Simba Sports Club achaneni na nia yenu ya kumfukuza kocha wetu Patrick Aussems kwani tutakuja kujuta na kulia akiondoka

Ajabuu sana mkuu.
After all hiyo timu iliyofanya vizuri ilianza kuandaliwa misimu mitatu iliyopita sasa hii waliyokusanya wao kama national team wanataka ifanye vizuri all of a sudden ?
 
Huyo Aussems mwenyewe amekuja kwa 10 per cent, haiingii akilini unamwacha Leschante na Masoud Jouma unamleta kocha ambae hata kufanya sub ni issue.

Ulipomtaja huyo Masoud Djuma Irambona ndiyo nimekuona ' Mpuuzi ' kabisa na kumbe huijui Simba SC na yaliyokuwa yakiendelea kati ya Wachezaji wa Simba SC na huyo Kocha wako ambayo kwa bahati mbaya siyo ya Kimaadili kwa Mimi kuweza Kuyaanika hapa ila Watu wa Mpira na Watoto wa Mjini tunayajua na ndiyo maana tulipiga Kelele zetu ili aondolewe mapema kabla hali haijawa mbaya na nashukuru Uongozi ulitusikia na ukaachana nae.
 
Lewing ni wa wapi

Anaitwa Patrick Leiwig ambaye alishawahi kuwa Kocha Wetu na baadae tukaachana nae akaenda Stand United ya Shinyanga ambako huko nako alishindwa na kuamua Kuondoka Kwake kurudi Kwao. Ni Mzee na kwa taarifa za sasa zinasema kuwa hata Afya yake sasa siyo nzuri na amezidi Kudhoofu tu huko aliko. Alikuwa ni Kocha mwenye kupenda mno Kutumia Vijana na ndiyo huyu alifanya Wachezaji kama akina Said Ndemla, Jonas Mkude, Christopher Edward na wengineo Kuanza Kuaminiwa ndani ya Klabu.
 
Kumuondoa uchebe kwa sasa ni upopoma tuu. mo atakua anataka kuleta uleule uswahili

Na ndiyo maana nimemuonya na kuionya Simba SC mapema sana juu ya hili. Simba SC wakiachana na Kocha Aussems watajuta.
 
Hapa popoma umechemsha hao vijana uliowataja wamepita chini ya makocha zaidi ya watatu kabla Patrick Liewing hajaja simba.

Mathalan Mkude na Edward Christopher wlianza kupata nafasi ya kikosi cha kwanza chini ya Milovan Cirkovic.

Said Ndemla alipandishwa kikosi cha kwanza na Abdallah Kibadeni pamoja na Ramadhan Singano baadae akaja kuwa regular starter chini Goran Kuponovic.


 
Aondoke zake hana adabu. Anaondoka kwenda kutafuta timu nyingine kihunihuni. Atuachie timu yetu. Wanakuja wenye weledi zaidi. Simba tuna pesa za Mo. Mtu akilete ujinga tunatimua tu.
 
Timu inaongoza ligi. Imefungwa mechi moja imetoa sare mbili. Ligi ndio kwanza hata nusu ya msimu haijafika.

Kuna mishabiki inataka kufukuza kocha. Wakati huo shabiki huyo ni shabiki pia wa Chelsea ya pale Uingereza lakini husikii akimshikia bango Lampard aondolewe ukizingatia timu inashika nafasi ya nne. Anaamini msimu bado anaweza fanya vizuri zaidi.

Kuna Mbumbumbu nyingine hapo juu inasema haiwezekani Kocha unafungwa na timu moja(Kagera Sugar) nje ndani. Wakati huo anaona kawaida tu Barcelona kufungwa nje ndani na Levante tena kwa goli nyingi tu.

Halafu atokee mtu aniambie type hizi za mashabiki zinafikiri kwa kutumia kichwa na sio kiungo kingine ntamtia mkwenzi huo hatakuja nisahau.
 

Duh kweli katika hili nimekuwa Popoma kwani ' nimekengeuka ' mno kwa Rekodi zangu. Suala la Patrick linanipa taabu Mkuu.
 
Kuna mdau anamtaka Lechantre arudi Simba. Kiukweli Lechantre ni kocha mzuri ila falsafa ya kudefend kama Mourinho inaondoa utamu wa mpira. Timu inamiliki mpira muda wote wa mchezo lakini ushindi unakuwa moja bila tu. Na tabia yake ya kupanga wachezaji kuanzia beki na mbili mpaka kiungo mshambuliaji wote wazuiaji inaondoa zile amsha amsha. Huyu kocha ndio alikuwa anampanga Kapombe namba nane.

Raha ya mpira ni zile amsha amsha za washambuliaji na mawinga kupiga kambi kwenye goli la timu pinzani sio unaangalia mpira kama unatazama drafti au bao
 
Nadhani na Mimi sitokuwa mbali Kuyaiga haya Maamuzi yako na nitabaki zangu tu Kushangilia Timu zangu pendwa za Liverpool, Barcelona, AC Milan, PSG, Borussia Dortmund, Kaizer Chiefs, Corinthians, River Plate na Makabi Haifa.
Siku wakikutana Liver na Barca utashabikia timu gani?
 
MO hawezi kukubali kulipa uchebu milioni 23 kwa mwezi wakati wametolewa klabu bingwa caf, lazima atimuliwe
 
Imethibitishwa na vyanzo vya ndani kuwa hata Kitambi anaondoka anakuja Matola.

Wenyewe wana sema mafanikio ya msimu uliopita ni viongozi siyo Kocha,ndiyo hapo ujiulize viongozi walichangia kwa namna gani?
 
Imethibitishwa na vyanzo vya ndani kuwa hata Kitambi anaondoka anakuja Matola.

Wenyewe wana sema mafanikio ya msimu uliopita ni viongozi siyo Kocha,ndiyo hapo ujiulize viongozi walichangia kwa namna gani?

Acha Kusema Vyanzo vya ndani na badala yake sema tu kwamba hii tetesi umeisikia katika ile ' Segment ' ya ' Chabo Chabo ' ya Sports Headquarters ya Efm ya leo.
 
Mi nilidhani tangu timu iwe chini ya Mo ukiritimba kama huu umeisha kumbe bado,,,,kama ni kweli wana au watamfukuza bwana mandevu utakua uamuzi wa kibumbavuuuu kwa klabu ya simba tangu huu mwaka uanze katika nchii kwenye mpira.
 
Alifanya hivyo baada ya kumuona ni effective zaidi kwenye defence na attack tofauti na Mkude na Mzamiru ambao wote ni defence midfielders.

Kapombe anafanya vitu viwili kwa usahihi uwanjani lateral movement na vertical movements

Anauwezo mkubwa kwenye battle za one against one kuliko Mzamiru.

Passing accuracy yake iko juu kuliko Mzamiru au Ndemla ambao ndiyo walikuwa viungo wajuu baada ya Kotei kurudishwa kucheza kama defender.

Anaweza kuwin aerial duels zaidi kuliko Mzamiru kulingana na height yake.

Lechantre was right.
 

Mwalimu Kashasha ni Pacha wako kwa Kuzaliwa au ni Baba yako Mzazi hivyo Umerithi Uchambuzi wake au labda ni Yeye Mwenyewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…