Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) | Special thread
Jaman, ni kwel msimbazi tumelowa 5 had sasa! Tusimlaumu mtu, mpira ndo ulvyo tusimlaumu Kaseja
 
kandambili imeingiaingiaje hapo?Acha upuziii wewe nyie mlifikiri mtanunua kama kwa wale wazimbabwe wenye njaa?
au ulifikiri hapo yupo Dihile wa JKT umtumie kaburu kumhonga?
5-1 SAAAAAAAFIIIIIIIIIIIIIII LEO TUTALALA ALIMCHEKA MAPUNDA KUFUNGWA 4 LEO KALA 5
 
Washukuru mungu
leo niliona sita kwenye ulimwengu wa roho
nahisi mmoja wa wachezaji amewapa thawabu kwa kuyapunguza
 
Full time score Haras 5 Simba 1 poleni watani nadhani mmejuwa kiwango chenu kipoje, sasa tusubiri mechi ya Stars na Amavubi
 
[[COLOR="magenta" said:
COLOR="magenta"]Masatu;905820]Umekwisha 5-1 turudi kwenye mipira yetu ya fitna ya akina Wambura nk[/COLOR]
[/COLOR]


Sioni tatizo la Wambura...tatizo ni TFF kuingilia mambo ya Simba. Hiki kipigo ni kwa sababu ya migogoro. Sijui itakuwaje msimu ujao...tunaweza kushuka daraja
 
Full time score Haras 5 Simba 1 poleni watani nadhani mmejuwa kiwango chenu kipoje, sasa tusubiri mechi ya Stars na Amavubi

Bwana una haki ya kufurahi lakini picha yako inatunyima uhuru wa kutembelea thread hii sehemu za heshima. Itakuwa uungwana ukiioondoa (Replace)
 
Poleni watani ndoto zoteeeeeeeeeeeeee zimeishia hapa. Karibuni kwenye vurugu za ligi yetu ya Yanga na Simba. Wababe wa mchangani. Tena, Rudini kwenye vurugu zenu za uchaguzi. Ubaya zaidi lazima mfungiwe na TFF kwa kupeleka kesi mahakamani. Wambura kawaponza. Anapenda madaraka sana yule. Alitoswa TFF sasa anataka alazimishe na kwenu. Haya.
 
Wambura anatumwa na yanga;;;wataanza hivyo uwajui hao
 
Watani jamani kumbe kiwango duniiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Mimi siyo mpenzi wa Simba lakini sikubaliani nawe. Simba kwa standard zetu za huku wako juu - kwa wakati huu naweza kukiri kuwa wanaizidi hata Yanga.
Personally sina tatizo na Simba...it's a great club, great history, great tradition. Hiki kipigo kutoka kwa Mafarao si cha kufurahia hata kama wewe si mpenzi wa Simba kwa sababu kuna suala la uzalendo ndani yake.
Mimi na-support Yanga, lakini am not a natural Yanga supporter (usishangae, wee vp?). Lakini, lack of humility ya wapenzi wa Simba ndiyo ikanifanya nijikute na-support Yanga pengine bila ya hiari yangu (yaani nimekuwa a synthesised Yanga supporter - ironically synthesised by Simba fans!!). So, nitaendelea kuwaomba na kuwakumbusha wapenzi wote wa Simba...punguzeni arrogance. Be humble in whatever little achievement you stumble onto. Vipigo kama hichi cha leo viwe vinawasaidia kuwakumbusha unyenyekevu hata mkipata mafanikio kidogo.
 
aisee ntakukata makofi... ohoooooooooo:target:

Sikujua kuwa we ndo Wambura!!! Kama ndo hivyo elewa kuwa maisha siyo kuongoza klabu mbona katika utafiti wangu inaonyesha kuwa akina mama bado wanashonesha nguo!? Rudi kwenye ufundi cherehani!!!! agggghhrrrrr!
 
Kiko wapi?
sasa mrudi kisha mtulize viuno chini.

5-1 duh, lazima hii itakuwa ni kinyume na maumbile.
 
Hakuna cha arrogance, mpira tunaucheza na kipigo cha jana ni sababu ya mgogoro tu. Sasa we timu itashinda vipi wakati haina hata Kiongozi mmoja. Wote wapo Dar wanawania uongozi!!! Halafu nyie Yanga nendeni kwenye thread yenu...impeparalyze!
 
Mimi kama mwana simba nimekubaliana na matokeo, tujipange kwa Kagame nako kwani tuko kundi gumu sana
 
Back
Top Bottom