Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) | Special thread
Hii so mcehzo vipi wafungaje wa leo ni wa kina nani? Simba imenifanya nirudi ligi ya Bongo na Arsenal imenikimbiza EPL kwa sasa
 
Mpira ni wa TFF, ni jukumu la vilabu kuzungumza na TFF na wala sio na mdhamini. Linapokuja suala la udhamini wa timu hapo ni jukumu la klabu ila kwenye suala la utangazaji ni sualal la chama husika. Hata Supersport inapoonyesha ligi mbali mbali inaingia mkataba na FA yenye ligi then FA inajua namna ya kumalizana na members wake!

Ok! mnyalukolo hapo umeongea vizuri sana, Je unadhani kulikuwa na makubaliano yeyote kati ya TFF na vilabu juu ya kuonyesha mpira moja kwa moja (Live), na kama yalikuwepo kwa nini vilabu kikiwemo Yanga walipo anza kulalamika TFF hawakutoa tamko? Kuonyesha mpira ni biashara na kama utakubaliana nami huwezi kufanya biashara kupitia jasho la mwingine bila mtoa jasho kunufaika, Pia huwezi kuingia makubaliano na mtu mwingine (stranger) bila mtu anayethirika moja kwa moja na makubaliano hayo kujua nini mmekubaliana.
 
TFF wababaishaji kwenye suala hili wanaendesha mambo kiswahili swahili tu. Wapenzi wenzangu wa simba na wangineo tumeshuhudia hata maamuzi wanayotoa yamekuwa ya kiubabaishaje kamati zinatoa hukumu kiubabaisha ndio maana huyu kafungiwa leo kesho kamati ile imemuachia huru. Mfumo wa mawasiliano kati ya TFF na vilabu vinavyotegemea mapato ya uwanjani na wadhamini lazima urekebishwe kwani TFF ilitakiwa iwe wazi toka mapema kuhusu vyombo vya habari kuonyesha huo mpira udhamini wake ukoje na vilabu vitafaidikaje. ITV kama iliwasiliana na TFF kabla ya kupewa kibali cha kuonyesha ilitakiwa kwanza TFF iwasiliane na vilabu husika na nini vitapata. Kama ITV ilikubaliwa na TFF kuonyesha mechi za ligi kuu basi ITV haikuwa na makosa kuonyesha na ndio maana nailaumu TFF moja kwa moja na huyo kiongozi wa simba hakuwa na makosa kwani hakutaarifiwa. Baadhi yetu hapa tunamlaumu kiongozi wa simba kwa sababu Tanzania tumezoea mtindo wa feedback yaani unyeshewe na mvua kwanza ndio ukumbuke mwamvuli. nadhani TFF ilitakiwa kuweka makubaliano kwanza na vilabu simba waliona kuwa hilo lilishalalamikiwa na TFF haijalifanyia kazi sasa kuliko kuendelea kupata hasara wakaona wachukue hatua mapema na nafikiri TFF wamejifunza kwani washapata feedback na mwakani watalifanyia kazi. na Utendaji wao wasipojirekebisha utawafanya wakose wadhamini kwani utakuwa ubabaishaji kama walivyoahirisha pambano la simba na yanga wanajua kuna hasara itakuwa imepatikana kwa wadhamini na watu wengine nikupe mfano kuna rafiki yangu alikuja kunitembelea akasema ataondoka pindi pambano lile litakapoisha ndio arudi kwake mwanza lilipoahirishwa ilibidi alisubiri kwa hiyo muda wake ulipotea na muda ni mali na hasara kwa taifa kwani alishindwa kuzalisha kwenye kipindi alichokuwa analisubiria pambano.

ITV/Redio one nitawalaumu kwakutoichukulia hiyo kama changamoto katika kazi na sijui wataalamu wa sheria wanasemaje hapa maana sisi tuna haki ya kupata habari toka vyombo vya habari kwahiyo watakuwa wanakiuka sheria na ukomavu na hii itawasababishia kukosa udhamini wa kipindi cha michezo.

Fikiria kama chombo cha habari kisema sitatangaza habari za DSM halafu serikali ikae kimya hivi tume ya mawasiliano IPO. na huko ndiko tuendako kuna wakati tutafikia vyombo vya habari vigome kutangaza habari za rais na serikali yake na baadhi ya mikoa. hehehe huo ni mtazamo tu maana ndio tuendako

BTW kwa kuendeleza mimi kama simba sipeleki tangazo langu lolote ITV na Redio one. Sitatumia bidhaa yeyote ya IPP kwa mwezi mmoja ndio nimegoma kwani wao wamegoma kunipa habari mnaonaje wanasimba wote tukagoma kwani wao wamegoma hata kulitolea ufafanuzi mbona star TV walilionyesha kwanini wao TUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU

naomba kuwasilisha
 
Wamisri wagomea uwanja Dar Send to a friend Saturday, 24 April 2010 00:36 1diggdigg


Doris Maliyaga
WAPINZANI wa Simba kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, Haras El-Hodood ya Misri, wamegoma kufanya mazoezi kwenye viwanja vya nyasi bandia vya Karume walivyopangiwa kufanyia mazoezi jana.
Uongozi wa timu hiyo ulisema mchezo wao hivi sasa umepangwa kuchezwa kwenye uwanja wenye nyasi za kawaida hivyo ni vizuri kwao kutafuta uwanja wa aina hiyo kwa ajili ya mazoezi kuliko kufanya mazoezi kwenye uwanja wenye nyasi bandia.
''Tunahitaji kufanya mazoezi, lakini hatutaki kufanya kwenye kiwanja chenye nyasi bandia, tunahitaji Uwanja wenye nyasi za asili kwa kuwa ndiyo tutakaotumia kwenye mchezo wetu,"alisema kocha msaidizi wa Haras El-Hodood Abuutwalib El Asaw
Kutoka na hali hiyo wachezaji waliamua kufanya mazoezi vyumbani kwao katika hoteli ya Movenpick waliyofikia kwa ajili ya mchezo wao wa kesho.
"Hatuwezi kutumia uwanja wa Karume kwa sababu ya nyasi za bandia kisheria hatukupaswa kuutumia kwa siku ya jana," alisema kocha huyo.
Akiuzungumzia mchezo wao kocha huyo msaidizi Abuutwalib El Asaw alisema Simba ni timu nzuri na anaifahamu kwa zaidi ya miaka minane tangu alipokuwa na klabu ya Ismailia na kusema anategemea utakuwa mchezo nzuri.
Alisema; ''Naijua Simba tangu zamani, tuliwahi kukutana nikiwa naifundisha Ismailia na walitufunga 1-0, tukiwa ugenini na kwetu tulishinda 2-0 ndipo tukafanikiwa kuendelea mbele.
''Lakini tumekuja tumejiandaa vizuri na nina imani tutashinda, tuna timu nzuri na tumefanya maandalizi ya kutosha,''aliongeza El Asaw.
Wakati huo huo, Clara Alphonce anaripoti kuwa msemaji wa klabu ya Simba, Cliford Ndimbo alisema wao wamejipanga vizuri kuhakikisha wanashinda kwa kishindo nyumbani ili kupata urahisi watakapocheza mchezo wa marudiano utakaofanyika wiki mbili zijazo nchini Misri.
Alisema baada ya kumaliza mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu Tanzania bara timu yao iliingia kambini katika hoteli ya Ablaa iliyopo Victoria kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo wakiwa chini ya kocha wao Patrick Phiri.
Simba ni wawakilishi pekee waliobaki katika michuano ya CAF baada ya timu zote tatu za Tanzania kutolewa katika hatua ya awali ya michuano ambazo ni Yanga,Miembeni na Mafunzo.
Viingilio katika mchezo huo ni VIP A 30,000, VIP B 20,000, huku VIP C 10,000 na viti vya rangi ya kijani na machungwa itakuwa ni Shilingi 5,000 na tiketi zitaanza kuuzwa leo.
Hawa kiwewe kimewashika mapemaaaaaa lazima tuwatandike hawa bwaaaaa
kumbe hata kocha wao tushawahi kumtandika bana
 
Mashuhuda bila shaka mpo kwenye foleni, msisahau kutimiza wajibu. Asanteni sana
 
The stadium is half empty mechi inaanza saa kumi kamili, wachezaji ndo wanaingia vyumbani kujiandaa baada ya pasha pasha ya hapa na pale, Simba watapiga uzi mwekundu na Wamanga wau wanapiga mweupe, kazi ipo...
 
Mechi bado kuaanza wachezaji ndio wanatoka vyumbani... Waarabu wanaonekana wa kawaida sana hawana miili ya kutisha kama tulivyowazoea
 
Mechi bado kuaanza wachezaji ndio wanatoka vyumbani... Waarabu wanaonekana wa kawaida sana hawana miili ya kutisha kama tulivyowazoea
Mashabiki vipi uwanjani?najua watani watakuja kuwashangilia wamisri kama hawaajaachja utoto wao ule...
 
Back
Top Bottom