Simbachawene: Kijana wangu Mshugulikieni hadi awe na adabu kwa mujibu wa Sheria

Nakumbuka those big days of ours ,wakati wa Mwalimu Julius Nyerere ,watoto wake au wadogo zake walikuwa wakitolewa report kuwa wamekutwa sehemu fulani,wanaofanya fujo.Mwalimu pia aliwambia wahusika wawachukulie hatua Kali Sana hao vijana wake au wadogo zake.Kwa hiyo huyo mtoto wa Simba chamwene ,mm nafikiri makosa yake yasimwadhibu mzazi pia.
 
Huyo dogo kasemaje Kwan wengine simu zetu hazifungui hizo video
 
Heshima ni bora kuliko ugali was fedheha
 
Kuna watoto wa mashekh na wachungaji pamoja na kulelewa kwenye misingi ya dini tabia zao ni tofauti.
Si sahihi kumshambulia Simbachawene Kwa kosa alipofanya mwanae
 
Hii movie ingenoga kama angegonga gari ya mahita junior

Hapo vyuma vingeumana
 
Huyu dogo pamoja na ucheck-bob wake na kujiona mwamba baada ya miaka 10 ijayo utashangaa kavaa magwanda ya kijani anaomba kura zenu aingie bungeni na mtamchagua.. Kama yule mtoto wa Rita
 
Kijana tumia pesa ya mzazi kamaipo kula maisha..kunawengine wana pata faida kupitia wewe huko ulipo kula tungi tyar kashaingiza pesa huyo uliemgonga kipasso chake kilichochakaa siajabu akavutakipya..ndoinatakiwa msumbue mzee hela sianazo nyingi chota leta kwa wahuni ukikuta gari imechakaa chakaa gonga ila ulipe ..NB ukiwa na kiburi uwe nahela yakulipia hapo utaendanao sawa
 
Njia pekee yakuwafanya polisi wamshughulikie huyu kijana kwa kuvunja sheria, kudhalilisha jeshi letu, kuonea watu, kuikosea heshima serikali nk, NI KWA SIMBACHAWENE KUJIUZURU AU KUWAJIBISHWA.

AKIWA HAYUKO KAZINI polisi wetu watamshughulikia huyu kijana, kitendo cha yeye kuwepo kazini na eti kutoa maagizo ashughulikiwe ni sinema tu.

IMPACT YA YEYE KUJIUZURU AU KUWAJIBISHWA ITALETA HESHIMA KWA NDUGU NA WATOTO WENGINE WA VIONGOZI SIKU ZA USONI LAKINI PIA ITALETA KUJIAMINI KWENYE UTENDAJI WA KAZI KWA WATENDAJI WA SERIKALI.
 
Umenena mkuu, kuna kitu kiko wrong mahali. Waswahili husema; "embe hudondoka chini ya mti husika"
 
PUBLIC OFFICE...huku tunatambua hilo?.
 
Huyu jamaa naye vip...,yaani unakurupuka unakuja kutuandikia upuuzi namna hii......eti mkapime DNA.
 
Maza atasema "Hilo nalo muende kulifanyia kazi" imeisha hiyo
Ingekuwa enzi za Mzee wa Chato sheria ingechukua mkondo ili Mtu akiulizwa atoe jibu harakaharaka "tumeshamfungulia mashtaka mheshimiwa".
 
Acha porojo. Unaona kila mtu anamjua mtoto wa Simbachawene Kama anavyomjua Rais wa nchi eenhe!? Huyo baba yake mwenyewe sio kuwa anajulikana kiviile. Bila kutamka yeye mwenyewe kuwa Ni mtoto wa Simbachawene, hao ambao gari zao ziligongwa wangefahamu vipi kuwa Ni mtoto wa Simbachawene.!? Au number plate yake imeandikwa "Simbachawene Son"!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…