Bishop Hiluka
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 7,147
- 14,699
- Thread starter
- #261
162
“Nashukuru sana!” nilisema huku nikiinamisha kichwa changu kuonesha heshima kwake. Miguu yangu nilikuwa nimeibana na mikono nimeishika pamoja kwa mbele kama nanawa.
“Unaitwa nani? Sogea… sogea karibu!” Jerome aliniuliza huku akinitazama kwa umakini zaidi kama mtu aliyekuwa ananifananisha.
Nikasonga karibu na kumtazama usoni. “Naitwa Mgeni…” nilisema huku nikiwa sina uhakika wa jina la pili kwani hilo ndilo jina pekee lililokuja kichwani mwangu.
“Mgeni!” Jerome alionesha kustaajabu kidogo.
“Ndiyo, Mgeni Mwema!” Zainabu alidakia huku akiachia tabasamu.
“Oh… jina zuri kabisa!” Jerome alisema huku akiendelea kunitazama kwa umakini. Kisha akaendelea, “Kwa sababu ya Zai, jihesabie kuwa kazi umepata.”
“Sawa,” nilijibu kwa unyenyekevu mkubwa.
“Na utatakiwa kuripoti kesho hapa hapa majira ya saa moja na nusu asubuhi. Umenielewa?” Jerome aliniuliza akiwa ameweka mkono wake begani mwangu.
“Ndiyo, nimeelewa,” nilimjibu na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.
Kama ndoto, siku iliyofuata nikawa mfanyakazi wa kampuni hiyo ya kandarasi ya ujenzi wa reli ya kisasa na makazi yangu yakiwa hapo Kilosa, nyumbani kwa Zainabu. Sikujali kuhusu ukaribu uliokuwepo kati ya Jerome na Zainabu na wala sikuwaonea wivu, kikubwa mno kilichonifurahisha ni kwamba nilikuwa nimepata kazi, basi.
Baada ya kupata kazi watu huwa wanakuwa na matarajio fulani kwenye maisha, jinsi watakavyotumia kipato wanachopata kuboresha maisha yao na ya jamaa zao. Kwangu, niliwaza pia kujitegemea ili nisiwe mzigo kwa Zainabu, maana nilihisi maisha yangu yote yalikuwa yakimtegemea Zainabu. Niliapa kufanya kazi kwa bidii ili niweze kupanga chumba changu na kuanza maisha mapya.
Sasa ratiba yangu ikawa kila siku naamka alfajiri na mapema nafanya mazoezi mepesi ya viungo na karate kabla sijaenda kazini, nikitoka kazini jioni nakwenda uwanjani kucheza mpira, nikirudi namsaidia Zainabu kazi za nyumbani, na sikusahau kujisomea vitabu na machapisho mbalimbali ili kujua yanayoendelea duniani.
Siku za mwisho wa wiki, siku ambazo sikuwa nakwenda kazini nilikuwa na tabia ya kucheza na watoto wa pale mtaani kisha jioni nilitoka na kwenda gym kufanya mazoezi. Aina hiyo ya maisha ikanifanya niwe maarufu mjini Kilosa.
Wakati nikiwa bado sijafanikisha azma yangu nikajikuta nikiangukia kwenye uhusiano wa kimapenzi na Zainabu. Ingawa nilishaziona dalili mapema lakini muda wote nilijifanya sielewi. Nilianza tu kuona mabadiliko ya kimavazi kwa Zainabu akiwa mle ndani. Wakati mwingine alibaki na khanga moja tu au alivaa nguo fupi, wakati mwingine bukta! Dah… na lile umbo lake zuri nikajua tu hapa nakaribishwa.
Ndipo ilipotokea usiku mmoja ambao niliishiwa na uvumilivu na kujikuta nikilimega tunda. Siku hiyo nilijisikia vibaya baada ya tendo maana nilihisi kama nimeyachukulia matatizo ya Zainabu kuwa fursa ya kumpata. Ndiyo, nilijua alikuwa na maisha ya shida na alihitaji faraja ila nilishindwa kuzuia hisia zangu. Kwa kifupi nilitenda kinyume kabisa na itikadi yangu. Itikadi yangu ipi? Nilijiuliza lakini sikuwa na jibu…
Ilianza tu baada ya yeye kutoka kuoga, akarudi akiwa amejifunga khanga moja tu kifuani pasipo nguo nyingine ndani na hivyo kuifichua hazina ya mwili wake ulioumbika. Wakati huo mtoto Mariam alikuwa amelala. Alisimama mlangoni akawa ananiangalia kwa aibu. Mimi wakati huo nilikuwa nimejilaza kitandani nikiwa nimevaa bukta na singlendi. Macho yetu yakakutana ila bado hakuna aliyesema lolote. Nilijua wazi alichokuwa anataka lakini nilijifanya sielewi nikitamani aniambie. Nikahisi na yeye alikuwa anasubiri niseme. Lakini hakuna aliyesema kitu.
Zainabu aliendelea kusimama pale pale kama aliyepigiliwa misumali miguuni. Nikajifanya kuinuka niende nje, wakati naanza kupiga hatua kumsogelea akawa anatabasamu pasipo kusogea kando ili nipite.
“Mbona unatabasamu?” nilimuuliza huku nikimtazama machoni. Hakunijibu badala yake akainamisha uso wake chini akionekana kuwa na haya kidogo. Nikampita na kutoka nje.
Huko nje sikuwa na chochote cha maana cha kufanya, nilikaa kwenye gogo la mti kando ya nyumba kama niliyekuwa napunga upepo, niliwaza hili na lile na baadaye sana nikaamua kurudi ndani, ilikuwa ni baada ya dakika therathini, nikakuta ameshalala. Ameangalia upande mwingine. Alilala katikati huku mtoto akiwa amemlaza ukutani. Nami nikapanda kitandani na kuzama kwenye shuka. Nikashtuka baada ya kugundua kuwa Zainabu alilala uchi kama alivyozaliwa.
Hapo mwili ukanisisimka sana, sema shida ikawa naanzishaje! Mara nikasikia pumzi yake ikibadilika kuashiria yupo usingizini. Nikalala nikiwa mtulivu huku nikijitia kupitiwa na usingizi ingawa ukweli nilishindwa kupata usingizi. Na baada kama ya nusu saa nikaona akijigeuza na kupitisha mkono kiunoni kwangu, akawa kama amenikumbatia huku kifua chake kilichobeba matiti madogo yaliyosimama utadhani hayajawahi kunyonyesha mtoto yakinigusa mgongoni kwangu. Moyo wangu ukasimama kwa muda.
Sikutaka papara. Nilijikausha ili nione kitakachoendelea. Nikaona ule mkono ukianza kutambaa taratibu mwilini kwangu na kushuka hadi kiunoni na kisha taratibu akauzamisha ndani ya bukta yangu na kuanza kunichua taratibu mbeleni… dah, kufika hapo nikashindwa kuvumilia, nikaamua kumkabili.
Kilichoendelea baada ya hapo kilibadili kabisa mkondo wa maisha yetu na kutufanya tuanze kuishi maisha ya mke na mume, tukiishi pale pale kwenye nyumba aliyokuwa amepanga, eneo la Manzese B.
Kuanzia hapo maisha yalikuwa ya kupendeza sana, chumba chetu kimoja sasa kilionekana kutotosha tena. Nililazimika kufanya kazi kwa bidii na wakati huo Zainabu naye akawa anafanya kazi zake.
Kwa kuwa nilifahamu kuwa Zainabu alikuwa na kiwanja alichoachiwa na mama yake mkubwa katika eneo la Kichangani, nikafanya juhudi na kufanikiwa kujenga kijumba cha chumba kimoja, sebule na jiko katika eneo hilo, kisha nilifanikiwa kununua kitanda cha futi nne na nusu na godoro jipya, na samani zingine za ndani, kisha mimi na Zainabu tukahamia hapo.
“Sikutarajia kabisa!” Zainabu alisema siku ya kwanza tu baada ya kuhamia kwenye nyumba hiyo huku akiwa ameweka viganja vyake vya mikono mashavuni kwa mshangao. Kisha alinikumbatia mara kadhaa. Sikuwahi kumwona Zainabu akiwa na furaha kiasi kile.
Kisha alinikumbatia na kuanza kunipapasa maungoni. Mikono yake ilipanda juu mpaka kichwani na kisha kushuka chini karibia na kiuno. Alikuwa amejifunga khanga moja tu nyepesi ambayo ilisadifu umbo lake.
Macho yake yalikuwa yamelegea na mdomo wake ameuweka wazi kana kwamba amebanwa na mafua. Alikuwa akinitazama kwa matamanio. Kisha hakusema jambo. Nami sikusema jambo. Tulitazamana macho yetu yakisema kila kitu.
Kisha sikujua nini kilitokea, nilijikuta nipo mdomoni mwa Zainabu huku nikiwa nimeuficha mwili wake kwenye mikono yangu.
tulikuwa juu ya kitanda, alinibusu kwa ustadi na kunishika kiutaalamu. Hatukuongea chochote wala hatukujali uwepo wa mtoto aliyekuwa amelala kwenye kitanda, mpaka ilipopita saa moja na nusu, tena mimi na yeye tukiwa tunatazama kwa macho yaliyo hoi.
“Nakushukuru sana, Mgeni. Ilikuwa ni ndoto yangu kubwa kupaendeleza mahali hapa,” Zainabu alisema kwa sauti ya puani.
“Kwa nini haukuwahi kusema?” nilimuuliza huku nikimtazama machoni.
Inaendelea...