Uzuri ni kwamba Young Africans ni timu na sio mchezaji mmoja. Kwenye mechi ya Young Africans vs Mamelodi hawakuwepo Pacome, Aucho, na Yao lakini kila mmoja kawa shahidi jinsi gani Mamelod walivyokutana na upinzani mkubwa kutoka Young Africans. Hivyo ni rahisi kuziba mapengo ya hao wachezaji kama lilivyozibwa pengo la Lomalisa, nina imani na scout ya Yanga italeta chuma zaidi ya hao hivyo wachukueni tu wala chemistry ya Yanga haitovurugika kama ilivyoshindikana kuvurugika baada ya kuondoka Mayele, Feisal, Djuma Shaban na Bangala na benchi zima la ufundi.