Huzioni ajali zinazotokea kila uchao na hakuna hatua zozote anazochukua!?
Tatizo la Ajali linahusika Vipi na IGP ? Nani mwenye Jukumu la kwanza la kuzuia ajali ni Dereva au IGP? Na pia unasema ajali zimeongezeka , Kwa Takwimu ipi na ukilinganisha na ya mwaka Gani ? Kwa Ratio ipi ukilinganisha na wingi wa magari ya mwaka Gani?. Ulitegemea ajali zibaki Kwa ratio ya miaka ya 80 wakati pikipiki vijjini zilikua za mabwana Shamba tuu. Leo Kuna pikipiki maelfu Huko vijijini na Malaki mijini unategemea IGP atazuia Vipi ajali wakati miundo mbinu ni Ile Ile isiyokidhi.
Magari yaliambiwa yafungwe Speed governor watu wakapiga.Wakaziharibu wenyewe,wanasiasa ambao wengi ndio wanaomiliki magari Mengi wakaja na mambo ya GPS wakawapa Jukumu Hilo Sumatra au Latra wakapiga vita tochi ya Polisi akasema haiaminiki. Leo Kuna watu wanazima mpaka data za Latra ili zisisome mwendo wa magari. Watu wanapiga pesa magari yanakimbia unamlaumu IGP.
Unaonaje magari binafsi yamavyokimbia Huko Tanzania kwenye miundo mbinu isiyokidhi. Watu wanajenga Barabarani . Watu wanauza bidhaa Barabara. Kila sehemu ni speed 50 kwenye HIGHWAY na matuta juu. Unaonaje kama wangejenga Barabara za Juu kweye magari ya watu ili Watu wenye haraka zao wapite zao.
Badala ya Kuibana Serikali ijenge Barabara za Pembeni na kutanua njia ili magari yapite Kwa wepesi watu wanapambana na IGP.
Afrika tumelogwa , Badala ya kufunga Kamera Barabarani watu wanapeana ulaji Kwa kuteuana na kuhamishana vitenge etu watapata mtu wa kuzuia ajali. Labda aendeshe magari yote yeye Mwenyewe kama sijui Malaika au ayaendeshe kama Drone.
Mfano TU miaka ya Nyuma Barabara ya kutoka MOROGORO kuanzia Chalinze palikua na ajali kila siku na mamia ya watu walipoteza maisha.
JPM alijitahidi kujiongeza upana Ile Barabara na kuiwekewa njia nyingi za michepuko ,leo hii pametulia kabisa husikii ajali Moro DSM pamoja na kuwa na magari Mengi kuliko Barabara zote za Highway nchi. M
Unafikiri JPM alikua mjinga kuwa na wazo la kizalendo la kujenga miundo Mbinu.
Jengeni Miundo mbinu , wekeni Kamera, Badilisheni Sheria Magari yafungwe Speed governor badala ya kingamuzi Cha Sasa ni dili za watu Kupiga Hela tuu.
Polisi wakipiga tochi watu wanalalamika ,wakiacha wanalalamika. Gari zikikamatwa watu wanalalamika ,zikiachwa watu wanalalamika.
Mbunge Mstaafu Bwege apewe digree ya heshima kama Musukuma
Vivuko vilivyokua vinazama wanakufa maelfu ilikua ni Siro? Acheni kukosa Shukrani. Siro amefanya mambo makubwa sana kuifanya nchi hii itulie.Wale Magaidi waliopo Msumbuji walikua hapo Tanzania kwenu na walikua wamebakiza kidogo TU kuingia Ikulu kutokea Kibiti. Walikua na mtandano mkubwa ambao huwezi kuamini na walikua na wakubwa wengi nyuma yao na watu walitajirika sana Kwa kujifanya wanataka kuigeuza Afrika kuwa nchi ya Imani hiyo waliokua nao hao Magaidi. Nchi ilifikia pabaya sana. Kagera Ujambazi ulizoeleka na ikawa ni jambo la kawaida kuteka mabasi,kubaka watu na kupora Mali za wasafiri. Ni Simon Nyonkoro Siro aliyewadhibiti majambazi kule Kagera. Watu walikua wanaporea mchana kweupe. Mabenki yalikua yanavunjwa na Polisi kuuawa. Siro alifanya kazi kubwa sana. Alisacrifice maisha yake Kwa ajili ya amani ya nchi . Wezi ,majambazi , wahuni, Magaidi na wadhamini wao ndio wanaomsema vibaya Siro.
Na Amini usiamini Historia ya Siro imetukuka sana.Hata Elimu yake kuanzia kule Seminari alikosoma huwezi kumdhalilisha au kumdharau Kwa namna yoyote.
Nchi hii imeharibiwa na wanasiasa waovu na wasio na dura ambao wamejenga roho ya uhalifu kwenye nchi hii. Uovu umejijenga kwenye mioyo ya Watanzania ndio maana watu waadilifu ,wakweli na wenye misimamo wanapigwa vita.