Simpendi nataka kuachana naye ila sijui namwachaje?

Simpendi nataka kuachana naye ila sijui namwachaje?

A
mwambie mama yako, mwambie muhusika na umwambie mchungaji kwamba hujawahi kumpenda jamaa kabla hujaingia kwenye ndoa, maana jamaa ashajua kwamba humpendi na yeye atakuja kukuonesha kwamba amekujua mda tuu ukiwa tayari katika ndoa, hapo ni wewe ndio utakuwa mtumwa wake...wakati ndio huu wa kufanya maamuzi....ila una tabia mbaya sana.....
Ahsante kwa ushauri but nami ni hofu yangu kubwa atakuja kunilipia cause nimeshamuumiza sana.So huu uhusiano bora niuvunje tu.
 
Rejea uzi uliopita kuwa nilikuwa na wanaume wawili.Utapata jibu but inshort nimemfanyia vituko vingi ili tuachane but haijafanikiwa.
Kwahiyo ulitumikia farasi wawili kwa wakati mmoja?? Miaka mitano umedumu naye ulikuwa unagombea mkuu [emoji847][emoji847][emoji847]
 
Mtu mpaka kaja hapa mjue limemfika kooni kuna uzi niliwahi leta kuwa nina wawili but wote siwapendi wengi mlinishauri nibaki na anayenisaidia but katika kusema kuvumilia kumbe ndo nazidi kuivisha jipu .Kumbukeni kuna wakati mtu akija na shida kuieleza anajua atapata msaada na si kejeli kumbukeni wengi hapa tunatumia fake identity na hatujuani japo wapo baadhi najuana nao ila naamini naweza pata cha kunisaidia.
haya chukua ushauri wangu......siku ya kufunga ndoa kanisani padri akiuliza au shekhe huseme chakubali kuolewa na bwana huyu......au huseme mapema kabla vitu havijaenda mbali...mambo ya mamam haez kunielewa tunaomba husitujibu hvo sababu kama mama hakuelewi na ww ndio unaolewa ndio maana tunakujibu kama ushajua haiwezekani hapa umefuata ushauri gani?sababu ushauri utakaopewa unafanana watakwambia kataa kuolewa.
 
Mimi ni binti wa makamo nipo na mahusiano na mtu kwa miaka mitano sasa ila tangu nimeanza nae kwa kweli sijawahi mpenda.

But nilikuwa najipa moyo kuwa nitajifunza kumpenda lakini naona jitihada zote nilizofanya ili nimpende zimeshindwa kuwork out.

Sasa shida inakuja hivi sasa tupo kwenye process za ndoa lakini ndani ya nafsi yangu naona amani inapotea juu ya hii ndoa yani nazidi kumchukia daily.Nanaona kama nikiiforce hii ndoa kwa kweli nitakuja kuwa msaliti na sitaki kuja kuishi maisha hayo.

Sasa nashindwa naanzia wapi kusema hili jambo maana ni mtu ambaye anapendwa mno na wazazi wangu sasa sijui nitaelewekaje nyumbani na sitaki kupoteza heshima na upendo niliopewa na wazazi wangu na mchungaji wangu tangu utoto wangu kwa ajili ya huyu mtu.

N.B mpaka tunaanza process za ndoa si kwamba niliridhia ila alimtumia mama yangu kama mtego wa kuninasa.
Hivi miaka mitano humpendi na hukutafuta mwingine imebaki mingapi ili ufe wewe hayawani
 
Kabla ya ndoa si mwanaume anapropose? Yaani hiyo ndo ikikua chance yako nzuri ya kumkataa...
Kwasasa vuta tu nguvu na umwambie ukweli kabla mambo hayajaiva kisawasawa!
Wazazi wako na hao wachungaji hawatakua nawe kwenye nyumba yenu... Wafurqhishe ila be wise!!!
 
Kabla ya ndoa si mwanaume anapropose? Yaani hiyo ndo ikikua chance yako nzuri ya kumkataa...
Kwasasa vuta tu nguvu na umwambie ukweli kabla mambo hayajaiva kisawasawa!
Wazazi wako na hao wachungaji hawatakua nawe kwenye nyumba yenu... Wafurqhishe ila be wise!!!
huyu bana hajielewi kabisaa.....we umekaa nae 5 yrears afu unakuja kutulilia hapa...inaonekana njaa ndio ilimueka basi...afu ni kitu kibaya sana hicho
 
Usipige wala kupokea simu, usichati nae na mkikutana mkwepe. Baada ya week tatu atajua haumhitaji. Huyoo ataenda zake kwa wengine. Maana mko wengi sana siku hizi. Ni hivyo tu.
Kama uliyoeleza hapo juu yote ni kweli basi mzani umekuwa hivi
Furaha yako vs Heshima yako (wazazi na mchungaji)
Utakacho chagua,kinginge utakikosa automatic....
And u cant have them both,no middle ground
nb. Wakati ni huu,fanya maamuzi sasa
 
Sina nimpendae.

Kama huna unaye mpenda endelea naye huyo..........vinginevyo ipo siku utakuja mtafuta na itakuwa too late kwako.
Wana semaga ni heri ww upendwe zaidi kuliko ww upende zaidi katika maisha ya ndoa au uhusiano.
 
basi huyu utakuta anapenda asipopendwa daah ni shida
 
afu wewe ni muongo sana, kuna uzi uliutoa hapa kipindi cha nyumba ulisema wewe ni kijana wa kiume

Labda anazo jinsia zote mbili na huwa anazitumia zote kwa pamoja(natania tuu Mkuu)
Wengi huwa wana andika humu JF ili wapate likes
 
Kama huna unaye mpenda endelea naye huyo..........vinginevyo ipo siku utakuja mtafuta na itakuwa too late kwako.
Wana semaga ni heri ww upendwe zaidi kuliko ww upende zaidi katika maisha ya ndoa au uhusiano.
Kweli kabisa! Mimi mtu akinipenda inatosha aisee!
 
Kumpenda humpendi lakini nina hakika hela yake ushaila sana...

Kenge kasoro mkia
 
Yaani wanawake sijui mtaacha umalaya Lini.humpendi ila akikupa hela hukatai
 
mademu ka nyie ndio uwa mnaishia kuwa michepuko ila bora umwambie mapema japo itauma lakini atapata mwingine zaidi yako anayempenda
 
Labda anazo jinsia zote mbili na huwa anazitumia zote kwa pamoja(natania tuu Mkuu)
Wengi huwa wana andika humu JF ili wapate likes
Swala si likes swala ni shida niliyonayo cause hata ukichunguza mi huwa si mtu wa kuchangia sana mada za JF na kuhusu swala la thread ya ile wa kiume nishaelezea sana sidhani kama nahitaji kurudia.
 
Binti wa makamo ,,,Five yrs ,,,,, saizi ndo unawaza utamwachaje ??? Kwann uliamua kupoteza muda kwakua namtu usompenda akakutumia ,,now ni miaka mitano ndo unatafuta pakutokea ???? Nisababu umemzoea nakuzoea pesa zake??? .

Wanawake baan ....pole sana ,Mimi pole nakupa wewe kwasababu nimpotezaji ,,,,naukumbuke thaman ya mwanamke inakwenda na umri ..angalia usije rudi tena humu ,unaomba ushauri namna yakumrudia jamaa !!!.
 
Back
Top Bottom