Simba ikikosa ubingwa wa CAF Shirikisho ni kwa sababu mbili kuu

Simba ikikosa ubingwa wa CAF Shirikisho ni kwa sababu mbili kuu

Nimefanya tafakuri juu ya hizi sababu nimeona ni vyema nikakaa kimya. Ikitokea tukakwama itatusaidia mbele ya safari kutorudia haya makosa.

Naombea sababu hizi zisiwe kikwazo kwa Simba kutwaa ubingwa wa CAF msimu huu.
Ungekuwa mke wangu ningekupa talaka moja

hukuwa na sababu ya kuongea kwa mafumbo ungekaa kimya au ungewafuata wahusika ukawapa angalizo kuja hapa na kuongea ulichoongea ni uoga kama uoga mwengine hicho ambacho unakiona kama kitisho huwenda ndo sababu ya Simba kutoboa.

Na unaonekana mpenda sifa za kijinga kama Genta.
 
Ambao hawajawahi kusoma threads zako zilizopita hawawezi kukuelewa.

Shida hapa JF kila mtu ni mjuaji, ila mtu alisema jambo na likaja kutokea exactly ndo unaona thread inafufuliwa na mtoa Uzi anaanza kupongezwa "Aisee we jamaa noma, hivi ulijuiaje?".
Sasa huyu atasifiwa kwa lipi alilopatia au wewe unajua hivyo alivyovisema?

Ikija kutokea Simba imetwaa kombe ni mpila na ikiukosa ni mpila.
 
Nimefanya tafakuri juu ya hizi sababu nimeona ni vyema nikakaa kimya. Ikitokea tukakwama itatusaidia mbele ya safari kutorudia haya makosa.

Naombea sababu hizi zisiwe kikwazo kwa Simba kutwaa ubingwa wa CAF msimu huu.
Bado unazunguka tu kutafuta sehemu ya kunya, hujataja hizo sababu.
 
Mimi ni mmoja wa watu wachache sana ambao tuliitabiria makubwa Simba kabla hata msimu huu haujaanza. Kwa maana hiyo mimi ni mmoja wa watu wachache ambao tuna kibali cha kuona na kutafsiri kwa usahihi sehemu ambapo klabu au timu imeteleza.

Wakati timu ikijiandaa kwenda Morocco kwa ajili ya mechi ya kwanza ya fainali ya CAFCC, wapenzi na mashabiki wa Simba tuna matarajio makubwa katika fainali hii ili kombe hili libaki Tanzania.

Bila kusema mengi, pamoja na kwamba hata mchezo mmoja wa fainali bado haujachezwa ila kuna makosa mawili makubwa ya kiufundi yamefanyika ambayo kuna uwezekano yakaenda kuigharimu Simba katika harakati zake za ubingwa huu wa CAFCC.

Nitahifadhi na nisingependa kutaja hayo makosa waziwazi kwa wakati huu ili yasije yakazua mijadala ambayo kwa kipindi hiki haina faida sana.

Kwa bahati mbaya moja kati ya makosa haya, klabu haipo kwenye nafasi ya kulirekebisha ila moja lipo ndani ya uwezo wa klabu kama utashi wa kulifanyia kazi utakuwepo. Shida ni kwamba sioni hata kama kuna mtu ndani ya klabu amelitilia maanani au ameona umuhimu wake kwa hiyo najua hili nalo halitafanyiwa kazi na ndiyo maana yananitia wasiwasi. Najua hata nikijaribu kulipenyeza kwa uongozi hawatanielewa au kutaka kulifanyia kazi.

Iwapo Simba itakosa ubingwa wa CAFCC, nitarudi katika uzi huu nitaje hizo sababu mbili kuu.

Nimalizie kwa kusema, nafasi ya Simba kuwa bingwa wa CAFCC msimu huu bado ni kubwa sana na dua na maombi ya wanasimba wote yanaelekezwa katika kufanikisha hilo.
Hawa wanajimu wapumbqvu sana
 
Au tuseme sababu ya kwanza ni hiyo ya kubadilishwa kwa uwanja wa mkondo wa pili wa fainali ya CAFCC? Maana mleta uzi alisema kuna sababu moja iko juu ya uwezo wa Viongozi wa Simba, ila ya pili iko ndani ya uwezo wao.
 
Ule ni ushabiki tuu lakini yeye alisema ni SIMBA si kisoka la hasha bali kiroho
Hapo
Au tuseme sababu ya kwanza ni hiyo ya kubadilishwa kwa uwanja wa mkondo wa pili wa fainali ya CAFCC? Maana mleta uzi alisema kuna sababu moja iko juu ya uwezo wa Viongozi wa Simba, ila ya pili iko ndani ya uwezo wao.
Mtachukua Kombeo
 
Mbereko Fc acha porojo na kutafuta visingizio hapa! Wewe unafahamu fika kwenye hayo mashindano ya Kimataifa waamuzi wote ni aina ya Ahmed Arajiga, ambao kwa hapa kwetu huwa hamumtaki achezeshe mechi zenu, kisa tu mnadekezwa na baba yenu Karia! Na kwa maana hiyo wachezaji wenu wakijiangusha, hakutakuwa na penati za mchongo!

Kule hakuna waamuzi aina ya Tatu Malogo, Kepha Kayombo, Japhet Smart, au Shomary Lawi! Kwa mtatakiwa kupambana. Kinyume na hapo, mtaliaibisha Taifa. Kaka yenu Yanga alikosa hilo kombe kwa sababu tu ya kanuni. Ila ukija kwenye uhalisia, utakuta alilingana matokeo ya aggregate ya 2 - 2 na timu iliyo chukua ubingwa. Na hapa maana yake alipambana.
Said it all....
 
Back
Top Bottom