Hapa hoja siyo "utoto wa Simba" hapa hoja ni MKATABA! Hakuna ziada wala pungufu, hoja ni Mkataba. BM bado ana mkataba na SSC, hivyo wote - BM na SSC - lazima waendane na yalimo lkwenye Mkataba wao. Yeyote atakaye VUNJA huo Mkataba ni lazima AWAJIBIKE. SSC au BM hawawezi kufanya kosa hilo. Hivyo basi, cha kufanya ni kila upande kusubiri hadi mwisho wa Mkataba husika ili waachane vizuri.
SSC haiwezi kumpa BM hiyo barua, kufanya hivyo ni sawa na kuvunja Mkataba na BM na hivyo kuwajibika kumlipa BM mahela. Hili haliwezekani, vivyo kwa BM ambaye analijua sana hilo ndiyo maana anaomba SSC impe hiyo RELEASE LETTER kwa upole ili aende aendako badala ya kwenda huko aendako na kusaini nao Mkataba mpya kabla ya huu alionao SSC haujaisha. Akifanya hivyo, atawajibika kuwalipa SSC mihela kwa kuvunja Mkataba. Hilo BM hawezi kufanya, kwani anajua matokeo yake! Hivyo hapa hoja ni MKATABA! Siyo"utoto wa Simba".