ZionGate
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 6,362
- 2,991
Kaunzia board mpaka mtendaji mkuu wote wababaishaji, hawa sio waaminifu hata kidogo wanawadanganya wanachama na wapenzi wa club kwa kujiamini kabisa, yale matangazo ya nn kimewekezwa na nani kawekeza, mikataba mbalimbali kumbe yote changa la macho eti leo timu ikiwa na huyuhuyu mtendaji mkuu Barbara wamenyang'anywa basi, hivi ni kipi Leo Simba wamenunua wajivunie utumbafu tu.Niliwai kusema hapa ya kuwa hii mikataba ambayo hivi vilabu vinaingia na wanatutangazia uhalisia wake utaonekana muda sio mrefu na kinachotokea simba ndio uhalisia wenyewe wamekuwa na mambo mengi ya ujanja ujanja kuwadanganya wanachama wao juu ya mikataba wanayoingia kwa kuongeza sifuri kwenye ile mikataba lakini kiuhalisia ni uongo,, auwezi kuwa na akili timamu eti timu ina mikataba kama mbet b.26, matangazo ya mhindi wa bombay yamejaa kwenye jezi, na bado timu inapokonywa bus kwa kushindwa kumalizia malipo, na bado wachezaji wanalia njaa bonus zao imekuwa dana dana, na bado usajili wa wachezaji wanaangaliwa free agent au wachezaji wa milion 20 ndio wasajiliwe,,Uwekezaji gani wa ajabu ajabu namna hiyo? Bado zile b.20 za mwekezaji azijulikani ziliwekwa benk gani na zinafanya nini, maana zingekuwepo tusingekuwa tunaona aya yanayoendelea kwenye klabu,,Timu kubwa imebaki inakodi costal kuwapeleka mazoezini haina tofauti na maji maji ya songea,,Timu kubwa inakuwa haina kocha wa makipa, haina kocha mkuu wanakwenda kumuazima mgunda aje kupiga deiwaka? Kwakweli kuna vituko vinapatikana Tanzania pekee
Ifike sehemu serikali iwe inaingilia kati haya mamikataba wakipumbavu na watendaji wasiotekeleza majukumu Yao wachukuliwe hatua.