Simba SC irekebishe upesi sana 'Mapungufu' ya hawa Wachezaji Watatu Inonga, Sakho na Morisson kwani yanaigharimu Timu

Punguza Chuki na wivu, Kila mchezaji anaefanya vizuri wewe unaleta wivu na chuki,

Chuki chuki chuki, wivu wivu wivu wa kipimbi
 
1. Henock Inonga
Nakiri ni Beki mzuri sana na nimekuja Kugundua pia kuwa kumbe ni Versatile na kwamba anaweza hata kucheza vyema tu Namba 6, Namba 8 na hata Namba 2.

Mchezaji huyu tokea aicheze vyema ile Kariakoo Derby na kupata Sifa nyingi nae ameshajaa Upepo kiasi kwamba sasa anajiona ndiyo Mchezaji mzuri Kikosini Simba SC kuliko wengine waliopo au aliowakuta.

Inonga amekuwa akipenda Kulaumu mno Wenzake Uwanjani huku muda mwingi akitaka Kuonekana kama Yeye ndiyo anacheza kwa Bidii kuliko Wenzake na hupenda sana Kucheza na Akili ya Kocha Pablo ili apendwe na aaminike zaidi Kwake.

Inonga aambiwe ukweli kuwa katika ile 'Kariakoo Derby' Kazi ya Kumkaba Mshambuliaji hatari na ninayemuogopa wa Yanga SC Fiston Mayele hakuifanya peke yake kama adhaniavyo bali alikabwa Collectively and Strategically na Mabeki Wenzake Wote na tena kama kuna Mtu ambaye Mimi GENTAMYCINE niliona ndiyo alimkaba vilivyo Mayele ni Beki Joash Onyango na siyo Yeye Henock Inonga.

2. Bernard Morrison
Huyu nadhani GENTAMYCINE nilishamsoma mno hapa JamiiForums na mpaka Kuutaka Uongozi wa Simba SC Kumkanya na Kumrekebisha ila naona Jana katika Mechi na Mlandege FC yamejirudia tena yale yale.

Uongozi wa Simba SC leo ngoja sasa niwapasulieni Ukweli wangu kwa Kuwaambia kuwa hakuna Mchezaji nisiyempenda Kikosini Simba SC na asiye na Faida Kwetu ( japo baadhi yenu hasa CEO Barbara Gonzalez ) mnamlea na Kumdekeza kama huyu Bernard Morrison.

Na nimepata Taarifa za Jikoni kabisa kutoka kwa Mmoja wa Kiongozi wa Simba SC na Mchezaji Mwandamizi Kikosini kuwa kumbe hata Kocha Mkuu Pablo Franco Martin nae si tu hamtaki bali hampendi kama ilivyo Kwangu ila anakingiwa Kifua.

Morrison ana Kiburi, Morrison Mjeuri, Morrison ana Hasira za Kipumbavu ( Kipopoma ), Morisson analazimisha Ufalme asioustahili kwa sasa ndani ya Simba SC, Morrison anapenda Kucheza sana na Jukwaa na ni mpenda Matukio yasiyo na Faida ama Kwake au hata kwa Klabu yetu pia, Morrison ana Dharau iliyopotiliza na isiyovumilika na mwisho kabisa nahisi Morrison ni Psychopath Case ila huenda Uongozi wa Simba SC bado haujaligundua hilo.

Akina Barbara Gonzalez ( CEO ), Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC Salim Abdallah Mhene 'Try Again', Mwenyekiti wa Simba SC ( Wanachama ) Murtaza Mangungu na Wewe 'Poti' wangu kabisa kutoka Mkoani Mara ( Musoma ) Kwetu Crescetius Magori ( Mshauri Mkuu wa Mwekezaji Mo Dewji ) na pia Mshauri wa CEO na Benchi la Ufundi la Simba SC endeleeni tu Kumlea na Kumdekeza huyu Mchezaji Bernard Morrison ila GENTAMYCINE nawaambia hapa hapa JamiiForums kuwa kuna Siku atatugharimu na ataigharimu pakubwa mno Simba SC yetu.

3. Pape Ousmane Sakho
Ni Mchezaji mzuri sana na mwenye Kipaji cha Kipekee kiasi kwamba kwa anavyocheza natabiri mapema kuwa huenda huko mbeleni Simba SC ikatajirika zaidi kwa Kumuuza Nje kwa Gharama za hata Kuwazidi akina Chama na Miquissone.

Hata hivyo pamoja na hizi Kongole ( Pongezi ) zangu Kwake Sakho nae ana Mapungufu yanayotakiwa Kurekebisha haraka kwani akiachwa namuona nae ana 'Elements' za akina Inonga na Morisson.

Sakho anapenda Kukurupuka, Sakho anapenda Sifa ( hasa Kucheza na Majukwaa ), Sakho ameshaanza Kuota Majipu Kwapani ( namaanisha Kuringa na kujiona ni kila Kitu sasa Kikosini ), Sakho anataka Kuulazimisha Ufalme wake sasa Simba SC wakati muda wake wa kuwa Mfalme nauona upo ndani ya miaka Miwili ijayo.

Sakho anataka kila Kitu cha Uwanjani awe anakifanya Yeye tu hata kama Kiufundi kwa Mazingira yaliyopo hapaswi kuyafanya Yeye, Sakho anapenda sana Kukaa na Mpira na Kupiga Chenga nyingi ( Over Dribbling ) kitu ambacho ni Hatari mno Kwake Kiafya kwani uwezekano wa Kuumizwa vibaya na kupata Majeraha makubwa mfano akikutana na Mabeki 'Wahuni' na 'Masela' akina Kelvin Yondan na Juma Nyosso ( ambao Wote sasa wako Geita Gold FC ) kwa Kocha Fred Felix Kataraiya Majeshi Minziro ni mkubwa.

Tafadhali waambiwe na wajitathmini!!!!
Ndo maana Chama na Luis,mnaendelea kuwaota kila kukicha...Wanaujua sana mpira halafu sijawahi kuwaona wakiringa kwa kujua kwao ndiki
 
Inonga anapenda Sifa, Yes ( kama ilivyo kwa binadamu wote).
Kupenda kwake sifa, ndio kunamfanya ajitume zaidi ( Anapenda sifa lakini hajawahi tuchomesha).
Kuhusu kugombeza kila mtu, nadhani inonga ni experienced player kuliko wengi walioanza jana ( hasa beki za pembeni, zina makosa mengi mno) hivyo wanapofanya tofauti wacha warekebishwe.....
Mchezaji wangu bora kwa sasa, Ni Inonga baka " Varane". Mechi zote anacheza kwa performance ileile ya hali ya juu......
Hakuwahi cheza chini ya kiwango.
Inonga jamaa japo anapenda sifa ila kila mechi aliyocheza perfomance ile ile ipo juu consistency, kuhusu kufokea wenzake wanapofanya makosa ni kukumbushana majukumu, ndan yake kuna captain spirit japo sio captain

Sacko mchezaji mzuri ila kuna kitu anapaswa atuonyeshe mashabik wa simba ili tumuingize kwenye kundi la ufalme, kila kitu cha kumfanya awe mfalme anacho, ni juu yake tu kutudhibitishia ila aache kukaa na mipira miguun muda mrefu ataumizwa

Morrison huyu nadhan baada ya msimu huu kuisha sidhan kama ataongezewa mkataba, ni mchezaji mzuri ila ana mapungufu fulan fulan hasa timu ikiwa haina mpira hanakua hana msaada pia kuna muda anapaswa kuachia pasi haraka kutengeneza shambuliz ila yeye atang'ang'ania kumpiga chenga
 
Kuna mahala nimeona GENTAMYCINE nimeambiwa nimeleta Uzi huu kwa CHUKI, UJUAJI na WIVU na Wewe 'umelaiki' pia sasa inakuwaje tena Unauchangia?

Mnafiki mkubwa Wewe na nilishakugundua Kitambo tu na sijui ni kwanini huwa unapenda Kujipendekeza ama Kufungua au Kusoma Mada zangu nyingi na mbalimbali hapa JamiiForums?

Mnanichukia 24/7 ila hamuachi Kunisoma hapa JamiiForums. Kwani hao mnaowapenda na Kuwakubali wameisha hapa Jamvini? Kwanini usiwe / msiwe mnasoma Mada zao ili muachane nami ninaowakera ila niliyewazidi vingi tu kwa Kubarikiwa navyo na Mwenyezi Mungu?
Safi Sana kaka popoma mpe mawe huyo jinga asiejua kitu.
Japo mimi ni yanga huu uzi nimeukubali kabisa una manufaa kwa Team zote tu sio simba tu.
Kwamba wachezaji wote wenye tabia ya kuvimba waache haifai.
Mimi naona aucho ana tabia hizo. Kila mara anaomba likizo kwenda kwao matatizo ya kifamilia hayaishi..

Safi Sana popoma.
 
Uyo Inonga anapenda sifa ambazo wala hana, hasira zake za kipumbavu cku moja zitamgharimu, Angekuwa anatoa ata asist kama yannik bangala si angewapanda watu kichwani kabisa
Kwa sasa anawapanda Migongoni tu mnalalamika hivi ....😁😁😁😁😁😁😁😁
 
Tusiwe na haraka ya kuongea. Ongea pale tu ukiwa umejiridhisha.
 
Wachezaji ni kama Wasanii, kwamba pamoja na mazuri yao basi pia wana mapungufu yao.

Bob Marley, Michael Jackson,Elton John, Tupack n.k.

Huenda kuwaondolea hayo basi utakosa kabisa kile kizuri kutoka kwao.

Tuzingatie zaidi ile bidhaa ya mwisho tunayoipata kutoka kwao...Huku wakiendelea kushauriwa ili kuboresha kazi zao.
 
Inonga yupo vizuri ila mkude, mzamiru na wawa wajifunze kuweka mpira chini na kupiga pasi za macho, mipira yao mirefu mingi inapotea. Mkude na mzamiru wanapenda sana kurudisha mpira nyuma badala ya kupeleka mbele tatizo ambalo pia analo mwenda. Back pass zimekuwa nyingi
Timu nzima ya simba hakuna mchezaji anaepiga pasi ndefu na kwa usahihi kama mkude
 
1. Henock Inonga
Nakiri ni Beki mzuri sana na nimekuja Kugundua pia kuwa kumbe ni Versatile na kwamba anaweza hata kucheza vyema tu Namba 6, Namba 8 na hata Namba 2.

Mchezaji huyu tokea aicheze vyema ile Kariakoo Derby na kupata Sifa nyingi nae ameshajaa Upepo kiasi kwamba sasa anajiona ndiyo Mchezaji mzuri Kikosini Simba SC kuliko wengine waliopo au aliowakuta.

Inonga amekuwa akipenda Kulaumu mno Wenzake Uwanjani huku muda mwingi akitaka Kuonekana kama Yeye ndiyo anacheza kwa Bidii kuliko Wenzake na hupenda sana Kucheza na Akili ya Kocha Pablo ili apendwe na aaminike zaidi Kwake.

Inonga aambiwe ukweli kuwa katika ile 'Kariakoo Derby' Kazi ya Kumkaba Mshambuliaji hatari na ninayemuogopa wa Yanga SC Fiston Mayele hakuifanya peke yake kama adhaniavyo bali alikabwa Collectively and Strategically na Mabeki Wenzake Wote na tena kama kuna Mtu ambaye Mimi GENTAMYCINE niliona ndiyo alimkaba vilivyo Mayele ni Beki Joash Onyango na siyo Yeye Henock Inonga.

2. Bernard Morrison
Huyu nadhani GENTAMYCINE nilishamsoma mno hapa JamiiForums na mpaka Kuutaka Uongozi wa Simba SC Kumkanya na Kumrekebisha ila naona Jana katika Mechi na Mlandege FC yamejirudia tena yale yale.

Uongozi wa Simba SC leo ngoja sasa niwapasulieni Ukweli wangu kwa Kuwaambia kuwa hakuna Mchezaji nisiyempenda Kikosini Simba SC na asiye na Faida Kwetu ( japo baadhi yenu hasa CEO Barbara Gonzalez ) mnamlea na Kumdekeza kama huyu Bernard Morrison.

Na nimepata Taarifa za Jikoni kabisa kutoka kwa Mmoja wa Kiongozi wa Simba SC na Mchezaji Mwandamizi Kikosini kuwa kumbe hata Kocha Mkuu Pablo Franco Martin nae si tu hamtaki bali hampendi kama ilivyo Kwangu ila anakingiwa Kifua.

Morrison ana Kiburi, Morrison Mjeuri, Morrison ana Hasira za Kipumbavu ( Kipopoma ), Morisson analazimisha Ufalme asioustahili kwa sasa ndani ya Simba SC, Morrison anapenda Kucheza sana na Jukwaa na ni mpenda Matukio yasiyo na Faida ama Kwake au hata kwa Klabu yetu pia, Morrison ana Dharau iliyopotiliza na isiyovumilika na mwisho kabisa nahisi Morrison ni Psychopath Case ila huenda Uongozi wa Simba SC bado haujaligundua hilo.

Akina Barbara Gonzalez ( CEO ), Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC Salim Abdallah Mhene 'Try Again', Mwenyekiti wa Simba SC ( Wanachama ) Murtaza Mangungu na Wewe 'Poti' wangu kabisa kutoka Mkoani Mara ( Musoma ) Kwetu Crescetius Magori ( Mshauri Mkuu wa Mwekezaji Mo Dewji ) na pia Mshauri wa CEO na Benchi la Ufundi la Simba SC endeleeni tu Kumlea na Kumdekeza huyu Mchezaji Bernard Morrison ila GENTAMYCINE nawaambia hapa hapa JamiiForums kuwa kuna Siku atatugharimu na ataigharimu pakubwa mno Simba SC yetu.

3. Pape Ousmane Sakho
Ni Mchezaji mzuri sana na mwenye Kipaji cha Kipekee kiasi kwamba kwa anavyocheza natabiri mapema kuwa huenda huko mbeleni Simba SC ikatajirika zaidi kwa Kumuuza Nje kwa Gharama za hata Kuwazidi akina Chama na Miquissone.

Hata hivyo pamoja na hizi Kongole ( Pongezi ) zangu Kwake Sakho nae ana Mapungufu yanayotakiwa Kurekebisha haraka kwani akiachwa namuona nae ana 'Elements' za akina Inonga na Morisson.

Sakho anapenda Kukurupuka, Sakho anapenda Sifa ( hasa Kucheza na Majukwaa ), Sakho ameshaanza Kuota Majipu Kwapani ( namaanisha Kuringa na kujiona ni kila Kitu sasa Kikosini ), Sakho anataka Kuulazimisha Ufalme wake sasa Simba SC wakati muda wake wa kuwa Mfalme nauona upo ndani ya miaka Miwili ijayo.

Sakho anataka kila Kitu cha Uwanjani awe anakifanya Yeye tu hata kama Kiufundi kwa Mazingira yaliyopo hapaswi kuyafanya Yeye, Sakho anapenda sana Kukaa na Mpira na Kupiga Chenga nyingi ( Over Dribbling ) kitu ambacho ni Hatari mno Kwake Kiafya kwani uwezekano wa Kuumizwa vibaya na kupata Majeraha makubwa mfano akikutana na Mabeki 'Wahuni' na 'Masela' akina Kelvin Yondan na Juma Nyosso ( ambao Wote sasa wako Geita Gold FC ) kwa Kocha Fred Felix Kataraiya Majeshi Minziro ni mkubwa.

Tafadhali waambiwe na wajitathmini!!!!
Umenena mkuu. uko sahihi 100%. Nyongeza kwa wachezaji wote ni kwamba waongeze speed ya uchezaji na waachane na back pass. Mchezaji anapata mpira katikati ya uwanja halafu anamrudishia kipa. inaudhi sana
 
Back
Top Bottom