PostGE2025 Simbachawene: Rais Samia ameagiza mabadiliko Polisi ili kurejesha mahusiano mazuri na wananchi

PostGE2025 Simbachawene: Rais Samia ameagiza mabadiliko Polisi ili kurejesha mahusiano mazuri na wananchi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Wakisha watumia kutekeleza azma yao, wanawatupa.

Wao wanazidi kuneemeka wewe unaenda kulia na familia yako nyumbani.

Kazi za upolisi na uanajeshi, barani Afrika ni kama Toilet paper 🧻.

Mkishatumiwa mnatupwa kule.

Mnakaa kuyapambania mafisadi ambayo yakishawatumia yanawatupa kule.
Jamaa ni kama vile wanadraft kitu kabla na baada ya tukio.Hata Polepole asisemaga kutakuwa na maridhiano baada ya uchaguzi wananchi wakatae.. maana yake walipanga mchoro wote utakuwaje. Hata polisi na jeshi waliambiwa wajiandae kwenye uchaguzi wa Oct29, na tuliona maandalizi yake yaliyopelekea vifo vingi sana. Sahizi anataka kuwatupa nje ya mfumo.Acha tuone hii Cinema!
 
Hili tumelisema miaka 10 iliyopita kwa sasa haliwezekani hadi tuwe na Katiba na sheria mpya. Jeshi la Polisi kimafunzo na kiutendaji ni Paramiritary (Ni nusu Jeshi kamili ) haiwezekani moja kwa moja ikawa huduma, itabidi nusu au 2/3 wahamishiwe JWTZ na wapewe mafunzo mapya ya Kijeshi.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene ameweka wazi maelekezo aliyoagizwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo yanaenda kugusa jeshi la polisi nchini.

Mabadiliko makubwa yakidhamiriwa ili kuboresha utendaji kazi wa jeshi hilo na kuweza kurejesha mahusiano mazuri na wananchi huku akiweka wazi mabadiliko hayo kuwa ni kulibadili jeshi la polisi kutoka matumizi ya nguvu na kuwa jeshi la kutoa huduma na urekebishaji wa sheria katika suala la ukamataji wa watuhumiwa wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali.

Amesema hayo wakati wa mahojiano maalumu na waandishi hivi karibuni ambapo pia ameahidi kuyafanyia kazi maoni ya tume ya kuangalia jinsi ya kuboresha taasisi za haki jinai nchini iliyoongozwa na Mwenyekiti Jaji Mohamed Chande iliyoundwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Januari 2023.

"Hivi ninavyovifanya wako watu wanafikiri ninafanya mimi tu kwa matakwa yangu, hapana ninafanya haya nimeelekezwa na Rais nifanye nini kwamba lazima uhakikishe mahusiano kati ya polisi na wananchi yanakua mazuri, kwamba wananchi wawapende polisi.Leo hii hata polisi akipata shida wananchi wanashangilia nadhani sio sawa maana polisi anatoa huduma kwa wananchi lazima tuboreshe mahusiano" amesema Simbachawene

Ametaja maeneo mawili ambayo ameahidi katika kipindi chake ametumwa kuyafanyia kazi ili kupunguza na kuondoa malalamiko ya wananchi hali inayopelekea wananchi kutotii maelekezo mbalimbali ya serikali.

"Kwanza,mabadiliko ya kimfumo, mabadiliko ya kiutashi kwa mfano mafunzo yetu ya jeshi la polisi lazima tuyaangalie je tunawapa mafunzo ya kwenda kupambana na wananchi au wakawalinde wananchi, wenzetu wale wa tume ya haki jinai, iliyoundwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, wametoa mawazo mazuri sana na rais ameagiza tuyasimamie maoni yao na mimi sasa nitakaa na uongozi wa Juu wa Jeshi la Polisi,tume ya haki jinai wanasema tusiwe na 'Police Force' bali tuwe na 'Police Service' " amesema Simbachawene

"Hatima ya nchi ya Tanzania iko mikononi mwa watanzania, uwe una rafiki yako yuko nje ya Tanzania, uwe unampenda vipi, awe amekusaidia vipi lakini huku Tanzania ndio wako ndugu zako, watoto wako,watanzania wenzako sasa lazima ujue kwamba ipo siku nitahitaji utulivu Tanzania na endapo amani itatoweka tukawa kama nchi za wenzetu,je wewe utakapokua umekaa peke yako moja ya majuto utakayojuta ni kama hukutoa mchango wa kurekebisha hali ikae vizuri na kumbuka katika kurekebisha vizuri sio kutia utambi ili watu waelewe unachosema." amesema Simbachawene.

Chanzo: Nipashe
Hili limeshawashinda labda wabuni mbinu mpya ya kuwaleta polisi kwenye jamii

Humu katikati walianzisha polisi kata kwa lengo la kuwasogeza polisi wawe karibu na raia lakini matokeo yake polisi hao hao wa kata hata ukipata shida wanakuelekeza uende kituo kikubwa.

Wanachotakiwa kuboresha zaidi ni mafunzo ya awali kwa polisi wapya na mafunzo ya mara kwa mara kwa hawa polisi waliopo. Haya mafunzo yaendeshwe na wanasaikolojia na wataalamu wa mambo ya jamii

Mentality ya polisi imekaa kupambana na raia wala sio kumlinda raia. Kitakachowasaidia ni kubadili mentality zao. Wajitambue kuwa kazi nzuri haikutenganishi na jamii badala yake inatakiwa ikuunganishe na jamii
 
Tatizo la polisi ni mfumo wa kisiasa unaowasimamia, utendaji wa polisi hauwezi kubadilika kama mfumo wa siasa na utawala wa nchi hautabadilika.
 
..mahusiano ya Polisi na vyama vya upinzani haswa Chadema yanapaswa kubadilika.
Mahusiano kati ya polisi na raia yakiboreshwa, bila shaka hata mahusiano yake na vyama vya siasa yataboreshwa. Wakiangalia zaidi vyama vya siasa basi hali itakuwa hivi hivi pindi chama kikingine kikitawala.

Amandla...
 
Police force- police service
SISI HAKUNA TUNACHO KIWEZA MASIKINI NA WAPUMBAVU SISI.
Hiki kitu nimekizungumzia sana huku jf, police force tuliyanayo sasa ni ya kikoloni from uendeshaji , mafunzo na mambo mengine

Waziri simba chawene yuko right, police kufumuliwa. Ila amechelewa sana
 
Back
Top Bottom