Idawa nimesoma michango au comments zako zote ni kuponda tu. Kweli "nyani haoni kundule". Sisi tunawaanika wachezaji professionals wetu kwenye TV kuomba michango ya dona hamuoni kama ni udhalilishaji tunawafanyia.
Mfano kama Kamusoko ndugu au nchini kwake wanajua ni mchezaji professional; amesajiliwa kucheza mpira, wanashangaa wananwona kwenye TV anaomba michango ya kulipwa yeye mishahara!!! Aibu hii ndogo ukilinganisha na mchezaji personal kuomba kiatu au jersey? Lakini mmekomalia, eti ooo umaskini, ooo hana kiatu, utadhani wamefanya dhambi!!
Ni kawaida mtu mweye nongwa kuangalia mambo madogo madogo ili kutafuta umbea.
WAKATI MWINGINE MNANIAIBISHA SANA WANA YANGA WEZANGU.
Saa nyingine tunajitakia au tunajitafutia wenyewe kuchambwa na kusimangwa na watani zetu. Najua haitakupendeza kusikia mpenzi au shabiki mwenzako kuyanena haya. Nadhani tupambane tuinusuru timu yetu kuliko kufuatilia mambo madogo kabisa ya mtani wetu. Tusiwatafutie nafasi ya kutusema vibaya.
Mkuu nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa, lakini hali anayopitia Yanga na vilabu vingine vya Tanzania ni jambo la kawaida hii inatokana na mfumo wa soka letu kutotaka kubadilika.
Ukiachana na Azam, Kagera na Mtibwa hivi vilabu vingine vyote hali zao zinafanana.
Yanga tumekubali, tumejikubali kuwa sisi ni maskini hivyo hatuna vyanzo vingine vya mapato zaidi ya kutoka kwa wanachama wetu wenye mapenzi mema na timu yao.
Hii hali ni kawaida hata kwenye makampuni binafsi hata serikalini mambo yanavyoenda kombo kunakupunguza mishahara ama kupunguza wafanyakazi....sio swala la aibu.
Tatizo ni pale inapotokea kwenye club ambayo imechukuliwa kuwa mfano kwenda kwenye soka la kisasa.
Simba kwa sasa ina mwekezaji ambaye alitangaza kuingiza zaidi ya bilioni 20 kwenye uendeshaji wa club.
Lakini kinachoonekana ni kama kiinimacho tu, Mo ni tajiri ila Simba ni Maskini tu.
Salamba wakati anaomba viatu alionyesha kabisa anashida ya viatu vya kuchezea na si kwa ajili ya kumbukumbu..
Hitimisho ni kwamba Simba na Yanga haziitaji kuchekana kuhusu umaskini na utajiri wote tuko sawa.....
Wote tunahitaji mabadiliko ya kweli kufika kwenye soka la kisasa.