Simba SC irekebishe upesi sana 'Mapungufu' ya hawa Wachezaji Watatu Inonga, Sakho na Morisson kwani yanaigharimu Timu

Simba SC irekebishe upesi sana 'Mapungufu' ya hawa Wachezaji Watatu Inonga, Sakho na Morisson kwani yanaigharimu Timu

1. Henock Inonga
Nakiri ni Beki mzuri sana na nimekuja Kugundua pia kuwa kumbe ni Versatile na kwamba anaweza hata kucheza vyema tu Namba 6, Namba 8 na hata Namba 2.

Mchezaji huyu tokea aicheze vyema ile Kariakoo Derby na kupata Sifa nyingi nae ameshajaa Upepo kiasi kwamba sasa anajiona ndiyo Mchezaji mzuri Kikosini Simba SC kuliko wengine waliopo au aliowakuta.

Inonga amekuwa akipenda Kulaumu mno Wenzake Uwanjani huku muda mwingi akitaka Kuonekana kama Yeye ndiyo anacheza kwa Bidii kuliko Wenzake na hupenda sana Kucheza na Akili ya Kocha Pablo ili apendwe na aaminike zaidi Kwake.

Inonga aambiwe ukweli kuwa katika ile 'Kariakoo Derby' Kazi ya Kumkaba Mshambuliaji hatari na ninayemuogopa wa Yanga SC Fiston Mayele hakuifanya peke yake kama adhaniavyo bali alikabwa Collectively and Strategically na Mabeki Wenzake Wote na tena kama kuna Mtu ambaye Mimi GENTAMYCINE niliona ndiyo alimkaba vilivyo Mayele ni Beki Joash Onyango na siyo Yeye Henock Inonga.

2. Bernard Morrison
Huyu nadhani GENTAMYCINE nilishamsoma mno hapa JamiiForums na mpaka Kuutaka Uongozi wa Simba SC Kumkanya na Kumrekebisha ila naona Jana katika Mechi na Mlandege FC yamejirudia tena yale yale.

Uongozi wa Simba SC leo ngoja sasa niwapasulieni Ukweli wangu kwa Kuwaambia kuwa hakuna Mchezaji nisiyempenda Kikosini Simba SC na asiye na Faida Kwetu ( japo baadhi yenu hasa CEO Barbara Gonzalez ) mnamlea na Kumdekeza kama huyu Bernard Morrison.

Na nimepata Taarifa za Jikoni kabisa kutoka kwa Mmoja wa Kiongozi wa Simba SC na Mchezaji Mwandamizi Kikosini kuwa kumbe hata Kocha Mkuu Pablo Franco Martin nae si tu hamtaki bali hampendi kama ilivyo Kwangu ila anakingiwa Kifua.

Morrison ana Kiburi, Morrison Mjeuri, Morrison ana Hasira za Kipumbavu ( Kipopoma ), Morisson analazimisha Ufalme asioustahili kwa sasa ndani ya Simba SC, Morrison anapenda Kucheza sana na Jukwaa na ni mpenda Matukio yasiyo na Faida ama Kwake au hata kwa Klabu yetu pia, Morrison ana Dharau iliyopotiliza na isiyovumilika na mwisho kabisa nahisi Morrison ni Psychopath Case ila huenda Uongozi wa Simba SC bado haujaligundua hilo.

Akina Barbara Gonzalez ( CEO ), Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC Salim Abdallah Mhene 'Try Again', Mwenyekiti wa Simba SC ( Wanachama ) Murtaza Mangungu na Wewe 'Poti' wangu kabisa kutoka Mkoani Mara ( Musoma ) Kwetu Crescetius Magori ( Mshauri Mkuu wa Mwekezaji Mo Dewji ) na pia Mshauri wa CEO na Benchi la Ufundi la Simba SC endeleeni tu Kumlea na Kumdekeza huyu Mchezaji Bernard Morrison ila GENTAMYCINE nawaambia hapa hapa JamiiForums kuwa kuna Siku atatugharimu na ataigharimu pakubwa mno Simba SC yetu.

3. Pape Ousmane Sakho
Ni Mchezaji mzuri sana na mwenye Kipaji cha Kipekee kiasi kwamba kwa anavyocheza natabiri mapema kuwa huenda huko mbeleni Simba SC ikatajirika zaidi kwa Kumuuza Nje kwa Gharama za hata Kuwazidi akina Chama na Miquissone.

Hata hivyo pamoja na hizi Kongole ( Pongezi ) zangu Kwake Sakho nae ana Mapungufu yanayotakiwa Kurekebisha haraka kwani akiachwa namuona nae ana 'Elements' za akina Inonga na Morisson.

Sakho anapenda Kukurupuka, Sakho anapenda Sifa ( hasa Kucheza na Majukwaa ), Sakho ameshaanza Kuota Majipu Kwapani ( namaanisha Kuringa na kujiona ni kila Kitu sasa Kikosini ), Sakho anataka Kuulazimisha Ufalme wake sasa Simba SC wakati muda wake wa kuwa Mfalme nauona upo ndani ya miaka Miwili ijayo.

Sakho anataka kila Kitu cha Uwanjani awe anakifanya Yeye tu hata kama Kiufundi kwa Mazingira yaliyopo hapaswi kuyafanya Yeye, Sakho anapenda sana Kukaa na Mpira na Kupiga Chenga nyingi ( Over Dribbling ) kitu ambacho ni Hatari mno Kwake Kiafya kwani uwezekano wa Kuumizwa vibaya na kupata Majeraha makubwa mfano akikutana na Mabeki 'Wahuni' na 'Masela' akina Kelvin Yondan na Juma Nyosso ( ambao Wote sasa wako Geita Gold FC ) kwa Kocha Fred Felix Kataraiya Majeshi Minziro ni mkubwa.

Tafadhali waambiwe na wajitathmini!!!!
Acha wachezaji wacheze, ungetaka na wewe ungekuwa mchezaji ili uwe na hizo tabia ulizotaja.....au kaombe ukocha, kumbuka wale wapo kazini kama wewe unapokuwa kazini na unaamini unafanya kaz vizuri..Tupunguze maneno wakati hata danadana tu huwez
 
Watu wengine mnatuchosha tu. Mnakuwa kama wehu. Wewe na Pablo naniwenye jicho la kuangalia wachezaji.
Utukome nyambafu.
 
Andiko limejaa CHUKI, UJUAJI na WIVU.
Halafu huyo huyo GENTAMYCINE mnayemchukia na hata Kutompenda ndiyo kila Siku mkiingia tu hapa JamiiForums ni lazima mtamfuatilia na Kumsoma kila anachokiandika. Tangia muanze Kunichukia mpaka Kuimba kila Siku mmetajirika na chochote kile au Mimi GENTAMYCINE ambaye 'Fame' yangu Kubwa hapa JamiiForums inayowanyima Usingizi nimekufa au hata tu Kupungukiwa na lolote lile?

Hivi Members wasio na CHUKI, UJUAJI na WIVU kuliko Mimi wameisha hapa JamiiForums ili muwe mnawasoma Wao 24/7 kuliko Kutwa tu Kuteseka na Kuhangaika nami niliyebarikiwa Shani ( Tunu ) nyingi za Kiupendeleo na Mwenyezi Mungu kuliko Mpumbavu Mmoja na Wenzako baadhi hapa?
 
Uyo Inonga anapenda sifa ambazo wala hana, hasira zake za kipumbavu cku moja zitamgharimu, Angekuwa anatoa ata asist kama yannik bangala si angewapanda watu kichwani kabisa
Kwa hili Mkuu nakubaliana nawe 100%.
 
Halafu huyo huyo GENTAMYCINE mnayemchukia na hata Kutompenda ndiyo kila Siku mkiingia tu hapa JamiiForums ni lazima mtamfuatilia na Kumsoma kila anachokiandika.

Hivi Members wasio na CHUKI, UJUAJI na WIVU kuliko Mimi wameisha hapa JamiiForums ili muwe mnawasoma Wao 24/7 kuliko Kutwa tu Kuteseka na Kuhangaika nami niliyebarikiwa Shani ( Tunu ) nyingi za Kiupendeleo na Mwenyezi Mungu kuliko Mpumbavu Mmoja na Wenzako baadhi hapa?
Kwa hiyo watu kusoma uzi wako we umeona ni kwa sababu wewe ni bora na wa maana JF than others sasa wewe ungekuwa mchezaji hao uliowakosoa si wangeonekana wana afadhali? Unakemea tabia ambayo wewe naye unayo huku ni kujitoa ufahamu

Na wewe badilika ,kama unajua toa maoni yako then quit sifa zitakuja zenyewe
 
Ngoja wanywe chai waje kukupiga.
Silaha yangu Kubwa GENTAMYCINE ni Kujiamini, kuwa na Msimamo na Akili nyingi nilizobarikiwa nazo na Mwenyezi Mungu kuliko Wao na nawasubiri ili ikiwezekana niwafundishe Kufikiri na hata Kujenga Hoja vile vile pindi wawapo hapa Mtandaoni JamiiForums.
 
Ngoja misukule ya mudi ije kukushambulia
Nami pia nawasubiri kwa hamu sana Mkuu wangu na uzuri ni kwamba hata Moto wangu wanaujua na Falsafa yangu haijabadilika ambapo Ukiniheshimu nami Nitakuheshimu zaidi, ila Ukijamba tu basi Mimi Nitakunya kabisa.
 
Jamaa umeongea kitu ambacho nilikua nacho akilin mwangu.

Sijui Simba Kuna mdudu gani anawatafuna hasa wachezaji .

Yaan akibahatisha mechi moja na kupewa sifa Basi mchezaji husika ataanza kuvimba kujiona mkubwa atacheza kwa kujiamini Sana.
Huyo Innonga kiukweli ameanza kulewa sifa na anajiamini kupitiliza Sana hata Jana kala njano kidogo atucost kwa upuuz wake .Mwambien apunguze sifa acheze mpira Simba Ni kubwa kuliko yeye na ataiacha.

Kuhusu Sako Ni kweli anapaswa wamtime maana nae ameanza kulewa sifa na kutaka kila kitu afanye yeye .Kona zake mbovu ,freekick mbovu alafu apunguze kukaa Sana na mpira ,kwenye lig ya bongo watamvunja kabisa.

Kuhusu Morrison hii ndio takataka kabisa Alafu et ndie mchezaj anayelipwa pesa nyingi hapo Simba.

Morrison Hana mpira wa kuamua matokeo ,Leo awe vzr kesho hovyo .

Wachezaj wengi wa Simba wanatabia ya kulazimisha ufather wakat hawana huo ufather ,na kulingana na ujinga wao washatucost Mara kadhaa ,hata kaizer alitutoa sabab hiyo hiyo ya kujiamin kupita kiasi.

Simba hata akipata goli mbili tu wanaanza show game Kama kawaida yao na Mara nyingi hufanya uzembe na kupigwa goli na kufuta clean sheet kwa upuuz wao wenyew.

Mfano Simba ikatokea ametanguliwa na timu yoyote kwenye lig hiyo mechi Simba lazima apoteze maana hawana spirit ya kujituma Kama walivyo watan zangu yanga ,yanga nawasifu kwa Hilo yaan ukimfunga goli Ni Kama unakua umekorofisha nyuki Ila kwa Simba hicho kitu hakipo kabisa.

Mwisho wa siku nasemaje hata huko shirikisho nayaona makosa yanaenda kujirudia Kama Yale ya kaizer na Galaxy sabab ya ujinga wa baadhi ya wachezaji.
Mkuu nimependa sana haya Madini yako.
 
Mimi sina la kusema ndugu yangu, umeongea ukweli na acha ukweli ukuweke huru.
1.INONGA
Anataka kubeba hata kisicho chake, anafokea hadi nahodha wake badala ya kumshauri. Back passes za ovyo na kujiamini kulikopitiliza hadi anaharibu. Mechi aliyojisifu kumdhibiti Mayele ni kweli tuhesabu matukio ambayo Mayele aliyodhibitiwa na Onyango kulinganisha na yake.
2.MORRISON
Huyu ni mchezaji mzuri anayetoa faida anapopenda yeye. Hana uchungu na timu, kwake sifa binafsi ni muhimu kuliko sifa ya timu. Ile faulo iliyompa kadi Jana dhidi ya Mlandege ilikuwa na faida gani zaidi ya kuendeleza ubabe usio na faida?
3.SAKHO
Mcheza na jukwaa maarufu, kila akifanya kitu anageukia jukwaa kuliamsha limshangilie. Ni aina ya SAID SUED "SCUD". Aache umaarufu umfuate, akiufuata utamwangamiza.
Umemaliza kila Kitu Mkuu Asante sana.
 
Morison huu ndo msimu wake wa mwisho hawezi kuongezewa mkataba
Nitakuwa wa Kwanza kabisa Kushangilia pale tu nikisikia kuwa Klabu yangu pendwa ya Simba imeachana nae ( imemtema ) rasmi kwani kiukweli Simpendi mpaka namuona ni Kero na kama siyo Takataka iliyoko Msimbazi.
 
Inonga anapenda Sifa, Yes ( kama ilivyo kwa binadamu wote).
Kupenda kwake sifa, ndio kunamfanya ajitume zaidi ( Anapenda sifa lakini hajawahi tuchomesha).
Kuhusu kugombeza kila mtu, nadhani inonga ni experienced player kuliko wengi walioanza jana ( hasa beki za pembeni, zina makosa mengi mno) hivyo wanapofanya tofauti wacha warekebishwe.....
Mchezaji wangu bora kwa sasa, Ni Inonga baka " Varane". Mechi zote anacheza kwa performance ileile ya hali ya juu......
Hakuwahi cheza chini ya kiwango.
Kuna mahala popote pale katika Maelezo yangu GENTAMYCINE nimesema Henock Inonga ni Mchezaji mbaya?

Tafadhali Siku zingine mkijijua hamna Akili au Wazito Kuelewa au Uwezo wenu wa Kuchambua Masuala Mtambuka ni mdogo ( haba ) acheni Kushoboka Kufungua na Kusoma Mada zangu mbalimbali hapa JamiiForums sawa?

Mnakera.. .!!!
 
Inonga yupo vizuri ila mkude, mzamiru na wawa wajifunze kuweka mpira chini na kupiga pasi za macho, mipira yao mirefu mingi inapotea. Mkude na mzamiru wanapenda sana kurudisha mpira nyuma badala ya kupeleka mbele tatizo ambalo pia analo mwenda. Back pass zimekuwa nyingi
Kuna mahala nimeona GENTAMYCINE nimeambiwa nimeleta Uzi huu kwa CHUKI, UJUAJI na WIVU na Wewe 'umelaiki' pia sasa inakuwaje tena Unauchangia?

Mnafiki mkubwa Wewe na nilishakugundua Kitambo tu na sijui ni kwanini huwa unapenda Kujipendekeza ama Kufungua au Kusoma Mada zangu nyingi na mbalimbali hapa JamiiForums?

Mnanichukia 24/7 ila hamuachi Kunisoma hapa JamiiForums. Kwani hao mnaowapenda na Kuwakubali wameisha hapa Jamvini? Kwanini usiwe / msiwe mnasoma Mada zao ili muachane nami ninaowakera ila niliyewazidi vingi tu kwa Kubarikiwa navyo na Mwenyezi Mungu?
 
Nifaida kwa Simba Kama inonga na sakho wakijiamin nakujiona wao niwachezaji muhimu kikosini, Banda kanoute nimuhimu wakiiga mentality yakujiamin nakujiona muhim kikosin.
Shida ya mleta uzi niushamba mwingi wakujikuta mjuaji wakila ktu

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
Halafu huyo huyo GENTAMYCINE mnayemchukia na hata Kutompenda ndiyo kila Siku mkiingia tu hapa JamiiForums ni lazima mtamfuatilia na Kumsoma kila anachokiandika. Tangia muanze Kunichukia mpaka Kuimba kila Siku mmetajirika na chochote kile au Mimi GENTAMYCINE ambaye 'Fame' yangu Kubwa hapa JamiiForums inayowanyima Usingizi nimekufa au hata tu Kupungukiwa na lolote lile?

Hivi Members wasio na CHUKI, UJUAJI na WIVU kuliko Mimi wameisha hapa JamiiForums ili muwe mnawasoma Wao 24/7 kuliko Kutwa tu Kuteseka na Kuhangaika nami niliyebarikiwa Shani ( Tunu ) nyingi za Kiupendeleo na Mwenyezi Mungu kuliko Mpumbavu Mmoja na Wenzako baadhi hapa?
 
Kwa hiyo watu kusoma uzi wako we umeona ni kwa sababu wewe ni bora na wa maana JF than others sasa wewe ungekuwa mchezaji hao uliowakosoa si wangeonekana wana afadhali? Unakemea tabia ambayo wewe naye unayo huku ni kujitoa ufahamu

Na wewe badilika ,kama unajua toa maoni yako then quit sifa zitakuja zenyewe
Pumbavu.
 
Watu wengine mnatuchosha tu. Mnakuwa kama wehu. Wewe na Pablo naniwenye jicho la kuangalia wachezaji.
Utukome nyambafu.
Uzi huu nimewaandikia Wana Simba SC na Wanamichezo Werevu ( Intelligent ) pekee na haukuwa kwa ajili yako Wewe Mpumbavu Mwandamizi ( Senior Damn Fool ) na wale Wenzako kadhaa mliochangia huu Uzi wangu sawa?
 
Acha wachezaji wacheze, ungetaka na wewe ungekuwa mchezaji ili uwe na hizo tabia ulizotaja.....au kaombe ukocha, kumbuka wale wapo kazini kama wewe unapokuwa kazini na unaamini unafanya kaz vizuri..Tupunguze maneno wakati hata danadana tu huwez
Damn Fool.
 
Back
Top Bottom