Simba SC irekebishe upesi sana 'Mapungufu' ya hawa Wachezaji Watatu Inonga, Sakho na Morisson kwani yanaigharimu Timu

Punguza Chuki na wivu, Kila mchezaji anaefanya vizuri wewe unaleta wivu na chuki,

Chuki chuki chuki, wivu wivu wivu wa kipimbi
 
Mkuu nitakuwa mkali kwa mwanasimba yoyote atakayemsema vibaya Inonga....
Anafurahisha sana, Ni beki zile zenye akili..
Akipona lwanga, Simba tutakuwa na ukuta mgumu ever ( Inonga na Onyango mbele DM wao ni Lwanga).
Umesomeka mkuu, big up!
 
Ndo maana Chama na Luis,mnaendelea kuwaota kila kukicha...Wanaujua sana mpira halafu sijawahi kuwaona wakiringa kwa kujua kwao ndiki
 
Inonga jamaa japo anapenda sifa ila kila mechi aliyocheza perfomance ile ile ipo juu consistency, kuhusu kufokea wenzake wanapofanya makosa ni kukumbushana majukumu, ndan yake kuna captain spirit japo sio captain

Sacko mchezaji mzuri ila kuna kitu anapaswa atuonyeshe mashabik wa simba ili tumuingize kwenye kundi la ufalme, kila kitu cha kumfanya awe mfalme anacho, ni juu yake tu kutudhibitishia ila aache kukaa na mipira miguun muda mrefu ataumizwa

Morrison huyu nadhan baada ya msimu huu kuisha sidhan kama ataongezewa mkataba, ni mchezaji mzuri ila ana mapungufu fulan fulan hasa timu ikiwa haina mpira hanakua hana msaada pia kuna muda anapaswa kuachia pasi haraka kutengeneza shambuliz ila yeye atang'ang'ania kumpiga chenga
 
Uzi huu nimewaandikia Wana Simba SC na Wanamichezo Werevu ( Intelligent ) pekee na haukuwa kwa ajili yako Wewe Mpumbavu Mwandamizi ( Senior Damn Fool ) na wale Wenzako kadhaa mliochangia huu Uzi wangu sawa?
[emoji23][emoji23]Genta mzee wa makavu kazini
 
Safi Sana kaka popoma mpe mawe huyo jinga asiejua kitu.
Japo mimi ni yanga huu uzi nimeukubali kabisa una manufaa kwa Team zote tu sio simba tu.
Kwamba wachezaji wote wenye tabia ya kuvimba waache haifai.
Mimi naona aucho ana tabia hizo. Kila mara anaomba likizo kwenda kwao matatizo ya kifamilia hayaishi..

Safi Sana popoma.
 
Uyo Inonga anapenda sifa ambazo wala hana, hasira zake za kipumbavu cku moja zitamgharimu, Angekuwa anatoa ata asist kama yannik bangala si angewapanda watu kichwani kabisa
Kwa sasa anawapanda Migongoni tu mnalalamika hivi ....😁😁😁😁😁😁😁😁
 
Tusiwe na haraka ya kuongea. Ongea pale tu ukiwa umejiridhisha.
 
Wachezaji ni kama Wasanii, kwamba pamoja na mazuri yao basi pia wana mapungufu yao.

Bob Marley, Michael Jackson,Elton John, Tupack n.k.

Huenda kuwaondolea hayo basi utakosa kabisa kile kizuri kutoka kwao.

Tuzingatie zaidi ile bidhaa ya mwisho tunayoipata kutoka kwao...Huku wakiendelea kushauriwa ili kuboresha kazi zao.
 
Timu nzima ya simba hakuna mchezaji anaepiga pasi ndefu na kwa usahihi kama mkude
 
Umenena mkuu. uko sahihi 100%. Nyongeza kwa wachezaji wote ni kwamba waongeze speed ya uchezaji na waachane na back pass. Mchezaji anapata mpira katikati ya uwanja halafu anamrudishia kipa. inaudhi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…