Simba yatangaza mkataba wa TSH Bilioni 26.1 kuanzia leo Agosti 1, 2022

Simba yatangaza mkataba wa TSH Bilioni 26.1 kuanzia leo Agosti 1, 2022

Simba gani inafungwa hovyo hovyo
Unahoja nzuri sana mkuu, ila unapojaribu kuiegemeza kwenye swala la Simba Sc kufungwa inaanza kukosa mashiko.

Swala la team kufungwa ni given, as long as inaendelea kushiriki mashindano mbalimbali kwa miaka na miaka.

Man Cty imetokwa kubugizwa goli za kutosha juzi licha ya kuwa na kikosi chenye gharama EPL nzima, Simba Sc ni kitu gani???
 
Club zishauriwe zisiwe zinaingia mikataba zaidi ya miaka 3. Miaka 5 ni mingi mno, mambo yanaweza kubadilika kwa kiasi kwamba ukiwa na mkataba wa muda mrefu unaweza baki unaugulia maumivu ya mkataba.
Issue sio miaka issue ni masharti ya mikataba inasemaje, unaweza ukawa wa mda mrefu na masharti mazuri, au ukawa wa mda mfupi na masharti magumu.
 
Hongereni Mikia,ila mjiulize timu yenu Ina thamani ya bil 20 toka Kwa Mwamedi? Msipopata majibu maneno ya Rage yataendelea kuishi

"Zile zama za kuwa na mkataba sare sare maua zimepita. Kwa miaka ya hivi karibuni Simba tumewekeza vya kutosha ili kuhakikisha brand yetu inakua,"- Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally.

“Process ya mdhamini mpya tulianza tangu mwaka jana. Tumepokea boss nyingi za kutaka kuwa main sponsor, lakini M-Bet ndio wamekidhi vigezo vyetu vyote,” - CEO wa Simba, Barbara Gonzalez.

"Kwa ukubwa wa Simba ni lazima kujihusisha na kampuni ambayo inaongoza kwenye biashara ambayo wanafanya. Mkiangalia takwimu M-Bet wanaongoza kwa ukubwa Tanzania."- Barbara

"Hii ni mara ya kwanza mdhamini mkubwa anakuwa na senior team pekee, huko nyuma mdhamini mkuu alikuwa kwa timu zote lakini sasa timu zingine tunaweza kuzitafutia mdhamini wake,"- CEO

Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet, Allen Mushi ametaja mchanganuo wa udhamini mpya wa Klabu ya Simba:

Mwaka wa kwanza - Bil 4.670
Mwaka wa pili - Bil 4.925
Mwaka wa tatu - Bil 5.205
Mwaka wa nne - Bil 5.514
Mwaka wa tano - Bil 5.853
Jumla ni Bilioni 26, Milioni 168 na Tsh. 5,000.

=================================

TUJIKUMBUSHE MKATABA WA YANGA
Yanga SC ilisaini mkataba mpya wa Udhamini Mkuu na Kampuni ya kubashiri ya Sportpesa Tanzania, wenye thamani ya Tsh 12.3B kwa miaka mitatu (3), ambayo ni sawa na 4.1B kwa kila mwaka.

Mkataba huo ni ongezeko la Tsh bilioni 2 kwa mwaka kutoka kwenye mkataba awali wa bilioni moja kwa mwaka mmoja.



Pia soma:
Yanga FC yaingia mkataba mpya na SportsPesa wa miaka 3 wenye thamani ya Tsh Bilioni 12
 
Inaonekana watu wanaliwa vibaya sana hizo pesa ni mingi sana.
Hivi hakuna sheria zinazoyabana makampuni ya betting kutoa Audited and Detailed Financial statements kila mwaka?
Ikiwekwa hii sheria tutajua mbivu na mbichi inaonekana Market share ni kubwa sana
 
Huwezi kujua kila kitu ana majukwaa yake ya kujidai,na inapokuja swala la simba na yanga profesa na mzoa taka wote huwa na akili sawa[emoji1][emoji1][emoji1]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mwenye Financial statements za M-bet atuwekee hapa tujadili kwa uhalisia sasa.
Unafikiri TRA wasingeingilia deal ikiwa kungekuwa na ubadhilifu wa hela kwa namna yoyote ile??


Yani ujitaje umeingia mkataba wa mabilioni ilihali umesaini mamillion, kisha utegemee kujiendesha vizuri bila kupigwa pin na hizo mamlaka?

Sio kizembe hivyo mkuu.
 
Mbona unapovuka mkuu kuna ubaya gani Simba ikijenga uwanja wake?
Ujenzi wa uwanja? Kwani mnataka tenda?

Kwa bahati mbaya kwenye jersey hatujaona tangazo la uwanja zaidi ya magofu ya kale

Ikitokea dili la ujenzi wa nyumba tutawastua
 
Tunatisha manina. Tik Tok waje tuwape bega kwa 1b kwa mwaka. Barbara lete matangazo mwili mzima [emoji3059][emoji3059][emoji3059][emoji3059]
Nilisikia watakaa begani na tayari deal lipo jikoni, na bonasi mbalimbali kutokana na perfomance ya team kwenye interclub competitions( CAFCL & CAFCCL)

Ni swala la muda tu.
 
Back
Top Bottom