuigharimu Simba katika harakati zake za ubingwa huu wa CAFCC.

Nitahifadhi na nisingependa kutaja hayo makosa waziwazi kwa wakati huu ili yasije yakazua mijadala ambayo kwa kipindi hiki haina faida sana.

Kwa bahati mbaya moja kati ya makosa haya, klabu haipo kwenye nafasi ya kulirekebisha ila moja lipo ndani ya uwezo wa klabu kama utashi wa kulifanyia kazi utakuwepo. Shida ni kwamba sioni hata kama kuna mtu ndani ya klabu amelitilia maanani au ameona umuhimu wake kwa hiyo najua hili nalo halitafanyiwa kazi na ndiyo maana yananitia wasiwasi. Najua hata nikijaribu kulipenyeza kwa uongozi hawatanielewa au kutaka kulifanyia kazi.

Iwapo Simba itakosa ubingwa wa CAFCC, nitarudi katika uzi huu nitaje hizo sababu mbili kuu.

Nimalizie kwa kusema, nafasi ya Simba kuwa bingwa wa CAFCC msimu huu bado ni kubwa sana na dua na maombi ya wanasimba wote yanaelekezwa katika kufanikisha hilo.
Wanapigwa nje ndani
 
Tumemwambia kama anaipenda Simba amwambie meneja wa Simba sc Patric Rweyemamu...ila kama anaona akae kimya basi akae tuu mwisho wa siku simba ikifeli hakuna kuleta humu porojo...Patric ndo anahusika na benchi zima la ufundi na wachezaji....
Aende tuu inbox au amfikishie Ahmed Ally ampe meneja taarifa
Hapo uko sahihi. Ila kwa mujibu wa mleta uzi, anasema ameshawatonya Viongozi kadhaa wa Simba wenye nafasi ya maamuzi Klabuni ila ushauri wake ni kama umeangukia kwenye deaf ears. Na kwa Simba hili tatizo lipo japo kama ulivyosema SAYVILLE asichoke, ajaribu tena kushauri.
 
Nipe huo ujumbe niufikishe Simba moja kwa moja
 
Sasa kasema nini?? Ww umeona alichokisema...angekua ametoa sbb tungesubiri hizo sbb zikitokea kweli tutafufua uzi ila yy kabaki na nadharia...

Tumemwambia kama anaipenda Simba amwambie meneja wa Simba sc Patric Rweyemamu...ila kama anaona akae kimya basi akae tuu mwisho wa siku simba ikifeli hakuna kuleta humu porojo...Patric ndo anahusika na benchi zima la ufundi na wachezaji....
Aende tuu inbox au amfikishie Ahmed Ally ampe meneja taarifa

Hapo uko sahihi. Ila kwa mujibu wa mleta uzi, anasema ameshawatonya Viongozi kadhaa wa Simba wenye nafasi ya maamuzi Klabuni ila ushauri wake ni kama umeangukia kwenye deaf ears. Na kwa Simba hili tatizo lipo japo kama ulivyosema SAYVILLE asichoke, ajaribu tena kushauri.

Nipe huo ujumbe niufikishe Simba moja kwa moja
Makosa yameshafanyika, tusonge mbele tu tukapambane. Nafasi ya kuchukua ubingwa bado ipo.

Ila daah....mpira wetu huu, nahisi mpaka Mungu aje kuingilia kati ndiyo tutatoboa.
 
Mpira ni mchezo wa wazi wote tumeiona Simba jinsi ilivyokua ukipata Matokeo.
Ata kwenye Ligi ya NBC, kazi iliyofanywa na baadhi ya marefa ni kubwa mno na wana stahili pongezi.

Wanastahili Tuzo baada ya msimu kumalizika maana iyo nafasi ya pili mliyonayo wameitolea jasho na fedheha kubwa.
Hata michepuko ya Gsm Imeisaidia sana Yanga kufika hapo ilipo Timu nane zimechangia magoli 50+ hii si kazi ndogo!

Fanyeni mpango mukammalizie pesa yake John Noble.
 
Ili uwafunge wale kirahisi ni lazima uwe na Top quality mfano
1. Inonga au Job. 5
2.Bangala kwenye Prime.6
3. Aucho Au debora wa Yanga 8.
4. Mayele au sowa 9.
5.Azizi, chama, fei,pakome 10.

Hapa unachukua ubingwa Asubuhi.

QUALITY.
QUALITY.
QUALITY.
Lakini wakaishia makundi!

Huku ni kutia nazi supu.
 
Back
Top Bottom