Hivi wanasiasa mnapo preach uhuru mnakuwa mnalenga uhuru upi?Leo hii mtu kuchagua kujadili mpira imekuwa kikwazo kwa maendeleo ya taifa?
Unataka wajadili siasa za Membe na ACT au Membe na CCM,Zitto na CHADEMA au Zitto na ACT.Hivi mtu akae ajadili vitu vya hivi?wanasiasa mnabadilika kama vinyonga, hakuna anayeweza kuaminika, kwa hiyo acha vijana wajadili kitu wanachopenda kwa maana nyie ndio kila kukicha mnapreach uhuru.
Kikubwa,tafuta pesa ukipata tumia ni zako na ukikosa pia ni juu yako.Achana na vijana katika chaguzi zao na msipende kuwa madikteta kabla ya kupewa mamlaka