SIMULIZI: Asali haitiwi kidole

SIMULIZI: Asali haitiwi kidole

Kwanza huyu siwema atakuwa sio mtoto wa mzee makame
Roho gani mbaya namna hiyo?
Naye radhia Mpole sana yaani alitakiwa awalaze polisi hao ndugu zake .

Halafu bwana iddi naona wazi anaenda kupigwa na kitu kizito sana kutoka kwa Ashura mayutiai😀

Abou Shaymaa mkuu twendeeeee
 
upole wa radhia unanikera sana,uwiiii sema ni hadithi tu
Huo sio upole ni ujinga sasa yaani alitakiwa aite maafande wakawalaze ndani hao ndugu zake week 2 halafu siwema akitoka akutane na barua ya contract termination

Hayo yakina zuhura naona yataenda kumuaibisha mzee wao tusije sikia yamepelekewa moto yakarekodiwa
 
Hadithi ina reflect maisha halisi ya kitanzania chuki wivu vinyongo umbea maneno maneno eeehh !!
 
Huo sio upole ni ujinga sasa yaani alitakiwa aite maafande wakawalaze ndani hao ndugu zake week 2 halafu siwema akitoka akutane na barua ya contract termination

Hayo yakina zuhura naona yataenda kumuaibisha mzee wao tusije sikia yamepelekewa moto yakarekodiwa
mimi hata nisingewalaza ndani,namalizana nao hapo hapo nyumban
 
Vile naingia sasa baada ya kutoka kazini
1733680339164.jpg
 
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA TISINI NA TANO
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA TISINI NA NNE: Lakini pia taarifa ilieleza kuwa, mwalimu Makame ata apishwa kesho, kwenye ukumbi wa ikulu, “naomba isiwe hivyo, mbona Radhia atazidi kulinga” alijisemea Idd, ambae licha ya tamaa aliyonayo juu ya Radhia, lakini ameshindwa kumiliki mke mwingine, ambae leo amempatia taraka. ......... ENDELEA….
Taarifa hii ilipokelewa kwa furaha na familia ya bwana Makame, siyo tu pale nyumbani kwao, au kule kwa Edgar, pia sehemu nyingi sana, kwa ndugu jamaa na marafiki, toka kila kona ya kisiwa iki cha unguja, pia pemba na sehemu nyingine zote ambazo walisikia na kumfahamu mzee Makame.
“kesho tutakuwa wote kwenye kiapo cha baba yako pale ikulu” alisema Edgar, ambae bado alikuwa amejilaza kwenye kochi, huku Radhia akiwa melala kifuani kwake, “kwani wanaluhusu familia nzima kwenda kuona?” aliuliza Radhia, huku anageuza uso wake kumtazama Edgar usoni.
“yah!, naluhusiwa, lakini kwa watoto wadogo, pia na wale wakina mama” alisema Edgar, “sasa mimi nitaendaje?” anauliza Radhia, kwa sauti ya mshangao, “kwani kwenye afla ikulu, ulienda kama nani?” aliuliza Edgar, huku nae anamtazama Radhia, “nilienda kama mwanafamilia wako?” alijibu Radhia, huku anaachia tabasamu, maana alikumbuka mbali sana.
“basi na kesho utaenda kama mwanafamilia wangu, na muda wote utakuwa na mimi” alisema Edgar na kumshtua Radhia, “mh!, kwahiyo baba anione kabisa kuwa nipo na wewe?” aliuliza Radhia huku anacheka kwa aibu.
Mwanzo aikuwa rahisi, lakini ukweli mpaka mida ya saa mbili za usiku, siku iliyofuata, kwa walio bahatika kuiona taarifa ya habari, akiwepo Idd, waliweza kumwona Radhia, ambae kwakifupi kila alie iona taarifa ile, alijikubaria kimoyo moyo kuwa leo amemwona mschana mzuri, na ukizingatia kuwa taarifa hii, ililushwa na vituo vingi vya television, vya bara na visiwani.
Aikuwa nzuri kwa Idd, ambae alijikuta anazidi kuumia mala dufu, akuwa peke yake, Siwema nae alikuwa hivyo hivyo, wakati baadhi ya watu wanaendelea kufurahia mafanikio ya mwalimu Makame, yeye alikuwa anaumia kwa kumwona Radhia katika tukio lile.
Kibaya zaidi ni kwamba, haikuwa mwisho wa maumivu, kwa Idd na Siwema, ambao hawakuacha kumwombea mabaya Radhia, kwamba ifikie wakati aachike kwa kukosa ujauzito.
Kwa upande wa Mariam na Zahara, wao ilikuwa tofauti kidogo, maana siku tatu baadae familia ya mzee Makame iliamia kwenye nyumba kubwa ya serikali, na huku Radhia licha ya kuwa na chumba chake katika jumba ilo la kisasa, lakinipia nikama alikuwa ameshaamia nyumbani kwa Edgar.
Siwema kwa kuona uhuru wa kujipatia mwanaume na pengine kulewa pombe, akaomba fedha kwa mdogo wake Radhia, na kwenda kupanga chumba, maeneo ya michenzani, kule anakoishi Idd.
Mariam na Zuhura licha ya kuishi kwenye jumba la kifahari, na kupata huduma muhimu, na heshima mtaani, lakini bado waliona kuwa hawakuwa na uwezo kumfikia Radhia, kwa fedha na ufahari walio nao.
Awakuweza kumwona baba yao fedha mala kwa mala, maana baba yao alikuwa anaanza ujenzi wa nyumba yao, kule kule jang’ombe kwa soud, hivyo awakuwa na budi kurejea kwa Radhia na kumwomba msaada wa fedha ndogo ndogo za kuwa saidia.
Ilikuwa lahisi kwao, sababu awakuwa na mtu wa kuwaunga mkono, kwenye ujinga wao wa chuki zisizo na sababu, maana dada yao Siwema tayari alisha ondoka pale nyumbani, kwa msaada wa Radhia, mama yao mzazi, sasa alisha hacha kumsimganga Radhia, nikutokana na kusababisha mzee Makame, kupata nafasi nzuri serikalini, chanzo kikiwa ni Radhia, na pia Siwema kurudishwa kazini, sababu ikiwa ni Radhia.
Tayari Mariam na Zuhura, walisha waacha na kuwasahau wakina Mahadhi, kwakuona siyo hadhi yao tena, maana wao walikuwa wanaitaji fedha ya urojo tu toka kwao, sababu kuhusu dudu, awakuwai kuwalizisha ata mala moja, ni kwamba licha ya kupoteza bikira zao kwa tamaa ndogo ndogo, lakini awakuwai kufurahia dudu.********
Week inakatika Radhia akiwa nyumbani kwa Edgar, wanaishi kama mke na mume, sasa Radhia alianza kuwasiliana na kupeana salamu na wanafamilia wa Edgar, kwamaana ya baba na mama Edgar, kaka yake Edgar yani Deus Nyati na mke wake, pia wifi yake Dorin yani dada wa Edgar.
Kikubwa ni kwamba, sasa Radhia alikuwa amesha wapokea wageni toka #Mbogo_Land, ambao ni timu ya mpira wakikapu iliyokuwa na watu kumi na tano, yani wachezaji kumi na mbili, na walimu wawili na Doctor mmoja.
Ziara ilikuwa nzuri, ikisimamiwa na ofisi ya barizi Edgar, chini ya usimamizi wa Radhia, akisaidiwa na Monica, huku Edgar akiudhuria kila mechi, ambayo ilicheza na wanamichezo hao toka #Mbogo_Land, ikiwepo mechi yao na timu ya wakina Mukhsin.
Mala baada ya kumaliza michezo yao, wanamichezo wale toka shule ya sekondari ya King Eugen wa pili, walitembelea vivutio mbali mbali vya utarii, huku wakipiga picha na kuweka kwenye tovuti ya shule, na shirikisho la mpira wakikapu nchini #Mbogo_Land, yani MBA.
Picha na video za vivutio vya kitarii, zilkisambaa eneo kubwa duniani na kujizolea umaarufu, na kutazamwa na watu maarufu duniani, wakiwepo wanamichezo, wanasiasa, wacheza filam, wanamusic na watu mashuhuri wa mitandaoni.
Sifa kubwa zilienda kwa Radhia, kwa maandalizi mazuri, na ubinifu alio ufanya, uliosababisha kuiletea sifa nchi yake, ata siku nne baada ya wanamichezo kuondoka nchini, alifanya maojiano na waandishi wa habari, huku watu wengi wakishuhudia kwenye TV na mitandaoni, pamoja na kwenye maredio.
“imekuwa ghafla sana bi Radhia, hapo mwanzo hukuwai kuonekana wala kufanya kitu kama iki, ebu tueleze wazo ili ulilipata wapi, na umewezaje kufanikiwa” alisema mmoja kati ya waandishi wa habari.
Idd akiwa kwenye TV yake, anamwona Radhia mbele ya waandishi wengi wa habari, akiwa amependeza na kuwa mtamu kweli kweli, hakuka anajikuta anaumia roho, huku Siwema aliekuwa amekaa sebuleni kwake anakunywa bia zake ambazo alikosa kwa muda mrefu, nae pia anatazama kwenye TV, kama ilivyokuwa nyumbani kwao.
“kwanza kabisa nimshukuru mwenyezi mungu, maana yeye ndie mwenye kupanga kila jambo kwa mja wake, pili niwashukuru wazazi wangu kwa kunipatia nafasi” hivyo ndivyo alivyoanza Radhia, ambae kila alietazama habari hii, alivutiwa na mambo matatu, moja sura nzuri ya mwanamke huyu, pili sauti yake tamu, tatu ni umaarufu wake wa ghafla.
Radhia anatabasamu kidogo, nikama anaona aibu, “tatu nimshukuru barozi Edgar, kwa kuniamini na kunipatia nafasi ya kuonyesha ninacho kiweza, huku akinishika mkono kwa kila hatua, mpaka nimefanikiwa kufikia malengo, tumejenga urafiki kati ya wanamichezo wetu, tumetoa njia kwa wanamichezo wetu, kufikia mafanikio katika mchezo wampira wakikapu, pia tumeitangaza nchi yetu katika utarii” alieleza Radhia.
Maswali ya waandishi ayakuishia hapo, “tunafahamu wewe ni mwenyeji wa zanzibar, na hupo karibu sana na barozi Edgar, je una uhusiano gani na barozi Edgar?” aliuliza mmoja kati ya waandishi wa habari. ......... ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPA HAPA jamii forums
 
Kitu kinazidi kunogaaaaa shushaaaaaa kaka
 
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA TISINI NA SITA
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA TISINI NA TANO: Maswali ya waandishi ayakuishia hapo, “tunafahamu wewe ni mwenyeji wa zanzibar, na hupo karibu sana na barozi Edgar, je una uhusiano gani na barozi Edgar?” aliuliza mmoja kati ya waandishi wa habari. ......... ENDELEA…. KUFWATILIA

Hapo Radhia anaonekana anaachia tabasamu pana, lenye uzani wa aibu, Idd anasubiri jibu lakini hatamani kulisikia, Siwema anatamani Radhia apatwe na ububu wa ghafla ashindwa kujibu swali ilo, “sidhani kama hii ni sehemu sahii ya kulijibu ilo, ila kwa kifupi ni mume wangu na ninaishi nae” alljibu Radhia, huku akiendelea kucheka kwa aibu.

Hakika jibu ili lilimuumiza sana Idd, ni kama lilivyo muumiza Siwema, lakini hawakuwa na lakufanya, zaidi waliombea siku zifike na Radhia aachike kwa kushindwa kushika ujauzito.********

Naaaaam!, ilikatika week ya tatu, toka mzee Makame aanze kutumika majukumu mpya aliyo pewa na rais, ni week ya pili toka familia ya bwana Makame iamia kwenye nyumba mpya ya serikali, ikiwa ni week ya tatu toka Idd alipo achana na mke wake Shani, na pia ni week ya tatu, toka Ashura yani mke mkubw wa Idd alipo ondoka nyumbani, akiaga anaenda nyumbani kwa wadada yake.

Hii pia ni waki ya tano, toka Radhia alipo ampatia Edgar kitumbua, na kufurahia dudu kwa mala ya kwanza, na niweek ya tatu toka alipoanza kuishi nyumbani kwa barozi Edgar.

Ukweli ni kwamba, kila mmoja alihisi kuwa upendo umesha rudi nyumbani kwa mzee Makame, maana Mariam na Zuhura sasa waliongozana na Zahara sehemu zote nzuri walizo tembelea, na safari hizo zilifadhiriwa na Radhia, ambae alikuwa patiwa kila kitu pamoja na fedha za matumizi kama mke wa barozi, ikiwemo heshima kila anapopita mitaani au kwenda kwenye ofisi za serikali, na huduma za kijamii.

Mama Mariam na mama Radhia, walikuwa wanakaa na kuongea kwa pamoja, wakifurahia maisha pamoja na mume wao, hakuna alie msema mtoto wa mwenzie, wala kukosoa jambo lolote zuri.

Hakika hakuna ata mmoja alie fikilia kuwa, Siwema bado alikuwa na kinyongo moyoni mwake, sijuwi alikuwa anawaza nini, lakini kuna wakati alikuwa anajisemea mwenyewe, “sijuwi yule mwanaume amefwata nini kwa Radhia au ule uarabu koko wake” alijisemea Siwema, ambae aliona kama vile Radhia akustahili kuwa na Edgar, “wanaume wengine ata awaangalii wanawake wakuwachagua” hayo maneno yalikuwa nayamchomoka Siwema mala kwa mala.*******

Siku hizo ndizo siku ambazo, yalitokea matukio mawili makubwa, moja likiwa ni tukio la kustaajabisha kama siyo kusisimua na kuleta furaha kwa watu wengi, asa wanafamilia wa mzee Makame, ambae aliona kuwa mwaka huu ni mwaka wake, na ujio wa kijana Edgar umemletea Baraka nyumbani kwake.

Huku tukio la pili likiwa ni tukio zuri la kufurahisha, kwa Ashura na Shaban, huku matukio yote mawili, yakiwa ni matukio magumu na machungu kwa Idd, ambae akuamini kama ni kweli anacho kiona na kukisikia, au yupo katika ndoto.

Ilikuwa hivi, mapema siku ya ijumaa, Siwema alikuwa anaingia kazini asubuhi, ile anafika kazini tu, akaambiwa kuwa anatakiwa kumpeleka mgonjwa hospital ya mnazi mmoja, kwamaaana mgonjwa alikuwa na hali mbaya, hivyo alitakiwa kuamishwa hospital, na kupelekwa mnzani mmoja kwa gari maalumu la wagongwa, yeye akiwa muuguzi atae msindikiza mgonjwa huyo.

Wakati huo huo, toka jana usiku Radhia alikuwa anajihisi dalili tofauti za mwili, kutapika mala kwa mala kwa mala, pia kukosa hamu ya kula baadhi ya vyakula, japo kiukweli hamu ya dudu iliongezeka, mala dufu, na ikiwa ni mala ya kwanza kuomba dudu kwa mdomo wake mwenyewe.

Ilikuwa hivyo baada ya Edgar, kuto kuonyesha dalili ya kula kitumbua, kutokana na hali ya mpenzi wake huyo, alie onyesha dalili za wazi kuwa alikuwa anaumwa, ndipo Radhia akupo jikuta anatamka wazi wazi, “kwani leo unifanyi, mwenzio nimesha zowea kila siku” Edgar akuwa na la kufanya, zaidi ya kuhakikisha anakula kitumbua kwa mtindo wa taratibu, mtindo wa kubembeleza.

Hapakuwa na wakati wakusimama wala kuinama, leo walimaliza mitondo yote wakiwa wamelala, kuanzia kifocha mende, kiubavu ubavu, wakitazama upande mmojo, au wametazamana, moja tu Radhia aljikuta amepanda juu ya Edgar, napo tendo lilikuwa la taratibu, huku Radhia akiomba siulumiwe, “usnilulimie mume wangu ni tamu sana, nifanye unavyoweza” yalimtoka Radhia.

Japo ilikuwa ni kwaajili ya kuhisi mpenzi wake ni mgonjwa, lakini ukweli ni kwamba, mtindo ule wataratibu, ulimfanya Radhia ajihisi leo amekutana na kitu kipya kabisa, tena kitamu kuliko jana na juzi, ata walipomaliza walilala hoi.

Siku ya pili barozi alihamkia hospital, yeye mwenywe ndie alie msindikiza Radhia hospital, maana ukweli hii homa ya mke wake, ilimshangaza sana, ndio maana alipofika hospital, na kumpeleka mke wake kwenye upande wa VIP, aliagiza kuwa Radhia, afanyiwe vipimo vingi na kwa umakini mkubwa.

Kati ya wauguzi waliompokea Radhia, ni Amina, ambae alikuwa chini ya Doctor bingwa wa magonjwa ya ndani, ambae ni mwanamke, ambae alianza kazi mala moja, akisadiana na wauguzi wawili, akiwepo Amina, na mwenzio mmoja, Radhia alitolewa damu na achukuliwa mkojo, na vipimo vikaanza.

Wakati huo ndio wakati ambao, Idd alikuwa anaingia dukani kwake, ndipo alipoiona simu yake inaita, na alipoitazama akaona jina ni mama Abdi, huyo ni dada wa mke wake mkubwa, yani Ashura.

Ukweli hapo ndipo kengere ya tahadhari, ilipo gonga kichwani kwa Idd ambae sasa anakumbuka kuwa week ya tatu sasa hakuwa amemjulia hali mke wake, ambae ni mjamzito, tena anae karibia kujifungua, nae akaipokea simu haraka na kuiweka sikioni.

Kwanza anakutana na kelele za honi za magari, sambamba na sauti za watu, ikionyesha wazi kuwa shemeji yake huyo alikuwa katikati ya mji, na siyo nyingine ni darajani, “asalam ayekum shemeji” alisalimia Idd kwa sauti yenye tahadhari, “aleykum salama shemeji, mkeo yupo hospital mnazi mmoja, ameshikwa na uchungu toka jana usiku” alisikika mama Abdi ambae alionekana mwenye haraka nyingi, sawa na mimi nakuja sasa hivi” alisema Idd ambae aliacha kufungua duka na kuelekea hospital kwakutumia usafiri wa baiskeri.

Idd akiwa njiani anajionea ufahari mkubwa, kuwa na watoto watatu, kwa mke wake mkubwa, huku akiwazodoa wakina Radhia na Shani kwa kushindwa kushika ujauzito, “wapuuzi sana, yani wanashindwa kushika mimba, alafu wanaongea ujinga ujinga tu, tuone sasa wapeleke ugumba wao kwa wanaume wajinga wajinga” alijisemea Idd huku anaparaza pederi za baiskeri.*********

Tukitangulia kule hospital kwenye ward ya wazazi gred A, ward ambayo chumba kimoja ulazwa wazazi wawili, mpaka wanne, tuna mwona Ashura akiwa amelala kitandani, na mtoto mchanga pembeni yake, wamejifunika mashuka ya hosital, juu ya kitanda kizuri, kachumba hiki cha ward zenye gharama kubwa.

Pembeni yake amesimama kijana Shaban, aliekuwa anamtazama mtoto kwa umakini na huku uso wake ukiwa wenye tabasamu pana la furaha, “watoto watatu Ashura, nivyema tukiwalea kwa pamoja” alisema Shaban kwa sauti ya chini, yenye furaha Ashura anatabasamu kwa furaha, “hakuna namna inabidi tuishi pamoja” alisema Ashura, akionyesha furaha isiyo kifani. ......... ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPA HAPA jamii forums
 
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA TISINI SABA
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA TISINI NA SITA: Pembeni yake amesimama kijana Shaban, aliekuwa anamtazama mtoto kwa umakini na huku uso wake ukiwa wenye tabasamu pana la furaha, “watoto watatu Ashura, nivyema tukiwalea kwa pamoja” alisema Shaban kwa sauti ya chini, yenye furaha Ashura anatabasamu kwa furaha, “hakuna namna inabidi tuishi pamoja” alisema Ashura, akionyesha furaha isiyo kifani. ......... ENDELEA….

Mala mlango unafunguliwa, anaingia mama Abdi au Aziza, yani dada yake Ashura, akiwa na kapu lenye hot port, “tunakusumbua sana shemeji, vipi umesha mjulisha Idd?” anauliza Shaban, huku anapokea hot port na kuanza kuandaa urojo kwaajili ya Ashura wake.

“nimesha mwambia nazani sasa yupo njiani, ungefanya utoke asije kuleta rabsha hapa hospital, siunamjuwa kwa wivu” alisema mama Abdi, na wakati huo mlango unafunguliwa na anaingia nurse akiwa na file mkononi.

“lisiti yenu hii hapa, hongera sana, mke atapata matibu kuanzia sasa mpaka kesho kutwa atakapo luhusiwa, zaidi ya hapo utatakiwa kulipia malipo mengine yatakayozidi” alisema yule nurse huku anampatia Shaban kipande cha karatas kilicho tolewa kwenye mashine ya malipo.

“asante sana dada yangu, hakika umetupokea vizuri na umetuhudmia vizuri, nakuandalia zawadi yako” alisema Shaban, akimweleza yule nurse, “usijari kaka yangu, kwamaana nijukumu langu, ila nakupongeza kwa kuweza kumjari mkeo na kumsimamia bila kuchoka wala kuitaji kwenda kupumzika” alitoa sifa yule nurse, ambae alikuwa anamtazama Shaban anaendeea kuandaa urijo kwenye bakuri na kumsogezea mke wake.

“nijumuku langu kama baba, hivyo sipaswi kupewa hongera wala kusifiwa” alisema Shaban, kabla ya kuaga na kuondoka zake, akimwacha Ashura anakunywa urojo, huku dada yake akimsaidia kwa mambo madogo madogo, “dada umesahau maji” alisema Ashura, na hapo dada mtu akatoka nje kufwata maji.*******

Wakati huo huo huko, hapo hapo hospital ya mnazi mmoja, Siwema anamaliza kumkabidhi mgonjwa, anatakiwa kuondoka kwa dala dala, maana gari ni la hapa hapa mnazi mmoja, lakini Siwema anaonelea kuwa asiondoke bila kumwona Amina, ambae kiukweli ni week ya nne kama siyo ya tano sasa, ajamwona wala kuwasiliana, ni toka sikuile alipo achika na kufukuzwa kazi.

Baada ya kuulizia akaelekezwa aende kule upande wa VIP, ambako Siwema alimkuta Amina ana amesimama nje ya mlango wa Doctor, upande wa store, ambako kulikuwa na vent inayopitisha sauti toka chumba cha Doctor.

Ile anaingia tu, Amina akamwonyesha ishala ya kukaa kimya, ni kama amanina alikuwa anasikiliza jambo flani toka upande wapili wa chumba, ambacho ni chumba wanachoudumiwa wagonjwa VIP,

Chumba ambacho Edgar na Radhia walikuwa ndani yake, yani ofisini kwa kwa Doctor, wamekaa viti vya karibu, wanapokea majibu ya vipimo, alivyofanya Radhia.

“unafanya nini?” anauliza Siwema kwa sauti ya kunong’ona, “mdogo wako ameletwa na mume wake, kuja pima, ndio na sikiliza majibu” anasema Amina, kwa sauti ya kunong’ona, hapo Siwema anashikwa na mshtuko kidogo, anaamua kujiunga na Amina ilikusikiliza kinachoendelea upande wapili.

“tumepima vipimo vingi kama ulivyoagiza mheshimiwa, lakini bi Radhia, ajakuwa na tatizo lolote, yani hana maralia wala taifodi, hana UTI, sukari yake hipo sawa, ata damu yake pia hipo sawa, aina maambukizi yoyote” alisema yule mwanamama ambae ni Doctor, na kuwashangaza Edgar na Radhia.

“inawezekanaje, mbona nimetapika sana toka jana?” aliuliza Radhia kwa sauti ya mshangao, huku Edgar akionekana kushangaa kwa majibu ya Doctor huyu, “mna uhakika na vipimo vyenu, kama mnawasi wasi basi nimsafirishe kwenda kutibiwa #Mbogo_Land, au Dar es salaam?” anauliza Edgar, na kumfanya Radhia ajitabasamulie bila kificho, maana kipimo tu anatakiwa asaifirishwe, vipi kama kuna inshu kubwa.

“mheshimiwa tuna uhakika na vipimo vyetu, ndio maana tumegundua kuwa mkeo anaujauzito wa mkadilio wa mwezi mmoja, ambao mala nyingi usababisha dalili alilozonazo” sidhani kama Radhia alisikia kauri ya mwisho ya Doctor, maana alihisi mwili unamsisimka furaha isiyo kifani inamshika, “mimba?, siamini” anasema Radhia kwa sauti ya kunong’ona, huku analaza mkono wake kwenye tumbo lake, na kuutembeza taratibu.

Edgar anamtazama Radhia, ambae pia anamtazama Edgar, “Edgar ni kweli nimeshika mimba” alisema Radhia, tabasamu la furaha likiwa limetawara usoni mwake, na machozi yakimtililika mashavuni.

Radhia ajazowea mambo ya kizungu, ikiwa ni kukumbatiana adharani, lakini leo alijikuta tayari amesha jaa kifuani kwa Edgar, ambae alimpokea bila ubishi, “Edgar nitakuzalia mtoto, mala yangu ya kwanza” alisema Radhia kwa sauti yenye kilio cha furaha, “utaende kuwa mama wa mtoto wangu” alisema Edgar kwa ile sauti yake nzito sasa ilizidi kuwa tulivu, “nitamsikia mwanangu anakuita baba” alisema Radhia akiwa bado amemkumbatia Edgar.

Hii ilikuwa mni chumbani kwa Doctor, balaha lilikuwa upande wa chumba cha store, ambako Siwema na Amina walikuwa wametazama kwa mshangao kama wameona nyoka mwenye miguu, ata walipo gundua kuwa wanashindwa kuongea lolote, wakatoka nje ya kile chumba haraka.

Huko ndani Edgar na Radhia wanakumbatiana kwa sekunde kadhaa, kisha wanaachiana lakini bado Radhia ameegemea kifuani kwa Edgar, anatilikwa na machozi, Edgar anamtoa kitambaa chake, na kumfuta machozi huku anaongea na Doctor.

“hii ni habari njema Doctor, ilikuwa muhimu kuliko ata vipimo vingine” hakika umefanya siku yangu na mke wangu kuwa njema sana” alisema Edgar, akionyesha furaha ya hali ya juu, huku anaebndelea kufuta macho kwenye mashavu ya Radhia, ambae ni kama aliongeza kudeka.

“kwanini mheshimiwa, mbona nyie bado wadogo, vijana wenzenu uwa hawa ofii uzazi na wala awakimbilii kuzaa” alihoji Doctor akishangaa namna taarifa ile ilivyopokelewa nwa wapendwa nao wale, “nivigumu kuelezea Doctor, ila hipo siku utafahamu huyu mtoto wa kwanza ni muhimu kiasi gani kwetu” alisema Edgar.

Wakati maongezi yanendelea Doctor akaita “nurse mmoja aniletee file la clinic” aliagiza Doctor, na wakati huo, Amina alikuwa anaongea na Siwema ambae kiukweli ni kama alishikwa na bumbuwazi, kwa kusikia kuwa Radhia ni mjamzito, roho inamuuma ghafla kama vile na yeye ajazaa.

Amina akaenda kwenye sekta ya wazazi na kurudi na jarida kwaajili ya mauzilio ya maendeleo ya mama na ujauzito wake, na hapo ndipo alipo pata nafasi ya kuingia ofisini, ambako amlimkuta Radhia akiwa amejiegemeza kifuani kwa Edgar.

Mshangao wa msisimko anaoupata Amina, siyo mdogo ata kidogo, anaweka file mezani, huku anawatazama kwa macho ya wizi, anashindwa kuuliza wala kutoa hongera ya kinafiki, anatoka nje bila kuongea lolote, anamwacha Radhia akiwa amekaa vile vile, yani kwakuegemea kifuani kwa Edgar.

Huku nje Siwema anaona pale aliposimama hapamfai, maana akutaka Radhia ajuwe kama amesikia kuwa ni mjamzito, hivyo akaamua kutembea mpaka eneo la mbele, la hospital ili asubuiri kuona kama ni kweli Radhia ata toka mle hospital.

Wakati Siwema akiwa amesimama mita kadhaa, toka kwenye mlango wa kuingilia hospital, macho ameyaelekeaza kwenye mlango huo, ambao ulikuwa na watu wengi, mala anashtuka akisalimiwa na mtu toka nyuma yake.

“shemeji asalam aleykum” Siwema anageuka na kumtazama alie salimia, anamwona Idd, yani shemeji yake wa zamani, aliekuwa amesimama karibu yake na baiskeri yake, huku uso wake ukionyesha kuwa na jambo flani, yani alikuwa katika taharuki, “aleykum salam, shemeji vipi mbona hapa tena, unamgonjwa?” anauliza Siwema, kutokana na jmwonekano wa shemeji yake wazamani.

“Ashura yupo hapa amekuja kujifungua” alisema mama Idd, huku anainua uso wake kutazama kwenye lango la kuingialia hospital, Ashura ambae anapomwona Idd, anakumbuka jinsi alivyo mtimua Radhia kwa shutuma za kushindwa kubeba mimba, “huyu mpuuzi amefwata nini hapa” anauliza Idd kwa sauti ya juu, huku ana mtazama Shaban, aliekuwa anatoka ndani ya hospital nakuelekea upande wa nje ya hospital.

Siwema nae anamtazama Shaban, anamfahamu kijana huyu, lakini ajuwi kinacho endelea kati yake na Idd, ambae sasa alisha tokomea nje ya lango kuu la uzio wa hospital.

Idd anajishtukia na kukumbuka kuwa alikuwa pamoja na Siwema, na wakati huo huo anamwona Amina anakuja mbio mbio, “mdogo wako anajuwa kudeka, yani nimemwona amejiegemesha kwa kaka wa watu, huku machozi ya mtililika kwa furaha” alisema Amina ambae ni wazi akuwa anamfahamu Idd, licha ya kusikia kuwa Radhia aliachika kwa mume wake wakwanza. ......... ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPA HAPA jamii forums
 
Ningekua mukhsin huyo siwema angekoma.
Kuna dada binamu alikuwa na maneno ya shombo km hayo Aisee mi ni kimya tu.
Siku alinigusa tu, nilipiga yule mtu mpaka kazimika.
Na sikuwa hata na wazo kumchapa lakini baada ya kuchomwa vidole vya macho ndio nikamtwanga.
 
Back
Top Bottom