NostradamusEstrademe
JF-Expert Member
- Jul 1, 2017
- 3,402
- 4,532
Huo ni msimamo wako sio wa wote ila kwa kunusuru afya na uhai wako uko sawa.Kama kichwa Cha habari kinavyosema sitokuja kutoa miguu yangu kuingia barabarani kuandamana tanzania hii Ili ufe wengine waishi Jana Kuna jamaa KAPIGWA risasi kafa lamadi raia wanawakimbia polisi ndio ujue Tanzania usijifanye kielele aliyechomwa picha ya raisi mbeya Nate wameshazika Kuna mizee ambayo ilichezea maisha ujanani kwao Sasa hivi inawaambia vijana waandamane hicho kitu hakipo Kila nikiangalia Salio langu bank Hala unakuta mjinga mmoja humu mtandaoni anasema vijana tuingie barabarani kisa yeye ana njaa hua namuangalia nasemahivi kweli anaakili timamu Tanzania ni ya kuandamana
Ngoja nikupe story kidogo
Kwa asili sisi Tanzania sio watu wa vurugu ni wapole sana au inshort ni waoga sana hata viongozi wetu wanajua hili.Kuwa muoga sio dhambi ni asili na tabia ya mtu.
Je ni kwanini Tanzania tuko hivyo
Nature ya jinsi tulivyo dai uhuru wetu hatukumwaga damu kitaifa achilia mbali vita vya babu zetu vya mishale.
Ukilinganisha Kenya na Tanzania unakosea sana historia ya Kenya Uhuru waliupata kwa kumwaga damu mno na MAU MAU walikuwa wanachinja hadi wazungu.Hii hali imewakaa wananchi wake kuwa na roho ngumu hivyo inaridhiwa kizazi na kizazi.Hii pia ni kwa Africa Kusini.
Ona raia wa Uganda na Zambia na wenyewe ni watulivu kidogo kutokana na nature walivyo dai uhuru.