...Mie ni mshabiki wa Simba, lakini kipigo hiki ni fundisho kwa uongozi...imezembea kwenye usajili, ingawa bado dirisha halijafungwa.

Simba imeondokewa na wachezaji wake watatu muhimu, lakini ikashindwa kuziba mapengo yao. Alianza kuondoka Samatta, pengo lake halikuonekana kwakuwa Okwi alitimiza wajibu wake kama Straika; halafu akaondoka/akafariki Patrice Mafisango (Kiungo mshambuliaji); huyu pengo lake lipo wazi. Na sasa Okwi ndo huyo anatimka.

Timu ina wachezaji wengi wapya ambao hawakupata kucheza pamoja katika kikosi cha kwanza...then wakaingia katika mashindano makubwa! Hapa kupata kipigo toka kwa Azam iliyotimia, ni haki tupu.

Kwenye ulinzi, wamefanya uzembe, Yondani akasepa...hapa ni mchemsho mwingine wa nguvu.

Rage na viongozi wenzake wakae kitako na kutumia muda huu uliobaki kufanya usajili makini, hasa kwenye maeneo ya ushambuliaji! Hatuna straikas kabisa! Kwa timu tuliyonayo, hadi wachezaji wafahamiane na kucheza kitimu na kiushindani...itachukua muda kidogo!
 
[h=3]


SIMBA WAMDHALILISHA MAMA MOJA TAIFA HADI HURUMA[/h]Mashabiki wa Simba, leo wamemtembezea kichapo mama mmoja aliyekuwa amevalia jezi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars yenye nembo ya Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), kosa kukaa kwenye jukwaa walilokuwa wamekaa wao. Sasa haikuweza kufahamika mara moja, mashabiki wa Simba wana bifu na TFF au hawapendi timu ya taifa. Mama huyo alikimbizwa huku akipewa kichapo hadi kutokwa damu, kabla ya kuokolewa na Polisi waliomteremsha jukwaani. Aliporwa vitu vyake kama pochi na kadhalika. Baadaye akiwa amekwishaokolewa na askari, ndipo msamaria mwema mmoja, albino akamuokotea baadhi ya vitu na kuwakabidhi askari. Huwezi kulipa jina lingine tukio lile, zaidi ya udhalilishaji wa kijinsia. Alikuwa anatia huruma mama huyo wakati anahangaika kujitoa kwenye kundi la mashabiki wa kiuma wa Simba, iliyofungwa 3-1 na Azam leo katika Robo Fainali ya Kombe la Kagame.


 
maskini pole yake...........
 
kwa kweli ni aibu jamani, jana nilivaa T shirt nyekundu nilitamani iwe blue, nilikua naona aibu kama nimevaa nguo ya kike lol. lakini bado nitaipenda simba daima
 
simba alikuwa panya jana . kwi kwi kwi kwi kwi kwi..........................................................
 
Shawambia simba ni timu ya wahuni mnabisha azam awapige nyie mnanza mpiga mama wa watu,. Huo ni uhuni
 
Kweli boko mnyama hatari inafika kipindi kaseja anakimbia goli ili boko apite
 


Ona walivyoonyesha vidole vi'3 walifikiri Azam watacheza ki'urafiki-urafiki tena kama kwenye Urafiki Cup wawafunge goli 3 tena hata kama za penalt.
Poleni watani,mkajipange upya Simba bila Okwi na Mafisango inawezekana kabisa,mwambieni hata Kocha wenu siyo kila siku - nanukuu "Its very difficult to fill Okwi's gap" - mwisho wa kumnukuu Prof Milovan
 

Attachments

  • Simba.jpg
    52.6 KB · Views: 388

siyo tu kikosi kilichopangwa ila kikosi kizima cha Simba hakina ubora wowote, ukiangalia usajiri uliofanywa hamna kitu ni bora wangeacha kabisa kufanya usajiri.

Hawa wa-Kongo waliosajiriwa hawajaweza kuzibitisha ubora wao, na akina Danny Mrwanda, Abdalah Juma na Kiggi Makasi nao pia bado wanashangaashangaa, wote walienda Zanzibat kwenye kombe la urafiki tukazani watarudi wameiva kumbe ndo wanazidi kutota: sasa, ili kuwanyoosha inastahili tuwafanyishe mazoezi saa7 mchana na fimbo juu, vinginevyo tufute usajiri mzima wa mwaka huu na ikibidi kwenye ligi tutumie Simba B.

Lkn pia wa benchi la ufundi nao inabidi watueleze ni nini kimefanyika kuiletea Club ya Simba mafanikio; na pia watueleze ni kwanini timu kwenye mashindano ya Kagame Cup walicheza mpira usiokuwa na kiwango.
.
 
Unaweza ukaona kuwa ni mzaha kumbe hili suala simba walilichukulia kama serious kwa kiasi fulani. Baada ya TFF kumuidhinisha Kelvin Yondani kuitumikia Yanga kwenye michuano ya kagame simba wakaibuka sana wakisema TFF wanawaonea sana na kudiriki kusema kwamba wanawapendelea sana Yanga, mimi binafsi nafahamu siasa za mashabiki wa simba na yanga. Kipindi Mwasika anampiga mwamuzi na kufungiwa miezi kadhaa baadhi ya mashabiki wa yanga walithubutu kusema kuwa TFF wanashirikiana na simba na azam ili kuikandamiza yanga, na hili la yondani kuna baadhi wakadai kuwa asilimia 75% ya viongozi wa TFF ni yanga damu. Hivi jamani kwa akili ya kawaida kweli soka letu litafika. Nakumbuka David Dein alikuwa kiongozi wa arsenal na wakati huohuo alikuwa ana cheo FA lakini kwenye vikao hakuwahi kuitetetea arsenal wala kuipiga vit united kinachoangaliwa ni kanuni na taratibu za ligi. Na nyie TFF hivi kweli suala la Yondani mnalichukulia vipi? Au mnataka simba wagomee ligi? Haiwezekani suala la usajili likapelekwa kwenye kamati ya nidhamu na maadili kweli jamani tutafikaaaaa?
 
Bado wapenzi na mashabiki wa Simba wamekosa imani na timu yao wakiamini kutokuwepo kwa wachezaji hawa mahiri waliondoka yaani Yondani, Mafisango na Okwi imekuwa sababu kubwa kwa Simba kuondolewa kwenye michuano hii ya Kagame. Wadau mna maoni gani ni kweli hata kuonyesha kandanda safi tushindwe kwa kizingizio cha kukosekana kwa baadhi ya wachezaji? Maoni yangu Simba imeondolewa mapema kwa kukosa kujituma au kucheza kitimu..Nawapongeza sana Mafunzo kwa kucheza kandanda safi na la kuvutia..Yanga nao wameonyesha nia pamoja na Azam! Sina shaka kombe hili litabaki Tanzania. Mungu ibariki Tanzania! Mungu zibariki Timu zilizosonga!
 
kwa kweli kuna kila sababu bench la ufundi kufumua usajili huu uliofanywa na akina kaburu na watumie baadhi ya wachezaji kutoka simba B.
Hakuna sababu ya kubaki na wachezaji ambao wamepewa kucheza mech zaidi ya 4 lakini hakuna ubora walionyesha.
Tubaki na Sunzu na Okwi kama hatapata timu nje wachezaji wengine wote kutoka nje ya tanzania pigeni chini.
Pia wafanyisheni mazoezi ya nguvu ili wenye kilo nyingi kama salim kinje uzito wao ushuke na uwe wastani wa kilo 55-65
 

alafu pia inatakiwa apatikane mwalimu wa saikolojia wachezaji kama Nyosso,Kiemba, Haruna Shamte ata na Sunzu kuna kitu kinawasumbua vichwani mwao si bure.
 
Nyie hamumjui Rage,baada ya kuchemsha kwenye issue ya usajili wa Yondani anachojaribu kufanya Rage na mwenzake Kaburu ni kuwazuga wanachama na wapenzi wa Simba kuficha uzembe wao ambao kwa kiasi kikubwa umeanza kuwaathiri,kama kweli kina Rage wangekuwa wana uhakika wamemsajili Yondani wasingehangaika na kina Lino Mosombo sijui Masambo,kwanza hata Nyoso mwenyewe wangemuacha si walishaanza kumuonyesha mlango wa kutokea.
 

Maoni yangu ni kuwa mpaka watakapowakilisha rambirambi za Marehemu Mafisango (RIP) ndo Simba itakaa vizuri,hii ni laana ya Mafisango imeanza kuwatafuna na itawatafuna sana,OVER!
 
Kwenye Mpira kuna kitu huwa tunaita Mgongo wa Timu yaani Namba 1,5,6 na 9. Ukiangalia hapo utaona K.Yondan(5),Mafisango(6) na Okwi (9). Na hata Kaseja hayupo ktk hali yake. Mgongo wa Timu usipokuwa ktk hali yake au ukiwa na mapungufu makubwa basi matokeo yanaweza yasiwe mazur ktk timu. Hata Man U msimu uliopita walikuwa wanasumbuliwa na kitu kama hiki. Pongezi Sana John Boko Adebayor kwa kupiga 3 peke yake. Wana wa JANGWANI tujiandae kulipokea kombe tena. YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO
 
kiukweli kwa sasa simba haina straika wa kutumainiwa,kwamba katika mashambulizi 2 au 3 atatupia walau 1,qualities hzo alikuwa nazo okwi na kidoogo the late mafisango(r.i.p),wanatakiwa waache siasa watafute goalgetter wa ukweli ama sivyo gogoro linanukia msimbazi,timu haitii moyo kabisaaaa kiukweli,sunzu shati,ni tegemezi mno hata hatishi kwa mabeki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…