Simba na Yanga ni ngao ya kupumbaza wananchi wasifuatilie mambo muhimu ya nchi

Simba na Yanga ni ngao ya kupumbaza wananchi wasifuatilie mambo muhimu ya nchi

Hakuna kitu kisichowezekana ni
Huu ujinga wa simba na yanga ukiendelea nchi yetu utazidi kuwa masikini

Wananchi wengi wanahangaika na hizi timu ni wajinga lazima tuwabadilishe
Unabishana na kada wa Kijani hapo,utakesha nakwambia.
 
Kweli kabisa kila kijiwe dar ni Simba na Yanga tu.

Sio Dar tu boss, huo ujinga ni nchi nzima kuanzia wake kwa waume. Ukiongea habari za siasa unaonekana ni mpinzani, ama umsifie rais ndio wangalau watu wanaona wana afadhali. Na watawala wanafurahi ile mbaya wakiona watu wanajadili mpira badala ya maisha yao.
 
Serikali ina uwezo wa kutoa Burudani ya Simba na Yanga ?!!!!

Shukuru kama vile ilivyo religion being the Opium of the Mass vilevile kuna hili kimbilio la watu kujiliwaza kutokana na kupigwa na maisha..., ama sivyo watu wangekuwa wanavaa chupi kichwani wala pagekuwa hakuna Amani popote pale.....

Na tukiendelea / hawa watawala wakiendelea sooner rather than later there shall be no place for any of Us to Hide....
 
Mkuu Kama wewe hupo serikalini basi fanya juhudi na kizazi chako kijeekuingia serikalini na Kama wewe sio mchezaji wa mpira basi fanya juhudi kizazi chako kiingie kwenye timu za mpira afu ndio utajuwa kwann watanznia tumekua wajinga na haya mambo kwa saiv ni mabaya haya kwa sababu wanaofanya family baki ila Kama zingekuwa ni familia zetu basi tungeona utamu wa hili
Muhimu ni mtu kupambana na hali yake tukijali mambo ya watu amabo hana nguvu ya kuwamnia tutapoteza

Mkuu jitahidi kuandika kwa usahihi, huku ukizingatia matumizi ya koma, nukta,kuacha nafasi na herufi kubwa. Maana ni aibu kwa uandishi huu, au ww ndio hao mnaojadili mipira siku nzima nini?
 
Anzisha hayo maandamano kama hujaishia kupigwa bomu au risasi na ukaishia hapohapo. Sanasana familia yako ndiyo itapata shida. Sasa nani anayataka hayo?? Ndiyo maana tunaishia kuwa keyboard warriors

Mbona huachi kusafiri na wakati kila siku kunatokea ajali na kuua watu? Au watu wanaofariki kwenye ajali na kupata ulemavu mbaya wa kudumu familia zao haziteseki?
 
Mayeleeeeee!Tz,Ronaldooooo!Messiiiiii!.Dunia nzima mpira ndiyo burudani penda ukiondoa ngono.[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Uko Sahihi
Hakuna kitu kisichowezekana ni
Huu ujinga wa simba na yanga ukiendelea nchi yetu utazidi kuwa masikini

Wananchi wengi wanahangaika na hizi timu ni wajinga lazima tuwabadilishe
 
Serikali imewapa wananchi ajenda ya simba na yanga
kila kona ukipita watu wanajadili simba na yanga
Hawana habari na gharama za maisha kupanda
Hawana habari na ufisadi unaofanywa
Hawana habari na ngorongoro
Hawana habari na wanyama kusafirishwa kwenda uarabuni
Hawana habari ndani ya mwaka mmoja mafuta yamepanda bei kwa zaidi ya aslimia 130%

Wanaimba mayele, wanaimba Chama
Wanatambiana uzuri wa jezi
Wanatambiana idadi ya wafuasi mitandaoni

Wanananchi wasiojitambua wameingia kwenye huu mkumbo

Ni upumbavu mkubwa eti simba day,yanga day media kuanzia alfajir hadi usiku zinajadili mpira!!!

Nyuma ya pazia inawezekana pesa zinazopelekwa kwenye hizi timu ni za watu wakwepa kodi na wanaohujumu uchumi wa nchi

Wanasiasa wamewekeza sana kwenye haya matimu ili waendelee kulamba asali bila kelele

Lengo mama la simba na yanga ilikuwa kijiwe cha kuwakutanisha wapigania uhuru
Kupanga mikakati ya kujikomboa lkn kwa sasa ni kichaka cha serikali kupumbaza wananchi

Ili tufikie uhuru wa kweli haya matimu yatakiwa yafutike kwenye ramani ya Tanzania
Haman hii sio hoja tatizo ni uzezeta tu watz na unafiki na ubinafsi ambao unatengenezwa toka shule na ngazi ya familia
Ukiona wanajadili mpira ujue maisha yako poa wakibanwa wataacha tu hahahaha

Acha timu zetu ziendelee kuwepo hasa timu yetu wananchi
 
Hakuna kitu kisichowezekana ni
Huu ujinga wa simba na yanga ukiendelea nchi yetu utazidi kuwa masikini

Wananchi wengi wanahangaika na hizi timu ni wajinga lazima tuwabadilishe
Tembea uone kaka usihukumu kwa sababu ya ukosefu wa kuijua dunia ipo vipi, nenda Misri uone watani wa jadi wanavyopendwa na mambo yanakwenda.

Nenda Afrika ya Kusini uone derby ya Kaizer Chiefs na Mamelodi inavyowapagawisha wenyeji na bado mambo yao yamenyooka.

Ushabiki wa mpira unakwenda sambamba na maendeleo ya matumizi ya mitandao, ndio dunia ya sasa huwezi kukwepa uhalisia wake.
 
mamilioni ya wafuasi wanaofuatilia vitu visivyo na faida ya maana kwenye mambo muhimu
Ndio dunia ya sasa ilivyo, bado hujaongelea wala kuwafikiria wale wapenzi wa Arsenal, Man United na Man City.

Maisha yanaboa sana bila ya kuwepo michezo kama soka, yamejaa upweke.
 
Tanzania wajinga ni wengi mno...
Elimu bure inasababisha wajinga waongezeke
 
Sijawahi kuwaona wazungu wanashindana, kuzodoana na kupigiana makelele wiki nzima au mwezi kwa mechi moja ya Man United na Man City au Madrid na Barcelona iliyochezwa weekend moja. Huu utopolo upo bongo tu.
Ndio dunia ya sasa ilivyo, bado hujaongelea wala kuwafikiria wale wapenzi wa Arsenal, Man United na Man City.

Maisha yanaboa sana bila ya kuwepo michezo kama soka, yamejaa upweke.
 
Na wajinga wengi ndo mijadara yao hiyo kuanza kwenye vijiwe vya kahawa vya Buza mpaka kwenye vyombo vya habari
Zama zile kabla ya uber na bolt wale maderevq taxi unaweza mwita hadi koo likauke yupo busy kubishania habari ya simba na Yanga...

Watanzania ni watu wa hovyo sana.
 
Yaani Mimi mwenyewe nashangaa sana saa 2 wanakusanyika mtu kama 6 ajenda Simba na Yanga.
 
Simply watanzania ni maskini wa kila kitu kuanzia akili mpaka mali
 
Back
Top Bottom