PostGE2025 Simbachawene: Rais Samia ameagiza mabadiliko Polisi ili kurejesha mahusiano mazuri na wananchi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene ameweka wazi maelekezo aliyoagizwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo yanaenda kugusa jeshi la polisi nchini.

Mabadiliko makubwa yakidhamiriwa ili kuboresha utendaji kazi wa jeshi hilo na kuweza kurejesha mahusiano mazuri na wananchi huku akiweka wazi mabadiliko hayo kuwa ni kulibadili jeshi la polisi kutoka matumizi ya nguvu na kuwa jeshi la kutoa huduma na urekebishaji wa sheria katika suala la ukamataji wa watuhumiwa wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali.

Amesema hayo wakati wa mahojiano maalumu na waandishi hivi karibuni ambapo pia ameahidi kuyafanyia kazi maoni ya tume ya kuangalia jinsi ya kuboresha taasisi za haki jinai nchini iliyoongozwa na Mwenyekiti Jaji Mohamed Chande iliyoundwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Januari 2023.

"Hivi ninavyovifanya wako watu wanafikiri ninafanya mimi tu kwa matakwa yangu, hapana ninafanya haya nimeelekezwa na Rais nifanye nini kwamba lazima uhakikishe mahusiano kati ya polisi na wananchi yanakua mazuri, kwamba wananchi wawapende polisi.Leo hii hata polisi akipata shida wananchi wanashangilia nadhani sio sawa maana polisi anatoa huduma kwa wananchi lazima tuboreshe mahusiano" amesema Simbachawene

Ametaja maeneo mawili ambayo ameahidi katika kipindi chake ametumwa kuyafanyia kazi ili kupunguza na kuondoa malalamiko ya wananchi hali inayopelekea wananchi kutotii maelekezo mbalimbali ya serikali.

"Kwanza,mabadiliko ya kimfumo, mabadiliko ya kiutashi kwa mfano mafunzo yetu ya jeshi la polisi lazima tuyaangalie je tunawapa mafunzo ya kwenda kupambana na wananchi au wakawalinde wananchi, wenzetu wale wa tume ya haki jinai, iliyoundwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, wametoa mawazo mazuri sana na rais ameagiza tuyasimamie maoni yao na mimi sasa nitakaa na uongozi wa Juu wa Jeshi la Polisi,tume ya haki jinai wanasema tusiwe na 'Police Force' bali tuwe na 'Police Service' " amesema Simbachawene

"Hatima ya nchi ya Tanzania iko mikononi mwa watanzania, uwe una rafiki yako yuko nje ya Tanzania, uwe unampenda vipi, awe amekusaidia vipi lakini huku Tanzania ndio wako ndugu zako, watoto wako,watanzania wenzako sasa lazima ujue kwamba ipo siku nitahitaji utulivu Tanzania na endapo amani itatoweka tukawa kama nchi za wenzetu,je wewe utakapokua umekaa peke yako moja ya majuto utakayojuta ni kama hukutoa mchango wa kurekebisha hali ikae vizuri na kumbuka katika kurekebisha vizuri sio kutia utambi ili watu waelewe unachosema." amesema Simbachawene.

Chanzo: Nipashe
Alichaguliwa na nani
 
Nani hata anamsikiliza huyo Simbachawene? Ni hivi hakuna uwezekano wa jeshi la polisi kubadilika kiutendaji wakati ccm inakaa madarakani kwa mabavu. Polisi itakapoanza kufanya kazi kwa weledi, itakuwa ndio mwisho wa ccm. Jeshi la polisi na sasa JWTZ wote wamepuuzwa na wananchi kutokana na kutumika na ccm kulazimisha kubaki madarakani kwa shuruti

Ertugrul Bey HAYA LAND HOV
 
Yaani turejeshe mahusiano na shetani🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Wananchi na sisi tumezidi upole sana. Kama hii story ni ya kweli, mpaka sasa mwili wa ndugu yao hawakaupata, polisi waliyemkabidhi pesa wanamfahamu, aliyewapa namba ya simu wanamfahamu, wanasubiri nini kushughulika nao hata kimtaa mtaa tu?

Tumejengewa nidhamu ya woga sana kiasi kwamba tunachukuliwa kama "mafala" wakati mwingine. Vitu kama hivi ambavyo haviko kisheria inabidi tuanze kuvipeleka hivyo hivyo kama wanavyotaka

Hivi mnafikiri yule jamaa bonge wa mbezi asingepambana na wale wahuni waliotaka kumpakia kwenye gari na kumvisha pingu wakijifanya ni polisi (japo kweli mmoja wao alikuwa polisi na ninamfahamu vizuri sana), leo hii angekuwepo duniani??

Wananchi tuamke tusikubali kupoteza haki zetu kinyonge namna hii? Yaani mwili wamechukua na pesa pia wamechukua halafu ndugu wanamuangalia tu huyo polisi mtaani anadunda.
Hali ilikuwa tete Sana kuanzia tarehe 30 Oktoba - 03 Novemba, 2025 halafu kumbuka wanafamilia pia walikuwa wanatishwa na kuzungushwa Kila siku mpaka wakaamua kuzika nguo zake huku Ndugu Wachache Sana wakihudhuria mazishi hayo.

Tanzania familia masikini hazipewi nafasi ya kupewa Haki zao, halafu Hawa mapolisi wanalindana Sana. Ndugu waliamua kumuachia MUNGU
 
Tatizo la polisi ni mfumo wa kisiasa unaowasimamia, utendaji wa polisi hauwezi kubadilika kama mfumo wa siasa na utawala wa nchi hautabadilika.
Uko sahihi mno, kuna mwingiliano wa moja kwa moja wa utendaji wa polisi na ccm kukaa madarakani, ni lazima ccm itoke madarakani ili mabadiliko ya kweli ya kitaasisi yapatikane.
 
Asiwatwishe mzigo polisi! Wale wanafanya kazi kwa maelekezo yake!
 
Ivi mnahitaji nini mana kila kitu ni nongwa kiwe kizuri au kibaya..... Busara ni kueleza kipi kifanyike nadhani kwa uzingativu wa mada husika.
Ushauri mwingi ulitolewa kuhusu kufanya mabadiliko kabla ya uchafuzi mkatia pamba masikioni. Sasa mmekaa madarakani bila ridhaa ya wananchi mnataka ushirikiano. Ushirikiano gani wakati hamko madarakani kwa ridhaa ya umma?
 
Nani hata anamsikiliza huyo Simbachawene? Ni hivi hakuna uwezekano wa jeshi la polisi kubadilika kiutendaji wakati ccm inakaa madarakani kwa mabavu. Polisi itakapoanza kufanya kazi kwa weledi, itakuwa ndio mwisho wa ccm. Jeshi la polisi na sasa JWTZ wote wamepuuzwa na wananchi kutokana na kutumika na ccm kulazimisha kubaki madarakani kwa shuruti

Ertugrul Bey HAYA LAND HOV

Je unahisi mbinu ya kususa itawasaidia ?
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene ameweka wazi maelekezo aliyoagizwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo yanaenda kugusa jeshi la polisi nchini.

Mabadiliko makubwa yakidhamiriwa ili kuboresha utendaji kazi wa jeshi hilo na kuweza kurejesha mahusiano mazuri na wananchi huku akiweka wazi mabadiliko hayo kuwa ni kulibadili jeshi la polisi kutoka matumizi ya nguvu na kuwa jeshi la kutoa huduma na urekebishaji wa sheria katika suala la ukamataji wa watuhumiwa wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali.

Amesema hayo wakati wa mahojiano maalumu na waandishi hivi karibuni ambapo pia ameahidi kuyafanyia kazi maoni ya tume ya kuangalia jinsi ya kuboresha taasisi za haki jinai nchini iliyoongozwa na Mwenyekiti Jaji Mohamed Chande iliyoundwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Januari 2023.

"Hivi ninavyovifanya wako watu wanafikiri ninafanya mimi tu kwa matakwa yangu, hapana ninafanya haya nimeelekezwa na Rais nifanye nini kwamba lazima uhakikishe mahusiano kati ya polisi na wananchi yanakua mazuri, kwamba wananchi wawapende polisi.Leo hii hata polisi akipata shida wananchi wanashangilia nadhani sio sawa maana polisi anatoa huduma kwa wananchi lazima tuboreshe mahusiano" amesema Simbachawene

Ametaja maeneo mawili ambayo ameahidi katika kipindi chake ametumwa kuyafanyia kazi ili kupunguza na kuondoa malalamiko ya wananchi hali inayopelekea wananchi kutotii maelekezo mbalimbali ya serikali.

"Kwanza,mabadiliko ya kimfumo, mabadiliko ya kiutashi kwa mfano mafunzo yetu ya jeshi la polisi lazima tuyaangalie je tunawapa mafunzo ya kwenda kupambana na wananchi au wakawalinde wananchi, wenzetu wale wa tume ya haki jinai, iliyoundwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, wametoa mawazo mazuri sana na rais ameagiza tuyasimamie maoni yao na mimi sasa nitakaa na uongozi wa Juu wa Jeshi la Polisi,tume ya haki jinai wanasema tusiwe na 'Police Force' bali tuwe na 'Police Service' " amesema Simbachawene

"Hatima ya nchi ya Tanzania iko mikononi mwa watanzania, uwe una rafiki yako yuko nje ya Tanzania, uwe unampenda vipi, awe amekusaidia vipi lakini huku Tanzania ndio wako ndugu zako, watoto wako,watanzania wenzako sasa lazima ujue kwamba ipo siku nitahitaji utulivu Tanzania na endapo amani itatoweka tukawa kama nchi za wenzetu,je wewe utakapokua umekaa peke yako moja ya majuto utakayojuta ni kama hukutoa mchango wa kurekebisha hali ikae vizuri na kumbuka katika kurekebisha vizuri sio kutia utambi ili watu waelewe unachosema." amesema Simbachawene.

Chanzo: Nipashe
Haiwezekani wakati Chura kiziwi akiwepo
 
Tatizo ni Mama sio Polisi🤦🏾‍♂️
 
Source ya hii habari ilitolewa na chombo gani.

Habari kama hizi Bashungwa alipoteuliwa aliongea script kama hii. Hata mwigulu pia enzi za magu aliongea same script.

Nadhani hii habari imeanza kuzungumzwa enzi JK ni raisi na hajawahi kufanyiwa kazi ya kuli transform police force to police service.

Juzi Lema kaongea habari hii aliiongea Mizengo Pinda akiwa waziri mkuu.

Dunia ya leo.sio ya ulaghai.na.maneno matamu ni ya.matokeo.

Simbachawene atende na utendaji utajiongelea wenyewe sio.
 
..kwa hapa tulipofikia Chadema ndio watetezi, na saiti ya wananchi.

..Polisi wakiishi vizuri na Chadema milango mingi zaidi ya HAKI itafunguliwa nchini kwetu.
Tukitegemea chama chochote tutarudi hapa hapa. Polisi wanatakiwa kuishi vizuri na wananchi bila kujali chama, period. Chadema kina wakilisha baadhi ya watanzania sio wote.

Amandla...
 
Safi kabisa...

Simbachawene big brain namkubali sana mwamba
 
Back
Top Bottom