Simtetei Dr. Nawanda, ila binti anaweza kuwa ni tatizo?

Kusoma tu hii mistar, na kichwa cha mada husika inaondoa hamu ya kuendelea na hiyo mistari mingine huko chini.
Huu ndio uandishi wa kiajabu sana!
 
La haulah! Tuhuma nzito hizo.
 
Pole Sana mwanakwetu. Hii sheria inawaumiza Sana wanaume kwani hata ukisingiziwa na wajanja mashahidi wa mchongo una hatari ya kuangukiwa na mvua thelathini.
Asante sana ...Kuna mmama ni mkuu wa shule anaposoma Binti ndo alisimama na Mimi mwanzo mwisho kwamba sio kweli wananionea ndo ikawa pona pona yangu...yaani yule mama mpaka Leo ni best yangu sana nampenda sana
 
Bandiko la maana kabisa na lenye mrengo wa kisheria hili.
 
Hapa mzee wangu wewe umechemka isee kama nsio mnaandika hivi sababu ya njaa basi tunasafari ndefu sana kama taifa.

Unataka kusema boda boda alionewa wakati unajua kabisa kutembea na mtoto chini ya miaka 18 ni kosa la jinai hata kama mtoto huyo ametaka mwenyewe boda alipaswa kumkwepa.

Kingine mkuu wa mkoa kwanini alikwenda kujianika club na hako katoto ka 21 year na huku akijua kabisa yeye ni mkuu wa mkoa na anafamilia..

Inaweza kana amefanya au pia ametegewa ila inaonyesha tu huyo Nawanda hafai kuwa na hiko cheo maana hana nidhamu..

kuna vyeo ukifika unakuwa mpole na starehe unafanya kwa machale sana sio unajiachia kama umerithi cheo vile.
 
Aisee,

Malipo ni hapa hapa duniani, kama amewafanyia hila litamkuta jambo huyo hatokaa aamini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…