Simba SC 1-0 Namungo FC | Ligi Kuu | Benjamini Mkapa

Kwa habari nilizo nazo ni kwamba, Namungo wamekuja na masheykh wanne, balaghashea zime wasimama kama mlima wa Kilimanjaro.
Simba jiandaeni na kichapo tu.
 
Tuambieni kabisa kakosekana nani.
 
Naona Simba tunaenda kucheza 4 4 2 kibu na boco up front naiona shida kwa mhilu na Morrison maana si wakabaji Sana .

Nahisi full Back zetu zitakua nakazi kubwa sana leo kama watashindwa kuwakumbusha kurudi hawa mawinga .

Leo tuna Centre backs wote ambao wako slow inabidi akili itumike sana aisee.

Kila la khery Mnyama
 
Simba kuna mgogoro ndani ya uongozi na bado inahujumiwa na wapinzani. Kupata matokeo na ubingwa msimu huu ni inatakiwa wawe makini sana ktk hayo mawili
 
Wachezaji wa kigeni wanastahili kuanza kwa sasa ni watatu tu
Inonga
Bwalya
Morrison
 
Nimemsikia kocha akihojiwa na Azam.

Yaani kocha ni mlalamikaji na Muoga.

Kwa spirit alionesha kocha wetu, basi simba tuna kazi kubwa sana
 
Kuna kila dalili Namungo atachezea leo
 
Kocha anasemaje mkuu

Analalamika Mechi zimekuwa karibu karibu sanaa anakosa muda wa kufanyia kazi matatizo anayo yaona, so anategemea hiki kipindi cha Mapumziko kwenda kujirekebisha [emoji28], Simba inapitia wakati mgumu anasema, kwa hiyi lolote linaweza kutokea.

Anamalizia kwa kusema hii hali ni kwa binadamu yeyote na Hata club kubwa duniani hupitia.

Huyu ndio kocha wetu
 
Alie leta Hawa wachezaji amezingua haiwezekan haiwezekan washindwe kuanza first eleven yani ametupiga na kitu kizito kichwan
 
Wamekaa preseason siku za kutosha afu Leo anaongea utumbo gan
 
Mtapigwa kuanzia bao 2 na kuendelea Chirwa na Molinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…