Simba Sc 4-0 Us Gendarmerie | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa Stadium

Kama nilivyosema hua nashabikia timu zikicheza kimataifa tu.

Leo asee kidogo nipasue simu ninayostream. Viungo Bwalya na Kanoute waliwatoa wapi? Chances ya pass unakuta mtu anafanya upumbavu hadi anatolewa.

Morrison attention seeking sio sahihi kipindi cha kufa na kupona.

Robo natumai wataifanyia kazi suala la wachezaji kuchelewa kufanya maamuzi hasa Bwalya na Kanoute (Hongera kwa Goli lakini).

Kingine nimegundua kelele na sifa za mashabiki zinaharibu wachezaji kuwafanya kutaka kuchukua sifa hata sehemu isiyotakiwa. (Morrison na Sakho kipindi cha kwanza).

Simba sasa ni kubwa natumai scouting itakua ya maana ilitakiwa vijana kama Miquissone na Chama ndio wanakua scouted, watu walio comfortable na Ball.
 
Ila nyie USGN sio vizuri mlivyofanya...!

Yaan hadi HT ...Mkabana hamtaki Kutoa...!

Utopolo wakajazana ndani ya huu Uzi Wakiamini kbs HAMTOI...!

Baadae Mkaachia...Mashosti Wenzenu Utopolo Limewashuka..! Msikubali Msiondoke mpaka Wawasindikize..!!
 
Hivi ligi kuu ni timu ipi yenye beki wanafanya clearance ya kueleweka?

Namaanisha ile ball clearance ya kuupiga mpira kutoka golini kuutupa sehemu ya mbali.

Maana Unakuta wanabahatisha, kawaida yao ni mtu anapiga mpira kwa nguvu na mpira unaenda juu unarudi kudundia pale pale alipoupiga. 😂😂

Simba leteni Beki mwakani Simba iwe Tishio itambulike Dunia nzima, ifanye nchi iwe kituo cha Scouting kwa matimu ya ulaya mabilioni yaingie kwa mzunguko bei tuihimili.
 
Kukubwa tupewe mwarabu tu hii robo fainali, tukimleta kwenye jua tunashindilia kama za leo halafu huko kwao tunafunga mahesabu.
 
Kwa wenye mapenzi na wanaojali hakinza binadamu pamoja na kukerwa na vitendo vya uvunjifu wa heshima walimfata USGN na wakampa angalizo kuwa Simba ule ni moto

Team yuda wakajivika ugadafi wakampa maneno ya kishujaa naye USGN akajaa

Watu wa mwanzo kumfata USGN wakawa wanajiuliza huyu bwana tumemuambia ule ni moto alipaswa kukimbia sasa yeye ana anaufata, atakuwa ana matako ya sufuria nini?

Dakika 45 za mwanzo USGN wakawawaona wale washauri wa mwanzo ni waongo na watu ambao ni wanafiki

Dakika 25 za kipindi cha pili USGN wakaguna "mmmh! inawezekana kuna ka ukweli hapa ebu ngoja tuendelee tuone itakuwaje"

Mpaka dakika ya 80 USGN alikuwa kwenye majuto ya kiburi chake kwa kupuuza ushauri wa wale watu wakwanza na sasa wameshaona kuwa wale wapambe wapili hawakutakiwa kupewa kipaumbele ni bora wangetafuta namna ya kukaa mezani na Simba na kuongea walau wafungwe hata goli 2 pekee
 
Mzee cheki page ya kwanza ya mechi nimeandaa kabisa Poster mwenyewe kwa ajili ya mnyama. Go first page
 
TBL na SBL amkeni mlete Bia hapa Baa za Nje Uwanja wa Taifa hali ni Kucheleeeeee, sherehe kubwa inaendelea na WanaMsimbazi wanakula Bheer hatari. Sooon kreti zote zitaisha
nipo huku Sokota,sijui nitimbe hapo chap
 
Tusipewe Mazembe, hao wengine rahisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…