Simu gani ninunue kwa bajeti ya laki nne?

Simu gani ninunue kwa bajeti ya laki nne?

Loh! Ni kweli hiyo helioG99 ni superior kwa spaSD 680 . Lakini kuna dhana tu ...mfano mimi processor ikiwa mediatek hata iwe nzuri vipi sitaichukua
Hiyo dhana ni sahihi kama tunalinganisha simu zinazofanana kila kitu mfano S21 Ultra ya Exyonos dhidi ya S21 Ultra ya Qualcomm Snapdragon.
Na penyewe tunaangalia processor speed, clock, GHz, power consumption, processing power na vitu kama hivyo.

Au kulinganisha flaships za mwaka uleule kwa processor ni sawa. Sasa unalinganisha simu za laki tatu tatu unaitaja SD wakati iliyotumika humo ni low end. Yani mtu ajenge Moshi mitaa ya Soweto kiwanja milioni 40 na umtishe kisa kuna aliyejenga Dar kwa mfuga mbwa kiwanja milioni 2 na pembeni yake kuna danguro. Ukikariri brand utasema aliyejenga Dar anaishi pazuri. Kinacholinganishwa ni specific models na editions zake, sio brands.
 
Hii imenichekessha sana. Mfano unanihusu
 
Habari,

Nahitaji ushauri wa simu ya bajeti ya laki 4. Nahitaji kununua simu mbili zawadi kwa watu wawili muhimu, bajeti kila moja isizidi laki nne.

Thanks in advance
Xiaomi redmi note 12 Tigoshop 430,000 kama unataka ku stretch budget kidogo, probably simu nzuri zaidi Mpya kwa hio budget.

Kwa budget kidogo chini ya Hapo Samsung A15 sio mbaya around 300,000-350,000
 
Kiswaswadu smartmbupu
Cc : ephen_
Nimenunua na kiswaswadu. Yani nanunua simu kama zawadi na kiswaswadu kama tochi😬
Screenshot_20240816_164017_Gallery.jpg
 
Nunua mpya Samsung A15 4G 4/128 bei yake 350,000 unapata. Faida zake:

1. Battery kubwa ya 5000 mAh muhimu kwa watu wazima na wa vijijini.
2. Samsung ina software updates nyingi hivyo haiwezi lag na kuwa outdated mapema kama hizo Infinix na Tecno.
3. Samsung ina stable software, camera inayodumu quality na reliability ya parts kama mic, speaker, etc.
4. Kioo kikubwa, three camera lenses kwa ajili ya "washamba" wa kijijini ambao huamini lenzi tatu "macho matatu" ni simu nzuri zaidi. Ukitoa zawadi zingatia mapokeo ya mpokeaji sio mtazamo wako.
5. Vifaa vya A series ni bei nafuu kuliko vya Note, Z na S series. Hasa screen bei inavumilika.

Ninahisi ni simu za wazazi. Usisahau kununua Samsung adapters za type C to C maana A series haziji na chaja, price about @13k. Pia nunua cover around @7k , protector ni @3k.
Ni type A to type C, cable ya type c to c zinatumika kwa simu zenye uwezo wa reverse charging, au chaja zenye c type outlets. Ambazo si nyingi.
 
Ni type A to type C, cable ya type c to c zinatumika kwa simu zenye uwezo wa reverse charging, au chaja zenye c type outlets. Ambazo si nyingi.
Samsung A05s na A15 nilizotaja humu zinakuja na USB C to C cable kwenye package. Unatakiwa kununua adapter ya outlet ya C ndio uweze kutumia cable inayokuja na simu.

Kama hutaki C to C adapter unanunua chaja complete ya USB A to C na unatupa hiyo cable unayonunulia na simu. Pia C to C inaweza tumika kwa simu yeyote ile yenye C port haijalishi ina reverse charging au haina.
 
Moja ya simu ninayoikubali ni Samsung s10, ikiwa na uwezo wake wa kipekee wa kusearch hadi herufi mpaka kwenye picha ndani ya simu hadi kwenye message kitu ambacho sijakiona kwenye simu yoyote ile,
 
Back
Top Bottom