Simba na Yanga ni ngao ya kupumbaza wananchi wasifuatilie mambo muhimu ya nchi

Siyo kweli, duniani kuna zaidi ha simba na yanga, kuna kina boca juniors hulo na river plate, madrid na barca/atletico madrid, Liverpool na man u, arsenal Tottenham, inter na ac milan, al ahly na zamaleki, soweto derby.. Derby ya kina partizan Belgrade, acha kabisa..

Hapa ishu ni ujinga wa mtanzania mwenyewe, tukubali tu sisi soote kwa pamoja ni MAPOPOMA, hatma ya hili taifa liko mikononi mwetu, utasikia waziri kaiba bilioni 800 tutapiga kelele mtandaoni siku mbili kisha linapita, kodi za hovyo zinakuja, baada ya siku mbili inavuja picha ya uwoya suala linapita, tunakubali UNYONGE. Utasikia mtu anajinadi mimi nipo kwwa ajili ya watanzania wanyonnge, watu huku ndio baba 😂🤣
 
Tatizo Linatokana na Watanzania kukosa viongozi imara wa vyama vya upinzani.
Upinzani upo kwa ajiri ya kujipatia ridhiki binafsi tu basi.

Mpinzani wa kweli alikuwa ndugu Christopher Mtikila na kwa bahati mbaya alifariki kwa Ajari ya Gari.

Hawa wanao ota usiku na mchana wakanywe chai Ikulu ni hamna kitu kabisa.

Viongozi wa vyama vya upinzani wametusaliti watanzania tulio wengi na kufikia kukosa hamu ya mambo ya Siasa.

Wakianza akina Mrema, Lamwai na Mabere Marando.
Wakafuata Lipumba, Mbatia Mbowe na Zito kabwe.

Hawa tuliwamini sana na wakaishia kuwa Vibaraka wa CCM.

Maalim Seif kidogo alisimama lakini akashindwa naye akaishia huko huko.

Ni bora japo tujiflahishe kwenye mambo ya Mpira.

Takukuru wapo, Mahakama Zipo, Wabunge wapo, Jeshi Lipo, Polisi wapo.
Kwanini hawachuki hatua kwenye Ufisadi hali ya kuwa

Ripoti ya Mkaguzi Mkuu ipo ?

Unataka wananchi tuandamane ili watuue sio ?
We utakuwepo kwanye hayo maandamano ya kupinga ufisadi ?

Au unataka wananchi tufanyeje ?

Weka hapa unachotaka tufanye ili kuupiga vita ufisadi sisi kama sisi wananchi.
 
Kwenye hizo. Mechi unakuta mashabiki wanabebwa mabango ahsante mama
 
Kweli kabisa !
 
Mimi sizungumzii mpira
Nazungumzia simba na yanga, ukiangalia mashabiki wa hizi timu wengi ni wajinga hata mpira hawajui

Ni jukumu letu kuwabadilisha
Mpira haukwepeki labda kama wewe ni pumbavu ndiyo unaweza kubeza ushabiki!
 
Mwizi ni Mwizi tu, kwa hiyo kama Wananchi wanajadilia Simba na Yanga wengine ndio muwaibie?. kwani msipoiba na kuwadhulumu mnapungukiwa nini kwenye Dunia hii yetu sote.

Hii ni sawa na kusema "baba yangu akilewa mimi namsachi" kwa nini wewe usiache wizi?.
 
Mbona huachi kusafiri na wakati kila siku kunatokea ajali na kuua watu? Au watu wanaofariki kwenye ajali na kupata ulemavu mbaya wa kudumu familia zao haziteseki?
Sasa rafiki mbona unalinganisha vitu viwili tofauti???
 
Una akili kubwa sana.
 
Hata ukiondoa Simba na Yanga watu wanaopenda mijadala hiyo watajadili hata Coastal Union na African Sports, au hata fantasy Cricket.

Watu wote hawawezi kuongea siasa muda wote
 
Hata ukiondoa Simba na Yanga watu wanaopenda mijadala hiyo watajadili hata Coastal Union na African Sports, au hata fantasy Cricket.

Watu wote hawawezi kuongea siasa muda wote
Kwa nini wapo wanaoweza kuongea mipira muda wote?!

Unaweza kuwa ndani ya bus mtu hakujui anaanza kukupigia kelele za Simba na Yanga bila mpango wowote!
 
Hii inanikumbusha wakati wa mubarak huko misri. Vijana wengi walitumia muda mrefu kubishana kuhusu zamalek na arsenal wakati wao wana njaa..yaani TV zote zilikuwa mpira tu all the time.

Kumbe ilikuwa diversion tactic ya serikari. Ila walivyoamka tu waligundua upuuzi huu, wakaanza harakati.Tz tuko hiyo stage sasa ya kudumazwa na mambo yasio na msingi
 
Tumefika hapa baada ya vyama vya upinzzni kupigwa pini haya ndio matokeo yake, watu wako kama zezeta tu, na matokeo zaidi yataonekana 2025 wakati wa kupiga kura, %70 huenda wasijue umuhimu wa kuchagua viongozi wao.
 
Kwa nini wapo wanaoweza kuongea mipira muda wote?!

Unaweza kuwa ndani ya bus mtu hakujui anaanza kukupigia kelele za Simba na Yanga bila mpango wowote!
Kwa sababu wengine ndiyo uwezo wao ulipoishia.

Kwa sababu, hata kama mtu anajua mengi zaidi, hicho ndicho kitu ambacho watu wanafikiri kila mtu ni lazima awe anafuatilia, kwa hiyo kinakuwa kama kianzisha maongezi (icebreaker).

Kwa sababu, ni mambo ambayo watu wanaweza kutaniana bila kuumizana sana, si maongezi magumu kama ya siasa au dini.

Kwa sababu ni maongezi ambayo hayahitaji kuwa na mantiki sana, ni maongezi ya opinion na ushabiki, hivyo kila mtu anawez akuongea. Can you imagine mtu asiyekujua anakuanzishia maongezi na mjadala wa jinsi gani benki kuu ya Tanzania inaweza kudhibiti upandaji wa bei za vitu bila kuathiri ajira za watu ?

Inabidi watu wasichukulie poa tu kwamba kila mtu anapenda mazungumzo haya, na angalau watu waanze na swali kama "Unafuatilia mpira?".
 
Ungelikuwa unaelewa Kifaransa ningekutumia video fulani kuhusu timu za Ufaransa ila kwasababu uelewi kabisa amini ivo unavyo amini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…