Simon Sirro amefanya kosa gani mpaka akaondolewa u-IGP kabla ya kustaafu kama Venance Mabeyo?

Simon Sirro amefanya kosa gani mpaka akaondolewa u-IGP kabla ya kustaafu kama Venance Mabeyo?

Sakata la mauaji yaliyotokea Mtwara ambapo Askari polisi walimpora na kumuua mfanyabiashara wa madini na kisha kumuua askari mwenzao aliyetoa siri za mauaji, kisha Sirro akatumika kufunika issue nzima kuwalinda askari wake (kuficha aibu ya jeshi la polisi) ndio chambo iliyotumika kumng'oa Sirro, lakini kiuhalisia Sirro alikuwa hatakiwi na Samia tangu Samia anaapishwa kuwa raus. Kwanini? Sirro aliwekwa na Magufuli kwa "kazi maalum", baada ya kifo cha Magufuli ilipaswa ang'olewe pale haraka sana maana angekuwa ni 'security threat' ya utawala wa mama.
Sasa mbona ndo kapewa ubalozi badala ya kuwa demoted hata wamrudishe kuwa ACP
 
Kuna jambo itakua limemnukisha.

Huyu na yule aliyekuwa mungu mdogo wa mjengoni tabia zao zilikuwa sawa,kila wakipata nafasi walikuwa wakimjibu Mother house wanavyotaka hawakujua Mhimili uliojichimbia mizizi mirefu unaweza kufanya yake wakati wowote muda wowote.

Kifupi Mother house alilalamikia utendaji mbovu wa jeshi la Police badala ya Mkuu wake kuangalia wapi pa kurekebisha akarusha vijembe kwamba unaweza kumchikia yeye kama yeye lakini usilichukie jeshi la police.

Mother house 'nikisema najibiwa' nyenyenyenye something like that nikajisemea huyu Mwamba nafasi ya UBALOZI inanukia.
 
Nje ya mada mleta mada. Naomba kuuliza huyu Camilius Wambura ana undugu na Benard Membe kachero mbobezi na mwanadiplomasia mzoefu? Kwasababu majina Yao yanafanana. Pia Membe Jina lake la kati ni Camilius.
Membe kusini, Wambura Kanda ya ziwa Musoma, labda kama ni sibling
 
Katiba mpya itasimamia vema sheria zetu Ili uonevu KWA Raia na teuzi zenye utata za wakuu wa vyombo VYA usalama kutoka mfukoni mwa Rais aliepo madarakani zitasimamiwa Ili wateule kuwatumikia watanzania na Sio matakwa Binafsi ya mteuzi kama ilivyo Sasa!!

Kiasi kwamba hata akiteuliwa yeyote ataongozwa na katiba kutekeleza majukumu yake na sio kufuata maelekezo ya Rais KWA faida yake Mwenyewe Binafsi!!

Ndio maana Wenye hekima humu jamvini tunaimba WIMBO mmoja ambao ni huu hapa:-

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA""!!
 
Nje ya mada mleta mada. Naomba kuuliza huyu Camilius Wambura ana undugu na Benard Membe kachero mbobezi na mwanadiplomasia mzoefu? Kwasababu majina Yao yanafanana. Pia Membe Jina lake la kati ni Camilius.
Hapana mkuu huyo ametoka kanda ya ziwa port wake na Sirro mkoa wa Mara
 
Ubalozi ni cheo kikubwa kuliko IGP lakini kimajukumu IGP ndio mpango mzima.Ubalozi kwa Tanzania ukizingua wanakurusha mbali uache kiherehere.Rejae issue ya Polepole.
Na huo ubalozi baada ya mwaka unaisha maana ubalozi unastaafu ukifikisha 60
 
Ilikuwa imebaki mwaka mmoja tu Simon Sirro atimize miaka 60 na yeye kustaafu kwa heshima.

Ametibua nini? Mpaka akag'olewa ?View attachment 2297927
Ikiwa umepanga chumba kimoja harafu una watoto 2 waliopevuka kidogo ukahitaji falagha watoto utawatuma kwa Mangi wakanunue bigbom harafu wewe nyuma unafanya yako.
 
Kuna watu wapuuzi sana humu JF, Sirro kaongezewa tu muda wa utumishi saafi kwa kazi isiyo na mikiki mikiki.
Anaenda kutulia zake yeye ni vikao vikao na yeye kusign, kunywa chai, kupumzika maisha posh kabisa akitaka anabeba familia 5-10 years hakuna gharama Serikali inamlipia kila kitu akiwa huko.

Kama Samia angetaka kumkomoa si angesubiri mpaka astaafu apewe chake kisha aende kama hamjaskia kawa mkuu wa sungusungu wapi huko mbeleni.

Acheni hizo
 
Watu huwa tunafurahia sana kunapokuwa na mabadiliko. Lakini ninakumbuka inapotimia miezi sita ndipo tena wabongo wanaanza kuonyesha kukereka na aliyepo na kuanza kumfagilia aliyeondolewa. Muda ni Mwalimu
 
Back
Top Bottom