Kitoabu
JF-Expert Member
- Jul 7, 2011
- 10,677
- 11,768
Vijana wa Simba wanatakata.
Watakate kisoka sio kisura wakani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Vijana wa Simba wanatakata.
Bakhresa ndiye anawalipa startv ili warushe mipambano ya Azam wakati timu nyingine zikisubiri kulipwa na wenye tv ili warushe mechi zao. Yani Azam wanakwenda anti clockwise movement lakini wanelekea kufika.
Simba wamefunga vitambaa mikononi sijui vya nini,na inavyoonyesha Yanga tunaanza kusukuma ngozi ya ng'ombe.
Ahaa okeyyyyy!Tunakumbuka mwaka mmoja wa kifo cha Mafisango.
Acha umbea! Azam tuna kwenda na wakati.Mkuu Mwita Maranya kumbe na huku unaingia safi sana nimefurahi kukuona huku.Mkakati wa Bhakhresa ni kuhakikisha kwamba Azam inapendwa na ndio maana mechi zote za azama zinaonyeshwa na hasa siku ambayo simba inacheza ama Yanga,huu ni mkakati wake na analipia fedha nyingi sana mkuu.
Leo nimeamua kusikiliza radio ya CCM, kweli kila kitu kina faida na hasara, leo naona faida ya CCM kuwa na radio, nimehangaika kutafuta radio yoyote iliyo online inayotangaza hii mechi; nimeanzia TBC Taifa bila bila, Kiss FM bila bila, Radio One hakuna kitu, cha kushangaza radio ya CCM imeniokoa. Leo ndo nimefaidi kodi yangu inayoenda CCM kama ruzuku.
Mbona mapema..?sekunde ya 52 Twite anapata kadi ya njano.