Simba Sc 4-0 Us Gendarmerie | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa Stadium

Simba Sc 4-0 Us Gendarmerie | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa Stadium

Wakumbuke pia TFF watapata 5% ya kiasi hicho kutoka CAF.

Hela nzuri ya kuweza kununulia utopolo waamuzi.
Hii ndio point ambayo TFF anapokea pesa kwa sura ya aibu huku ameinama chini akikumbuka vile vitimbwi vya GSM na mkataba hewa

Sometimes TFF anajishuku na kujiona mkosaji ila anakosa namna ya kuwasilisha hisia zake kuoensha ana apologize
 
Takwimu kabla ya mkeka wa robo

TANZANIA
Msimu ujayo wa 2022/2023 Tanzania inakuwa na Mwanzo wa POINT 20.5 kabla ya kuongezwa Point za Simba itazopata msimu huu sasahivi mashindano yanavyoendelea.
1. Simba ikiwa ya Nne kwenye Kundi Tanzania itabaki na Point 23
2. Simba ikiwa ya Tatu kwenye Kundi Tanzania itabaki na Point 25.5
3. Simba ikivuka kwenda Robo Fainali Tanzania itakuwa na Point 30.5

NIGERIA
Msimu ujayo inaanza na Point 26 na hakunanyongeza ya Point msimu huu kwakuwa Nigeria haina Ushiriki wa Timu katika Makundi.

ZAMBIA
Msimu ujayo inaanza na Point 22 kabla ya kuweka nyongeza ya msimu huu kwa Ushiriki wa Timu ya Zanaco iliyopo Makundi
1. Zanaco ikiwa ya Nne kwenye Kundi Zambia itabaki na Point 24.5
2. Zanaco ikiwa ya Tatu kwenye Kundi Zambia itabaki na Point 27
Kutokana na Matokeo ya sasa havuki zaidi ya hapo.

LIBYA
Inawakilishwa na Timu 2 zote Confederation Cup (Al Alhy Tripoli na Al Ittihad)
Msimu ujayo inaanza na Point 8 kabla ya kuweka nyongeza ya msimu huu wa Timu zake zilizoingia Makundi.
1. Timu zote mbili zikitolewa katika makundi Libya itabaki na Point 13
2. Timu moja ikiingia Robo Fainali na Moja ikashindwa Libya itakuwa na Point 23
3. Timu zote mbili zikiingia Robo Fainali Libya itakuwa na Point 28
4. Timu moja zaidi ikicheza Nusu Fainal Libya itakuwa na Point 33

CAMEROON
Msimu ujayo inaanza na Point 12 kabla ya kuweka nyongeza ya msimu huu kwa Ushiriki wa Timu ya Coton Sports iliyopo Makundi
1. Coton ikiwa ya Tatu kwenye Kundi Cameroon itabaki na Point 17
2. Coton ikivuka kwenda Robo Fainali Cameroon itakuwa na Point 22
3. Coton ikivuka Nusu Fainal Cameroon itakuwa na Point 27
4. Coton ikicheza Fainal Cameroon itakuwa na Point 32

IVORY COAST
Msimu ujayo inaanza na Point 5.5 kabla ya kuweka nyongeza ya msimu huu kwa Ushiriki wa Timu ya Asec Mimosa iliyopo Makundi
1. Asec ikiwa ya Nne kwenye Kundi Ivory Coast itabaki na Point 8
2. Asec ikiwa ya Tatu kwenye Kundi Ivory Coast itabaki na Point 10.5
3. Asec ikivuka kwenda Robo Fainali Ivory Coast itakuwa na Point 15.5
4. Asec ikivuka Nusu Fainal Ivory Coast itakuwa na Point 25.5
5. Asec ikichukua kombe Ivory Coast itakuwa na Point 30.5
Tanzania Timu moja (Simba) na Libya Timu zake Mbili (Al Ittihad na Al Alhy Tripoli zote zimeingia Robo Fainali bila kuangalia matokeo yeyote maana wamechukua nafasi za Zambia na Nigeria.
 
Bado kuna watu wana wasiwasi na takwimu za IFFHS?

Wapo sio?

Kama wapo basi watakuwa wanalaumu kwanini simba awe wa 90 ilihali anaucheza ule kama wa yule aliyekaa nafasi ya 5

Kamuangalieni huyo namba 5 ni nani
 
Itafika hatua mechi za hapa kwa Mkapa timu pinzani zitakuwa haziji

Ni bora zipitishe ushindi moja kwa moja kwa kukaa mezani na kujichagulia magoli kuliko kukutana na zahma kama hii

Halafu pia itasaidia ku-manage bajeti, hawa USGN isingekuwa kiburi chao hizo nauli wangezitumia na familia zao kwenye msimu huu wa ramadhani mara nyingi mihogo inakuwa bei juu
 
Aiseh sijui tutapangiwa nani tu hii robo fainali, sitaki awe ngozi nyeusi, tukipewa waarabu sahivi hata nusu tutakuwa na waarabu.

Ikiwa hivyo, fainali naiona kabisa.
 
Simba hongereni, hizi timu za bongo nazishabikia zikiwa kimataifa tu, maana zinaitangaza Tanzania 🇹🇿 nchi yangu na kufanya iwe juu kisoka. Ila Yanga upuuzi mtupu mnatolewaje vile.

Biashara United ilichofanyiwa acha tu inakera.

Namungo hongera kwa kusaidia pamoja na simba msimu uliopita kupeperusha bendera.

Ila Simba ilipaswa kufahamu inahitaji magoli mengi iwe Top of group ambayo advantage ni Kuanzia ugenini then kufanya mauaji kwa mkapa. Ila Hongereni sana kwenda Robo fainali si haba.

Tanzania 🇹🇿 imewakilishwa ipasavyo.
Wamefeli hapo ilibaki goli moja tu ku top group kumbuka wamekosa mangapi?
 
Goli la Mugalu lilivyokuwa la shida
 
Kama nilivyosema hua nashabikia timu zikicheza kimataifa tu.

Leo asee kidogo nipasue simu ninayostream. Viungo Bwalya na Kanoute waliwatoa wapi? Chances ya pass unakuta mtu anafanya upumbavu hadi anatolewa.

Morrison attention seeking sio sahihi kipindi cha kufa na kupona.

Robo natumai wataifanyia kazi suala la wachezaji kuchelewa kufanya maamuzi hasa Bwalya na Kanoute (Hongera kwa Goli lakini).

Kingine nimegundua kelele na sifa za mashabiki zinaharibu wachezaji kuwafanya kutaka kuchukua sifa hata sehemu isiyotakiwa. (Morrison na Sakho kipindi cha kwanza).

Simba sasa ni kubwa natumai scouting itakua ya maana ilitakiwa vijana kama Miquissone na Chama ndio wanakua scouted, watu walio comfortable na Ball.
Webwana sie tulisha shinda na kusonga mbele hayo mengine Bakinayo
 
Screenshot (142).png
 
Back
Top Bottom