Simiyu: Baada ya kutenguliwa Ukuu wa Mkoa, Kafulila amshukuru Rais Samia kwa kumpa nafasi ya kulitumikia Taifa

Kafulila amshukuru Rais Samia, awaaga wananchi wa Simiyu​

kafulilapic

  • Siku moja baada ya kuachwa katika mabadiliko ya wakuu wa mikoa, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu, David Kafulila amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kumpa nafasi ya kulitumikia taifa.

Siku moja baada ya kuachwa katika mabadiliko ya wakuu wa mikoa, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu, David Kafulila amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kumpa nafasi ya kulitumikia taifa.

Alhamisi Julai 28, 2022, Rais Samia alifanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa ambapo amewateua wapya tisa, amewabadilisha vituo baadhi yao na wengine wakibaki katika vituo vyao vya kazi.

Katika mabadiliko hayo, wakuu wa mikoa tisa wameachwa na nafasi zao kuchukuliwa na wengine, miongoni mwa walioachwa ni pamoja na Kafulila.

Wengine ni Ally Hapi (Mara), Robert Gabriel (Mwanza), Steven Kagaigai (Kilimanjaro), Charles Mbuge (Kagera), Wilbert Ibuge (Ruvuma), Marco Gaguti (Mtwara), Joseph Mkirikiti (Rukwa), Binilith Mahenge (Singida).

Akizungumza na Mwananchi, Kafulila amemshukuru Rais Samia na kuwaaga wananchi wa Simiyu huku akiwataka wampe ushirikiano mkuu wa mkoa mpya, Dk Yahya Nawanda na kuendeleza walipokuwa wamefikia.

“Kwanza nitoe shukran za kipekee kwa Mhe. Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kuniamini kumsaidia katika nafasi ya Mkuu wa Mkoa. Ni heshima kubwa kwangu ambayo sikuwahi kuipata hapo kabla.

“Pili, ni kuwatakia heri wana Simiyu wote na kuwaomba waendeleze yote tuliyofanikisha pamoja na mengine zaidi ambayo hatukuweza kufanya ambayo watafanya na RC mpya. Binafsi nitaendelea kuitumikia nchi yetu kwa nguvu ile ile kama raia mwema.

“Natoa wito kwa wana Simiyu Kushirikiana RC mpya na zaidi kuendelea kumuunga mkono Rais wetu katika kazi kubwa anayoifanya ya kujenga Mkoa wetu wa Simiyu hasa kwa mapinduzi ya zao la pamba na miradi mingi ya maendeleo inayotekelezwa kila kona ya Mkoa,” amesema Kafulila.

Amewataka wananchi wa Simiyu kuendelea kumuunga mkono Rais Samia katika kufanikisha maono ya kujenga Taifa mpya na kujenga mkoa wa Simiyu hasa katika mapinduzi ya zao la pamba na miradi mingi ya maendeleo inayotekelezwa kila kona ya mkoa.

Rais Samia ateua wakuu wa mikoa wapya, tisa watemwa

“Waendelee kumuunga mkono Rais wetu kufanikisha maono makubwa ya kujenga Taifa moja kubwa kiuchumi na hivyo kisiasa ma kujenga jamii kubwa ambayo kila mmoja anayo fursa ya kushiriki ujenzi bila kujali tofauti hizo,” amesema Kafulila
Naamini atapewa nafasi kubwa zaidi.

Kosa la Kafulila ni kubana mafisadi wengi wa ccm hapo..

Nadhani atarudi tena ila awe mtulivu kama Chalamila..
 
Ila ukichunguza hao waliotemwa walikuwa wanajikomba wazwaz kwa Samia. Yaan walikuwa hawaweza kumaliza sentesi Bila kumtaja Samia tena sifa za kulazimisha
 
“Kwanza nitoe shukran za kipekee kwa Mhe. Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kuniamini kumsaidia katika nafasi ya Mkuu wa Mkoa. Ni heshima kubwa kwangu ambayo sikuwahi kuipata hapo kabla.
LOoooh, alisahau kutoa spichi ya shukrani kwanza alipoteuliwa?

Mbona hii sasa ni kinyume kabisa na yaliyotokea?

Watu wanafiki mara nyingi huwa hawana busara kabisa.

Kwa hiyo hapa anamkebehi rais kwa kumpiga chini?
 
Kafulila amshukuru Rais Samia, awaaga wananchi wa Simiyu​

kafulilapic

  • Siku moja baada ya kuachwa katika mabadiliko ya wakuu wa mikoa, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu, David Kafulila amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kumpa nafasi ya kulitumikia taifa.

Siku moja baada ya kuachwa katika mabadiliko ya wakuu wa mikoa, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu, David Kafulila amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kumpa nafasi ya kulitumikia taifa.

Alhamisi Julai 28, 2022, Rais Samia alifanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa ambapo amewateua wapya tisa, amewabadilisha vituo baadhi yao na wengine wakibaki katika vituo vyao vya kazi.

Katika mabadiliko hayo, wakuu wa mikoa tisa wameachwa na nafasi zao kuchukuliwa na wengine, miongoni mwa walioachwa ni pamoja na Kafulila.

Wengine ni Ally Hapi (Mara), Robert Gabriel (Mwanza), Steven Kagaigai (Kilimanjaro), Charles Mbuge (Kagera), Wilbert Ibuge (Ruvuma), Marco Gaguti (Mtwara), Joseph Mkirikiti (Rukwa), Binilith Mahenge (Singida).

Akizungumza na Mwananchi, Kafulila amemshukuru Rais Samia na kuwaaga wananchi wa Simiyu huku akiwataka wampe ushirikiano mkuu wa mkoa mpya, Dk Yahya Nawanda na kuendeleza walipokuwa wamefikia.

“Kwanza nitoe shukran za kipekee kwa Mhe. Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kuniamini kumsaidia katika nafasi ya Mkuu wa Mkoa. Ni heshima kubwa kwangu ambayo sikuwahi kuipata hapo kabla.

“Pili, ni kuwatakia heri wana Simiyu wote na kuwaomba waendeleze yote tuliyofanikisha pamoja na mengine zaidi ambayo hatukuweza kufanya ambayo watafanya na RC mpya. Binafsi nitaendelea kuitumikia nchi yetu kwa nguvu ile ile kama raia mwema.

“Natoa wito kwa wana Simiyu Kushirikiana RC mpya na zaidi kuendelea kumuunga mkono Rais wetu katika kazi kubwa anayoifanya ya kujenga Mkoa wetu wa Simiyu hasa kwa mapinduzi ya zao la pamba na miradi mingi ya maendeleo inayotekelezwa kila kona ya Mkoa,” amesema Kafulila.

Amewataka wananchi wa Simiyu kuendelea kumuunga mkono Rais Samia katika kufanikisha maono ya kujenga Taifa mpya na kujenga mkoa wa Simiyu hasa katika mapinduzi ya zao la pamba na miradi mingi ya maendeleo inayotekelezwa kila kona ya mkoa.

Rais Samia ateua wakuu wa mikoa wapya, tisa watemwa

“Waendelee kumuunga mkono Rais wetu kufanikisha maono makubwa ya kujenga Taifa moja kubwa kiuchumi na hivyo kisiasa ma kujenga jamii kubwa ambayo kila mmoja anayo fursa ya kushiriki ujenzi bila kujali tofauti hizo,” amesema Kafulila
Akamalize kwanza Mgogoro wa kijinga wa ndoa aliozalisha
 
“Natoa wito kwa wana Simiyu Kushirikiana RC mpya na zaidi kuendelea kumuunga mkono Rais wetu katika kazi kubwa anayoifanya ya kujenga Mkoa wetu wa Simiyu hasa kwa mapinduzi ya zao la pamba na miradi mingi ya maendeleo inayotekelezwa kila kona ya Mkoa,” amesema Kafulila.
Rev. Daniel Mgogo ana ujumbe hapa
 
From ukuu wa mkoa to “ukuu wa kaya” overnight. Haya mavyeo ya kupeana kwa hisani ni shida sana.

Wazee (akina Kinana) wanawaonyesha makali watu kama Ally Hapi. Kuna haja ya kuweka akiba ya maneno na kuepuka kujipendekeza kupitiliza kwa watawala ambao hawaishi milele.
Unanikumbusha bwana Sabaya na kundi lake
 
Mabadiliko haya sehemu fulani yako kimkakati. Ukiangali kwenye jeshi letu Rtd CDF ameondoka na majenerali kadhaa, lazima hawa warudi kuchukua nafsi bila kulazimu kupandisha vyeo zaidi. Ally Hapi huyu wakati wowote Desemba atarudi kwenye Chama. Mkirikiti, Gabriel, Binith Mahenge hawa wanarudi nyumbani completely.
 
Akina Kafulila tuliwategemea sana kuimarisha siasa za upinzani.
Hawa ndio wanaifanya CCM itawale milele.

Siasa kwao ni ajira na sio nia ya kuimarisha demokrasia.
 
Back
Top Bottom