Simba na Yanga ni ngao ya kupumbaza wananchi wasifuatilie mambo muhimu ya nchi

Dunia gani hiyo? Hakuna nchi yenye mashabiki wajinga km Tanzania

Angalia brazil ulikozaliwa mpira,wao lunapokuja gharama za maisha kupanda huwa wanaweka mpira kando

Misri na afrika kusini ambao ndio mpira upo juu kwa ligi gharama za maisha zikipanda huwezi kuta watu wana deal na mpira ni maandamano mwanzo mwisho

Sasa Tanzania kwa ukondoo wa kujadili simba na yanga ufananishe na watu wa maana?
Anzisha hayo maandamano kama hujaishia kupigwa bomu au risasi na ukaishia hapohapo. Sanasana familia yako ndiyo itapata shida. Sasa nani anayataka hayo?? Ndiyo maana tunaishia kuwa keyboard warriors
 
Serikali imewapa wananchi ajenda ya simba na yanga
kila kona ukipita watu wanajadili simba na yanga
Hawana habari na gharama za maisha kupanda
Hawana habari na ufisadi unaofanywa
Hawana habari na ngorongoro
Hawana habari na wanyama kusafirishwa kwenda uarabuni
Hawana habari ndani ya mwaka mmoja mafuta yamepanda bei kwa zaidi ya aslimia 130%

Wanaimba mayele, wanaimba Chama
Wanatambiana uzuri wa jezi
Wanatambiana idadi ya wafuasi mitandaoni

Wanananchi wasiojitambua wameingia kwenye huu mkumbo

Ni upumbavu mkubwa eti simba day,yanga day media kuanzia alfajir hadi usiku zinajadili mpira!!!

Nyuma ya pazia inawezekana pesa zinazopelekwa kwenye hizi timu ni za watu wakwepa kodi na wanaohujumu uchumi wa nchi

Wanasiasa wamewekeza sana kwenye haya matimu ili waendelee kulamba asali bila kelele

Lengo mama la simba na yanga ilikuwa kijiwe cha kuwakutanisha wapigania uhuru
Kupanga mikakati ya kujikomboa lkn kwa sasa ni kichaka cha serikali kupumbaza wananchi

Ili tufikie uhuru wa kweli haya matimu yatakiwa yafutike kwenye ramani ya Tanzania
Mkuu maisha haya ni mafupi mno hakuna sababu ya kuishi na maumivu siku zote. Inapopatikana sababu ya kufurahi na kuongeza siku za kuishi kwa kufurahia mpira wa miguu watu hufanya hivyo.

Kama wewe hupendi mpira kumbuka kuna mamilioni ya walipa kodi wanaupenda sana mpira na kumbuka ni mchezo wenye mzunguko mkubwa sana wa pesa na umeajiri watu wengi sana.

Umeshajiuliza Drogba na pesa zake alizochuma Chelsea anawagusa watu wangapi wa kwao?. Umeshajiuliza Eto'o na biashara zake ambazo mtaji na malipo aliyoyapata ulaya ameajiri watu wangapi kwao Cameroon?.

Panua ubongo wako ili uweze kuifahamu picha pana ya mpira wa miguu na namna unavyogusa maisha ya mtu mmoja mmoja, jitahidi uondokane na akili hizi za kishamba za kulalamika 24/7.
 
Mpaka Tbccm nao wamo kuzungumzia upuuzi huu siku nzima. Vijana wote kutwa na vikaratasi vya ku bet , mchongo pesa, chota mihela, hela chapuchapu za karibu radio zote
We are living in a fools paradise
Kuna mtu amewakataza kufanya kazi?. Ndio maisha ya sasa mngependa kuona hao vijana wanaocheza kamari wakijihusisha na ukabaji?.
 
Duniani kote iko ivo.

Sidhani mkuu, ukitaka kuamini fuatilia page za twiter Cafonline uone pindi wakiposti simba au yanga jinsi comments zinavyomiminika ndani ya muda mfupi, mpaka kuna siku moja msouth mmoja aliuliza “hivi hwa jamaa wako online muda wote? Maana ni wengi alafu wanaongea kiswahili hata hatuwaelewi”
 
Tupo kwenye mjadala sio kuanzisha maandamano
Maandamano ni matokeo

By the way comment yako unakueleza wewe ni ntu wa aina gani
Anzisha hayo maandamano kama hujaishia kupigwa bomu au risasi na ukaishia hapohapo. Sanasana familia yako ndiyo itapata shida. Sasa nani anayataka hayo?? Ndiyo maana tunaishia kuwa keyboard warriors
 
Mimi sijazungumzia mpira,ninezungumzia simba na yanga

Kwasababu wengi wanashabikia hizi timu hawajui hata mpira ila wanajua simba na yanga
Usije ukaleta mfano wa drogba ile ni dunia nyingine

Tanzania simba na yanga zinatumika kama tool ya kisiasa uko kwa kina drogba mpira ni kazi
Kwahiyo utofautishe hilo usije km mtu usiyejua mpira ila unajua simba na yanga
Mkuu maisha haya ni mafupi mno hakuna sababu ya kuishi na maumivu siku zote. Inapopatikana sababu ya kufurahi na kuongeza siku za kuishi kwa kufurahia mpira wa miguu watu hufanya hivyo.

Kama wewe hupendi mpira kumbuka kuna mamilioni ya walipa kodi wanaupenda sana mpira na kumbuka ni mchezo wenye mzunguko mkubwa sana wa pesa na umeajiri watu wengi sana.

Umeshajiuliza Drogba na pesa zake alizochuma Chelsea anawagusa watu wangapi wa kwao?. Umeshajiuliza Eto'o na biashara zake ambazo mtaji na malipo aliyoyapata ulaya ameajiri watu wangapi kwao Cameroon?.

Panua ubongo wako ili uweze kuifahamu picha pana ya mpira wa miguu na namna unavyogusa maisha ya mtu mmoja mmoja, jitahidi uondokane na akili hizi za kishamba za kulalamika 24/7.
 
Ni kweli hata ukiangalia pages za timu kubwa africa mashabiki sio wajinga km hawa wa simba na yanga
Sidhani mkuu, ukitaka kuamini fuatilia page za twiter Cafonline uone pindi wakiposti simba au yanga jinsi comments zinavyomiminika ndani ya muda mfupi, mpaka kuna siku moja msouth mmoja aliuliza “hivi hwa jamaa wako online muda wote? Maana ni wengi alafu wanaongea kiswahili hata hatuwaelewi”
 
Mimi sijazungumzia mpira,ninezungumzia simba na yanga

Kwasababu wengi wanashabikia hizi timu hawajui hata mpira ila wanajua simba na yanga
Usije ukaleta mfano wa drogba ile ni dunia nyingine

Tanzania simba na yanga zinatumika kama tool ya kisiasa uko kwa kina drogba mpira ni kazi
Kwahiyo utofautishe hilo usije km mtu usiyejua mpira ila unajua simba na yanga
Hujui historia ya uwepo wa Simba na Yanga ndio maana umekuja na mada yenye kulaumu uwepo wa hizi timu bila ya kuzijua kwanza mwanzo wake.

Tafuta kwanza misingi ya uwepo wa hizi timu ndio uje na mjadala wako wa lawama zisizo na kichwa wala miguu.
 
Historia gani ya maana ya simba na yanga zaidi ya ile nikiyokua nimeitamka hapo juu kwenye post?
Simba na yanga ni ujinga usio na faida kwa jamii
Simba na yanga inazorotesha kujenga taifa imara la watu wanaojitambua

Wewe ni kijana mdogo kwa kuyasoma haya mawazo yako, umezaliwa umezikuta hizi timu mbili. Usioanishe masuala ya kiuchumi na Simba na Yanga moja kwa moja.

Misri wana Al Ahly na Zamalek ni wakubwa kuliko Simba na Yanga, wanao ushawishi kuliko hizi timu zetu na wana pesa na uchumi wao umesimama,

Simba na Yanga kupendwa na kuaminiwa n suala moja, uchumi wetu kudorora na suala jingine, msitafute sababu za uchumi kuonekana haupo vizuri mkadhani kwamba mpira ndio sababu.

Tafuteni visingizio vingine vyenye mashiko vya kwanini uchumi unaonekana kuyumba, kuliko hiki cha kulaumu ushabiki wa soka.
 
Alahily na zamalek hazijawahi kutumika kisiasa tofauti na simba na yanga

Kutumika kisiasa kwa Simba na Yanga kama kunakuuma basi utulie tu kwani hakuna la maana unaloweza kufanya katika kubadilisha hii hali.

Uhuru ulipatikana kwa kuwakutanisha watu wa mpira ambao ni Yanga na Simba. Na ni mchakato wa miaka na miaka haiwezekani leo hii eti wakaacha ghafla tu.
 
Wewe buana unakuwa na akili za mtoto

Hakuna kitu kisichowezekana kubadilisha iyo akili yako ipige rungu ushituke

Wewe ndio ubadilishe akili zako, uzijue kwanza Simba na Yanga na mamilioni ya wafuasi walionao ndio uje na mawazo yako ambayo kiuhalisia hayawezekani.
 
Hakuna kitu kisichowezekana ni
Huu ujinga wa simba na yanga ukiendelea nchi yetu utazidi kuwa masikini

Wananchi wengi wanahangaika na hizi timu ni wajinga lazima tuwabadilishe

Back
Top Bottom