Simulizi: Harakati za Jason Sizya

Simulizi: Harakati za Jason Sizya

Mgeni mwema.jpg

167

Almasi Dilunga


Saa 12:25 alfajiri…

ILIKUWA Jumamosi tulivu mno na hali ya hewa ilikuwa ya ubaridi kidogo, angani wingu zito la mvua lilikuwa likijitengeneza taratibu na hivyo kuashiria kuwa mvua ilikuwa mbioni kunyesha. Ndege angani walikuwa wanashindana kuimba na kuruka huku na kule kwenye vilele vya miti. Na kwenye mapaa na vibanda majogoo pia yalishindana kuwika.

Ni mwezi mmoja na nusu ulikuwa umepita tangu tutoke Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma na kurudi Kilosa. Mtoto Mariam alikuwa amepata nafuu na alikuwa akiendelea vizuri baada ya kuongezewa damu na kisha kupewa dawa ambazo tuliambiwa tuwe tukimpa kila wiki.

Alfajiri hiyo nilikuwa nafanya mazoezi ya kukimbia mbio za taratibu yaani jogging, pembezoni mwa reli ya kisasa inayotoka Morogoro kuelekea Dodoma. Nilikuwa nimevaa jezi ya Manchester United na raba nyepesi nyeusi miguuni.

Ilikuwa ni kawaida yangu kudamka alfajiri na mapema kila siku na kufanya mazoezi ya mwili ikiwemo ya kukimbia umbali wa kilomita zisizopungua tano.

Mbio zangu ziliishia kwenye kijumba chetu kilichojengwa kwa tofali za kuchoma, katika eneo la Kichangani, mojawapo ya mitaa maarufu ya Mji wa Kilosa. Hiki ni kijumba ambacho nilikijenga kwa nguvu zangu katika miezi miwili tu kutokana na kufanya kazi kwa bidii.

Kila mtu pale mtaani, eneo la Kichangani, alinipenda sana kwa sababu ya upole wangu na pia sikuwa na makuu hata chembe, niliishi vizuri na watu hasa majirani zetu.

Saa 2:30 asubuhi ilinikuta nikiwa nimeketi sebuleni nikiwa nasikiliza kipindi cha uchambuzi wa habari mbalimbali za michezo kwenye redio yangu ndogo ya kutumia betri, ni wakati huo ambao Zainabu aliingia ndani akiwa amebeba ndoo ya maji kichwani na mkononi alishikilia mfuko mdogo mweusi.

Alipoingia tu aliuachia ule mfuko mweusi ukaangukia chini karibu na miguu yake na kisha yaliitua ile ndoo, akajinyoosha huku akipumua kwa nguvu, halafu akatumia upande wa khanga aliyojifunga kujifuta jasho usoni.

Kisha aliliendea kabati dogo la vyombo lililokuwepo pale sebuleni, akalifungua na kuchukua kiberiti kilichokuwa nyuma ya jagi la sukari na kutoka nacho nje.

Baada ya dakika zipatazo kumi Zainabu aliingia tena ndani na kuniambia kuwa amepeleka maji ya kuoga bafuni. Niliinuka, nikavua nguo za mazoezi nilizovaa na kujifunga khanga kisha nikaelekea bafuni wakati Zainabu akipasha moto kiporo cha wali jikoni.

Huko bafuni nilijimwagia maji na kupiga mswaki, na dakika kumi baadaye nilitoka nikiwa nimechangamka kweli kweli. Kweli maji ni tiba kwani sasa nilikuwa najisikia safi zaidi. Nilipoingia ndani Zainabu alikuwa anaandaa meza, nikapitiliza moja kwa moja chumbani ambako nilivaa suruali nyeusi ya kadeti, singlendi nyeupe na shati jeupe lenye mistari myeusi.

Kisha nikatoka sebuleni na kumkuta Zainabu akiwa ameshaandaa kifungua kinywa; chai na kiporo cha wali na maharage yaliyoungwa na nazi. Kilikuwa chakula kitamu sana nilichoamini kingeisindikiza vizuri Jumamosi ile tulivu mno.

Nilipomaliza kunywa chai nilimwambia Zainabu kuwa nakwenda kumjulia hali rafiki yangu Almasi kwa kuwa siku iliyokuwa imetangulia nilimwacha akiwa na majeraha.

Kabla sijaondoka nilitandaza mikono yangu huku nikimtazama Zainabu kwa uso uliochanua kwa tabasamu. hii ilikuwa kawaida yangu kumkumbatia Zainabu na kisha kumbusu kwenye paji la uso wake kabla sijaondoka. Zainabu alinitazama kwa sekunde chache, tukawa tunatazamana. Kisha naye akatandaza mikono yake. Tukakumbatiana.

Tulibaki tumekumbatiana kwa kitambo fulani tukiwa kimya. Yaani hakuna aliyesema chochote ingawa nilihisi kuwa mioyo yetu ilikuwa inawasiliana. Mikono yake kaizungusha shingoni kwangu, mikono yangu nimeizungusha kiunoni kwake. Zainabu alionekana kujiachia mikononi kwangu… ile kifua chake kilivyokua kinanichoma, niliweza kusikia sauti ya mapigo yake ya moyo.

Pasipo kutarajia Zainabu alinishika kichwa changu akakiinamisha kumwelekea kisha aliniletea mdomo wake na kuuzamisha ulimi wake kinywani mwangu. Ndimi zetu zikakamatana vilivyo huku pumzi nyepesi ikipita puani. Mikono yangu chakaramu ikaanza kusafiri taratibu hadi kifuani kwake na hapo nikaanza kuyatomasa matiti yake taratibu kwa ufundi wa hali ya juu.

Zainabu aliachia sauti hafifu ya mguno wa mahaba kama mtu aliyekuwa amepagawa na wazimu wa mapenzi. Macho yake malegevu yalitaka kufumba lakini yaliishia katikati ya mboni zake na hivyo kumfanya aonekane kama aliyelewa.

Kisha ncha ya ulimi wangu ilifanya ziara kwenye tundu la sikio lake na hapo nikasikia tena sauti hafifu ya mguno wa mahaba kutoka kwa Zainabu sambamba na mapigo ya moyo wake kuanza kwenda mbio. Sasa Zainabu hakuweza tena kuvumilia badala yake kwa papara akaanza kunivua shati langu. Mara akaonekana kusita baada ya kuhisi kulikuwa na mtu mwingine aliyeingilia faragha yetu.

Wote tuligeuza shingo zetu haraka kutazama upande tuliohisi kulikuwa na mtu, tukamwona mtoto Mariam akiwa amesimama kando huku akitutazama kwa udadisi. Tukatazama.

“Lakini… kwani lazima leo uende kwa Almasi! Si unaweza kwenda hata siku nyingine?” Zainabu aliniuliza kwa sauti ya puani huku akiwa bado amenikumbatia. Alikuwa akinitazama kwa namna ambayo ilionesha utayari wake.

“Kwani sijakwambia kwamba Almasi yupo matatizoni? Ni mimi pekee ninayeweza kumsaidia,” nilimwambia Zainabu huku nikimtazama machoni. Kisha nikaongeza, “Kuna mambo hayapo sawa na maisha yake, hivyo siwezi kumwacha peke yake.”

Ni kweli. Almasi alikuwa rafiki yangu mkubwa. Tulielewana sana, pengine kwa kuwa wote tulikuwa na uwezo mkubwa kiakili na upeo wa kujua mambo ingawa niliamini Almasi alikuwa ni zaidi ya mtu wa kawaida, alikuwa genius.

Almasi alikuwa kichwa ile mbaya, yaani alikuwa ana akili sana na mwenye kujua mambo mengi mno. Alikuwa hivyo kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu, tatizo lake kubwa lilikuwa kuvuta sana bangi na misimamo yake. Bila hivyo bila shaka angekuwa anafundisha chuo kikuu na pengine angeshaukwaa uprofesa.

Hata hivyo, kwa upande wangu sikujua kuhusu kiwango cha elimu yangu kwa kuwa sikuwa nakumbuka chochote kilichotokea nyuma. Hata hivyo niliamini kuwa nayajua mengi kwa kuwa nilikuwa na tabia ya kumpa kila mtu nafasi ya kuwa mwalimu wangu. Kila mtu alinifunza kwa yale aliyoyafahamu na niliheshimu kauli na mawazo ya wote kwa uzito sawa. Hata hivyo, uelewa wa mambo ulibaki kuwa juu yangu mwenyewe.

Kukutana kwetu kulikuwa kwa bahati tu. Ilitokea tu mwezi mmoja uliokuwa umepita, siku moja baada ya kuachishwa kazi kwenye kampuni ya Yapi Merkezi iliyoshughulika na mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Morogoro hadi Makutupora Dodoma, nilikuwa na mawazo mengi nikiwa sijui nini nifanye.

Japo nilijitahidi kuonekana nipo sawa na kwamba sikujali kusimamishwa kazi lakini ukweli siku hiyo sikuwa sawa kihisia na hivyo jioni ya siku hiyo niliamua kutoka nifanye matembezi. Niliamua niende mbali na makazi ya watu, sehemu tulivu zaidi ili nikatafakari hatma yangu.

Ilikuwa majira ya saa kumi na mbili na ushee jioni, jua lilikuwa limekwisha anza kuzama na kiza kikianza kuchukua nafasi yake, anga la rangi nyekundu lilikuwa likinywea katika ukungu na nyota hafifu zilikuwa zinaanza kujitokeza moja baada ya nyingine, na kwa mbali, upande wa Magharibi, wekundu ulikuwa ukififia na kiza kikianza kuchomoza taratibu.

Muda huo nilikuwa nimerudi kutoka kuonana na Jerome baada ya lile Sakata la mchana wa siku hiyo. Nilikuwa nimemfuata nyumbani kwake baada ya saa za kazi, nilipanga kukutana naye uso kwa uso ili nimweleze kile nilichokusudia.

Endelea...
 
Mgeni mwema.jpg

168

Nilimkuta Jerome nyumbani kwake, nikamsalimia lakini hakujibu, badala yake nilimwona akiwa na hofu na alikuwa anatetemeka. Alinitaka niondoke nyumbani kwake kabla hajawapigia simu polisi, na baada ya mabishano ya muda mrefu sana nilifanikiwa kumtuliza na tukakaa chini tukaongea.

“Jerome, najua unampenda sana Zainabu, nafahamu sana uhusiano wenu, Zainabu amenieleza kila kitu lakini tafadhali nakuomba sana, heshimu uamuzi wake. Pamoja na yote yaliyotokea lakini mimi sina uadui na wewe, huna sababu ya kunichukia wala kuniwinda, nina mengi sana yanayonisibu na roho ya uvumilivu sina ndiyo maana nakuomba uache kuniwinda, kaa mbali na mimi. Nakuonya tu kwa kuwa mimi si mtu mzuri sana kama unavyonichukulia,” nilimwambia Jerome kisha nikaondoka zangu nikimwacha amepigwa na butwaa.

Kisha nilirudi nyumbani na kuchukua kiredio changu kidogo, nikamuaga Zainabu kuwa nakwenda matembezi na pengine ningechelewa kurudi, kisha nikatoka. Nikawa natembea taratibu kando kando ya reli ya kati huku nikitafakari. Nilikuwa naelekea nje ya makazi ya watu, nje ya mji.

Nilitembea kwenye mandhari nzuri ya uwanda mpana wenye eneo kubwa lenye vichaka, miti mikubwa kwa midogo. Wakati nikitembea niliweza kuwaona ndege wengi wa aina mbalimbali wakiruka huko na huko kwenye miti mikubwa, na walisikika wakiimba nyimbo za furaha kwa namna ya kuisifia jioni hiyo na kuifanya kuwa njema, ingawa kwangu jioni hiyo haikuwa njema kabisa. Tena ndege hao walionekana kuwa ni wenye furaha kubwa na kulipa uhai eneo lote lililoonekana kuwa tulivu mno.

Kuna muda nilijikuta nikisimama kwa muda kuwasikiliza wale ndege kwa umakini, nilijaribu kubashiri maana ya zile nyimbo nzuri walizokuwa wakiimba, nikayasikia hadi maneno yaliyotamkwa katika nyimbo hizo, ambayo ki ukweli yalionesha kubeba ujumbe mzuri wa ushindi na faraja. Na hapo nikajikuta nikifarijika kidogo.

Niliachia tabasamu na kuendelea kutembea kando kando ya ile reli nikizidi kwenda nje ya mji, safari hii niliongeza mwendo kidogo nikionekana kupata nguvu mpya. Sikwenda mbali zaidi nikasita na kuyakaza macho yangu kutazama mbele yangu.

Ingawa kiza kilishaanza kutanda lakini hiyo haikunizuia kuona taswira ya mtu kwa mbali akiwa kakaa relini. Sikuwa na shaka kwamba taswira hiyo ilikuwa ya mwanamume. Alikuwa anavuta sigara maana niliona moto mdogo ukipanda na kushuka.

Japo kulikuwa na hali ya baridi na upepo ulikuwa unavuma lakini mwanamume huyo alikuwa kavua shati lake na kuliweka begani. Mwonekano wake ulikuwa wa kutia huruma kidogo.

Nilisita na kutaka kurudi nilikotoka maana huwezi kujua yupi mtu mwovu na yupi mwema, lakini nikajikuta nikivutiwa kutaka kufahamu kwa nini mtu yule alikuwa katika hali ile, nikiwa bado namtazama kwa wasiwasi nikamwona akigeuza shingo yake kunitazama huku akiificha haraka sigara yake na kisha akainua mikono yake juu na kusema, “Amani, amani, mkuu!”

“Amani!” nilijibu huku nikimtazama kwa umakini kisha nikashusha pumzi za ndani kwa ndani.

Nilianza kumsogelea taratibu lakini kwa tahadhari kubwa huku nikimtazama kwa umakini. Wakati nikimsogelea nikamwona akinyanyuka na kunyoosha mkono wake wa kulia kunisalimia, macho yake yalikuwa makini. Tukasalimiana huku kila mmoja akimtazama mwenzake kwa umakini kwa namna ya kusomana mawazo yetu.

Wakati tukisalimiana niliweza kubaini kuwa alikuwa mrefu kama mimi lakini yeye alikuwa mwembamba na tumbo lake lilikuwa limeingia ndani kana kwamba alikuwa hajala kwa wiki kadhaa. Sura yake ilikuwa ya ucheshi ingawa wakati huo alionekana kuwa mwenye mawazo mengi.

Alikuwa amevaa suruali nyeusi ya dengrizi na kofia nyekundu aina ya mzula. Shati lake aina ya batiki alikuwa amelitundika begani na miguuni alivaa makubazi ya ngozi.

Dakika mbili tu za kuwa na mtu huyo zilitosha kunifahamisha nilikuwa nimekutana na mtu wa aina gani. Sikuwa nimepanga kukaa naye kwa muda mrefu lakini nilijikuta nikivutiwa sana kuongea naye hasa baada ya kugundua kuwa jamaa alikuwa ana ufahamu mkubwa sana, ingawa hata mara moja hakugusia kuhusu elimu yake.

Ufahamu wake kuhusu mambo mbalimbali ya kisiasa, uchumi na hata ya kijamii haukunishangaza sana, ila uwezo wake mkubwa wa kuchambua mambo ndiyo ulionifanya nijione bado sijui mambo mengi ukinilinganisha na yeye.

Aliweza kuchambua mambo kwa namna ambayo ungetamani uendelee kumsikiliza, na mwisho angekutaka ulitazame jambo hilo kwa mtazamo mpana zaidi.

Tulijikuta tukikaa pale relini na kuongea mambo mbalimbali kwa takriban dakika arobaini na tano, tukawa tumefahamiana hadi majina. Aliniambia anaitwa Almasi Dilunga na mimi nikamtajia jina ambalo nilikuwa nikiitwa au kujiita, jina la Mgeni Mwema.

Sasa akawa amefahamu kuwa sikuwa askari na hivyo nikamwona akifukua chini na kutoa msokoto, ni sigara aliyokuwa anavuta mwanzo kabla sijafika, ambayo ilikuwa imezimwa. Niliitazama kwa makini nikagundua ulikuwa ni msokoto wa bangi.

Aliubana ule msokoto kwenye pembe ya mdomo wake kisha alianza kuhangaika kutafuta kiberiti ili ajiwashie ule msokoto lakini kabla hajachukua kiberiti kuwasha aliniuliza kama nami nilikuwa navuta ganja nikatingisha kichwa kukataa, nikamwona akiahirisha kuwasha na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.

Kisha akaniambia namna ambavyo bangi imekuwa inamsaidia kumwondolea msongo wa mawazo baada ya matatizo makubwa sana ya kifamilia yaliyomtokea, kwani bila bangi labda angekuwa mhalifu. Hata hivyo, hakuwa tayari kunielezea matatizo hayo ni ya aina gani, na kwamba kila alipoyakumbuka yalikuwa yanamuumiza sana.

Niligundua kuwa hakuwa mtu wa kujichanganya na watu wengine, hakupenda kabisa kuongea mambo yaliyohusu maisha yake au familia yake, ndiyo sababu alipenda kujitenga au kuwa mkimya muda mwingi.

Nilichoweza kufahamu kutoka kwake ni kuwa Almasi alikuwa msomi wa Shahada ya Kwanza ya Uchumi aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Tangu siku hiyo tukawa marafiki. Tulijikuta tumezoeana sana. Akajua mishemishe zangu zote nami nikazijua mishemishe zake, kila mmoja wetu akawa mshauri wa mwenzake. Niliporudi nyumbani ilikuwa imetimia saa 5:00 usiku. Nilimkuta Zainabu akiwa ameketi sebuleni akiwa na wasiwasi.

“Ulikuwa wapi, Mgeni? Umenifanya nikae na wasiwasi muda wote,” Zainabu alinidaka kwa swali huku akishusha pumzi baada ya kuniona.

“Lakini si nilikwambia kuwa ninaweza kuchelewa kurudi!” nilimwambia Zainabu huku nimemshika mashavu yake na kumbusu, kisha nikamkumbatia.

“Ungelala tu!” nilimwambia. “Mimi ni mtu mzima, ningerejea tu, hakuna tabu!”

Zainabu alinitazama usoni kisha akaachia tabasamu na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.

_____

Endelea...
 
Mgeni mwema.jpg

169

Sasa tukirudi kwenye kisa cha fumanizi: siku iliyokuwa imetangulia Almasi alikuwa amemfumania mchumba wake Sofia akiwa na mwanamume mwingine aliyeitwa Bundala Philipo, na kisha akaambulia kutwangwa makonde na mwanamume huyo na kuachwa akiwa anavuja damu na hajielewi.

Kwa maelezo ya Almasi; aliwafuma Sofia na Bundala wakiwa wamekumbatiana kwenye kichochoro fulani nyakati za usiku. Walikuwa na furaha sana. Lakini pasipo kujua, Almasi alikuwa amesimama mahali akiwatazama, moyo wake ukiwa unavuja damu.

“Sofia,” Almasi aliita kwa kunong’ona. “Kwani nimekukosea nini?” aliuliza kana kwamba Sofia alikuwa amesimama pembeni yake kisha alijikongoja kuwafuata pale waliposimama.

Alipowafikia hakufanya kitu bali aliendelea kuwatazama mpaka pale aliposhtukiwa. Sofia alipigwa na bumbuwazi baada ya kumwona Almasi, na kwa kiasi fulani alionekana kuhofu, lakini kwa upande wa Bundala ilikuwa kinyume, ni kama vile alikuwa anatarajia ujio wa Almasi kwani hakuwa anahofu wala kuhenya, alimtazama Almasi kisha akampuuza.

“Sofia…” Almasi aliita kwa huzuni na kuuliza, “Nimekukosea nini, mama?”

Mashavu yake yalikuwa yamefunikwa na machozi na alikuwa anang’ata meno kwa uchungu. Sofia hakujibu, alikuwa amebanwa na haya.

Kadiri muda ulivyokuwa unaenda, Almasi akawa anapatwa na hasira. Akajikuta akitaka kumdaka Sofia na kumwadhibu kadiri awezavyo lakini Bundala akammudu mwanaume huyo na kumtwanga makonde kabla ya kumwacha hapo akiwa anavuja damu na hajielewi.

Nilipopata taarifa nilikwenda kumwona na nikamkuta akiwa na uso uliokuwa unavuja damu, jicho lake moja lilikuwa limevimba na tumbo lake lilikuwa linauma kwa kupigwa ngumi!

Kwa kuwa Almasi alikuwa anampenda sana Sofia, hivyo hakuwa anaumizwa sana na majeraha yaliyotokana na kipigo bali aliumizwa zaidi kutokana na kutendwa na Sofia.

_____

“Sawa,” sauti ya Zainabu ilinizindua aliposema kunikubalia, ingawa kukubali kwake kulionekana wazi kuwa ni kwa kishingo upande. Nikambusu na kwenda zangu nikimwacha anamalizia kazi za nyumbani ili akafungue biashara yake.

Siku ile hakuwa na mahitaji mengi ya kufuata sokoni kwa ajili ya chakula cha nyumbani. Ndani kulikuwa na mchele wa kutosha, vipande viwili vikubwa vya samaki kibua wakavu vilivyobaki siku iliyotangulia, na nazi moja na kifuu. Alichohitaji ni nyanya, kitunguu, ndimu na pilipili ndefu, vitu ambavyo hata hivyo vilikuwepo gengeni kwetu.

* * *



Saa 3:15 asubuhi…

Chumba kilikuwa kimya kabisa. Almasi alikuwa ameketi kitandani ndani ya chumba hicho. Kilikuwa chumba kikubwa na kizuri chenye kitanda cha futi tano kwa sita cha mbao ngumu za mkongo. Chumba kilikuwa na dirisha moja lililofunikwa kwa pazia jepesi na refu lenye nakshi za michoro ya maua mazuri.

Pia ndani ya chumba hicho, upande mmoja, kulikuwa na kabati la nguo na pembeni ya lile kabati kulikuwa na kochi moja kubwa na meza nyeusi ya mbao iliyokuwa katikati ya chumba. Pia chumba kilibeba majukumu mengine ya jiko na ghala.

Ukutani Almasi alikuwa ametundika picha yake kubwa iliyomwonesha akiwa amevaa joho siku alipohitimu chuo kikuu.

Nilipoingia nilimkuta Almasi akiwa ameketi pale kitandani amejiinamia, alikuwa na macho mekundu ila jicho la kushoto likiwa jekundu zaidi. Uso wake ulikuwa hoi na mchovu, ni kama vile alikuwa hajapata usingizi kwa juma zima. Alikuwa amechoka sana na pia alikuwa ameumizwa.

Kama kuna jambo linaweza kumpa msongo wa mawazo mtu basi ni pale anapopenda lakini huyo anayependwa asioneshe mrejesho chanya au akaingia mitini.

Niliketi pale kwenye kochi huku nikimtazama Almasi kwa huruma, nilijaribu kuyatafakari yote aliyokuwa akiyapitia. Nilikuwa nafahamu kile ambacho alikuwa anapitia. Nilikuwa nafahamu namna gani ambavyo mwanamume huyo alikuwa akimpenda Sofia, kwa moyo wake wote. Sasa ilikuwa vigumu sana kuukubali ukweli kwamba mwanamke huyo alikuwa amemsaliti.

Ukweli ulikuwa mchungu kuumeza ndiyo maana nilikuwa nafikiria kuwa majeraha ya mwili aliyoyapata yangeweza kutiwa dawa yakapona, lakini vipi kuhusu jeraha la moyo lililosababishwa na mapenzi?

Kwa kawaida sura ya Almasi ilikuwa ya ucheshi muda wote ila kwa siku hiyo alikuwa na uso uliojawa maumivu makubwa na macho yake yalikuwa yanadondosha machozi. Kifua chake kilikuwa wazi na alikuwa amevalia bukta pekee.

“Almasi, unapaswa uliache jambo hili lipite sasa,” nilimwambia Almasi huku nikimtazama kwa imani. Kisha nikaongeza, “Kuendelea kulibeba jambo hili hakutaleta lolote jema zaidi ya maumivu. Sawa, Almasi?”

Almasi alinitazama tu kana kwamba alikuwa hanisikii, uso wake haukuwa na tashwishwi yoyote zaidi ya kuonesha maumivu. Nikajua kuwa aliona kuwa nilikuwa namzingua tu.

No one is worthy of your tears… Usimng’ang’anie mtu aliyekuumiiza namna hiyo, achana naye ili mtu anayekustahili apate nafasi. Na umshukuru Mungu maana huenda amekuepusha jambo baya, pengine ungelia zaidi huko baadaye,” nilizidi kuongea.

Almasi aliendelea kunitazama tu kwa muda pasipo kusema neno. Macho yake yalikuwa yanadondosha machozi. Machozi na damu! Kisha aliniuliza, “Kumbe ulikuwa unayafahamu haya, Mgeni, sivyo?”

Nilivuta pumzi ndefu kisha nikazishusha taratibu. “Almasi, huu si muda mzuri wa kuongelea mambo haya,” nilisema nikijaribu kuyakwepa macho yake.

“Jibu swali langu, Mgeni; ulikuwa unafahamu, sivyo?” Almasi alikazia swali lake huku akinitazama machoni. Macho yake yalizidi kuwa mekundu kwa hasira.

Nilibaki kimya nikiwa nimetahayari kidogo. Ni kweli nilifahamu kuhusu jambo hili, jambo la kusalitiwa na Sofia, nililifahamu wiki kadhaa kabla ya hapo.

Na hapo kumbukumbu juu ya usaliti wa Sofia kwa Almasi ikaanza kuzunguka kichwani kwangu, picha ya usaliti wa Sofia ilijirudia kichwani kama filamu. Nikakumbuka kuwa siku moja jioni, jua lilikuwa limeshazama na kiza kuchukua nafasi yake, nyota pia zilishajitokeza nikiwa katika pilika pilika zangu eneo la Magomeni, nilishtuka kumwona Sofia akifungua mlango wa nyuma wa gari dogo aina ya Toyota Premio nyeusi lililokuwa limeegeshwa kando ya Mto Mkondoa.

Kisha aliingia haraka na kabla hajaufunga mlango nikamwona mwanamume mmoja aliyekuwa amenyoa kipara na alijaaliwa ndevu akishuka toka upande wa dereva na kuingia kule nyuma alikokuwa ameingia Sofia. Kisha mlango ukafungwa.

Kwa kupitia mwanga hafifu wa mbalamwezi niliweza kumwona mwanamume huyo vizuri, alikuwa amevalia bukta ya kadeti yenye mifuko mikubwa pembeni na shati la kijivu la mikono mifupi, mwili wake ulikuwa mpana. Nikamtambua. Jina la mwanaume huyu aliitwa Bundala Philipo…

Nilipatwa na mshawasha wa kutaka kujua kilichokuwa kinaendelea kati ya watu hawa wawili, nikajitahidi kusogea karibu zaidi pasipo kuwashtua waliomo ndani ya gari hilo, hata hivyo sikuweza kubaini kilichokuwa kikiendelea ndani ya gari hilo kwani mlikuwa na giza, ila mara moja moja nilishuhudia mwanga ukiibuka pale ambapo simu ilikuwa inaita.

Nilibana kwenye mti mkubwa ili kuchunguza maana nilishakuwa na wasiwasi na nyendo za watu hawa, nilishawaona kabla ya siku hiyo, kama mara mbili hivi, wakiwa pamoja.

Ilinichukua takriban dakika arobaini nikiwa nimebana hapo kwenye mti mkubwa pasipo kumwona Sofia akishuka wala gari hilo kuondoka. Hata hivyo mtikisiko wa gari hilo uliashiria kuwa kulikuwa na jambo… uzinzi ulikuwa ukiendelea humo ndani ya gari.

Baada ya muda mrefu wa kusubiri hatimaye mlango wa nyuma wa gari ulifunguliwa na Sofia alichungulia nje kwa tahadhari sana akionekana kulichunguza eneo hilo, aliporidhia kuhusu usalama wa eneo hilo akashuka haraka akionekana mwenye wasiwasi sana huku kijasho kikimtoka. Halafu akaanza kuondoka toka eneo hilo kwa hatua za haraka pasipo kutazama nyuma…

_____

Endelea...
 
Mgeni mwema.jpg

170

“Kwa nini hukuniambia muda wote huo, Mgeni?” sauti ya Almasi ilinizindua kutoka kwenye mawazo yangu, alikuwa akiniuliza huku akilengwalengwa na machozi.

“Almasi, naomba usinielewe vibaya. Sikutaka kukuumiza,” nilimwambia Almasi huku donge la fadhaa likiwa limenikaba kooni.

“Hukutaka kuniumiza, eh?” Almasi aliniuliza kwa uchungu huku akifuta machozi, “Mbona sasa naumia?”

“Samahani sana, Almasi… nilitaka nilishughulikie jambo hili kimya kimya, ni kwa vile tu nimechelewa,” nilisema kwa uchungu huku nikikumbuka jambo.

Nilikumbuka kuwa baada ya siku ile niliyomshuhudia Sofia akitoka kufanya uzinzi ndani ya gari la Bundala, siku mbili baadaye nilimfuma tena, wakati nikienda nyumbani kwa Almasi. Nilipokuwa naelekea kwenye kichochoro fulani ambacho kingeniongoza kwenda kutokea mbele ya nyumba aliyokuwa akiishi Almasi, nikahisi kuisikia sauti ya Sofia akiongea kwa tahadhari.

“Bundala… tafadhali naomba usinipigie simu kwa siku mbili hizi, sipendi Almasi ashtuke kabla ya muda mwafaka…” sauti ya Sofia ya kunong’ona ilinishtua na kunifanya nisite kidogo kuendelea na safari yangu, nikaamua kubana sehemu, kwenye upenyo wa ile nyumba na kisha nikachungulia kule ambako sauti hiyo ilitokea.

“…ndiyo naelewa, wewe ngoja mpaka pale nitakapokutaarifu, sawa?” Sofia aliendelea kusema huku akizungusha macho yake kuangalia kwenye kile kichochoro kwa nia ya kuhakikisha hakuna mtu mwingine aliyekuwa akisikia mazungumzo yao ya simu.

“Acha ubishi basi, ninavyokwambia hivyo nina maana yangu… huwezi kujua ila kuna mambo hayajakaa vizuri… nakuomba uwe mwelewa basi… kwaheri!” Sofia alisema na kukata simu, akaonekana kushusha pumzi ndefu akijiona mshindi.

Alipotaka kupiga hatua kuondoka eneo hilo nikakohoa na kumfanya ageuke nyuma haraka, na hapo nikamwona akishtuka sana baada ya kukutana uso kwa uso na mimi! Ni dhahiri kuwa moyo wake ulianza kwenda mbio na mwili wake ulikuwa unamtetemeka.

“Ulikuwa unaongea na nani, Sofia?” nilimuuliza huku nikimkazia macho usoni.

Nikamwona akibanwa na kigugumizi. Aliitazama simu yake kisha akayarudisha macho kwangu, hakuwa na cha kusema. Sikumwacha, nikarudia tena kuuliza, mara hii Sofia alinijibu kuwa hakuwa anaongea na mtu. Nikamtaka anipatie simu yake nione.

“Siwezi kukupatia simu yangu, nikupe wewe kama nani?” Sofia alijibu kwa jeuri huku akinikazia macho.

“Nadhani unajua kabisa kuwa mimi ni tofauti kabisa na Almasi. Sina uvumilivu wala ujinga kama wake. Naomba usinijaribu, sawa?” nilimwambia huku nikimsogelea karibu zaidi. Sura nilikuwa nimeikunja na macho yangu yalimtazama pasipo kupepesa.

Sofia aliduwaa. Ni wazi alikuwa akiniogopa sana, hata hivyo hakuthubutu kunipa simu yake. Nikaamua kumwambia ukweli kuwa nilikuwa nafahamu kinachoendelea kati yake na Bundala, na kwamba nilikuwa nawafuatilia kwa muda. Sofia alitaka kukana lakini nikasisitiza kufahamu kila kitu.

“Huwezi kuniongopea kitu, Sofia. Nataka tu nijue kwa nini unamsaliti rafiki yangu!” nilisema huku macho yangu yakiwa yametulia kwenye uso wake.

Sofia hakujibu, ni Dhahiri alionekana kushtuka sana! Aliweka kiganja chake kifuani akashusha pumzi ndefu kama aliyetoka kukimbia. Kisha aliinamisha kichwa chake kutazama chini…

_____

“Mgeni, kwa hiyo siku zote ulikuwa unajua kwamba Sofia alikuwa ananisaliti lakini ukaamua kukaa kimya! Kwa kweli umeniumiza sana,” Almasi alisema kwa hasira na kunizindua tena toka kwenye mawazo.

“Najua, Almasi… naomba nisamehe sana,” nilijitetea nikiwa nimetahayari sana, kichwa changu nilikiinamisha chini kwa wasiwasi.

Almasi alishusha pumzi kisha akatazama chini, alionekana wazi kuzama kwenye lindi la mawazo. Alibaki kimya kwa kitambo kirefu kisha akanyanyua uso wake uliosheheni maumivu na kunitazama.

“Kumbe ndiyo maana siku za karibuni Sofia alikuwa hataki mimi na wewe tuendelee kuwa karibu! Kumbe ndiyo maana alikuwa ananidadisi kama ulishaniambia chochote!” Almasi alisema huku akionekana kujitahidi kuidhibiti fadhaa iliyomkumba. “Kwa nini sikuyajua yote haya mapema? Kwa nini nilikuwa mpofu kiasi hiki?”

Nilijitahidi sana kumsihi Almasi aachane na fikra hizo kwani zingezidi kumuumiza, lakini suala hilo lilikuwa gumu sana. Almasi alishindwa kunyamaza, ilionesha wazi kuwa moyo ulikuwa unamuuma sana.

Mwishowe aliniomba nimletee pombe kali ili apate kujipumbaza. Kabla sijasema lolote Almasi akaongeza, “Ngoja kwanza nipate ngaja maana akili yangu haifanyi kazi, nahisi kuvurugwa sana… yaani nimevurugwa si kitoto aisee!”

Almasi alisema huku akiinuka na kufunua godoro akionekana kutafuta kitu, na baada ya muda mkono wake ukaibuka ukiwa umeshika msokoto mmoja wa bangi, akaubana kwenye pembe ya mdomo wake na kuanza kuhangaika kutafuta kiberiti ili ajiwashie ule msokoto.

Nilimtazama kwa umakini wakati akihangaika nikitamani kumzuwia lakini nikasita na kuishia kumtazama tu kama mtu niliyekuwa namwona kwa mara ya kwanza. Alipata kiberiti na kuwasha kisha alivuta kwa namna ya kuukoleza moto na kutoa moshi mwingi huku akiutazama kwa umakini.

Kwa takriban dakika mbili alivuta bangi huku akiwa amezama kwenye lindi la mawazo, hakukuwa na tashwishwi yoyote katika sura yake na badala yake aliendelea kuvuta bangi yake kwa utulivu mno. Kisha alipoitoa mdomoni alipuliza moshi wake pembeni huku akiendelea kuutazama kwa umakini.

Baada ya mikupuo kadhaa mikubwa ya moshi wa bangi alikuwa kama mtu aliyegutuka, akanitazama kwa mshangao mkubwa kama aliyestaajabishwa na uwepo wangu pale.

“Mgeni, mbona bado upo hapa? Nenda bwana kaniletee pombe kali nijidunge, nahitaji kutuliza akili yangu,” Almasi alisema kwa msisitizo.

Mwanzoni nilikuwa mgumu kutimiza agizo hilo lakini kadiri muda ulivyokwenda nilidhani kwamba pengine ingekuwa tiba ya muda kwa Almasi, nikainuka na kutoka nikimwacha Almasi akisonya kwa hasira.

Nilikwenda hadi kwenye baa moja iliyokuwa jirani, nikanunua mzinga mkubwa wa Konyagi na kurudi nao nyumbani kwa Almasi, nilipoingia tu ndani Almasi akainuka na kunipora ile chupa kwa mikono yake inayotetemeka, akaifungua na kuigugumia pombe yote iliyokuwemo kwenye chupa kama maji huku akionesha kusisimkwa mwili. Nilibaki nikistaajabu.

Haikuchukua muda mrefu sana nikamwona akianza kulemewa na kichwa, akajilaza pale kitandani na kupitiwa na usingizi. Nilipoona amelala nikamfunika shuka kisha nikakaa na kujikuta nikizama kwenye tafakari.

Nikiwa hapo kwenye kochi nilianza kufikiria juu ya Sofia, msichana mrembo lakini laghai wa mapenzi, na kisha nikamfikiria Bundala. Niliona kuwa watu hao wawili walistahili kuadhibiwa. Haiwezekani waishi maisha ya furaha tele wakati walikuwa wamemuumiza rafiki yangu, kimwili na kisaikolojia, tena pasipo na huruma!

Sasa niliazimia kuilipa kila ngumi iliyomgusa Almasi na ilipaswa kurudi mara tatu yake. Pia maumivu yote ya kiakili yalipaswa kulipwa. Niliapa kuhusu hilo.

* * *

Endelea...
 
Mgeni mwema.jpg

171

Nimeshakuzoea




Saa 6:15 mchana…

ZAINABU alikuwa ameketi juu ya stuli mbele, lakini nje, ya genge lake akiwa anafuma vitambaa. Alikuwa mahiri sana katika kufuma vitambaa vya uzi. Kando yake kulikuwa na ule mfuko mweusi niliouona asubuhi, ulikuwa na mabunda ya uzi yenye rangi tofauti.

Akiwa anaendelea kufuma vitambaa nilitokea kwa nyuma na kwenda kusimama mbele yake. Nikakwanyua ndizi mbivu toka kwenye kichana kimoja cha ndizi na kuanza kula taratibu. Zainabu aliinua uso wake kunitazama mara moja kisha akaendelea kufuma vitambaa vyake.

Nilichukua ndizi ya pili, nikaimenya na kula, na nilipomaliza nikajifuta mikono na midomo yangu kisha nikatoa pochi yangu na kutoa noti ya shilingi elfu tano, nikampa Zainabu.

Zainabu alinitazama kwa umakini usoni lakini hakusema kitu. Sura yake ilikuwa inaonesha udadisi na mashaka fulani, hata hivyo hakujivunga, aliipokea ile noti na kubaki kimya akisubiri kuona labda ningemwambia chochote.

“Chenji baki nayo,” nilisema huku nikiachia tabasamu.

Zainabu aliendelea kunitazama kwa umakini na kupandisha kope huku akitabasamu. bila shaka hakuamini kama ningeweza kuzilipia zile ndizi mbili nilizokula. Aliiangalia ile noti kwa umakini akiikinga juu kwenye mwanga wa jua kuhakikisha uhalali wake kisha akayarudisha tena macho yake kwangu.

Nilikohoa kidogo kama niliyetaka kusema jambo na kumfanya Zainabu aache kufuma kitambaa chake na kuyatumbua macho yake kwangu akionekana kuwa na shauku ya kutaka kusikia nilitaka kuongea nini.

Nilibaki kimya huku nikimtazama kwa tabasamu. Zainabu alishusha pumzi na kuonekana akirudisha fahamu zake pale kwenye kazi ya ufumaji, akaendelea kufuma kitambaa huku akinitupa jicho mara moja moja.

“Ni hivi…” nilisema huku nikisogea tena kibandani na kukwanyua ndizi moja, nikaanza kuila taratibu. Zainabu alinitazama akisubiri niseme lakini niliendelea kula taratibu. Kisha nikasema kwa utani huku nikiangua kicheko hafifu, “Au acha tu!”

Zainabu alinitazama tu kwa udadisi bila kusema neno lolote, bila shaka hakujua kuwa nilikuwa namfanyia mzaha.

“Nimekuachia chenji nyingi sana,” nilisema huku nikiendelea kutafuna ndizi.

“Hicho ndo’ ulichotaka kuniambia?” Zainabu aliuliza kwa mshangao huku akinikazia macho.

Sikumjibu, nilitoa leso toka kwenye mfuko wa suruali na kujifuta vizuri midomo na viganja vyangu na kisha nikairudishia mfukoni. Halafu nikasema, “Ngoja nikirudi tutaongea vizuri.”

“Nimeshakuzowea,” Zainabu alisema huku akiachia tabasamu. Nilicheka kisha nikaanza kupiga hatua zangu kuondoka huku nikiwa na uhakika kwamba macho ya Zainabu yalinisindikiza nyuma yangu.

* * *



Saa 9:30 alasiri…

“Nani?” sauti ya Almasi iliuliza kwa hasira.

“Mimi Mgeni!” nilijibu na sekunde chache zilizofuata nilisikia sauti ya komeo kisha mlango ukafunguliwa.

Almasi alichungulia nje, akanitazama machoni na kushusha pumzi ndefu kama aliyemaliza mbio ndefu za nyika. Macho yake yalikuwa mekundu yanayorembua na uso wake ulikuwa bado una uchovu. Bado kifua chake kilikuwa wazi akiwa amevalia bukta pekee.

Baada ya kuniona hakusema neno bali alirudi ndani, nami nikaingia ndani. Almasi alikwenda kuketi kitandani huku mkono wake wa kuume ukiwa umeshikilia chupa ya K Vant.

“Ulikuwa wapi, Mgeni? Mbona ulinitoroka?” Almasi aliropokwa na maswali kwa sauti yake ya kilevi. Alinitazama kana kwamba mzazi ambaye alikuwa amempoteza mwanawe wa pekee kwa majuma na sasa amerejea nyumbani.

“Kuna sehemu nilikwenda kuchukua fedha zangu kisha nikaenda mara moja home kumwona shemeji yako,” nilisema kwa sauti tulivu.

“Mgeni…” Almasi aliita kwa sauti tulivu huku akinitazama kwa mashaka lakini pia akionekana kukanganyikiwa. “Hujakutana na Sofia huko ulikotoka?”

Kabla sijajibu akaniomba nimpatie maji ya kunywa. Nilinyanyuka na kuchota maji kwenye ndoo, nikampa. Lakini nikakumbuka kumuuliza pia kama angehitaji na chakula.

“Hapana, nashukuru,” Almasi alisema akitazama chini. “Tangu nimempoteza Sofia nahisi maisha yangu yamebadilika. Ninahofia tu nisije kuwa mnyama zaidi kuliko binadamu.”

Kila alipokuwa anaongea kuhusu Sofia, macho yake yalikuwa yanabadilika na kuwa mekundu zaidi. Hali hiyo ilinifanya kuona ni namna gani Almasi alivyoumia kuongelea hilo jambo. Zaidi ya hilo, alinieleza juu ya nia yake ya kusafiri mbali ili kujaribu kumsahau Sofia.

Wakati akiongea, niliweza kuona haja ndani ya maneno yake, namna gani ambavyo uso wake ulimaainsha kile alichokuwa anakisema. Hivyo nilijikuta nikifikiria ni njia gani ya kumsaidia Almasi ili aweze kuondokana na kadhia hiyo.

* * *



Saa 3:00 asubuhi…

Ndiyo kwanza nilikuwa nimemaliza kunywa chai, Zainabu alikuwa ameketi akifuma vitambaa vyake, pembeni yake aliketi Mariam.

Siku hiyo sikujisikia kutoka kabisa. Nilibaki nyumbani nikisaidia shughuli ndogo ndogo za pale na muda ulienda na hatimaye mchana ukafika. Chakula kiliandaliwa. Tulipomaliza kula nikajisikia kutoka nje kwa ajili ya kupunga upepo na kukipa chakula nafasi kishuke vizuri.

Nje jua liliwaka lakini vivuli vya miti havikuwa haba. Nilisimama chini ya mti wa mwarobaini uliostawi sana, na hapo nikawa nalitazama eneo lote la nyumba kwa mbele. Niliitazama nyumba kwa makini kama vile ndiyo nilikuwa naiona kwa mara ya kwanza.

Niliitazama sana na kukiri kuwa bado ilihitaji maboresho makubwa. Nyumba ilihitaji kuongezewa vyumba kwani mafundi waliacha matoleo ya kuiendeleza na sasa niliona umuhimu wa kuviongeza vyumba kwani tulihamia hapo haraka kukwepa adha ya kodi. Nilijua tungeimalizia taratibu tukiwa mle ndani.

Sehemu ya mbele hasa barazani ilikuwa bado haijajengwa. Sehemu hiyo ndiyo ukawa ubao wa mazoezi wa Mariam maana tangu tulipomwanzisha chekechea alikuwa akichora chora herufi zisizo na kichwa wala miguu pamoja na michoro aliyoijua yeye mwenyewe. Tena alitumia mkaa.

Nilishusha pumzi baada ya kuifanyia nyumba tathmini. Ilinibidi nifanye kazi kwa bidii ili kuimalizia maana endapo nikicheza nitazeeka na nyumba ingebaki vilevile. Niliwaza kwa kuwa nilishaona nyumba nyingi zikiwa katika hali kama hiyo na wamiliki wake wakiwa na umri unaoelekea ukingoni.

Niliyaangalia tena yale maandishi pale ukutani nikatabasamu. Tarakimu niliyoiona angalau inaleta maana kidogo ilikuwa 1, mengine yote ni maluweluwe. Nikaanza kuizunguka nyumba taratibu na kutazama hiki na kile. Baada ya kuzunguka vya kutosha, nilielekea gengeni na kumkuta Zainabu akiendelea kufuma vitambaa vyake.

“Mi naenda kumtembelea Almasi,” nilimuaga Zainabu huku nikimtazama kupata jibu.

“Sawa, sisi tupo. Jioni ya leo nikuandalie nini?” Zainabu alijibu huku akinitazama usoni.

Nilimtazama mtoto Mariam aliyekuwa ameketi pembeni ya mama yake na kumuuliza, “Eti, utapenda kula nini leo usiku?”

“Wali maalage,” Mariam alijibu bila kusita.

“Imepita hiyo!” nilisema nikimtazama Zainabu. Kisha nikaondoka, sikusubiri jibu lake.

* * *



Saa 9:16 alasiri…

Baada ya mizunguko yangu niliingia ndani kwa Almasi majira ya alasiri nikamkuta akiwa ameketi kwenye kochi kubwa akiwa mwenye mawazo mengi, mkononi alikuwa ameshika chupa ndogo ya Konyagi na wakati huo redio ilikuwa imewashwa. Si kwamba alikuwa anasikiliza redio hiyo bali ilionekana kama vile ilikuwa inampa tu ‘kampani’ wakati akinywa Konyagi taratibu.

Aliponiona alitikisa kichwa chake na kunywa fundo moja la Konyagi na kusema, “Ulikuwa wapi Mgeni, mbona sijakuona tangu asubuhi?” Kisha alitazama chini kama mtu aliyekuwa anatafuta jambo.

“Ah, mambo mengi ila muda mchache… si unajua kunapokucha na mambo mapya yanaibuka!” nilisema na kuketi kwenye kochi huku nikimtazama kwa huzuni.

Hakika Almasi hakuwa sawa kiakili na alihitaji msaada wa haraka wa kisaikolojia. Kwa jinsi alivyoonekana tu isingekuwa tabu kujua kuwa alikuwa ameumizwa sana na tukio la kusalitiwa na Sofia. Kwa jinsi alivyokuwa amekaa usingeshindwa kubaini kuwa, mwili wake ulikuwa unapumzika lakini kichwa chake kilikuwa kinachemka.

“Dah! Sikuwahi kuwaza kama yatafikia hapa,” nilijikuta nikisema kwa huzuni. Almasi alinitazama tu pasipo kusema neno.

* * *

Endelea...
 
Mgeni mwema.jpg

172

Hunikumbuki?




Saa 9:00 usiku…

KIZA kilikuwa kimechukua nafasi yake na nyota hafifu zilianza kujitokeza moja baada ya nyingine. Nilikuwa nimesimama kando ya reli nikiwa safarini lakini sikujua nilikuwa natoka wapi wala naelekea wapi! nilisimama pale huku nikiitizama mbingu jinsi ilivyotandazika, na katika utulivu juu kule, niliziona sayari zikihangaika na kutapatapa.

Kisha nilitupa macho yangu kutazama huku na kule kuyastaajabia mazingira yale kwenye nchi ya kigeni ambayo sikuijua na wala sikujua nilifikaje hapo, ila nilichokumbuka ni kwamba nilikuwa nimekimbia mbio kutoka kusikojulikana. Hata pale nilipojitahidi sana kukumbuka jina la mahala nilipotoka ilishindikana kukumbuka jina hilo.

Hii ilikuwa baada ya kushuhudia gari la kifahari aina ya Toyota Lexus RX Hybrid la rangi ya maruni likiwa limeharibika vibaya baada ya ajali. Kila nilipojaribu kukumbuka sikuweza kukumbuka ilikuwaje lakini nilifahamu kuwa gari lile lilikuwa limegongana na lori la mafuta. Mimi nilishtukia tu kuona tayari ajali ikiwa imetokea na moto ukilipuka, maumivu makali yalikuwa yakiutesa moyo wangu.

Nikajaribu kutafakari lakini nikahisi kama vile akili yangu haikuwa ikifanya kazi sawasawa, hasa pale nilipotaka kukumbuka hata jina langu lakini nikashindwa. Sikukumbuka kitu chochote, nilikuwa katika hali ya tabu sana, kila kitu pale nilipokuwa nimesimama kilikuwa kipya kabisa!

Sikufahamu chochote katika eneo lile. Sikukumbuka nilipokuwa wala nilifikaje! Sikufahamu chochote kuhusu ulimwengu. Kila kitu kilikuwa ni giza ndani ya maisha yangu, sikutamani kuishi wala kufa kwa sababu sikujua nini maana ya kuishi na nini faida ya kufa!

Eneo nililokuwa nimesimama lilikuwa pana na tambarare katika nchi iliyokuwa kama jangwa. Eneo hilo lilikuwa na miti michache mikubwa aina ya mibuyu na vichaka vidogo vidogo, kwa mbali niliweza kuiona milima.

Kwa kitambo kirefu nilisimama hapo lakini sikuona chombo chochote cha usafiri. Pia sikuona binadamu yeyote aliyepita eneo lile. Hatimaye nilijikuta nikichoka kusubiri na kuondoka, nikatembea taratibu kutoka eneo lile ingawa sikujua nilikuwa nakwenda wapi. Niliifuata ile reli, nikaelekea upande wa Mashariki.

Wakati natembea niliwaona ndege wengi wa aina mbalimbali waliokuwa wakiruka huko na huko, na walisikika wakiimba nyimbo za huzuni. Nilijaribu kuzisikiliza vizuri sauti zao na kugundua kuwa ziliashiria uwepo wa hali fulani ya huzuni, na hapo nikajikuta nikizitafakari zaidi nyimbo za wale ndege kwa kitambo kidogo.

Kuna muda nilisimama nikasikiliza kwa umakini, lakini baadaye niliwadharau na kuendelea na safari yangu. Hawakunisumbua! Baada ya mwendo wa kama saa moja na nusu hivi, nikaanza kuzisikia sauti za mbweha kutokea mbali zikiwa zinaelekea kule nilikokuwa natokea.

Na muda si mrefu nililiona kundi kubwa la mbweha likipita mbele yangu mbio huku likifukuzwa na kundi kubwa la sokwe. Kila sokwe alikuwa ameshika fimbo mkononi mwake.

Niliyatazama yale makundi ya wanyama na kujiambia nafsini mwangu kuwa huenda kulikuwa na vita kali kati ya makundi yale mawili ya wanyama. Hata hivyo, sikuyajali. Niliyadharau nikabana taya zangu na kuuma meno kisha nikaendelea na hamsini zangu ingawa makundi yale ya wanyama yalikuwa yakinitazama sana kwa namna ya ajabu.

Bado sikujua nilikuwa naelekea wapi lakini nilizidi kwenda mbele mahali nisikokufahamu, na baada ya mwendo wa dakika kumi na tano nikakutana na kundi kubwa la fisi walioonesha ukali na kuhaha, waliachia midomo yao wazi tayari kwa mapambano dhidi yangu. Wale fisi walionesha kutaabika sana kama vile mbwa wenye kichaa.

Niliingiwa na hofu kubwa lakini sikujua ningewezaje kujiokoa na wale wanyama waliokuwa wakinitazama kwa uchu mkubwa. Wale fisi walinisogelea taratibu na kuanza kunizunguka huku wakinicheka kwa namna ambayo sikuweza kuifahamu. Walinizunguka na kuniweka katikati huku wakiendelea kunicheka. Nilisimama nikiwatazama kwa wasiwasi, sikujua walitaka kunifanya nini.

Nikiwa bado nashangaa, nikajikuta nikizabwa kibao na mtu ambaye sikumwona. Niliangaza macho yangu kila upande lakini nisiweze kuona kitu chochote wala mtu yeyote isipokuwa wale fisi tu waliokuwa wamechutama huku wakinicheka kwa sauti kubwa iliyotisha.

Kutahamaki nikajikuta nikizabwa kofi la pili lililonifanya nianze kuona vimulimuli machoni, na hapo kengele ya hatari ilianza kulia akilini mwangu, nikahisi kizunguzungu kilichofuatiwa na kuanguka chini.

Niliinuka na kuangaza macho yangu huku na kule lakini sikuweza kuona chochote isipokuwa wale fisi waliokuwa bado wamechutama wakinicheka. Sikutaka kuendelea kuzubaa pale, nikatimua mbio kwa kasi ya ajabu nikiwaacha wale fisi bado wamechutama wakiendelea kucheka kwa sauti.

Baada ya mwendo mrefu huku nikianza kukata tamaa, nikaiona nyumba moja kubwa, kwa mbali, ikiwa imejitenga peke yake kwenye ile nchi ya kigeni. Nyumba ile ilikuwa kiasi cha umbali wa nusu kilometa mbele yangu.

Ilikuwa nyumba nzuri na kubwa ya kifahari iliyokuwa imezungukwa na miti mizuri ya vivuli na sehemu za wazi zenye bustani nzuri ya maua na nyasi za kijani kibichi zilizokatwa vizuri.

Niliisogelea ile nyumba na kugundua kuwa ukuta wake kuizunguka ile nyumba ulikuwa mfupi na wenye nakshi za hapa na pale kiasi cha kumruhusu mtembea kwa miguu kuweza kuona mle ndani japo kwa shida kidogo. Hata hivyo, taa zote za ile nyumba zilikuwa zimezimwa na hivyo kuyafanya mandhari yake mazuri kutawaliwa na kiza.

Nilipoifikia ile nyumba nikapunguza mwendo na kuanza kutembea kwa tahadhari, mara kwa mara niligeuka nyuma na kutazama kama kulikuwa na hatari yoyote ikinifuata. Hakukuwa na hatari yoyote nyuma yangu na hali ilikuwa shwari kabisa, hivyo nilizidi kufarijika.

Hatimaye nikawa nimelifikia geti kubwa jeusi la ile nyumba, hata hivyo, nilisimama na kushawishika kubonyeza kitufe cha kengele kilichokuwa pembeni ya lile geti lililokuwa mbele ya ile nyumba lakini hali ilikuwa ya ukimya mno na kunifanya niahirishe kwanza mpango wangu.

Niliyatembeza macho yangu katika namna ya kujiridhisha na hali ya usalama wa eneo zima. Hali ilikuwa bado shwari kabisa na sikuweza kuhisi kitu chochote cha hatari katika eneo lile na hata eneo la jirani.

Kwa tahadhari niliusogelea mlango mdogo wa lile geti, nilipoufikia nikakishika kitasa na kuusukuma ndani ule mlango taratibu kwa tahadhari ya hali ya juu. Kumbe ule mlango ulikuwa wazi tofauti kabisa na matarajio yangu, hali ile ilinishangaza sana.

Nilisita kuingia lakini nilipowafikiria wale fisi sikutaka tena kurudi nyuma, hivyo niliusukuma ule mlango taratibu katika namna ya kuuzuia usipige kelele na kumshtua mtu yeyote ambaye angekuwemo mle ndani.

Mlango ulifunguka kabisa na kuniruhusu kuingia ndani, nikaingia kwa tahadhari na kuurudishia vyema nyuma yangu. Kabla ya kufanya mjongeo mwingine wowote nilitulia kwanza pale getini kwa kitambo kirefu huku nikiyatembeza macho yangu kutazama huku na kule nikijaribu kuyapeleleza mandhari ya ile nyumba.

Ilikuwa ni nyumba kubwa ya kisasa ya ghorofa moja iliyokuwa na madirisha makubwa ya kisasa ya vioo na baraza kubwa mbele yake.

Endelea...
 
Mgeni mwema.jpg

173

Nje ya nyumba ile upande wa kulia kulikuwa na banda la wazi la kuegeshea magari na nilipochunguza nikaona kulikuwa na gari la kifahari aina ya Toyota Landcruiser GX V8 la rangi nyeusi. Sehemu nyingine ya mandhari ya nyumba ile ilizungukwa na miti ya kivuli ambayo matawi yake yalitengeneza vichaka vilivyosababisha kiza fulani.

Nilisimama pale kwa tahadhari nikiendelea kuitazama ile miti kwa utulivu huku hisia zangu zikinieleza kuwa mtu yeyote mwenye hila angeweza kujibanza nyuma ya miti ile na kuitimiza nia yake mbaya.

Sehemu ya mbele ya ile nyumba ilikuwa imezungukwa na bustani nzuri ya maua ya kupendeza yaliyotoa harufu nzuri na katikati ya bustani ile kulitengenezwa njia nzuri ya kutembea kwa miguu kwa vitofali vidogo vilivyokuwa vinavutia.

Kwa sekunde kadhaa niliendelea kusimama pale getini huku nikiupisha utulivu kichwani mwangu, kwani ukimya ule katika nyumba hiyo uliongeza ziada nyingine katika hisia zangu, kwamba mle ndani ya ile nyumba hapakuwa na kiumbe hai yeyote.

Lakini pia utulivu wa mahali pale ulinifanya nihisi kuwa hali hiyo ingeweza kutumiwa vizuri na adui mwenye hila katika kutimiza nia yake.

Nilipofikiria kuhusu yale makundi ya mbweha, sokwe na hata fisi sikutaka kurudi nyuma, nilipiga moyo konde na kuondoka pale getini. Nikapiga hatua taratibu nikiisogelea ile nyumba, niliambaa ambaa upande wa kushoto wa lile geti sehemu kulipokuwa na kibanda cha mlinzi.

Jambo lililonishangaza ni kuwa mlango wa kile kibanda ulikuwa wazi ingawa hakukuonesha dalili yoyote ya kuwa na mtu mle ndani. Kwa tahadhari nikasogea karibu zaidi na kile kibanda na kuanza kuchunguza mle ndani. Ni kweli hapakuwa na dalili zozote za uwepo wa kiumbe hai mle ndani.

Nikaanza kutembea tena kwa tahadhari kuielekea ile nyumba huku nikiyazungusha macho yangu lakini sikuona chochote kilichonitia shaka. Nikashusha pumzi taratibu za ndani kwa ndani na kumeza funda kubwa la mate kulitowesha koo langu lililokauka kwa hofu.

Hali ya kutokuwepo kiumbe hai ikazidi kunishangaza sana, niliifuata baraza kubwa mbele ya ile nyumba na kusimama pale kwa muda huku nikishusha pumzi za ndani kwa ndani na kusikilizia kama kulikuwa na sauti yoyote iliyoashiria uwepo wa kiumbe hai mle ndani, lakini kulikuwa kimya sana.

Niliuma midomo yangu baada ya kuona hali ilikuwa bado shwari na hakukuwa na dalili zozote za uwepo wa kiumbe hai.

Nikashusha tena pumzi ndefu za ndani kwa ndani na kushika kitasa cha mlango, nikakinyonga na kuusukuma ule mlango, ukafunguka. Hali hiyo ikanifanya nisite na kusimama pale kwa kitambo kirefu hadi nilipohakikisha hali bado ni shwari, kisha nikaingia na kujikuta nikitokea kwenye sebule kubwa.

Hapo nilitulia kidogo nikayatembeza macho yangu kwenye lile giza hadi yalipolizoea giza. Kwa taabu niliweza kuona samani mbalimbali zilizotapakaa pale sebuleni.

Kutoka pale nilipokuwa nimesimama nilitazama upande wangu wa kulia na kuuona mlango mkubwa katikati ya madirisha mapana ya vioo yaliyofunikwa kwa mapazia marefu. Moja kwa moja nikatambua kuwa ulikuwa mlango wa kuelekea kwenye vyumba vya kulala vya ile nyumba.

Nyumba ilikuwa kimya kabisa, na mara giza liliongezeka na ukungu ukatanda kila mahali kiasi cha kunifanya niingiwe na hofu kubwa. Niliyakodoa macho yangu kwa hofu huku nikiyatembeza mle ndani kutazama huku na kule, na hapo nikakutana na ukungu wa giza nene machoni kwangu.

Hali ile ikasababisha jasho jepesi lianze kunitoka sehemu mbalimbali za mwili wangu, kisha mapigo ya moyo wangu yakabadili mwendo wake na kuanza kwenda mbio isivyo kawaida!

Mara nikaanza kusikia sauti za ajabu ajabu sana zisizoelezeka ambazo zilikuwa zinasikika kwa fujo pasipo mpangilio kutoka katika kila pembe ya ile sebule na kugeuka kero kubwa masikioni mwangu.

Sikuwa na namna nyingine ya kufanya, nikaamua kujipa ujasiri na hali ile ikanifanya niyatulize vizuri mawazo yangu huku nikijaribu kutafakari vizuri namna ya kujitoa pale. Swali kubwa lililonijia kichwani kwangu kwa wakati huo ni je, pale nilikuwa wapi na wenye ile nyumba ni akina nani? Sikupata jibu la haraka.

Katika kutafakari, mara nikaona mwanga mkali ukiwaka kutoka kwenye taa mbili ndogo zilizokuwa zikining’inia hewani bila kushikiliwa na kitu chochote. Cha ajabu sikuweza kumwona mtu aliyeziwasha zile taa.

Ule mwanga wa zile taa ulinistaajabisha sana kwani ulikuwa ukibadilika badilika rangi na kuwa kama taa za usalama barabarani zinazotumika kuongozea magari. Nikiwa bado nashangaa, mara zile taa zikageuka kuwa mwanga mkali sana na kunichoma machoni nisiweze kuona mbele. Kisha ule mwanga ukaanza kunisogelea karibu zaidi na kunitia hofu kubwa sana.

Mara ukapotea, kukawa na giza nene lililonifanya nisiweze hata kuona nilipokuwa nimesimama. Nikiwa sijui nifanye nini, sasa ukajitokeza mwanga wa kawaida kama wa jua na kuniwezesha kuona vizuri mle ndani.

Nikashangaa sana kuona picha mbili kubwa zilizokuwa zimetundikwa ukutani ambazo sikuwa nimeziona kabla. Picha moja ilionesha ajali ya magari mawili yaliyogongana. Gari moja lilikuwa Lori lenye tangi la mafuta na gari jingine lilikuwa la kifahari aina ya Toyota Lexus RX Hybrid la rangi ya maruni. Wakati nikiiangalia picha hiyo akili yangu ikawa inaniambia kuwa niliwahi kuishuhudia ajali hiyo sehemu fulani. Ila sikukumbuka ni wapi!

Picha ya pili iliwaonesha vijana wawili walioonekana kama mume na mke waliotoka kwenye fungate baada ya harusi yao. Kijana wa kiume alikuwa mtanashati ambaye mwonekano wake ulionesha alikuwa na umri wa miaka therathini na akiwa amemkumbatia kwa mahaba msichana mwenye uzuri usiomithilika ambaye hakuzidi miaka ishirini na sita.

Nilivutiwa sana kuiangalia hiyo picha ya pili, nikaisogelea na kuitazama kwa umakini zaidi. Sura za maharusi hao hazikuwa ngeni machoni kwangu. Nilihisi kuwafahamu lakini sikuyajua majina yao wala sehemu niliyowaona!

Nilibaki kujiambia moyoni kuwa niliwafahamu wale watu na nikajaribu sana kuvuta kumbukumbu pengine ningekumbuka niliwaona wapi na lini lakini sikuweza kupata jibu. Ili kujiridhisha nikanyoosha mkono wangu nikitaka kuitungua ile picha toka pale ukutani. Kabla sijaigusa nikasikia sauti ya nyayo za mtu nyuma yangu zilizosogea taratibu.

Niligeuka haraka na hapo nikamwona mwanamke wa makamo ambaye kiumri hakuwa chini ya miaka arobaini na tano, aliyekuwa kajiweka mapambo mbalimbali ya gharama mwilini kwake. Alikuwa ananisogelea huku akiwa amenikazia macho. Nilimtazama kwa umakini nikijaribu kukumbuka kama niliwahi kumwona popote lakini sikuweza kupata jibu.

Mwanamke huyo alikuwa mnene wa wastani, mng’avu kwa rangi ya ngozi yake na mwenye haiba ya kuvutia ingawa alionekana kuwa na umri mkubwa. Alikuwa mrefu wa wastani aliyejiweka vipodozi vilivyokolea vyema kwenye mwili wake na kumfanya aonekane mrembo hasa, ingawa nilihisi kuwa ukweli wa urembo wake ulitokana na vipodozi, ndiyo sababu alijikwatua.

Macho yake yalikuwa makali na yaliganda kwenye uso wangu yakinitazama bila kufumba. Nilibaki kimya nikimstaajabia yule mwanamke. Alipofika umbali wa takriban hatua tatu kutoka nilipokuwa nimesimama nikamwona akisimama na kugeuza shingo yake kutazama kushoto kwake kisha akaachia tabasamu.

Nami nikageuza shingo yangu kutazama upande huo na hapo nikajikuta nikipatwa na mshangao mkubwa zaidi. Nilikiona kioo kirefu cha kujitazama kilichokuwa ukutani ambacho sikuwa nimekiona mwanzo nilipoingia mle ndani.

Endelea...
 
Mgeni mwema.jpg

174

Yule mama alijiangalia kwa mbwembwe kwenye kile kioo, alijipinda akajiangalia upande wa kulia wa umbo lake na kufanya hivyo tena akijiangalia upande wa kushoto. Kisha alinyooka wima akajiangalia kuanzia usawa wa kitovu mpaka chini kidogo ya magoti na kuachia tabasamu.

Alionesha kuridhishwa na vipodozi vilivyokuwa vimekoleza vyema mwili wake na kumfanya aonekane mrembo hasa. Kisha aliitazama sura yake na kuonekana kuridhika kuwa alikuwa na urembo simulizi. Yote haya niliyasoma kwenye macho yake.

“Mgeni, bila shaka uko tayari tuishi wote, au sivyo?” yule mwanamke aliniuliza na kuachia kicheko hafifu baada ya kuridhika na mwonekano wake.

“Mgeni?” Nilijiuliza mwenyewe kimya kimya. “Kumbe naitwa Mgeni?” Sasa nililikumbuka vyema jina langu, na hapo nikashangaa sana. Sikujua yule mwanamke alilijuaje jina langu.

“Kwani wewe ni nani?” nilimuuliza yule mwanamke huku nikimtazama usoni, hakika sura yake ilikuwa ngeni kabisa machoni kwangu, sikumjua kabisa. Hata kama sikuwa na kumbukumbu lakini niliamini kuwa sikuwahi kumwona hata siku moja.

“Usiwe na wasiwasi, utanifahamu baada ya muda kidogo,” yule mwanamke aliniambia huku akisogea karibu yangu na kunikumbatia kwa nguvu huku akicheka kwa furaha. Nilishindwa kufanya chochote nikabaki kushangaa.

“Hallo!” mara nikasikia sauti nyingine ikitokea upande fulani ndani ya ile nyumba.

Sote tuligeuka kutazama upande ilikotokea ile sauti huku yule mwanamke akiniachia haraka. Na hapo nikamwona msichana mrembo akitujia kwa mwendo wa taratibu huku akinitazama usoni kwa huzuni kubwa, alikuwa anatokwa na machozi. Alikuwa msichana mzuri haswa mwenye macho mazuri na malegevu yaliyokuwa yakilengwalengwa na machozi huku yakinitazama kwa upendo.

Alikuwa na ule uzuri usiomithilika uwezao kumliwaza, kumpumbaza na hata kumlaza kitandani mwanamume yeyote aliye buheri wa afya. Alikuwa amevaa gauni refu lililochanganywa rangi nyeupe na maruni likiwa na ‘lace’ za kuvutia huku zikiwa na mwonekano wa kupendeza sana na nyuma lilijitandaza kama mkia wa tausi! Gauni lile lilishindwa kulificha tumbo lake lenye ujauzito.

Kichwani alikuwa amevaa kofia nzuri ya kimalkia iliyozifunika nywele zake ndefu na laini na miguuni alivaa viatu vya rangi ya maruni vya mchuchumio vyenye visigino virefu. Ukichanganya na urefu wake alionekana kama malaika aliyeshushwa duniani kimakosa!

Nilimtazama yule mwanadada kwa umakini, sura yake haikuwa ngeni kabisa machoni kwangu. Nilihisi kumfahamu vyema kwa sura na hata kwa jina lake, ingawa sikujua nilimwona wapi!

Wakati nikiendelea kumtazama kwa udadisi nikahisi jambo na kugeuza shingo yangu kuitazama ile picha ya wanandoa iliyotundikwa pale ukutani. Naam! Alikuwa ni yule mwanadada aliyekuwa kwenye hiyo picha.

Cha ajabu, muda huo huo nikajikuta nikiwa nimevaa suti ghali ya vipande vitatu ya rangi ya kijivu ya single button, kwa ndani nilivaa shati zuri la rangi ya samawati la mikono mirefu na tai nyekundu shingoni. Chini nilivaa viatu vyeusi vya ngozi. Nikashangaa sana!

Niligeuza tena shingo yangu kumtazama yule msichana ambaye alizidi kunisogelea huku akilia. Macho yake yaliendelea kunitazama kwa tuo yakiganda kwenye uso wangu bila kufumba. Nikabaki kimya nikiustaajabia uzuri wa yule mwanamke. Hata hivyo kilichonistaajabisha zaidi si kingine bali mwendo wake wakati alipokuwa akizidi kunisogelea.

Alipofika umbali wa kama hatua tatu kutoka nilipokuwa nimesimama, alisimama kisha akafuta machozi.

“Jason, namshukuru sana Mungu uko hai…” yule msichana alisema.

Nilijikuta nikishangaa sana kusikia sauti nzuri ya kuridhisha masikioni ikitoka kinywani mwa yule msichana. Niliendelea kumtazama kwa umakini huku nikijaribu kukumbuka ni wapi niliisikia sauti hiyo au kumwona maana sura yake haikuwa ngeni kabisa machoni kwangu. Ilijaa machoni!

Yule mwanamke wa makamo aliyefika kwanza akaongea kwa hasira huku akitaka kunishika mkono kwa nguvu lakini nikajisogeza kando ili kumkwepa. “Huyu haitwi Jason, anaitwa Mgeni!”

Nikazidi kustaajabu huku nikimtazama kwa umakini yule msichana mrembo. Sikujua yeye alilitoa wapi jina la Jason! Alinitazama kwa muda kisha aliangalia pembeni kana kwamba alikuwa akifuta machozi kwa siri.

“Kwa nini unalia?” nilimuuliza huku nikimsogelea na kumgeuza ili aniangalie.

“Silii ila nina furaha kubwa kwa kuwa leo nimekuona tena ukiwa hai,” aliniambia na kushusha pumzi ndefu.

Niligeuka kumtazama yule mwanamke wa makamo, nikamwona akiwa amenuna huku akimtazama yule msichana kwa jicho la chuki. Sasa kichwa changu kilijaa maswali mengi sana lakini sikujua namna ya kuyauliza, na nani nimuulize kati ya wale wanawake wawili waliokuwa mbele yangu. Kila kitu pale kilikuwa ni michoro kwangu isiyoashiria chochote, nilikuwa nimevurugwa akili na kila kitu kabisa.

Sikujua nani ni nani pale; sikujua yule mwanamke wa makamo ni nani kwangu wala yule msichana ni nani! Kilichonichanganywa zaidi ni kitendo cha yule msichana kusema kuwa amefurahi kuniona tena nikiwa hai. Hivi kauli yake ilimaanisha kuwa nilikuwa nimekufa? Na kwa nini kuniona tena nikiwa hai kumfanye atokwe na machozi? Halafu… kwa nini yule mwanamke mwingine achukie badala ya kuonesha furaha? Nani alikuwa nani kwangu? Na nilikuwa na thamani gani kwao?

Maswali hayo yalinifanya kuwa na jakamoyo ndani ya moyo wangu. Nilihisi nimekuwa kama teja lililokuwa likihudhuria kliniki ya ukichaa.

“Mbona sielewi chochote! Mmoja ananiita Mgeni na mwingine ananiita Jason! Mnaweza kunieleza ninyi ni akina nani na hapa nipo wapi?” hatimaye niliwauliza wale wanawake huku nikihisi machozi yakinitoka baada ya kujitahidi sana kukumbuka lakini ikashindikana.

Kwanza yule msichana mrembo aliachia tabasamu kisha tabasamu hilo likamezwa na uso uliojaa huzuni, machozi yakazidi kumtoka machoni.

“Vipi kwani?” nilimwuliza yule msichana mrembo kwa mshangao.

“Inamaana hunikumbuki?” yule msichana aliniuliza huku akiendelea kutokwa na machozi. Sikuweza kuelewa.

“Nitakukumbuka vipi wakati leo ndo nakuona?” nilimjibu kwa mshangao huku nikimtazama usoni.

Yule msichana alitaka kusema neno lakini akasita na kuangua kilio. Kilikuwa kilio cha kwikwi kilichobeba uchungu mkubwa ndani yake. Nikazidi kushangaa. Maswali lukuki kuhusu yule msichana yakaanza kupita kichwani kwangu, maswali ambayo sikuweza kuyapatia majibu sahihi: Yeye ni nani hasa? Nilimwona wapi? Alikuja pale kufanya nini?

Ni kama vile yule msichana alikuwa akiyasoma mwazo yangu nikamwona akiaachia mguno na kutingisha kichwa chake kwa masikitiko.

“Sijui kwa nini unahangaika kujiuliza maswali mengi kuhusu mimi…” yule msichana alisema kwa huzuni na kufuta machozi yaliyokuwa yakimtoka. Kisha akaongeza “Mimi ni mkeo…”

Endelea...
 
Mgeni mwema.jpg

175

Kabla hajamalizia kikakisika kicheko kikubwa cha kishambenga kilichotengeneza mwangwi ndani ya ile sebule na kumkatisha yule msichana. Kilikuwa kicheko cha yule mwanamke wa makamo.

“Usimsikilize huyo msichana, ni mwongo mkubwa na mnafiki,” yule mwanamke aliniambia kisha akamgeukia yule msichana, “Najua kuwa upo hapa kumtafuta mumeo lakini si huyu.”

Aliyasema hayo kisha akaachia tena kicheko. “Najua nia yako…” alisema tena yule mwanamke huku akizidi kumkazia macho yule msichana.

Yule msichana hakusema neno bali aliendelea kumtazama yule mwanamke kwa umakini zaidi. Kitambo kifupi cha ukimya kilipita huku wakitazamana.

“Najua wewe ni msichana mwema wa wema, binti mrembo, mcheshi, mkarimu na mwenye upendo wa dhati si tu kwa mumeo bali kwa watu wote lakini…” yule mwanamke alisita kisha alishusha pumzi, akaachia tabasamu na kuyahamisha macho yake kutoka kwenye uso wa yule msichana hadi kwenye uso wangu. Akanitazama kwa muda kisha akayahamisha tena macho yake na kutazama kando huku akiendelea kutabasamu.

Hata hivyo, tabasamu lake lilikuwa limeficha kitu fulani ndani yake. Halikuwa tabasamu la kawaida wala la furaha bali lilikuwa tabasamu la uchungu na lililoficha chuki na ghadhabu ndani yake.

Nilipojaribu kuyasoma mawazo yake niligundua kuwa tabasamu lake lilikuwa la kuulaani na kuukashifu umri wake mwenyewe, huku likiutukana ujana na urembo wa yule msichana. Na mara akasonya na kutema upepo wa dharau.

Yule msichana aliendelea kuwa mkimya tu akimtazama kwa mshangao yule mwanamke. Wakatazamana kwa kitambo bila kusema lolote. Yule mwanamke alionesha wazi roho ya chuki dhidi ya yule msichana, chuki iliyoonekana wazi machoni kwake.

Mithili ya samaki aliyetiwa limau kikaangoni, macho ya yule mwanamke yalitoka pima, uso wake ulianza kupoteza ile rangi yake ya kawaida na kuwa na wekundu ulioiviana na damu. Sasa niligundua kuwa alianza kutawaliwa na hasira.

Yule msichana alimtazama kwa hofu, na pengine moyo wake ulianza kwenda kasi isivyo kawaida maana alihisi hatari. Nikamwona akitazama huku na kule katika namna ya kujiandaa kutoka mbio, lakini yule mwanamke alionekana kuyasoma mawazo yake, akawahi kusimama mlangoni, kwenye mlango wa kutokea, kabla yule msichana hajafanya chochote.

Hivyo, yule msichana aliamua kukimbilia kule kwenye mlango wa sebule ile uliokuwa katikati ya madirisha mapana ya vioo yaliyofunikwa kwa mapazia marefu. Alipoufikia mlango huo aliupiga kumbo na kuingia ndani. Yule mwanamke alimfuata yule msichana huku akitembea kwa kishindo.

Nilijikuta nikiwafuata kule walikoelekea, nikapita kwenye ule mlango mkubwa wa sebuleni na kujikuta nikitokea kwenye korido fupi, kushoto kwangu nikaziona ngazi za kuelekea juu ya ghorofa. Na hapo nikazikwea haraka na kuelekea kwenye vyumba ambavyo niliamini kuwa ni vya kulala.

Nilipokifikia chumba cha kwanza cha upande wa kushoto, nikahisi wangekuwa wameingia humo, nikaingia. Na kweli nilimkuta yule msichana akiwa amejikunyata kwenye pembe moja ya chumba akitetemeka. Wakati huo yule mwanamke alikuwa ameshika kisu kikubwa cha kukatia mboga akikinoa sakafuni huku akioneka mwenye haraka na maya.

Moyo wangu ukaanza kugonga kwa nguvu na kasi mfano wa saa kubwa ya Jamatini. Nilimshuhudia yule mwanamke akitamka kwa sauti kali maneno ambayo sikujua ni lugha gani. Muda mfupi uliofuata, wanaume wawili, shababi kweli kweli, waliingia mle chumbani. Kufumba na kufumbua yule msichana alikamatwa na kufungwa kamba madhubuti kisha akawekwa mbele ya yule mwanamke. Halafu wale wanaume wakaondoka haraka kama walivyokuja, pasipo kunitazama.

Yule mwanamke alikishika vyema kile kisu na kumsogelea yule msichana, aliliangalia kwa hasira tumbo la yule msichana lililobeba ujauzito, akakielekeza kisu chake kwenye lile tumbo akitaka kumchoma nacho tumboni. Sasa yule msichana akawa analia kwa uchungu mkubwa huku akimsihi asimuue.

Yule mwanamke alionekana kuchekelea akionekana kuifurahia hali ile, alimtazama yule msichana kwa dharau na kusonya, kisha aligeuka kunitazama kabla ya kuyarudisha macho yake kwa yule msichana. Kisha aliinua kisu chake juu akiwa tayari kukikita juu ya tumbo.

Sikuweza tena kuvumilia, nilimrukia yule mwanamke wakati akikishusha kile kisu, nikampiga kikumbo na sote tukapiga mweleka chini, na mara mwanga mkali kama wa umeme ukapenya mle chumbani huku ukiambatana na sauti kali ya risasi, huenda ilikuwa imepenya dirishani. Sauti ile ilivuma mle ndani na kukaribia kupasua ngoma za masikio yangu. Nikakurupuka…

_____

Nilishtuka kutoka usingizini huku nikitweta na kugundua kuwa nilikuwa nimelala chumbani. Pembeni yangu alilala Zainabu na mtoto Mariam alikuwa amelala ukutani akikoroma. Nje ya nyumba mvua iliyoambatana na ngurumo kali za radi ilikuwa inanyesha.

Dah! Hakika ilikuwa ndoto ya ajabu kuhusu nchi ya ajabu na wanawake wa ajabu! Nilishusha pumzi za ndani kwa ndani huku mwili wangu ukitetemeka.

Niliitupia jicho saa ndogo iliyokuwa juu ya meza ndogo na kushtuka, ilikuwa imetimia saa tisa usiku. Baada ya hapo usingizi ulinipaa, kila nilipojaribu kuutafuta usingizi sikuupata. Sasa usiku huo ukawa mrefu kwangu kuliko kawaida. Ndoto hiyo ilinifanya nisipate tena usingizi! Ilikuwa ndoto ya ajabu sana na sikujua kama ilikuwa ni ndoto tu ya kawaida ama yalikuwa maono!

Kuanzia hapo sikuweza kupata usingizi, usiku kucha nilikuwa nahangaika kitandani kwangu kujaribu kutafuta usingizi bila mafanikio. Niliwaza hili na lile, nikajiuliza maswali mengi lakini sikuweza kupata majibu. Kila nilipoifikiria ile ndoto nilijikuta nahisi kuanza kupata wazimu.

Adhana zote mbili za alfajiri zilinikuta nikiwa macho nahangaika kitandani, tangu ile adhana ya kwanza ambapo mwadhini alikuwa anasema “Swala ni bora kuliko kulala…” na hata ile ya pili iliyotolewa kuwajulisha Waislamu kuwa wakati umefika ili wahudhurie kuswali.

Nilimtazama Zainabu, hakuwa na habari kabisa ya kile kilichokuwa kinaendelea kichwani kwangu, alikuwa anauchapa usingizi akiwa amekilaza kichwa chake kifuani kwangu. Mguu wake mmoja ulikuwa katikati ya mapaja yangu huku mkono wake mmoja alikuwa ameuzungusha shingoni kwangu na alikuwa anakoroma kwa sauti hafifu ya uchovu. Nilimtazama kwa umakini nikaachia tabasamu…

Kisha sikuweza kufahamu ni wakati gani usingizi mzito ulinichukua hadi pale niliposhtushwa majira ya saa tatu asubuhi baada ya kusikia sauti kwa mbali ikiniita, “Mgeni!”

Nilifungua macho yangu kiusingizi na kumtazama Zainabu ambaye alikuwa amesimama akinitazama kwa mshangao uliochanganyika na wasiwasi. Ilikuwa asubuhi tulivu mno yenye manyunyu hafifu ya mvua yaliyokuwa yanaanguka juu ya paa.

“Vipi Zai?” nilimuuliza huku nikimtazama kwa umakini.

“Vipi mwenzangu, mbona umelala hadi saa hizi? Leo hata mazoezi hujafanya!” Zainabu aliniuliza kwa mshangao huku akinitazama kwa umakini.

“Najihisi vibaya,” nilisema huku nikipiga miayo ya uchovu. “Leo nimeota ndoto ya ajabu sana, na baada ya ndoto hiyo sikupata kulala kabisa hadi alfajiri!”

Zainabu akataka kujua kuhusu ndoto niliyoota, nikamsimulia. Lakini cha ajabu sikulikumbuka lile jina nililoitwa na yule msichana mrembo! Hata pale nilipojitahidi kuvuta kumbukumbu bado sikulikumbuka!

Zainabu alinitazama kwa kitambo pasipo kusema neno, alionekana kushtuka kidogo na kuwa mnyonge, kisha aliniambia niamke nikaoge tunywe chai. Halafu akatoka na kuniacha.

Nilitoka nikamkuta Zainabu akiwa ameketi kwenye meza sebuleni akiwa mkimya sana, alikuwa ananisubiri nikaoge ili tunywe chai. Mtoto Mariam alikuwa ameshaondoka kwenda shule maana tulikuwa tumemwanzisha shule ya chekechea.

“Mbona umekaa tu, anza kunywa chai,” nilimwambia Zainabu lakini akatingisha kichwa.

“Usijali, nitakusubiri,” alinijibu akinitazama kama mama amtazamavyo mwanawe mpendwa.

Nilikwenda bafuni nikajimwagia maji na nilipotoka nilikwenda moja kwa moja kuketi naye. Tukatazamana na kuachia tabasamu, na kwa namna moja ama nyingine niliamini kwamba kila mmoja wetu alikuwa na matumaini juu ya siku za usoni.

Tulikunywa chai kimya kimya, macho ya Zainabu yalikuwa yananitazama kiwizi wizi na muda wote alionekana kutokukifurahia kile chakula pale mezani. Sikujua alikuwa anawaza nini, huenda ni ile ndoto niliyoota ilianza kumsumbua!

Endelea...
 
Mgeni mwema.jpg

176

Tulipomaliza kula alitoa vyombo kisha akarudi kuketi pale sebuleni, kando yangu huku akinitazama kwa wasiwasi kidogo. Nilimkumbatia na kumlaza kwenye mapaja yangu, akafumba macho. Kwa kitambo fulani sebule ikawa kimya, hakuna aliyekuwa anasema chochote.

Mapenzi raha sana, huwa raha isiyo kifani wakutanapo wawili wanaopendana kwa dhati halafu wasipishane mitazamo katika uwanja huo wa uhusiano wa kimapenzi. Muunganiko kati yangu na Zainabu ulikuwa wa aina yake, Waswahili wangeweza kusema upele ulikuwa umepata wakunaji.

Sasa mikono yangu ilikuwa inatambaa taratibu kwenye mwili wa Zainabu na kumfanya afumbue macho yake na kunitazama. Kisha taratibu akaanza kuyalegeza macho yake huku vidole vyake akivisogeza katika kifua changu, akaanza kunipapasa kifua changu taratibu.

Halafu akainuka na kupanda kwenye mapaja yangu, akanikalia, tukabaki tunatazamana huku mikono yake ikichezea nywele zangu kichwani pamoja na masikio yangu na kuufanya mwili wangu kuanza kusisimka. Kabla hatujaendelea zaidi mara tukasikia sauti ya mtu akigonga mlango taratibu.

Tulitazamana kama tuliokuwa tunaulizana “Nani?” na wakati tukiwa bado tunatazamana mlango ukagongwa tena, safari hii kwa nguvu zaidi. Zainabu alinyanyuka na kwenda mlangoni. Akashika kitasa na kuufungua mlango taratibu kisha akachungulia nje. Kikatokea kitambo fulani cha ukimya huku Zainabu akiwa anatazama huko nje.

“Nzuri, karibu!” sauti ya Zainabu ilipenya vizuri kwenye masikio yangu. Sasa nikawa nasubiria kuisikia sauti ya mtu aliyekuwa akigonga mlango.

“Samahani, sijui nimemkuta Mgeni?” niliisikia sauti ya mwanamke, ambayo nilihisi kuifahamu vyema ingawa sikukumbuka ni ya nani, jambo hilo lilinifanya nishtuke kidogo, mapigo ya moyo wangu yakaanza kwenda kasi.

“Ndiyo yupo…” Zainabu alisema na kugeuka kunitazama kisha akamgeukia tena mgeni aliyekuwepo nje. “Karibu pita ndani.”

Kikatokea tena kitambo kifupi cha ukimya kabla Zainabu hajageuka tena kunitazama, “Mgeni, una mgeni wako.”

Zainabu alisema na kurudi kuketi kwenye kochi na wakati huo huo nikiinuka na kwenda mlangoni kumsikiliza huyo mgeni. Nilishangaa sana kumkuta Sofia akiwa amesimama mlangoni, alikuwa ananitazama kwa wasiwasi, macho yake yalikuwa yamechoka kiasi kama aliyetoka kitandani muda si mrefu.

Niligundua kuwa alikuwa amepungua sana na alionekana kuwa na hisia za huzuni zilizosababisha machozi yamlengelenge machoni. Haraka alitoa kitambaa chake laini na kujifuta machozi.

Sofia alikuwa mrefu, mpana, na begani alitundika mkoba mzuri wa ngozi. Alikuwa amevaa sketi fupi nyeusi yenye miraba myeupe iliyoishia juu kidogo ya magoti yake na hivyo kuifanya miguu yake milaini na minene kidogo kuonekana kwa uzuri. Juu alivaa blauzi ya bluu ya mikono mirefu na viatu vyenye vikanyagio virefu vya mchuchumio. Mkononi alivaa bangili nyingi za pembe.

Japokuwa nilikuwa na hasira kwa sababu Sofia alikuwa amemsababishia maumivu makali Almasi, maumivu ya kimwili na ya kisaikolojia, tena pasipo na huruma lakini nilijikuta nikishangazwa na ujio wake wa ghafla nyumbani kwangu, hata hivyo nilijitahidi sana kuumeza mshangao wangu.

Ulikuwa ugeni ambao sikuwa nimeutarajia kabisa! Hasa baada ya kile kilichotokea kati ya Sofia na Almasi siku chache zilizokuwa zimepita. Kwa sekunde chache nilimtazama Sofia kwa chuki huku nikijiuliza ni kipi kilichokuwa kimemleta nyumbani kwangu.

Muda wote nilikuwa nimeikunja sura yangu jambo lililomfanya Sofia kubabaika sana, alikuwa anatazamana na sura ambayo alizoea kuiona ikitabasamu huku ikitokwa na maneno ya uchangamfu lakini siku hiyo sura hii ilikuwa imekasirika sana. Haikuwa na hata chembe ya furaha wala mzaha.

Kwa kweli nilikuwa nimepandwa na hasira kwa kumwona Sofia pale nyumbani kwangu. Midomo yangu ilianza kunitetemeka kwa hasira. Huyu na hawara yake Bundala ndio waliomuumiza Almasi. Sasa nilitamani kumshushia kipigo kitakatifu lakini nikaona si hekima. Nikaamua nimpe kwanza nafasi ya kumsikiliza nijue alifuata nini asubuhi ile pale nyumbani.

Ni kama alikuwa anayasoma mawazo yangu, Sofia aliniomba msamaha, kwa sauti ya chini iliyokuwa ikibembeleza, kwa yote yaliyotokea kisha alinitaka radhi kwamba alikuwa na maongezi machache na mimi.

Nilimtazama kwa kitambo kisha nikajisogeza kando nikimpisha aingie ndani lakini alionekana kusita sana.

“Kwani una shida gani nami?” nilimuuliza baada ya kuona bado amesimama pale pale kama aliyepigiliwa misumali miguuni.

“Ni kuhusu Almasi…” Sofia alisema akiwa ameangalia chini kuyakwepa macho yangu.

“Kafanya nini?” nilimuuliza nikiwa bado nimemkazia macho.

“Samahani, tunaweza kutafuta sehemu tukaongea?” Sofia alinisihi.

“Ongea hapa hapa. Kuna tatizo gani?” nilimwambia nikiwa nimeyatuliza macho yangu kwenye uso wake. Sofia alionesha kusita sana.

“Nimekuja ninahitaji msaada wako, shemeji,” alisema baada ya kitambo kifupi cha ukimya.

“Msaada gani?” nilimuuliza huku nikimpisha Zainabu aliyekuwa anatoka nje kuendelea na shughuli zake.

“Najua wewe ni rafiki mkubwa wa Almasi…” Sofia alisema kwa sauti tulivu huku akinitazama kwa namna ya mashaka kidogo.

“Kwa hiyo?” nilimuuliza Sofia nikiendelea kumtazama kwa tuo usoni.

“Shemeji, kwanza kabisa nachukua nafasi hii kukuomba wewe msamaha japokuwa nafahamu kwamba si rahisi kunisamehe kwa mambo niliyomfanyia rafiki yako. Nimekuwa sina amani tangu nilipoondoka nyumbani kwa Almasi, na jambo hili limenikondesha mno. Japokuwa inaweza kuwa ngumu kwake kunisamehe lakini naomba kaniombee msamaha… nikiri kwamba nimemuumiza sana, na pia nimemkosea sana,” Sofia alisema na kushusha pumzi ndefu.

“Yaani baada ya maumivu yote uliyomsababishia, leo unataka nikuombee msamaha! Nini kimekufanya utake kurudi kwake?” nilimuuliza kwa hasira huku nikionesha chuki ya waziwazi. Kisha nikaongeza, “Kwanza najua kabisa hujawahi kumpenda Almasi.”

“Naapa kwa Mungu sijawahi kuacha kumpenda, ni vile tu sioni kabisa kama yuko serious na maisha yake mwenyewe,” Sofia alisema huku akinitazama kwa wasiwasi. Sikusema kitu.

“Hata hivyo nilikuwa tayari hata kumkatia bima japo najua kufanya hivyo ni sawa na kucheza kamari,” Sofia aliongeza na kunifanya nishangae kidogo.

“Kumkatia bima! Unamaanisha nini?” nilimuuliza huku nikionesha mshangao wangu waziwazi.

“Kumzalia mtoto!” Sofia alisema huku akiyakwepa macho yangu na kutazama chini kwa aibu.

“Huo uongo wako kamdanganye mtu mwingine si mimi. Kama ungekuwa unampenda kiasi hicho usingemsaliti na mwanamume mwingine?” nilimwambia Sofia huku nikitaka kurudi ndani.

“Ni kweli, shem… nilijikuta nafanya hivyo kwa sababu ya hasira, Almasi alikuwa akinitamkia kuwa mimi si wa muhimu kwake, na kama akiambiwa achague kati bangi na mimi basi atachagua bangi!” Sofia alisema kwa huzuni huku akitokwa na machozi. Kisha akaongeza, “Isitoshe simwoni kama ana dalili yoyote kuhusu mipango yetu ya ndoa kwani tokea aliponivisha pete hadi leo sijajua lengo lake ni lipi!”

Okay, baada ya kukwambia hivyo na wewe ukaamua kuondoka na mwanaume mwingine ukimwacha ana majeraha. Kipi sasa kimekufanya urudi kuomba msamaha?” nilimuuliza Sofia huku nikiendelea kumtazama usoni kwa tuo.

“Pamoja na kuondoka lakini nimegundua kuwa bado nampenda sana, tena kwa dhati. Kuna muda…” alisema na kusita kidogo kisha akashika nywele zake huku akiinamisha uso wake chini “…nilitamani ninywe sumu hasa kila nikikumbuka kuwa labda kweli bangi ni muhimu kwake kuliko mimi,” Sofia alisema na kufuta machozi.

Nilimtazama Sofia huku zile hasira nilizokuwa nazo zikianza kuyeyuka taratibu. Nilifumbua mdomo wangu kutaka kusema lakini Sofia akanikatiza.

“Tafadhali, shem, naomba nisaidie…” Sofia alinisihi kwa sauti ya chini iliyobembeleza huku akitokwa na machozi.

“Sawa… mimi ni balozi wako, nitakwenda kumwambia…” nilimtia moyo na hapo hapo nikamwona akitabasamu. kisha nikaongeza, “Lakini… ni yeye ndiye mwenye uamuzi wa mwisho kama atakusamehe au la!”

Sofia alishusha pumzi ndefu kama aliyemaliza mbio ndefu. Lile tabasamu lililoanza kuchanua usoni kwake likayeyuka ghafla na wasiwasi ukachukua nafasi.

* * *

Endelea kufuatilia...
 
Mgeni mwema.jpg

177

Ulilala wapi?


Saa 10:30 jioni…

“ALMASI, lazima sasa ujifunze kuanza upya mambo yako, lazima ukubali kuwa mambo yametokea na usonge mbele zaidi. Hii ndiyo njia pekee ya kukusaidia kuwa mpya tena kifikra,” nilimwambia Almasi huku nikionesha kuhuzunishwa sana na namna alivyokuwa na mawazo.

Almasi alinitazama kwa kitambo kirefu bila kusema neno, alionekana yupo njia panda na asijue lipi la kufanya, kisha aliachia tabasamu lililojaa uchungu. “Ni kweli ila ni ngumu sana kusahau,” aliniambia kisha akanyanyua chupa ya Savanna na kupiga funda kubwa la pombe huku akiisikilizia wakati ikisafiri kwenye koromeo lake na kutua tumboni.

Ilikuwa jioni tulivu mno yenye manyunyu hafifu ya mvua yaliyoanguka juu ya paa la Colores Pub, baa ya kisasa iliyokuwa katika eneo la Mazinyungu. Mimi na Almasi tulikuwa tumeketi kwenye meza moja iliyokuwa imejitenga kwenye kona moja ya Pub hiyo.

Sehemu ile ilituwezesha kumwona kila aliyepita barabarani. Almasi alikuwa anakunywa Savanna na mimi nilikuwa nakunywa juisi ya passion. Niliamua kutoka na Almasi hadi kwenye pub hiyo ili kumfikishia ujumbe wa Sofia niliyekutana naye asubuhi ya siku hiyo. Tukiwa pale Colores Pub nilisubiri hadi pale Almasi alipokuwa amemaliza chupa mbili za Savanna zilizotosha kuanza kuichangamsha akili yake.

Taratibu nikaanza kumweleza Almasi kuhusu ujio wa Sofia nyumbani kwangu na yote aliyonieleza. Almasi hakuwa tayari kumsamehe Sofia. Aliniambia kuwa alishaanza kumsahau na asingependa kujihusisha na chochote kuhusu mwanamke huyo.

“Najua ni ngumu lakini kila lenye ugumu lina suluhisho ndani yake,” nilimwambia Almasi huku nikimtazama kwa tuo.

“Mgeni, kipindi namaliza chuo kikuu nilijiwekea misingi ya kuishi na namna ya kuishi, nilikuwa najua nguzo za kuishi na wapi nitapita. Baada ya kukutana na Sofia niliuona mwanga wa jinsi ambavyo ningetimiza ndoto zangu, na nilimwamini sana lakini angalia alichonitenda! Hayo yaliyotokea yamenivunja moyo kabisa!” Almasi alisema kwa huzuni kisha akaongeza, “Kwanza sidhani kama siku hizi kuna mapenzi ya kweli.”

“Na wewe usiingie kwenye mkumbo wa watu wanaojiaminisha kuwa siku hizi hakuna mapenzi ya kweli na ukiwauliza mapenzi ya kweli yalikuwepo lini hawana jibu… zaidi watasema enzi za wazee wetu kana kwamba waliishi enzi hizo na kuyashuhudia,” nilimwambia Almasi kisha nikaongeza, “Tafadhali, maneno hayo ni ya wakosaji, penzi la kweli chanzo chake ni wewe… amua sasa kuzalisha penzi la kweli. Usiishi kwa kufuata maneno ya watu.”

Almasi alitaka kusema neno lakini nikamzuwia kwa ishara. “Najua unapita katika kipindi kigumu lakini kumbuka wewe si wa kwanza, wala wa mwisho kwake. Kwa vyovyote aliwahi kupenda kabla na anaweza kupenda tena. Lakini naamini bado anakupenda sana licha ya yote yaliyotokea kati yenu. Yeye si mkamilifu, na wewe pia si mkamilifu…” nilimwambia Almasi, kisha nikaongeza.

“Nyote wawili hamuwezi kuwa wakamilifu pamoja, lakini kama anaweza kukufanya ucheke tena, akakufanya ufikiri mara mbili na anakiri kuwa yeye ni binadamu na ametenda makosa basi mrudie. Anaweza kuwa hakufikirii kila sekunde katika siku, lakini atakupa sehemu ya utu na mwili wake. Usimbadilishe, usimchambue, usitegemee makubwa zaidi ya yale awezayo kukupa au yale anayomudu. Kubali kuwa kila binadamu anakosea, na hapo utakuwa na furaha ya mapenzi na wasiwasi wa mapenzi utaondoka.”

Bado Almasi alionekana yupo njia panda, nikazidi kumsihi. “Kumbuka, ni wewe uliyenipa msemo wa Drew Barrymore aliosema kuwa; ‘furaha ndiyo humfanya mtu kuwa mzuri’… kwa maana hiyo watu wenye furaha ni wazuri. Maisha ni leo, Almasi, kesho ni majaaliwa. Unatakiwa ufanye uamuzi wa kukufanya uwe na furaha sasa hivi, unatakiwa uanze upya na ukubali kuwa mambo yametokea na sasa uangalie mbele zaidi.”

Maneno yangu yalionesha kumwingiza vilivyo Almasi, sasa alibaki kimya kwa kitambo kirefu, alionekana kuzama kwenye lindi la mawazo. Sikujua alikuwa anawaza nini ila nilichofanya ni kuwasiliana na Sofia kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu kumtaka ajitokeze. Muda wote nilipokuwa naongeza na Almasi Sofia alikuwa amejificha sehemu akifuatilia kwa karibu nyendo zetu na alisubiri muda ambao ningemruhusu kuja pale kwenye meza yetu.

Mara nikamwona Sofia akiingia pale Pub na kuja kwa mwendo wa madaha, na wakati anasogea pale kwenye meza yetu Almasi akawa kama kazinduka kutoka kwenye lindi la mawazo, akainua uso wake na kumwona Sofia. Macho yao yakagongana na hapo Almasi akajikuta akisimama. Nilizihisi hasira zikimjaa kifuani, huenda ni kwa kile alichokuwa amefanyiwa na Sofia. Hata hivyo hakusema kitu, alibaki kumtumbulia macho Sofia.

Sofia naye alisimama, akawa anamtazama Almasi kwa wasiwasi. Sasa walibaki wanatazamana tu kama majogoo yaliyotaka kupigana. Nilibaki mtulivu kwenye kiti changu nikiwatazama kwa zamu huku nikijaribu kuyasoma mawazo yao. Wote walionekana kutahayari kidogo na hakukuwa na aliyeonekana kuwa na uwezo wa hata kumsemesha mwenzake.

Mara ghafla nikaona michirizi ya machozi ikitiririka kwenye mashavu ya wote wawili. Walikuwa wanalia! Ishara ya machozi ikanifanya nihisi kuwa walikuwa wamesameheana. Hapana… ni Almasi ndiye aliyekuwa amemsamehe Sofia kwani ni yeye aliyefanyiwa makosa.

Kwa kuwa mwanaume kulia, tena kulia hadharani ni aibu, nilimwona Almasi akijifunika uso wake kwa kiganja cha mkono wake wa kulia. Na hapo Sofia akapata nguvu na kumsogelea kisha akazungusha mikono yake kwenye shingo ya Almasi. Almasi naye akazungusha mikono yake kwenye kiuno cha Sofia na kisha Sofia akatuliza kichwa chake kwenye bega la Almasi huku akilia kimya kimya, kwa kububujikwa na machozi.

Mwanzo niliona kabisa kuwa Almasi alikuwa amemkumbatia Sofia kinafiki kwa kuwa huyo ni mwanamke aliyemvunja moyo wake, lakini taratibu alijikuta akihisi mguso wa upendo aliouonesha Sofia katika hali ile ya kukumbatiana. Nyuso zao zikakaribiana na hatimaye papi za midomo yao zikakutana, wakaanza kunyonyana ndimi.

Walikuja kuachana baada ya dakika nzima, wakatazamana kimya katika namna ya kukumbukia raha walizopeana muda mfupi uliokuwa umepita. Niliendelea kuwa mtulivu kwenye kiti changu huku nikiwatumbulia macho.

“Sofia,” hatimaye Almasi aliuvunja ukimya kwa kulitaja jina la Sofia.

Lakini kabla Sofia hajaitika Almasi alimkumbatia tena, wakakumbatiana kwa nguvu na kulirudia tena lile tendo la kubusiana. Watu wengine waliokuwa ndani ya ile Pub waliduwaa kwa muda, wote waliwashangaa wapenzi hao waliokumbatiana na kubusiana hadharani. Na midomo yao ilipoachana Sofia ndiye aliyeanza kuzungumza.

“Almasi, nakupenda sana na nakuhitaji kuliko hata pumzi,” Sofia alisema kwa sauti ya puani huku macho yake yakiwa yamemlegea.

“Unadiriki kusema nini, Sofia? Baada ya kunisaliti na kuondoka na mwanaume mwingine leo unasema unanihitaji kuliko pumzi! Kwa lipi, Sofia? Kwa lipi?” Almasi alilalama huku akimkazia macho Sofia. Kwa vyovyote hasira zilikuwa zimeibuka upya ndani yake.

Ilionesha wazi kuwa maneno ya Almasi yaliuchoma sana moyo wa Sofia, na hatia ikajiunda ndani yake. Unyonge ukamshika na hofu ikajionesha wazi wazi usoni kwake.

“Najua nimekuumiza sana lakini nomba tukae chini, mpenzi,” Sofia alimrai Almasi, naye akatii.

Waliketi kisha ukimya wa dakika kadhaa ukatawala, walikuwa wanatazamana tu pasipo kusema neno na baadaye sana Sofia aliuvunja ukimya huo kwa kusema, “Nitakuwa sitendi haki endapo nitakana kuwa sikukukosea, Almasi… Nakiri mbele ya shemeji Mgeni kuwa nimekukosea sana…”

Endelea...
 
Mgeni mwema.jpg

178

Kisha Sofia alionekana kusita kidogo, akageuza shingo yake kunitazama kwa macho yaliyoonesha shukurani kwa kumuunganisha tena na Almasi. Kisha akamtazama Almasi na kuongeza, “Yaliyopita si ndwele, mpenzi, naomba tugange yajayo…”

“Ishia hapo hapo, Sofia… unajua ni kwa jinsi gani umeuvunja moyo wangu?” Almasi alimkatisha Sofia huku akiunyoosha mkono wake kama askari wa usalama barabarani anayezuia gari lililo katika mwendo.

“Naomba unipe nafasi nyingine, Almasi, naahidi kukuponya majeraha yote ya moyo wako…” Sofia alisema huku akisogeza kiti chake karibu na pale kilipokuwa kiti cha Almasi. Machozi yaliyokuwa yanamlengalenga sasa yalitoka kwa wingi na kukilowesha kifua chake.

Nikamwona Almasi akiingiwa na huruma, alitoa kitambaa laini toka mfukoni na kumpa Sofia ambaye alikipokea na kufuta machozi.

“Umeniumiza sana, Sofia… umeniumiza kimwili na kihisia, kama isingelikuwa Mgeni huenda ningeshakufa au ningeshafanya mauaji,” Almasi alizidi kulalamika kwa sauti tulivu, isiyo ya ukali.

Sofia alizidi kulia, majuto yake yalionesha kusababishwa na maumivu makali moyoni mwake na hivyo kumfanya ajione mwenye hatia, “Naelewa, Almasi… naelewa kuwa nimekuumiza sana, naomba unisamehe na unipe nafasi nyingine niyamalize maumivu yako,” Sofia alisema katika hali ya kumaanisha kile alichokisema.

Na hapo nikakumbuka kuwa niliwahi kusikia, kama si kusoma mahala fulani kuwa; ‘mapenzi yana nguvu kuliko kifo’. Hili lilijidhihirisha pale Almasi alipotamka kumsamehe Sofia na kwamba yupo tayari kuufungua moyo wake kwa mara nyingine.

Kwa kutambua eneo tulipokuwa, eneo ambalo lilikuwa na mkusanyiko wa watu ambao walifika hapo kwa ajili ya kustarehe kama ilivyokuwa kwetu, niliwasihi twende nyumbani ili wakayamalizie mazungumzo yao huko badala ya kuendelea kuwepo pale Pub.

Bila hiyana Almasi alitii, akainuka na kumwongoza Sofia, wote watatu tukaondoka kuelekea nyumbani kwa Almasi.

* * *



Saa 2:30 usiku…

Mimi na Marietta tulikuwa tumeketi kwenye kochi kubwa wakati Almasi na Sofia walikuwa wameketi kitandani. Muda huo tulikuwa chumbani kwa Almasi na mbele yetu, juu ya meza, kulikuwa na chupa kadhaa za bia, chupa kubwa ya Konyagi na bilauri nne.

Kila mmoja wetu alikuwa na bilauri ya pombe mkononi akiifurahia siku hiyo. Ilikuwa siku ndefu na hivyo tuliona kuwa haikuwa vibaya endapo tungejipongeza kidogo.

Marietta, rafiki mkubwa wa Sofia ambaye waliishi mtaa mmoja, alikuwa amefuatana nasi baada ya kukutana naye njiani tulipokuwa tunaelekea nyumbani kwa Almasi tukitoka Colores Pub. Ulikuwa ushauri wa Sofia kumtaka Marietta aambatane nasi ili kukamilisha jozi mbili, yaani watu wawili kwa wawili.

Marietta alikuwa msichana mwembamba mrefu mwenye umbile lililovutia. Alikuwa mweupe na mwenye nywele nyingi nyeusi tii na sura yake ilikuwa ndefu yenye mvuto. Shingo yake ilikuwa nzuri iliyokaa vyema katikati ya mabega yake ya kike na kifua chake kilibeba matiti madogo yaliyochongoka mbele utadhani yana hasira ya kutoboa blauzi aliyovaa.

Akiwa na umri wa miaka 21 tu tayari alikwisha olewa mara moja wakati akiwa na umri wa miaka 17, akaishi na mume kwa takriban miaka miwili na ushee kisha akaachika.

Tukiwa tumeketi kwa utulivu, vinywaji vyetu vilisindikizwa na muziki kwa mbali, muziki ambao haukutufanya tushindwe kusikilizana. Taratibu tukawa tunakunywa huku tukipiga soga. Kila muda ulivyokuwa unaenda tukazidi kuchangamka zaidi, hasa mimi.

Sikuwa na kichwa cha pombe kwa maana ya kwamba sikuwa mnywaji kabisa wa pombe. Hiyo ilikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza kunywa pombe tangu nipate fahamu zangu nikiwa mjini Kilosa. Ndiyo maana sikugusa kabisa pombe kali ya Konyagi bali niliishia kunywa bia tu. Hata hivyo, bia ya pili tu nilianza kuhisi kichwa changu kikianza kuwa kizito na mdomo kuwa mwepesi!

Nilijikuta nikiwa mwongeaji sana na nilicheka hata kwa jambo dogo lisilo la kuchekesha! Nilikuwa nimechangamka sana kiasi kwamba Almasi, Sofia na Marietta wakawa wanakonyezana kwa siri. Niligundua hilo lakini nikajifanya sioni.

Sasa ilifikia kipindi nilishindwa kabisa kuvumilia, uaminifu wangu kwa Zainabu ukaonekana kuanza kunishinda kwa kuwa macho yangu yalianza kunilaghai kwa kumwona Marietta ni mrembo kuliko wanawake wote duniani. Nilimkumbatia mara kwa mara na kumbusu na muda mwingine nilimtaka tuinuke na tucheze pamoja muziki.

“Mgeni, kwani nini shida?” Marietta aliniuliza akinitazama machoni. Alikuwa amelegeza macho yake na kinywa.

Sikumjibu na badala yake mkono wangu ulikiminya kiuno chake chembamba mithili ya dondola na kumsogeza karibu yangu. Nikamtazama kwa kitambo kidogo kabla sijasema, “Unataka kujua shida yangu?”

“Ndiyo,” Marietta alisema huku akitabasamu kwa mbali. Ni kama vile alikuwa ananisanifu.

“Nataka nikukumbatie hivi hivi usiku nzima,” nilimwambia Marietta huku nikiendelea kukiminya minya kiuno chake.

“Kweli?” Marietta aliniuliza huku akinikazia macho.

“Ndiyo. Kwani kuna shida?” nilimuuliza huku nikimkonyeza kilevi. Marietta akaachia kicheko hafifu.

“Hakuna shida… ila mwenzio naogopa…” Marietta alisema huku akipumua kwa nguvu.

“Unaogopa nini?” nilimuuliza huku nikimkazia macho. Na hapo nikamwona akinitazama machoni akiwa kimya kidogo.

“Namwogopa mkeo…” Marietta alisema kwa sauti ya chini huku akionekana kupumua kwa shida kidogo, “lakini pia najua hautaweza kuvumilia.”

Nikatabasamu kabla ya tabasamu langu halijaunda kicheko kidogo, kisha nikamminya tena kiunoni kabla sijamvuta na kumbusu shingoni, halafu kwenye shavu kabla ya mdomo wangu kuhamia kwenye mdomo wake.

“Naweza kuvumilia vinavyovumilika,” nilimnong’oneza sikioni. Sauti yangu ikaonekana kuusisimua sana mwili wake. Niligundua kuwa chuchu zake zilikuwa zimesimama na kuwa ngumu.

“Mgeni!” Marietta aliita kwa sauti ya chini ya kunong’ona. Mwili wake ulikuwa unatetemeka kwa ashki. Alikuwa ananitazama machoni kisha akatabasamu kwa mbali.

“Kwani utashindwa kuvumilia?” nilimuuliza huku nikimnyanyua juu kisha nikanyoosha mikono yangu kudaka makalio yake, nikayapapasa makalio hayo na kuyaminya. Halafu katika namna ya nguvu, nikambeba pasipo kujali uwepo wa watu wengine mle ndani.

Akiwa juu juu Marietta alizungusha miguu yake kwenye kiuno changu, tukatazamana kimapenzi na taratibu tukakutanisha midomo yetu na kuanza kubadilishana ndimi zetu. Almasi akakohoa kama vile alikuwa anasafisha koo lake na kutushtua, tukaangaliana na kutabasamu.

Endelea...
 
Mgeni mwema.jpg

179

Nikaamua kumshusha Marietta chini kisha kila mmoja akashika bilauri yake ya pombe na tukaendelea kunywa taratibu. Tulikunywa na kunywa zaidi kiasi kwamba hata wengine nao wakaanza kushindwa kujimudu. Niliwaona Almasi na Sofia wakikumbatiana na nyuso zao zikakaribiana, kisha papi za midomo yao zikakutana, wakaanza kunyonyana ndimi.

Nami kwa ulevi wangu wa siku ya kwanza sikujua nini nifanye na nini nisifanye. Kilichonijia akilini kwangu ni kumvuta Marietta kwa nguvu na kumbusu, na yeye akanibusu na kisha akanikumbatia kwa nguvu. Macho yake yalikuwa yamelegea na mwili wake ulikuwa umepata joto…

Baada ya hapo… dah, hata sikukumbuka kingine… hadi nilipokuja kuamka majira ya saa mbili na nusu asubuhi, kichwa kilikuwa kinanigonga sana na nilikuwa sijiwezi.

Nilipatwa na mshangao mkubwa nikijiuliza kulikoni! Nilifikiria kidogo lakini sikuweza kukumbuka chochote kilichotokea. Almasi alipogundua kuwa nimeamka aliniletea bilauri ya maji ya baridi yaliyochanganywa na ndimu na kunipa.

“Kunywa maji haya, yatakusaidia,” Almasi aliniambia.

Niliipokea ile bilauri ya maji pasipo kuhoji chochote, nikayanywa maji yote na kumrudishia ile bilauri. Kisha nilimuuliza Almasi kilichotokea, akanisimulia yale yote niliyoyafanya usiku.

Sasa kumbukumbu zangu zilianza kurudi taratibu, nilikumbuka vizuri kuwa baada ya kumvuta Marietta kwa nguvu na kumbusu, yeye pia alinibusu na kisha akanikumbatia kwa nguvu. Halafu nilimnyanyua na kumbwaga kitandani pasipo kujali kama Almasi na Sofia pia walikuwa hapo kitandani.

Kwa kuwa kitanda kilikuwa kikubwa, mimi na Marietta tulisogea ukutani kisha tukaanza kuvuana nguo na kuzitupia huko pasipo kujali uwepo wa watu wengine! Tulivuana upesi upesi kana kwamba tulikuwa tunawahi kuzima moto. Tukanyonyana ndimi zetu na kupapasana kwa fujo. Haikuchukua muda tukatimiza lengo letu na baada ya hapo nikalala usingizi mzito. Nikapitiliza mpaka asubuhi.

Sasa Almasi alikuwa ananicheka na aliniambia namna ya kufanya endapo siku nyingine ikinitokea hali ya ulevi kama hiyo.

“Hakutakuwa na siku nyingine, Almasi!” nilimwambia huku nikitikisa kichwa changu taratibu. “Sitakunywa tena pombe. Si kwa mateso haya!”

_____



Saa 4:30 asubuhi…

Nilifika nyumbani nikamkuta Zainabu akiwa ametulia sana kwenye kochi na nyumba ilikuwa kimya mno. Bila shaka alikuwa ametingwa na mawazo kwa kuwa hakujua nililala wapi. Haikuwa kawaida yangu kutorudi nyumbani, na hiyo ilikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza kulala nje.

Kichwa kilikuwa bado kinanigonga sana na mwili ulikuwa umechoka. Nilimsalimia Zainabu lakini hakunijibu na badala yake alitazama saa kwanza ndipo akaniuliza, “Mgeni, mbona jana hukurudi nyumbani, ulilala wapi?”

Nilijiuma nikimweleza kuhusu mkutano wangu na Almasi na Sofia, kisha nikamweleza kuhusu pombe nilizokunywa nyumbani kwa Almasi na kisha nikazidiwa. Jambo ambalo sikuthubutu kumweleza ni kuhusiana na Marietta.

Zainabu alinitazama kwa muda halafu akaniuliza, “Una uhakika hukuwa na mwanamke?”

Swali lake lilinishtua kidogo. Kabla sijazungumza chochote nilifikiri kwa sekunde kadhaa kisha nikasema, “Siwezi kukusaliti, kwa nini unifikirie hivyo?”

Akiwa bado ananitazama usoni kwa umakini aliniambia, “Kuwa mkweli tu, ndiyo maana jana ulilala huko unakokujua, sivyo?”

“Zai, kwa nini unifikirie hivyo! Ina maana siku hizi hatuaminiani kabisa?” nilimuuliza Zainabu huku nikijitahidi kuifanya sauti yangu iwe tulivu. Zainabu alibaki kimya akiendelea kunitazama usoni kwa mashaka kidogo.

“Kama huniamini basi mpigie simu Almasi umuulize nililala wapi,” niliongeza huku nikihisi hatia ya usaliti ikinikaba kooni, moyo wangu ulikuwa unapiga kwa nguvu na akili yangu ilikosa utulivu. Nilianza kujilaumu kwa nini nilitenda niliyoyatenda, sasa nilitamani kuomba msamaha na kueleza kila kitu kilichotokea.

“Nakuamini ila tahadhari ni muhimu. Wajua wewe ni mtanashati na kila msichana anatamani kuwa na wewe! Nikibweteka itakuwa hatari kwa upande wangu,” Zainabu alisema na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.

Niliachia tabasamu huku nikimshukuru Mungu kwa kunipa Zainabu, mwanamke asiye na makuu. Wakati nikiwaza haya sikujua kama nilikuwa nimemsogelea Zainabu na mkono wangu mmoja nikiuzungusha kwenye kiuno chake na kuanza kukiminya minya taratibu, mkono mwingine ukawa unafanya papaso maridhawa katika paja lake.

Na hapo nikamwona Zainabu akiyafumba macho yake, huenda hisia zake zilianza kupanda taratibu na kujikuta akiyasahau yote, halafu nikamsogeza karibu yangu huku nikimtazama kwa tabasamu na kusema, “Wala usihofu, mke wangu, nakupenda sana. Wewe ndiye usingizi wangu, wewe ndiye pumzi yangu, wewe ndiye malaika wangu… nakupenda sana Zainabu wangu.”

“Hata mimi nakupenda sana, mume wangu, sihitaji mwanaume mwingine zaidi yako, wewe ndiye uliyeyashikilia maisha yangu… nitahakikisha ninakulinda na wezi wa waume za watu,” Zainabu alisema huku naye akinikumbatia kwa mahaba.

Ama kweli hisia ndiyo kitu pekee ambacho husababisha mapenzi. Hisia kamwe hazizungumziki kwa njia ya mdomo. Hisia husema kupitia moyo kwa njia ya macho. Mioyo ikizungumza kamwe hakuna cha kuzuia, hata msiposema ninyi kwa ninyi lakini mioyo yenu itasema na hatimaye mtajikuta katika mapenzi.

Ni hisia hizi zilinena katika mioyo yetu, zikianza na moyo wangu na kisha zikanena pia katika moyo uliopondekapondeka wa Zainabu. Hisia hizi zikatuleta katika hali tuliyopo kimya kimya. Mioyo ikazungumza ikisema kuwa inahitaji faraja. Nani wa kusema hapana iwapo moyo umesema ndiyo?

Ni wakati huo Zainabu aliinuka na kunyoosha mkono wake kunielekea, nikaushika. Akaninyanyua na kisha tukaanza kupiga hatua za taratibu kuelekea chumbani. Tulipoingia tu chumbani nikamwegemeza ukutani na hapo tukakutanisha midomo yetu na kuanza kunyonyana huku taratibu tukiwa tunavua nguo mpaka tukabaki kama tulivyozaliwa.

“Dah… ni ukatili wa hali ya juu sana mwanamume kulala na mwanamke mwingine halafu unarudi nyumbani asubuhi na kutaka kushiriki ngono na mke wako!” Nilijikuta nikiyawaza hayo, nikakumbuka picha yote ya kilichotokea usiku na Marietta, yaani kila hatua ilikuwa ikijirudia kwenye akili yangu.

* * *

Endelea...
 
Mgeni mwema.jpg

180

Rehema ni nani?


Saa 4:30 asubuhi…

ZILIKUWA zimepita siku tatu tangu nifanikiwe kuwapatanisha tena Almasi na Sofia na baadaye nikaishia kulala na Marietta. Asubuhi ya siku hii hali ya hewa ya Mji wa Kilosa ilikuwa imepoa zaidi, manyunyu hafifu ya mvua yalikuwa yanaanguka kutoka angani kulikotanda wingu zito la mvua kiasi cha kuweza kuizuia miale ya jua la asubuhi kutua vizuri ardhini.

Muda huo nilikuwa nimemsindikiza Zainabu sokoni, katika soko kuu la Kilosa, ili kununua mahitaji muhimu ya nyumbani na kwa ajili ya duka-genge lake. Asubuhi hiyo Zainabu alikuwa amependeza zaidi katika mwonekano wa vazi la kitenge cha wax na kilemba kilichofungwa kwa ufundi wa hali ya juu kichwani kwake.

Wakati tukirudi Zainabu aliniomba tupitie kwenye jengo moja la ghorofa moja lililopo karibu na Masjidi Sunna eneo la Uhindini kwani alitaka kumwona fundi wake wa nguo. Tulifika kwenye jengo hilo tukaingia ndani na kisha tukaanza kupanda ngazi haraka haraka kuelekea juu. Wakati tukipanda ngazi nilisikia kama sauti ya mwanamke ikiita kwa mashaka, “Jason!”

Nilishtuka sana kusikia jina hilo, ilinichukua sekunde moja tu kutambua kuwa hii ilikuwa mara ya pili kulisikia jina hili, mara ya kwanza nililisikia kutoka kwa msichana mrembo wa kwenye ndoto ya ajabu niliyoiota siku chache zilizokuwa zimepita.

Kwa kuwa nilikuwa nakwea ngazi kwa mwendo wa haraka, hivyo nilipogeuka nyuma nilikuwa nimeshafika juu zaidi na hivyo sikumwona mtu.

“Kuna nini, Mgeni?” Zainabu aliniuliza huku akinitazama usoni kwa udadisi lakini sikuwa na la kumjibu.

Ukweli ni kwamba nilipokuwa nimegeuka baada ya kusikia jina hilo sikuwa nimemwona mtu yeyote lakini kwa uhakika kabisa nilifanikiwa kuona kivuli cha mwanamke niliyehisi kumfahamu, nikajua hata ningesema Zainabu asingenielewa.

“Hakuna kitu, hata sijui kitu gani kimepita?” nilimwambia Zainabu na yeye alinishika mkono, akaniongoza kupanda ngazi kama mama amwongozaye mtoto wake mpendwa.

Kule juu kwenye chumba cha mafundi wa kushona nguo, Zainabu alipokuwa anaongea na fundi wake akili yangu ilikuwa imelemewa na mawazo kuhusu yule mwanamke aliyeita jina la Jason. Nilihisi kama mapigo ya moyo wangu yalikuwa yakienda mbio. Nilianza kumfikiria sana yule mwanamke na sikujua hili jina la Jason lilikuwa linahusiana vipi na mimi! Kuna wakati nilihisi pengine hakuna mtu yeyote aliyeita jina hilo isipokuwa yalikuwa mawazo yangu tu! Sasa sikujua lipi la kushika na lipi la kuacha na hivyo kubaki nikiwa na wasiwasi.

Ilimchukua Zainabu takriban dakika kumi na tano kuongea na fundi wake kisha tukaondoka kuelekea nyumbani, na wakati tukishuka ngazi Zainabu alikuwa ananitazama kiwizi wizi, baadaye hakuvumilia akaniuliza kama kulikuwa na jambo lililokuwa likinitatiza lakini nilikataa. Sikutaka kumwambia chochote na badala yake nilitembea kimya kimya.

Zainabu alikuwa ametahayari, nilihisi kuwa hata yeye alikuwa amemsikia yule mwanamke wakati akiita jina la Jason, na hivyo sikujua kwa nini alikuwa amepatwa na wasiwasi kiasi kile! Sasa hali ilianza kuwa tete asubuhi ile.

Mara tukaona watu wakikimbilia sehemu ambapo kulikuwa na umati wa watu wakiwa wamemzunguka mwanamke mmoja aliyelala kando ya barabara huku akivuja damu kichwani, alikuwa nusu amepoteza fahamu na nusu akiwa hai.

“Nini kimetokea?” Zainabu aliniuliza huku akiyakaza macho yake kutazama kule kwenye tukio.

“Hata sijui kuna nini!” nilimjibu kisha nikamuwahi kijana mmoja aliyeonekana kuwa na haraka akiwa anatokea kwenye eneo la tukio. “Eti ndugu, kuna nini kimetokea hapo?”

“Kuna mdada amegongwa na gari kizembe kabisa. Hao ndio madereva wetu, dah!” yule kijana alijibu huku akiendelea na safari yake.

“Kwani ilikuwaje?” nilihoji huku wasiwasi ukianza kuniingia. Sikujua kwa nini nilianza kupatwa na wasiwasi

“Nenda kajionee, kaka…” yule kijana alinijibu na kutoweka huku akitikisa kichwa kwa masikitiko makubwa. Aliutangaza uchungu waziwazi.

Nilijikuta nikiwa na shauku ya kusogea karibu zaidi ili niweze kujua kulikuwa na nini, cha ajabu nguvu zilikuwa zinaniisha miguuni, sikujua kwa nini niliguswa na tukio lile. Nilijikuta nikiwa katika sintofahamu, na sasa nilikuwa navuta hatua moja baada ya nyingine ili nipate kujua kipi kilikuwa kimejiri. Zainabu alinifuata nyuma kimya kimya.

“Samahani, dada, kwani kuna nini?” nilimuuliza mwanadada mmoja aliyekuwa peku peku. Nilipomtazama usoni nikagundua kuwa alikuwa katika taharuki isiyofichika.

“Mh! We acha tu kaka’angu, hata sijui nielezeje lakini… hawa madereva wa siku hizi ni majanga matupu yaani ni Mungu tu atatuokoa… masikini dada wa watu,” yule mwanadada alinijibu kwa wasiwasi kisha akaongeza, “Sijui dereva kalewa maana huyu dada alikuwa anapita kando kabisa ya barabara, hata gari lilikotokea hatujui likamgonga na kumrusha huku…”

Kisha yule mwanadada akafumba macho kabla hajatokwa na mguno mkubwa. Ni kama alikuwa haamini kilichotokea. Na hapo nikashikwa na kihoro. Hata hivyo sikusubiri, nikausogelea ule mwili wa mwanamke uliolala barabarani nikiamini kwa namna yoyote ile kuwa jibu la maswali yangu ningelipata pale.

Nikiwa nimesimama karibu zaidi macho yangu yakatua kwenye sura ya mwanamke huyo, akili yangu ikaniambia kuwa nilikuwa namfahamu, tatizo likaja, ni wapi nilikuwa nimemwona!

“Ni nani huyu?” nilijiuliza nikiwa nimetahayari kidogo. Nilimkodolea macho, nikakumbuka kuwa muda mfupi uliokuwa umepita wakati tukipanda ngazi za jengo kuelekea kwa fundi wa Zainabu, mwanamke huyo aliita jina la Jason. Sikuwa nimemwona vizuri lakini kupitia kivuli chake niliweza kumtambua.

Nikazidi kujiuliza; huyu ni nani na alinifahamu vipi? Sasa nilitamani sana kumwinua ili ajibu maswali yangu kwani nilitaka kujifahamu. Nikiwa sijapata jibu nikashtuliwa na sauti ya ving’ora vya magari yaliyokuwa yanakuja eneo lile kwa kasi.

Nilipotazama vizuri nikagundua kuwa yalikuwa magari mawili, moja lilikuwa gari la Polisi na jingine lilikuwa gari la wagonjwa. Watu wakayapisha magari yale. Nikiwa bado nashangaa nilishuhudia mwili wa mwanamke yule ukibebwa juu juu na wanaume wawili na kuingizwa kwenye gari lile la wagonjwa kisha gari lile likaondoka kwa mwendo wa kasi na kuliacha gari la Polisi.

Polisi wawili walikuwa wameshuka na kuanza kuchukua maelezo toka kwa mashuhuda wa ile ajali. Na hapo nikawa kama nimezinduka toka mawazoni, nikatimua mbio nikitaka kuliwahi lile gari la wagonjwa, akili yangu haikuwa na utulivu kabisa wakati huo na nilitamani kuyajua mambo mengi kuhusu yule mwanamke. Kuna wakati roho ilinisukuma waziwazi kutaka kuwauliza watu maswali ambayo kwa vyovyote wasingeweza kunipatia majibu.

Hata hivyo mbio za sakafuni huishia ukingoni… wakati nakimbia sikuwa nimeuona utelezi na dimbwi dogo la maji na hivyo nikajikuta nikiteleza, sikutaka kuanguka kizembe nikajaribu kuutafuta muhimili lakini nikaukosa, na hapo miguu yangu ikatangulia mbele.

Sasa nilikuwa naelekea kuanguka chali. Nikafanya juhudi kutokana na mazoezi yangu, nikajipinda huku nikijigeuza juu kwa juu na kutanguliza mikono yangu chini. Huu ukawa mwisho wa kiherehere changu cha kutaka kujua nini kilikuwa kimejiri kwa yule mwanamke aliyepatwa na ajali.

Niliinuka haraka huku nikimtupia jicho Zainabu nikamwona kama alikuwa amechanganyikiwa kwa yote ambayo macho yake yalikuwa yameshuhudia ndani ya dakika chache tu. Alikuwa ametahayari sana na alinitazama kwa macho yaliyokuwa na maswali mengi sana.

Endelea...
 
Back
Top Bottom