PostGE2025 Simbachawene: Rais Samia ameagiza mabadiliko Polisi ili kurejesha mahusiano mazuri na wananchi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Jamaa ni kama vile wanadraft kitu kabla na baada ya tukio.Hata Polepole asisemaga kutakuwa na maridhiano baada ya uchaguzi wananchi wakatae.. maana yake walipanga mchoro wote utakuwaje. Hata polisi na jeshi waliambiwa wajiandae kwenye uchaguzi wa Oct29, na tuliona maandalizi yake yaliyopelekea vifo vingi sana. Sahizi anataka kuwatupa nje ya mfumo.Acha tuone hii Cinema!
 
Hili tumelisema miaka 10 iliyopita kwa sasa haliwezekani hadi tuwe na Katiba na sheria mpya. Jeshi la Polisi kimafunzo na kiutendaji ni Paramiritary (Ni nusu Jeshi kamili ) haiwezekani moja kwa moja ikawa huduma, itabidi nusu au 2/3 wahamishiwe JWTZ na wapewe mafunzo mapya ya Kijeshi.
 
Hili limeshawashinda labda wabuni mbinu mpya ya kuwaleta polisi kwenye jamii

Humu katikati walianzisha polisi kata kwa lengo la kuwasogeza polisi wawe karibu na raia lakini matokeo yake polisi hao hao wa kata hata ukipata shida wanakuelekeza uende kituo kikubwa.

Wanachotakiwa kuboresha zaidi ni mafunzo ya awali kwa polisi wapya na mafunzo ya mara kwa mara kwa hawa polisi waliopo. Haya mafunzo yaendeshwe na wanasaikolojia na wataalamu wa mambo ya jamii

Mentality ya polisi imekaa kupambana na raia wala sio kumlinda raia. Kitakachowasaidia ni kubadili mentality zao. Wajitambue kuwa kazi nzuri haikutenganishi na jamii badala yake inatakiwa ikuunganishe na jamii
 
Tatizo la polisi ni mfumo wa kisiasa unaowasimamia, utendaji wa polisi hauwezi kubadilika kama mfumo wa siasa na utawala wa nchi hautabadilika.
 
..mahusiano ya Polisi na vyama vya upinzani haswa Chadema yanapaswa kubadilika.
Mahusiano kati ya polisi na raia yakiboreshwa, bila shaka hata mahusiano yake na vyama vya siasa yataboreshwa. Wakiangalia zaidi vyama vya siasa basi hali itakuwa hivi hivi pindi chama kikingine kikitawala.

Amandla...
 
Police force- police service
SISI HAKUNA TUNACHO KIWEZA MASIKINI NA WAPUMBAVU SISI.
Hiki kitu nimekizungumzia sana huku jf, police force tuliyanayo sasa ni ya kikoloni from uendeshaji , mafunzo na mambo mengine

Waziri simba chawene yuko right, police kufumuliwa. Ila amechelewa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…