Wamisri wagomea uwanja Dar Send to a friend Saturday, 24 April 2010 00:36 1diggdigg
Doris Maliyaga
WAPINZANI wa Simba kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, Haras El-Hodood ya Misri, wamegoma kufanya mazoezi kwenye viwanja vya nyasi bandia vya Karume walivyopangiwa kufanyia mazoezi jana.
Uongozi wa timu hiyo ulisema mchezo wao hivi sasa umepangwa kuchezwa kwenye uwanja wenye nyasi za kawaida hivyo ni vizuri kwao kutafuta uwanja wa aina hiyo kwa ajili ya mazoezi kuliko kufanya mazoezi kwenye uwanja wenye nyasi bandia.
''Tunahitaji kufanya mazoezi, lakini hatutaki kufanya kwenye kiwanja chenye nyasi bandia, tunahitaji Uwanja wenye nyasi za asili kwa kuwa ndiyo tutakaotumia kwenye mchezo wetu,"alisema kocha msaidizi wa Haras El-Hodood Abuutwalib El Asaw
Kutoka na hali hiyo wachezaji waliamua kufanya mazoezi vyumbani kwao katika hoteli ya Movenpick waliyofikia kwa ajili ya mchezo wao wa kesho.
"Hatuwezi kutumia uwanja wa Karume kwa sababu ya nyasi za bandia kisheria hatukupaswa kuutumia kwa siku ya jana," alisema kocha huyo.
Akiuzungumzia mchezo wao kocha huyo msaidizi Abuutwalib El Asaw alisema Simba ni timu nzuri na anaifahamu kwa zaidi ya miaka minane tangu alipokuwa na klabu ya Ismailia na kusema anategemea utakuwa mchezo nzuri.
Alisema; ''Naijua Simba tangu zamani, tuliwahi kukutana nikiwa naifundisha Ismailia na walitufunga 1-0, tukiwa ugenini na kwetu tulishinda 2-0 ndipo tukafanikiwa kuendelea mbele.
''Lakini tumekuja tumejiandaa vizuri na nina imani tutashinda, tuna timu nzuri na tumefanya maandalizi ya kutosha,''aliongeza El Asaw.
Wakati huo huo, Clara Alphonce anaripoti kuwa msemaji wa klabu ya Simba, Cliford Ndimbo alisema wao wamejipanga vizuri kuhakikisha wanashinda kwa kishindo nyumbani ili kupata urahisi watakapocheza mchezo wa marudiano utakaofanyika wiki mbili zijazo nchini Misri.
Alisema baada ya kumaliza mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu Tanzania bara timu yao iliingia kambini katika hoteli ya Ablaa iliyopo Victoria kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo wakiwa chini ya kocha wao Patrick Phiri.
Simba ni wawakilishi pekee waliobaki katika michuano ya CAF baada ya timu zote tatu za Tanzania kutolewa katika hatua ya awali ya michuano ambazo ni Yanga,Miembeni na Mafunzo.
Viingilio katika mchezo huo ni VIP A 30,000, VIP B 20,000, huku VIP C 10,000 na viti vya rangi ya kijani na machungwa itakuwa ni Shilingi 5,000 na tiketi zitaanza kuuzwa leo.
Hawa kiwewe kimewashika mapemaaaaaa lazima tuwatandike hawa bwaaaaa
kumbe hata kocha wao tushawahi kumtandika bana