Ulimwengu wa Giza, Ulimwengu wa Mwanga.
Mashabiki wa Ua Jekundu wanaishi kwenye Dunia ya hisia,wanayatazama Mambo kichwa chini Miguu juu wapo kwenye Ulimwengu ambao Giza ni Chakula chao pendwa hawajui Vivuli vya ukweli na ukweli wenyewe
Kwasababu maamuzi yao ya msingi kuhusu maisha yanatengemea hisia zilizolala kwenye kesi ya VVIP.Kuwepo Kwao kwenye Hisia na Akili zao kuviringishwa na mgando wa fikra za kinazi kumewafanya wanaamini mnara wa Babeli ulijengwa Kwa fedha za kashata,waamini Nou Camp ilijengewa Kwa mafuta ya Vitumbua.
Pia Kufungwa Kwao minyororo ya Giza la ujinga na kutumia tumbo kutoa maamuzi ya msingi kumewafanya kuamini project ya kujenga Uwanja ni kama kukanda ngano,Waamini Samaki anaweza kupanda juu ya mti Kwa vipande vya shilingi vilivyolala mfukoni mwa waashi.
Nafikiri huu ni wakati wa kuzamisha vichwa vyao kwenye vilindi vya maji,Ni wakati ambao wanapaswa kuangalia Kila jambo kwenye Ulimwengu wa Mwanga,kwenye Ulimwengu ambao kanuni inasema kujenga Uwanja kunahitaji busara kuliko Hisia za Mtoto kunyinwa Maziwa ya VVIP.
Haya yanatokea kwasababu ya uvivu wao kufikiri na kuamua kuwa walevi wa Hisia kuliko mantiki na Ujinga mtamu umetawala pembe zote za Dunia yao iliyojaa Giza.