ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA TISINI NA TANO
MTUNZI:
edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA TISINI NA NNE: Lakini pia taarifa ilieleza kuwa, mwalimu Makame ata apishwa kesho, kwenye ukumbi wa ikulu, “naomba isiwe hivyo, mbona Radhia atazidi kulinga” alijisemea Idd, ambae licha ya tamaa aliyonayo juu ya Radhia, lakini ameshindwa kumiliki mke mwingine, ambae leo amempatia taraka. ......... ENDELEA….
Taarifa hii ilipokelewa kwa furaha na familia ya bwana Makame, siyo tu pale nyumbani kwao, au kule kwa Edgar, pia sehemu nyingi sana, kwa ndugu jamaa na marafiki, toka kila kona ya kisiwa iki cha unguja, pia pemba na sehemu nyingine zote ambazo walisikia na kumfahamu mzee Makame.
“kesho tutakuwa wote kwenye kiapo cha baba yako pale ikulu” alisema Edgar, ambae bado alikuwa amejilaza kwenye kochi, huku Radhia akiwa melala kifuani kwake, “kwani wanaluhusu familia nzima kwenda kuona?” aliuliza Radhia, huku anageuza uso wake kumtazama Edgar usoni.
“yah!, naluhusiwa, lakini kwa watoto wadogo, pia na wale wakina mama” alisema Edgar, “sasa mimi nitaendaje?” anauliza Radhia, kwa sauti ya mshangao, “kwani kwenye afla ikulu, ulienda kama nani?” aliuliza Edgar, huku nae anamtazama Radhia, “nilienda kama mwanafamilia wako?” alijibu Radhia, huku anaachia tabasamu, maana alikumbuka mbali sana.
“basi na kesho utaenda kama mwanafamilia wangu, na muda wote utakuwa na mimi” alisema Edgar na kumshtua Radhia, “mh!, kwahiyo baba anione kabisa kuwa nipo na wewe?” aliuliza Radhia huku anacheka kwa aibu.
Mwanzo aikuwa rahisi, lakini ukweli mpaka mida ya saa mbili za usiku, siku iliyofuata, kwa walio bahatika kuiona taarifa ya habari, akiwepo Idd, waliweza kumwona Radhia, ambae kwakifupi kila alie iona taarifa ile, alijikubaria kimoyo moyo kuwa leo amemwona mschana mzuri, na ukizingatia kuwa taarifa hii, ililushwa na vituo vingi vya television, vya bara na visiwani.
Aikuwa nzuri kwa Idd, ambae alijikuta anazidi kuumia mala dufu, akuwa peke yake, Siwema nae alikuwa hivyo hivyo, wakati baadhi ya watu wanaendelea kufurahia mafanikio ya mwalimu Makame, yeye alikuwa anaumia kwa kumwona Radhia katika tukio lile.
Kibaya zaidi ni kwamba, haikuwa mwisho wa maumivu, kwa Idd na Siwema, ambao hawakuacha kumwombea mabaya Radhia, kwamba ifikie wakati aachike kwa kukosa ujauzito.
Kwa upande wa Mariam na Zahara, wao ilikuwa tofauti kidogo, maana siku tatu baadae familia ya mzee Makame iliamia kwenye nyumba kubwa ya serikali, na huku Radhia licha ya kuwa na chumba chake katika jumba ilo la kisasa, lakinipia nikama alikuwa ameshaamia nyumbani kwa Edgar.
Siwema kwa kuona uhuru wa kujipatia mwanaume na pengine kulewa pombe, akaomba fedha kwa mdogo wake Radhia, na kwenda kupanga chumba, maeneo ya michenzani, kule anakoishi Idd.
Mariam na Zuhura licha ya kuishi kwenye jumba la kifahari, na kupata huduma muhimu, na heshima mtaani, lakini bado waliona kuwa hawakuwa na uwezo kumfikia Radhia, kwa fedha na ufahari walio nao.
Awakuweza kumwona baba yao fedha mala kwa mala, maana baba yao alikuwa anaanza ujenzi wa nyumba yao, kule kule jang’ombe kwa soud, hivyo awakuwa na budi kurejea kwa Radhia na kumwomba msaada wa fedha ndogo ndogo za kuwa saidia.
Ilikuwa lahisi kwao, sababu awakuwa na mtu wa kuwaunga mkono, kwenye ujinga wao wa chuki zisizo na sababu, maana dada yao Siwema tayari alisha ondoka pale nyumbani, kwa msaada wa Radhia, mama yao mzazi, sasa alisha hacha kumsimganga Radhia, nikutokana na kusababisha mzee Makame, kupata nafasi nzuri serikalini, chanzo kikiwa ni Radhia, na pia Siwema kurudishwa kazini, sababu ikiwa ni Radhia.
Tayari Mariam na Zuhura, walisha waacha na kuwasahau wakina Mahadhi, kwakuona siyo hadhi yao tena, maana wao walikuwa wanaitaji fedha ya urojo tu toka kwao, sababu kuhusu dudu, awakuwai kuwalizisha ata mala moja, ni kwamba licha ya kupoteza bikira zao kwa tamaa ndogo ndogo, lakini awakuwai kufurahia dudu.********
Week inakatika Radhia akiwa nyumbani kwa Edgar, wanaishi kama mke na mume, sasa Radhia alianza kuwasiliana na kupeana salamu na wanafamilia wa Edgar, kwamaana ya baba na mama Edgar, kaka yake Edgar yani Deus Nyati na mke wake, pia wifi yake Dorin yani dada wa Edgar.
Kikubwa ni kwamba, sasa Radhia alikuwa amesha wapokea wageni toka #Mbogo_Land, ambao ni timu ya mpira wakikapu iliyokuwa na watu kumi na tano, yani wachezaji kumi na mbili, na walimu wawili na Doctor mmoja.
Ziara ilikuwa nzuri, ikisimamiwa na ofisi ya barizi Edgar, chini ya usimamizi wa Radhia, akisaidiwa na Monica, huku Edgar akiudhuria kila mechi, ambayo ilicheza na wanamichezo hao toka #Mbogo_Land, ikiwepo mechi yao na timu ya wakina Mukhsin.
Mala baada ya kumaliza michezo yao, wanamichezo wale toka shule ya sekondari ya King Eugen wa pili, walitembelea vivutio mbali mbali vya utarii, huku wakipiga picha na kuweka kwenye tovuti ya shule, na shirikisho la mpira wakikapu nchini #Mbogo_Land, yani MBA.
Picha na video za vivutio vya kitarii, zilkisambaa eneo kubwa duniani na kujizolea umaarufu, na kutazamwa na watu maarufu duniani, wakiwepo wanamichezo, wanasiasa, wacheza filam, wanamusic na watu mashuhuri wa mitandaoni.
Sifa kubwa zilienda kwa Radhia, kwa maandalizi mazuri, na ubinifu alio ufanya, uliosababisha kuiletea sifa nchi yake, ata siku nne baada ya wanamichezo kuondoka nchini, alifanya maojiano na waandishi wa habari, huku watu wengi wakishuhudia kwenye TV na mitandaoni, pamoja na kwenye maredio.
“imekuwa ghafla sana bi Radhia, hapo mwanzo hukuwai kuonekana wala kufanya kitu kama iki, ebu tueleze wazo ili ulilipata wapi, na umewezaje kufanikiwa” alisema mmoja kati ya waandishi wa habari.
Idd akiwa kwenye TV yake, anamwona Radhia mbele ya waandishi wengi wa habari, akiwa amependeza na kuwa mtamu kweli kweli, hakuka anajikuta anaumia roho, huku Siwema aliekuwa amekaa sebuleni kwake anakunywa bia zake ambazo alikosa kwa muda mrefu, nae pia anatazama kwenye TV, kama ilivyokuwa nyumbani kwao.
“kwanza kabisa nimshukuru mwenyezi mungu, maana yeye ndie mwenye kupanga kila jambo kwa mja wake, pili niwashukuru wazazi wangu kwa kunipatia nafasi” hivyo ndivyo alivyoanza Radhia, ambae kila alietazama habari hii, alivutiwa na mambo matatu, moja sura nzuri ya mwanamke huyu, pili sauti yake tamu, tatu ni umaarufu wake wa ghafla.
Radhia anatabasamu kidogo, nikama anaona aibu, “tatu nimshukuru barozi Edgar, kwa kuniamini na kunipatia nafasi ya kuonyesha ninacho kiweza, huku akinishika mkono kwa kila hatua, mpaka nimefanikiwa kufikia malengo, tumejenga urafiki kati ya wanamichezo wetu, tumetoa njia kwa wanamichezo wetu, kufikia mafanikio katika mchezo wampira wakikapu, pia tumeitangaza nchi yetu katika utarii” alieleza Radhia.
Maswali ya waandishi ayakuishia hapo, “tunafahamu wewe ni mwenyeji wa zanzibar, na hupo karibu sana na barozi Edgar, je una uhusiano gani na barozi Edgar?” aliuliza mmoja kati ya waandishi wa habari. ......... ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPA HAPA
jamii forums