Simba ikikosa ubingwa wa CAF Shirikisho ni kwa sababu mbili kuu

Ndugu yangu hapa umepiga porojo,ni zaidi ya Lamri chonganishi.
Sasa ulianzisha uzi kwa sababu gani?
 
Mshaanza kutafuta chaka la kujificha mkiukosa ubingwa.

Hapo ushajiweka safe kwa upande wako hapa jf, kwamba mkikosa useme "nilijua tu, si nilisema, makosana ni ....., mi najua mpira, nilishaona hilo, huu ubingwa nilijua tu tutaukosa, tulishakosea nk"

Halafu mkishinda uje na " simba ni kubwa, hakuna wa kutuzuia, kwa nkapa hatoki ntu" πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Simba wamekosea kwenye usajili hasa kule mbele ila Rushwa ndio imewafikisha apo walipo fika.
Wale wa South wametolewa kwa kibunda na si mchezo wa mpira wa miguu.
Mechi zote mbili walistahili Matokeo ila ugeni wa mashindano na kutojua fedha za rushwa anapewa nani kume waangusha.
Ni aibu kwa mpira wa kisasa timu kushinda kwa kutumia fedha, mafuta, chumvi na makafara.
 
Sasa boss, kusema baada ya kuukosa ubingwa inakufaidisha nini? Sema tu wasipofanyia kazi ulishafanya sehemu yako. And ukisema baada ya kuukosa ubingwa hakuna namna ya kuthibitisha kuwa ndicho ulichokiona kabla ya mechi, udhaifu wowote unaweza utumia.
Aseme kwa nani Sasa?
 
Ushauri wangu.
Usizitaje hizo sababu hapa.
Fanya juu chini umpate kiongozi wa Simba alie karibu na timu umuambie.
Wasipofanyia kazi wewe utakua huna kosa.
 
Vipi na timu hizi nazo zimetolewa kwa rushwa?
Al Masry
Bravos
CS Faxien
CS Constantine
Al Ahly Tripoli
 
Vipi na timu hizi nazo zimetolewa kwa rushwa?
Al Masry
Bravos
CS Faxien
CS Constantine
Al Ahly Tripoli
Mpira ni mchezo wa wazi wote tumeiona Simba jinsi ilivyokua ukipata Matokeo.
Ata kwenye Ligi ya NBC, kazi iliyofanywa na baadhi ya marefa ni kubwa mno na wana stahili pongezi.

Wanastahili Tuzo baada ya msimu kumalizika maana iyo nafasi ya pili mliyonayo wameitolea jasho na fedheha kubwa.
 
Naninajua sababu yake kuu aje aiseme selikari, mwamba anamatatizo binafsi na selikari
 
Sema labda kama Unataka Kupotosha.

Kuchukua Ubingwa Mbele ya Berkane ni ngumu sana, kuliko unavyodhania ni ngumu mno.

Kwa miaka hii mitano 2020-2025.
Imecheza Fainali tatu( 3).
imechukua ndoo mala mbili.

Kama ningeweza kutoa mizania ningeweka.
Simba 40 %
Berkane 60 %
 
Ili uwafunge wale kirahisi ni lazima uwe na Top quality mfano
1. Inonga au Job. 5
2.Bangala kwenye Prime.6
3. Aucho Au debora wa Yanga 8.
4. Mayele au sowa 9.
5.Azizi, chama, fei,pakome 10.

Hapa unachukua ubingwa Asubuhi.

QUALITY.
QUALITY.
QUALITY.
 

Uchambuzi wa kibwege Sana huu . Simba imefikaje fainali kama ina washambuliaji butu,beki zinakabia macho?
Mkicheza PS Akili zenu zinataka wachezaji wacheze kama PS


Tatizo la kwanza ni kumchezesha CHE MALONE, wakikwepa huu mtego basi nafasi ya kutwaa ubingwa ni mkubwa.

Nilisema wazi sababu ninazotaja mimi ni za nje ya uwanja. Kwa viwango vya wachezaji na timu, Simba na Berkane hawapishani sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…