Kwenye hizo. Mechi unakuta mashabiki wanabebwa mabango ahsante mamaSerikali imewapa wananchi ajenda ya simba na Yanga.
kila kona ukipita watu wanajadili simba na Yanga.
Hawana habari na gharama za maisha kupanda.
Hawana habari na ufisadi unaofanywa
Hawana habari na ngorongoro
Hawana habari na wanyama kusafirishwa kwenda uarabuni
Hawana habari ndani ya mwaka mmoja mafuta yamepanda bei kwa zaidi ya aslimia 130%
Wanaimba mayele, wanaimba Chama
Wanatambiana uzuri wa jezi
Wanatambiana idadi ya wafuasi mitandaoni
Wanananchi wasiojitambua wameingia kwenye huu mkumbo
Ni upumbavu mkubwa eti simba day, Yanga Day media kuanzia alfajir hadi usiku zinajadili mpira!!!
Nyuma ya pazia inawezekana pesa zinazopelekwa kwenye hizi timu ni za watu wakwepa kodi na wanaohujumu uchumi wa nchi
Wanasiasa wamewekeza sana kwenye haya matimu ili waendelee kulamba asali bila kelele
Lengo mama la simba na yanga ilikuwa kijiwe cha kuwakutanisha wapigania uhuru.
Kupanga mikakati ya kujikomboa lkn kwa sasa ni kichaka cha serikali kupumbaza wananchi
Ili tufikie uhuru wa kweli haya matimu yatakiwa yafutike kwenye ramani ya Tanzania.
Kweli kabisa !Kwenye hizo nchi watu wanaangilia michezo, wanaenda kwenye matamasha ya muziki, sanaa utamaduni ila wakimaliza wanaendelea na mambo mengine yanayowahusu.
Huko kukuta wanapigiana makelele na kufanya jokes za mpira muda wote kama hapa.
Lakini pia wao hata wangejikita kwenye mipira, tayari wemeshafanya maendeleo makubwa sana kwenye nchi zao sehemu zote.
Ni kweli lakini kitu chochote kikizidi sana kinakuwa ni matatizo !!Mpira haukwepeki labda kama wewe ni pumbavu ndiyo unaweza kubeza ushabiki!
Mpira haukwepeki labda kama wewe ni pumbavu ndiyo unaweza kubeza ushabiki!
Kuuondoa unazi kwenye soka mkuu ni ngumu sana! Sijui tutafanyaje!Ni kweli lakini kitu chochote kikizidi sana kinakuwa ni matatizo !!
Kuwabadilisha mkuu ni ngumu sana!Mimi sizungumzii mpira
Nazungumzia simba na yanga, ukiangalia mashabiki wa hizi timu wengi ni wajinga hata mpira hawajui
Ni jukumu letu kuwabadilisha
Sasa rafiki mbona unalinganisha vitu viwili tofauti???Mbona huachi kusafiri na wakati kila siku kunatokea ajali na kuua watu? Au watu wanaofariki kwenye ajali na kupata ulemavu mbaya wa kudumu familia zao haziteseki?
Kwani miozo ya ripoti zilizopita imefanywaje?Mimi nasubiri report ya CAG mwakani kama atazungumzia 7B za loyo twaa...
Una akili kubwa sana.Serikali imewapa wananchi ajenda ya simba na Yanga.
kila kona ukipita watu wanajadili simba na Yanga.
Hawana habari na gharama za maisha kupanda.
Hawana habari na ufisadi unaofanywa
Hawana habari na ngorongoro
Hawana habari na wanyama kusafirishwa kwenda uarabuni
Hawana habari ndani ya mwaka mmoja mafuta yamepanda bei kwa zaidi ya aslimia 130%
Wanaimba mayele, wanaimba Chama
Wanatambiana uzuri wa jezi
Wanatambiana idadi ya wafuasi mitandaoni
Wanananchi wasiojitambua wameingia kwenye huu mkumbo
Ni upumbavu mkubwa eti simba day, Yanga Day media kuanzia alfajir hadi usiku zinajadili mpira!!!
Nyuma ya pazia inawezekana pesa zinazopelekwa kwenye hizi timu ni za watu wakwepa kodi na wanaohujumu uchumi wa nchi
Wanasiasa wamewekeza sana kwenye haya matimu ili waendelee kulamba asali bila kelele
Lengo mama la simba na yanga ilikuwa kijiwe cha kuwakutanisha wapigania uhuru.
Kupanga mikakati ya kujikomboa lkn kwa sasa ni kichaka cha serikali kupumbaza wananchi
Ili tufikie uhuru wa kweli haya matimu yatakiwa yafutike kwenye ramani ya Tanzania.
Kwa nini wapo wanaoweza kuongea mipira muda wote?!Hata ukiondoa Simba na Yanga watu wanaopenda mijadala hiyo watajadili hata Coastal Union na African Sports, au hata fantasy Cricket.
Watu wote hawawezi kuongea siasa muda wote
Kwa sababu wengine ndiyo uwezo wao ulipoishia.Kwa nini wapo wanaoweza kuongea mipira muda wote?!
Unaweza kuwa ndani ya bus mtu hakujui anaanza kukupigia kelele za Simba na Yanga bila mpango wowote!