...Mie ni mshabiki wa Simba, lakini kipigo hiki ni fundisho kwa uongozi...imezembea kwenye usajili, ingawa bado dirisha halijafungwa.
Simba imeondokewa na wachezaji wake watatu muhimu, lakini ikashindwa kuziba mapengo yao. Alianza kuondoka Samatta, pengo lake halikuonekana kwakuwa Okwi alitimiza wajibu wake kama Straika; halafu akaondoka/akafariki Patrice Mafisango (Kiungo mshambuliaji); huyu pengo lake lipo wazi. Na sasa Okwi ndo huyo anatimka.
Timu ina wachezaji wengi wapya ambao hawakupata kucheza pamoja katika kikosi cha kwanza...then wakaingia katika mashindano makubwa! Hapa kupata kipigo toka kwa Azam iliyotimia, ni haki tupu.
Kwenye ulinzi, wamefanya uzembe, Yondani akasepa...hapa ni mchemsho mwingine wa nguvu.
Rage na viongozi wenzake wakae kitako na kutumia muda huu uliobaki kufanya usajili makini, hasa kwenye maeneo ya ushambuliaji! Hatuna straikas kabisa! Kwa timu tuliyonayo, hadi wachezaji wafahamiane na kucheza kitimu na kiushindani...itachukua muda kidogo!