Simba kufanya sajili tatu saa 10:30, 1:00 na saa 2:00

Simba kufanya sajili tatu saa 10:30, 1:00 na saa 2:00

Scars

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2017
Posts
48,055
Reaction score
116,512
Unadhani katika hao watatu ni wachezaji gani ambao unawapa karata ya kutia saini?

Najua katika hizo sajili lazima lihusishe eneo la goal keeping.

Kwangu nampa asilimia kubwa Luis Miquisson kutua. Na huyu lazima awe wa mwisho kutambulishwa.

**************

Update

16:30

Simba imekamikisha usajili wa mshambuliaji Shaaban Iddi Chilunda (25) raia wa Tanzania
simbasctanzania-20230720-0001.jpg



***************
Update

19:00

Simba imekamilisha usajili wa kiungo mkabaji Abdallah Hamis (24)

Awali alikuwa kwenye Club ya Muhoroni nchini Kenya.

Ni mtanzania mzaliwa wa Tarime huu ni usajili mbadala wa Mkude baada ya kuondoka Simba.
aggysimbasportsclub-20230720-0001.jpg (1)~3.jpg


******************

Update

20:30

Simba imekamilisha usajili wa beki wa kati Hussen Kazi kutoka Geita Gold.

Hussen Kazi alianzia Mbeya kwanza

simbasctanzania-20230720-0001.jpg
 
LUIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII.
Jana kulikuwa na tetesi kuwa anaenda South kwa Kaizer Chiefs ila manager wake amepinga kuwa hakuna mawasiliano yoyote yaliyofanyika kati ya Kaizer Chiefs na yeye
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Mwanzo kulikuwa na tetesi za Simba kuwa katika mazungumzo na kipa mbrazil Caique da Santos.

Lakini baadaye zikaja taarifa (ambazo ni tetesi pia) kuwa Simba imeachana na dili la kumsajili mlinda mlango huyo.

Inadaiwa huyu ni kipa ambaye alikuwa preferred na Rorbetinho.

Sababu za kusitisha dili na mchezaji huyo zinatajwa kuwa ni lugha.

Mchezaji anazungumza kireno na kiingereza ni kwa shida hivyo management ikaona kutakuwa na shida ya mawasiliano kati yake na mabeki.
 
Back
Top Bottom