Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) | Special thread
Tafadhali tupasheni hayo matokeo bandugu, si kung'ang'ana na siasa za Arumeru tu.
 
Asanteni sana kwa kutupa updates za mechi ya leo
 
Mungu bariki simba sport club hapo kesho iweze kuvuka hatua hii.Watie nguvu wachezaji na uwape hamasa ya kuona ushindi au draw itawafanya kuiwakilisha vzri tanzania katika michuano hii barani Afrika.
 
[h=2]SIMBA YAJIFUA SETIF[/h]
waki%20do.JPG



TIMU ya Simba leo imefanya mazoezi katika Uwanja wa Mei 8, 1945, ambao utatumika kwa mechi ya Kombe la Shirikisho (CAF) baina ya Wekundu wa Msimba na ES Setif ya Algeria.
Mazoezi hayo yalikuwa ya kwanza kufanywa na Simba katika mji huu wa milima milima na hali ya hewa ilikuwa ya baridi kali kwa kiwango cha nyuzijoto tisa.
Simba walianza mazoezi katika uwanja huo majira ya saa 12:30 kwa saa za hapa sawa na saa mbili na nusu usiku huko, na mazoezi hayo yalifanyika kwa muda wa masaa mawili na nusu.
Wachezaji wote wa Simba walihudhuria mazoezi hayo ambayo kama kawaida yalikuwa chini ya uangalizi wa benchi la ufundi na yalihudhuriwa na Watanzania waliokuja kuisapoti timu, wananchi wa Setif na askari waliokuwa wakiangalia mazoezi hayo na kulinda usalama.
Kabla ya Simba kufanya mazoezi, uwanja huo ulitumiwa na timu ya Setif kwa mazoezi pia na ilibidi wachezaji wa Simba wasubiri nje ya uwanja kwa takribani dakika 45, kabla ya

 
Back
Top Bottom