SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Kuna timu inajitapa eti imehusika kuleta uhuru wa Tanzania ila haijawahi kuvuja jasho na kucheza katika mazingira magumu ambayo unaweza hata kuwaza kama baada ya mechi utabaki na uhai wako. Simba ndiyo timu pekee Tanzania ambayo imepitia mazingira hayo mara nyingi kuliko timu yoyote ile.
Tuanzie miaka ya 70, Simba ilifanyiwa vurugu nchini Misri, kipa wake akanyang'anywa gloves ikatolewa katika mazingira ya kutatanisha sana. Kama sikosei hii ilikuwa hatua ya nusu fainali (nikosolewe kama nimekosea).
Kuna ile mechi ya Sudan miaka ya 90 Simba vs El Mereikh. Simba walifanyiwa vurugu mbaya sana uwanjani, wakapigwa mawe sana tu.
Tunakuja mechi ya jana, Simba vs Al Ahly Tripoli. Hivi unadhani Simba wangepata goli pale hali ingekuwaje? Unadhani hili halikuwa vichwani mwa wachezaji? Unafuu pekee kiusalama jana ulikuwa kukubali kufungwa ila wachezaji wakakomaa, hafungwi mtu hapa!
Naomba Simba ianze kupewa heshima inayostahili nchi hii, tafadhali.