Simba SC v Young Africans SC

Simba SC v Young Africans SC

Bakhresa ndiye anawalipa startv ili warushe mipambano ya Azam wakati timu nyingine zikisubiri kulipwa na wenye tv ili warushe mechi zao. Yani Azam wanakwenda anti clockwise movement lakini wanelekea kufika.

Mkuu Mwita Maranya kumbe na huku unaingia safi sana nimefurahi kukuona huku.Mkakati wa Bhakhresa ni kuhakikisha kwamba Azam inapendwa na ndio maana mechi zote za azama zinaonyeshwa na hasa siku ambayo simba inacheza ama Yanga,huu ni mkakati wake na analipia fedha nyingi sana mkuu.
 
Simba wamefunga vitambaa mikononi sijui vya nini,na inavyoonyesha Yanga tunaanza kusukuma ngozi ya ng'ombe.
 
Mkuu Mwita Maranya kumbe na huku unaingia safi sana nimefurahi kukuona huku.Mkakati wa Bhakhresa ni kuhakikisha kwamba Azam inapendwa na ndio maana mechi zote za azama zinaonyeshwa na hasa siku ambayo simba inacheza ama Yanga,huu ni mkakati wake na analipia fedha nyingi sana mkuu.
Acha umbea! Azam tuna kwenda na wakati.
 
Leo nimeamua kusikiliza radio ya CCM, kweli kila kitu kina faida na hasara, leo naona faida ya CCM kuwa na radio, nimehangaika kutafuta radio yoyote iliyo online inayotangaza hii mechi; nimeanzia TBC Taifa bila bila, Kiss FM bila bila, Radio One hakuna kitu, cha kushangaza radio ya CCM imeniokoa. Leo ndo nimefaidi kodi yangu inayoenda CCM kama ruzuku.

Tuko pamoja mkuu, hata mi nimetafuta radio iliyo online nimekutana na Uhuru pekee ndio walio mtandaoni; Ila sidhani kama nitaweza kumaliza maana, leo nna wasiwasi kama simba tutatoka
 
Sìmba anachapwa goli dk 5.ha haa nahama timu hii.
 
Back
Top Bottom