Simulizi: Harakati za Jason Sizya

Simulizi: Harakati za Jason Sizya

Mgeni mwema.jpg

162

“Nashukuru sana!” nilisema huku nikiinamisha kichwa changu kuonesha heshima kwake. Miguu yangu nilikuwa nimeibana na mikono nimeishika pamoja kwa mbele kama nanawa.

“Unaitwa nani? Sogea… sogea karibu!” Jerome aliniuliza huku akinitazama kwa umakini zaidi kama mtu aliyekuwa ananifananisha.

Nikasonga karibu na kumtazama usoni. “Naitwa Mgeni…” nilisema huku nikiwa sina uhakika wa jina la pili kwani hilo ndilo jina pekee lililokuja kichwani mwangu.

“Mgeni!” Jerome alionesha kustaajabu kidogo.

“Ndiyo, Mgeni Mwema!” Zainabu alidakia huku akiachia tabasamu.

“Oh… jina zuri kabisa!” Jerome alisema huku akiendelea kunitazama kwa umakini. Kisha akaendelea, “Kwa sababu ya Zai, jihesabie kuwa kazi umepata.”

“Sawa,” nilijibu kwa unyenyekevu mkubwa.

“Na utatakiwa kuripoti kesho hapa hapa majira ya saa moja na nusu asubuhi. Umenielewa?” Jerome aliniuliza akiwa ameweka mkono wake begani mwangu.

“Ndiyo, nimeelewa,” nilimjibu na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.

Kama ndoto, siku iliyofuata nikawa mfanyakazi wa kampuni hiyo ya kandarasi ya ujenzi wa reli ya kisasa na makazi yangu yakiwa hapo Kilosa, nyumbani kwa Zainabu. Sikujali kuhusu ukaribu uliokuwepo kati ya Jerome na Zainabu na wala sikuwaonea wivu, kikubwa mno kilichonifurahisha ni kwamba nilikuwa nimepata kazi, basi.

Baada ya kupata kazi watu huwa wanakuwa na matarajio fulani kwenye maisha, jinsi watakavyotumia kipato wanachopata kuboresha maisha yao na ya jamaa zao. Kwangu, niliwaza pia kujitegemea ili nisiwe mzigo kwa Zainabu, maana nilihisi maisha yangu yote yalikuwa yakimtegemea Zainabu. Niliapa kufanya kazi kwa bidii ili niweze kupanga chumba changu na kuanza maisha mapya.

Sasa ratiba yangu ikawa kila siku naamka alfajiri na mapema nafanya mazoezi mepesi ya viungo na karate kabla sijaenda kazini, nikitoka kazini jioni nakwenda uwanjani kucheza mpira, nikirudi namsaidia Zainabu kazi za nyumbani, na sikusahau kujisomea vitabu na machapisho mbalimbali ili kujua yanayoendelea duniani.

Siku za mwisho wa wiki, siku ambazo sikuwa nakwenda kazini nilikuwa na tabia ya kucheza na watoto wa pale mtaani kisha jioni nilitoka na kwenda gym kufanya mazoezi. Aina hiyo ya maisha ikanifanya niwe maarufu mjini Kilosa.

Wakati nikiwa bado sijafanikisha azma yangu nikajikuta nikiangukia kwenye uhusiano wa kimapenzi na Zainabu. Ingawa nilishaziona dalili mapema lakini muda wote nilijifanya sielewi. Nilianza tu kuona mabadiliko ya kimavazi kwa Zainabu akiwa mle ndani. Wakati mwingine alibaki na khanga moja tu au alivaa nguo fupi, wakati mwingine bukta! Dah… na lile umbo lake zuri nikajua tu hapa nakaribishwa.

Ndipo ilipotokea usiku mmoja ambao niliishiwa na uvumilivu na kujikuta nikilimega tunda. Siku hiyo nilijisikia vibaya baada ya tendo maana nilihisi kama nimeyachukulia matatizo ya Zainabu kuwa fursa ya kumpata. Ndiyo, nilijua alikuwa na maisha ya shida na alihitaji faraja ila nilishindwa kuzuia hisia zangu. Kwa kifupi nilitenda kinyume kabisa na itikadi yangu. Itikadi yangu ipi? Nilijiuliza lakini sikuwa na jibu…

Ilianza tu baada ya yeye kutoka kuoga, akarudi akiwa amejifunga khanga moja tu kifuani pasipo nguo nyingine ndani na hivyo kuifichua hazina ya mwili wake ulioumbika. Wakati huo mtoto Mariam alikuwa amelala. Alisimama mlangoni akawa ananiangalia kwa aibu. Mimi wakati huo nilikuwa nimejilaza kitandani nikiwa nimevaa bukta na singlendi. Macho yetu yakakutana ila bado hakuna aliyesema lolote. Nilijua wazi alichokuwa anataka lakini nilijifanya sielewi nikitamani aniambie. Nikahisi na yeye alikuwa anasubiri niseme. Lakini hakuna aliyesema kitu.

Zainabu aliendelea kusimama pale pale kama aliyepigiliwa misumali miguuni. Nikajifanya kuinuka niende nje, wakati naanza kupiga hatua kumsogelea akawa anatabasamu pasipo kusogea kando ili nipite.

“Mbona unatabasamu?” nilimuuliza huku nikimtazama machoni. Hakunijibu badala yake akainamisha uso wake chini akionekana kuwa na haya kidogo. Nikampita na kutoka nje.

Huko nje sikuwa na chochote cha maana cha kufanya, nilikaa kwenye gogo la mti kando ya nyumba kama niliyekuwa napunga upepo, niliwaza hili na lile na baadaye sana nikaamua kurudi ndani, ilikuwa ni baada ya dakika therathini, nikakuta ameshalala. Ameangalia upande mwingine. Alilala katikati huku mtoto akiwa amemlaza ukutani. Nami nikapanda kitandani na kuzama kwenye shuka. Nikashtuka baada ya kugundua kuwa Zainabu alilala uchi kama alivyozaliwa.

Hapo mwili ukanisisimka sana, sema shida ikawa naanzishaje! Mara nikasikia pumzi yake ikibadilika kuashiria yupo usingizini. Nikalala nikiwa mtulivu huku nikijitia kupitiwa na usingizi ingawa ukweli nilishindwa kupata usingizi. Na baada kama ya nusu saa nikaona akijigeuza na kupitisha mkono kiunoni kwangu, akawa kama amenikumbatia huku kifua chake kilichobeba matiti madogo yaliyosimama utadhani hayajawahi kunyonyesha mtoto yakinigusa mgongoni kwangu. Moyo wangu ukasimama kwa muda.

Sikutaka papara. Nilijikausha ili nione kitakachoendelea. Nikaona ule mkono ukianza kutambaa taratibu mwilini kwangu na kushuka hadi kiunoni na kisha taratibu akauzamisha ndani ya bukta yangu na kuanza kunichua taratibu mbeleni… dah, kufika hapo nikashindwa kuvumilia, nikaamua kumkabili.

Kilichoendelea baada ya hapo kilibadili kabisa mkondo wa maisha yetu na kutufanya tuanze kuishi maisha ya mke na mume, tukiishi pale pale kwenye nyumba aliyokuwa amepanga, eneo la Manzese B.

Kuanzia hapo maisha yalikuwa ya kupendeza sana, chumba chetu kimoja sasa kilionekana kutotosha tena. Nililazimika kufanya kazi kwa bidii na wakati huo Zainabu naye akawa anafanya kazi zake.

Kwa kuwa nilifahamu kuwa Zainabu alikuwa na kiwanja alichoachiwa na mama yake mkubwa katika eneo la Kichangani, nikafanya juhudi na kufanikiwa kujenga kijumba cha chumba kimoja, sebule na jiko katika eneo hilo, kisha nilifanikiwa kununua kitanda cha futi nne na nusu na godoro jipya, na samani zingine za ndani, kisha mimi na Zainabu tukahamia hapo.

“Sikutarajia kabisa!” Zainabu alisema siku ya kwanza tu baada ya kuhamia kwenye nyumba hiyo huku akiwa ameweka viganja vyake vya mikono mashavuni kwa mshangao. Kisha alinikumbatia mara kadhaa. Sikuwahi kumwona Zainabu akiwa na furaha kiasi kile.

Kisha alinikumbatia na kuanza kunipapasa maungoni. Mikono yake ilipanda juu mpaka kichwani na kisha kushuka chini karibia na kiuno. Alikuwa amejifunga khanga moja tu nyepesi ambayo ilisadifu umbo lake.

Macho yake yalikuwa yamelegea na mdomo wake ameuweka wazi kana kwamba amebanwa na mafua. Alikuwa akinitazama kwa matamanio. Kisha hakusema jambo. Nami sikusema jambo. Tulitazamana macho yetu yakisema kila kitu.

Kisha sikujua nini kilitokea, nilijikuta nipo mdomoni mwa Zainabu huku nikiwa nimeuficha mwili wake kwenye mikono yangu.
tulikuwa juu ya kitanda, alinibusu kwa ustadi na kunishika kiutaalamu. Hatukuongea chochote wala hatukujali uwepo wa mtoto aliyekuwa amelala kwenye kitanda, mpaka ilipopita saa moja na nusu, tena mimi na yeye tukiwa tunatazama kwa macho yaliyo hoi.

“Nakushukuru sana, Mgeni. Ilikuwa ni ndoto yangu kubwa kupaendeleza mahali hapa,” Zainabu alisema kwa sauti ya puani.

“Kwa nini haukuwahi kusema?” nilimuuliza huku nikimtazama machoni.

Inaendelea...
 
Mgeni mwema.jpg

163

“Huoni kama matendo yangu yalikuwa yanaongea mengi?” Zainabu alisema kisha akatabasamu na kunibusu, baada ya hapo tukapumzika kwa pamoja mpaka pale tulipokuja kuamka kesho yake saa kumi na mbili asubuhi. Ulikuwa ni muda sahihi wa sisi kujiandaa kwenda kazini.

Tuliishi maisha ya furaha sana na upendo wa Zainabu kwangu ulizidi, alionekana kukolea sana na siku moja tukiwa tumejipumzisha kitandani baada ya mechi ngumu ya kukata na shoka, Zainabu aliniambia, “Ujue, Mgeni… nikwambie tu ukweli, sijawahi kupenda maishani mwangu. Wewe ndo’ mwanaume wa kwanza kukupenda. Nakupenda sana.”

Nilishangazwa kidogo kisha nikamuuliza iliwezekanaje kuwa hajawahi kupenda? Vipi kuhusu Deus Mkuro? Na vipi kuhusu Jerome Mloka?

Zainabu alikuwa amelala kiupande upande tukiwa uchi, kichwa alikuwa amekiegemeza kwenye kiganja cha mkono mmoja, huku mkono mwingine ukiwa unatalii kifuani kwangu. Swali langu kuhusu Deus, baba mtoto wake, lilimfanya alale chali na kuangalia darini. Kisha alishusha pumzi.

“Ningekuwa na uwezo ningekwambia upasue moyo wangu, yote yameandikwa ndani yake lakini sina namna ya kukuthibitishia, wewe elewa tu kuwa wewe ndiye mwanaume wa kwanza kukupenda, kwa dhati. Naapa sijawahi kupenda kama nikupendavyo, Mgeni,” Zainabu aliniambia huku akiendelea kutazama darini.

Niliendelea kufanya kazi katika mradi ule wa ujenzi wa reli ya kisasa kwa miezi sita tu kisha nikaacha kazi baada ya kutofautiana na bosi wangu Jerome. Hii ilikuwa baada ya Jerome kubaini kuwa sikuwa binamu wa Zainabu bali mpenzi wake na tulikuwa tukiishi pamoja kama mke na mume.

Jerome alianza visa dhidi yangu huku akinitafutia sababu ya kuniondoa kazini. Siku moja nilichelewa kwa takriban dakika ishirini tu kufika kazini kwa sababu usiku ulioitangulia siku hiyo tulichelewa kulala kutokana na matatizo ya kiafya ya mtoto Mariam. Nilipofika kazini nilimkuta Jerome akinisubiri getini huku amekasirika sana.

“Unakuja kazini muda huu?” ilikuwa ndiyo salamu niliyopewa na Jerome. Alikuwa amesimama langoni yeye pamoja na vibaraka wake wawili.

Nilishangazwa sana na swali lake kwa kuwa muda huo ilikuwa ni saa moja na dakika hamsini.

“Samahani sana, bosi, kulikuwa na dharura…” nilimjibu nikitaka kuingia ndani.

Jerome akaniwekea mkono wake mpana kifuani mwangu akisema, “Si haraka hivyo!”

Nilishusha pumzi huku nikimtazama kwa umakini.

“Sikia we fala…” Jerome aliniambia huku akiwa amenikazia macho ya ghadhabu. “Nimepata taarifa zako… Nakuonya kaa mbali na Zai kabla sijakufanyia kitu ambacho hutakisahau maishani kwako. Tumeelewana?”

Nilimtazama Jerome kwa sekunde kadhaa, hasira za ghafla zilianza kunipanda.

“Hilo si tatizo langu, ungemtafuta huyo unayedai ni mwanamke wako muongee kuhusu matatizo yenu, sawa? Halafu siku nyingine ukinifanyia huu ujinga nitasahau kama wewe ni bosi wangu niyapoteze meno yako yote ya sebuleni. Tishia hao hao vibaraka wako nyuma!” nilimwambia pasipo woga wowote wala kupepesa macho.

Jerome alikasirika, akataka kunikwida shati lakini vibaraka wake wakawahi kumtuliza. Akaishia kunisonya huku akinitazama kwa hasira, uso wake ulizidi kuwa mwekundu kwa hasira. Sikujali, nikaelekea zangu ofisini pasipo kumjali. Nilibadili nguo zangu na kuchukua vifaa vya kazi, kisha nikaelekea kwenye majukumu yangu niliyopangiwa.

Nilifanya kazi hadi ilipotimu saa sita mchana, nikawa nimeketi kwenye eneo la mtambo wa kuchimbia mashimo huku nikiwa nina mawazo mengi wakati wenzangu wakiendelea kuchapa kazi. Mara nikamwona Zainabu akinijia akiwa na huzuni huku akilengwalengwa na machozi.

Alikuja akaniambia kwamba Jerome alikuwa amemfuata na kumtishia maisha yake kuwa angemfanyia kitu kibaya sana endapo asingeachana na mimi na alikuwa amempa siku mbili tu achague kati ya kuendelea na mimi au kazi vinginevyo angehakikisha hapati nafasi ya kuendelea kuwapika chakula hapo kambini. Pia Jerome alimwambia kuwa mimi lazima niondolewe kazini kama sikuwa tayari kuachana na Zainabu.

Nilihamaki sana, na zaidi nilipatwa na hasira. Sikutaka kuendelea kufanya kazi kwani nilishafahamu kuwa huo ulikuwa mwendelezo wa visa vya Jerome juu yangu, na hivyo hakupaswa kuchekewa. Nilimfuata! Damu yangu ilikuwa inachemka na kwenda kasi ndani ya mishipa ya damu.

Jamani msinichukulie poa. Linapokuja suala la kukipigania kitu changu nikipendacho basi nilikuwa bedui haswa! Hivyo kama mbogo aliyejeruhiwa nilikwenda kusimama mbele ya uso wa Jerome huku nikimtazama kwa hasira.

“Nisikie wewe, bwege!” nilipaza sauti yangu na kufanya wafanyakazi wengine waliokuwepo eneo hilo kugeuka na kunitazama kwa mshangao mkubwa.

“Hili ni onyo langu kwako. Onyo langu la mwisho, sawa? Usidhani wewe ndiye mgawa riziki kwenye maisha yetu, hivyo ukiendelea na vitisho vyako vya kipumbavu, kwa namna yoyote ile, nitakuvunja vunja usiamini macho yako!” nilimwambia Jerome kwa ghadhabu.

Jerome aliangua kicheko cha dharau huku akinisogelea karibu. “We fala umesemaje?” kabla sijajibu akaendelea, “Nitafanya chochote nitakacho na hakuna yeyote atakayeingilia. Si wewe wala fala yeyote!”

Sasa alikuwa karibu yangu na tulitazamana uso kwa uso. Kwa kuwa alikuwa amenizidi urefu basi akawa ananitazama kwa chini kidogo akiwa amefuma ndita zake usoni. Sikuwa namwogopa abadani, zaidi alikuwa ananipandisha hasira zaidi.

Nilijitahidi kwa nguvu zangu zote nisifanye jambo la kipumbavu ambalo lingenigharimu lakini niliona stara yangu ikiniponyoka. Kufumba na kufumbua nikamkwida shati na kumsogeza karibu zaidi na uso wangu, nilijiwa na wazo moja tu, nimtandike kichwa matata lakini kabla sijafanya chochote, watu waliingilia kati na kuamulia ugomvi.

Kilichofuata baada ya hapo ilikuwa kupelekwa kwa meneja na kisha nikakabidhiwa barua ya kuachishwa kazi kwa sababu ya utovu wa nidhamu. Sikujali. Nikaondoka hapo na kurudi nyumbani.

Tukio la kumwida Jerome nikitaka kumpiga na kusababisha niachishwe kazi lilimshangaza kila mtu aliyenifahamu hasa meneja na wafanyakazi wenzangu maana mara nyingi meneja alitolea mfano kwangu namna nilivyokuwa ninajituma kufanya kazi kwa bidii na bila kinyongo. Nilikuwa nikisikia hata akinisifia kwa upole na ukimya.

Ukweli ni kwamba, kama sijakuzoea ungeweza kudhani nilikuwa mpole na mkimya sana. Lakini kwa watu wachache sana tuliofahamiana walijua kuwa mimi ni mwongeaji mzuri sema si kwa sana kama ilivyokuwa kwa rafiki yangu Almasi Dilunga.

Hata hivyo, Zainabu alikuwa ameshangazwa zaidi, aliniuliza kwa nini nimefanya hivyo maana kazi hiyo ilikuwa msaada mkubwa kwetu.

“Nimelazimika kufanya hivyo kwa kuwa sipendi mtu yeyote akunyanyase, nitakulinda kwa nguvu zangu zote. Pia kumbuka mradi wa ujenzi wa reli si wa milele, siku moja utafikia mwisho na maisha yetu hayawezi kutegemea kibarua hicho milele,” nilimwambia nikiwa natazama macho yake.

Inaendelea...
 
Mgeni mwema.jpg

164

Zainabu aliendelea kunishangaa kwa muda kidogo halafu akatabasamu kiuongo. Kisha aliniuliza huku akinikazia macho, “Unadhani huo ni uamuzi sahihi kwa sasa?”

“Hata kama nisingeacha kazi sasa bado ingefika wakati nisingekuwa na kazi hii!” nilimwambia huku nikimshika mkono wake wa kushoto. “Najua tunahitaji fedha, nimejiandaa kukabiliana na hilo.”

“Najua utakuwa umejiandaa kwa hilo, nakuamini…” Zainabu alisema huku akiwa anatazama chini. Kisha alinitazama kwa upendo na kuniuliza, “Unaamini mambo yatakwenda vizuri?”

“Ndiyo, kwa nini isiwe hivyo?” nilimwambia kwa kujiamini. “Yatakwenda vizuri na wewe pia ndoto zako zitafanikiwa, nakuahidi hilo.”

Hapo nikamwona akiachia tabasamu la kweli na kunikumbatia kwa nguvu. “Nakupenda sana, Mgeni,” Zainabu alisema kwa sauti ndogo ya kunong’ona iliyopenya vyema kwenye ngoma ya sikio langu.

Nami nilimkumbatia kwa nguvu na kumweleza hisia zangu. Hakuna yeyote kati yetu aliyetaka kumwachia mwenzake, tulitamani tuhame kabisa toka dunia hii, twende kwenye sayari ya peke yetu, wawili tu, tukaishi huko, lakini haikuwa inawezekana. Muda mwingine ni bora ukaishi ndotoni kwani maisha halisi yanakuwa katili mno.

Kwa kutumia fedha kidogo niliyokuwa nadunduliza na kwa kuongezea na fedha aliyokuwa akiipata Zainabu tulifanikiwa kufungua biashara ya duka-genge ambalo alilisimamia Zainabu na mimi nikawa najishughulisha na shughuli mbalimbali za ujenzi.

_____

Nilizinduliwa toka kwenye mawazo yangu na sauti nzito ya Daktari Nasri Faiz, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Watoto, aliyenisalimia baada ya kuja moja kwa moja kwenye kitanda alipokuwa amelazwa mtoto Mariam. Daktari Faiz alikuwa ameambatana na madaktari wengine wawili na muuguzi wa wadi ile ya watoto.

Daktari Faiz alikuwa mwanamume mfupi na mnene, rangi ya ngozi yake ilikuwa ya maji ya kunde, akiwa na umri wa miaka 57 alikuwa na nywele fupi zenye mvi kiasi na uso wake ulikuwa mpana huku miwani yake mikubwa ikiwa imeyahifadhi macho yake makubwa.

Asubuhi hiyo alivaa suruali ya kitambaa cha kadeti cha rangi ya khaki, shati kubwa jeusi lililokuwa na mistari myeupe ya pundamilia na juu yake alikuwa amevaa koti refu jeupe la kidaktari na kuning’iniza shingoni kwake kifaa maalumu cha kupimia mapigo ya moyo, kwa kitaalamu kiliitwa ‘stethoscope’.

Sikukumbuka kama niliitikia salamu yake ila nilipozinduka nilimwona akiwa amesimama akiitazama kwa makini ile damu iliyokuwamo ndani ya ile chupa aliyokuwa ametundikiwa Mariam. Kisha alionekana kumchunguza Mariam kwa macho kabla hajamgusa kwenye paji la uso wake, halafu aliitazama tena ile damu ndani ya chupa kwa umakini.

Aliyatazama kwa muda matone ya damu jinsi yalivyokuwa yanadondoka na kuingia kwenye mrija maalumu uliopeleka damu kwenye mshipa wa damu kichwani kwa Mariam na kuonekana kuridhika kisha alipeleka macho yake kusoma maelezo kwenye faili la ugonjwa wa Mariam alilokuwa amelishika mkononi na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.

Baada ya kusoma maelezo kwa kitambo kifupi aliinua uso wake kuwatazama wale madaktari wenzake alioambatana nao. Sikuelewa mara moja iwapo wale walikuwa madaktari wanafunzi au ni madaktari bingwa kama yeye.

Alionekana kuwaeleza jambo fulani ambalo sikulifahamu kuhusiana na afya ya Mariam. Baada ya mazungumzo mafupi ya kitabibu kati ya Daktari Faiz na wale madaktari, Daktari Faiz aliandika taarifa fulani kwenye lile faili la ugonjwa wa Mariam kisha alimgeukia muuguzi wa wadi ya watoto aliyefuatana naye.

Muuguzi huyo alikuwa mwanamama mtu mzima mwenye umri wa kati ya miaka 40 na 45, mrefu wa wastani, si mweusi wala si mweupe kwa rangi. Alikuwa na mashavu mfano wa chungwa na alikuwa na nywele nyingi kichwani, nyeusi fii.

Alikuwa amevaa sare maalumu ya kiuguzi, gauni jeupe refu na pana kiasi. Kiunoni alikuwa amevaa mkanda mpana mweusi na kofia ndogo nyeupe ya kiuguzi yenye lesi iliyofunika sehemu ya utosi wa mbele kichwani kwake.

Kwa sekunde chache Daktari Faiz alionekana kumweleza jambo fulani yule muuguzi kwa lugha ya kitabibu kuhusiana na tatizo la Mariam. Kisha yule muuguzi alibetua kichwa chake kukubali.

Daktari Faiz akanitupia jicho mara moja tu na kumgeukia Zainabu.

“Poleni sana kwa kuuguza, Mungu atamuauni mtoto na maradhi haya na atakuwa sawa,” Daktari Faiz alisema na kuachia tabasamu.

“Ahsante sana daktari,” nilisema huku nikishusha pumzi za ndani kwa ndani na kumeza mate kutowesha koo langu lililokauka.

Zainabu hakusema neno bali alitabasamu na kushusha pumzi za ndani kwa ndani kisha nilimwona akimeza mate kutowesha koo lake, uso wake ulionesha kukata tamaa.

Daktari Faiz aliachia tena tabasamu pana la faraja na kuwapa ishara watu alioambatana nao kisha wakaondoka.

Walipoondoka nilijikuta nikianza tena kuzama kwenye lindi la mawazo: kumbukumbu ya ndoto kuhusu tukio fulani ambalo sikulijua ilinijia akili kwangu.

Ilikuwa ni kama niliyekuwa natazama filamu ya kuhuzunisha. Ndoto hiyo ilikuwa imejirudia kwa takriban mara tatu na sikuweza kuielewa tafsiri yake! Ilikuwa ndoto iliyonipa mawazo, ikanitisha na kunikosesha raha.

Ilikuwa ni mchanganyiko wa picha zisizoeleweka za ajali ya gari dogo lililogongana na roli la mafuta na kusababisha moto mkubwa, na katikati ya moto huo sauti ya mwanamke aliyekuwa akilia kwa hofu na uchungu mkubwa ikasikika…

Mara nikazinduka kutoka kwenye yale mawazo, nikazungusha macho yangu kutazama huku na huko na kisha nikamtazama Zainabu aliyekuwa ameketi kwa utulivu kitandani akimtazama Mariam kwa huzuni.

Nilimuaga Zainabu kuwa nilikuwa naenda kwenye mgahawa kumchukulia supu na chapati ili afungue kinywa maana alikuwa hajatia chochote tumboni tangu kumekucha. Zainabu alinitazama tu pasipo kusema chochote kisha akashusha pumzi ndefu. Nilitoka huku ile sauti ya mwanamke aliyekuwa akilia kwa hofu na uchungu mkubwa ikitengeneza mwangwi akili mwangu na kunitia wasiwasi zaidi.

Inaendelea...
 
Mgeni mwema.jpg

165

Nilipotoka ndani ya ile wadi ya watoto nilisimama katikati ya korido pana ndefu iliyokuwa tulivu japo kulikuwa na pilika pilika za watu waliokuwa wakienda na kurudi kutoka kwenye zile wadi. Kama ilivyokuwa katika mazingira mengine ya ile hospitali, mandhari yale yalikuwa ya kupendeza yaliyowakilisha ustaarabu, usafi na yenye kuvutia.

Kulikuwa na hewa safi iliyokuwa ikisambazwa taratibu na viyoyozi kadhaa vilivyokuwa juu ya dari ya ile korido pana iliyokuwa imetengenezwa kwa gypsum nzuri ya rangi nyeupe na katika sehemu za dari ile kulining’inizwa taa nzuri. Kamera za CCTV zilikuwa zimetanda kila kona.

Nilisimama kando nikampisha Muuguzi mmoja mwanamume aliyekuwa akisukuma kiti cha magurudumu kilichokuwa kimekaliwa na mgonjwa aliyeonekana kama nusu mfu akiwa na mrija wa drip kwenye mkono wake.

Muda mfupi uliofuata nililiacha lile eneo na kushika uelekeo wa upande wa kulia nikiipita sehemu ya maliwato iliyokuwa upande wa kushoto.

Mbele kidogo niliingia upande wa kushoto na baada ya hatua chache mbele yangu niliviona vyumba vya lifti za kupanda na kushuka katika ghorofa za lile jengo la hospitali. Niliachana na zile lifti nikazifuata ngazi na kushuka taratibu kuelekea chini kabisa ya lile jengo.

Bado kumbukumbu juu ya ndoto kuhusu ajali ya magari yaliyogongana ziliendelea kupita kichwani kwangu. Pia maswali mengi kichwani kwangu kuhusu asili yangu yaliendelea kunisumbua na yalihitaji majibu lakini sikujua ningeyapata wapi majibu hayo.

Nilipofika sehemu ya chini ya lile jengo nikajikuta katikati ya korido pana ambayo pia ilikuwa na pilika pilika lakini hakukuwa na kelele. Mazingira yalikuwa ya kupendeza na kulikuwa na hewa safi iliyokuwa ikisambazwa taratibu na viyoyozi vilivyokuwa juu ya dari ya ile korido pana kama ilivyokuwa kwa maeneo mengine ya hospitali ile.

Taratibu nilianza kutembea katikati ya ile korido huku nikipishana na wafanyakazi na watu wengine. Nilitembea taratibu hadi nilipofika mwisho wa ile korido na kutokea kwenye ukumbi mpana wa eneo la Mapokezi, hapo niliwakuta watu kadhaa waliokuwa wameketi kwenye viti wakisubiri huduma.

Nilishusha pumzi na kutaka kuendelea na safari yangu lakini nilisita na kusimama, macho yangu yalivutwa kumtazama mwanadada mmoja aliyekuwa ameketi kwenye kiti akisoma gazeti. Nilimtazama kwa umakini sana, sikujua kwa nini nilivutwa kumtazama mwanadada huyo kiasi kile, hata nilipotaka kuondoka nilijikuta nikisita tena na kumtazama kwa udadisi zaidi!

Mara nikapata wazo; nilidhamiria kumfuata yule dada kwa kuwa nilihisi pengine angeweza kuwa na msaada fulani kwangu katika kujibu maswali yaliyonizonga kichwani. Maswali kuhusu asili yangu na mengineyo.

Kimwonekano yule dada alikuwa na umbo kubwa lililovutia sana kiasi cha kulifanya kila jicho linalomwona kumtazama mara mbili mbili pasipo kukinai. Alikuwa mrefu wa wastani na mweupe, lakini si ule weupe wa kujichubua bali wa asili.

Rangi yake ya ngozi ilikuwa na mng’aro wa aina yake na ilipendeza kiasi cha kumfanya kuonekana bado msichana mdogo ingawa nilihisi hali hiyo ilikuwa tofauti na umri aliokuwa nao. Alikuwa na macho yaliyokuwa yanaita kwa mng’aro sadifu, yakiambatana na kope nyingi nyeusi ambazo ziliachia nafasi kwa nyusi ili zipate kujidai. Midomo yake ilikuwa minene yenye kingo nyepesi na mikunjo midogo midogo.

Nilisimama pale nikijishauri kwa kitambo kifupi kisha nikapiga moyo konde na kumfuata, nilipomfikia nilimgusa begani kwa nyuma. Yule dada aligeuka haraka huku mapigo ya moyo wake yakionekana kwenda mbio isivyo kawaida. Nilimwona akinitazama kwa umakini kama aliyekuwa anajiuliza aliniona wapi.

“Samahani dada, nimekushtua, eh?” nilimuuliza huku macho yangu yakionesha tabasamu la kuomba radhi.

Yule dada aliendelea kunitazama kwa umakini kwa nukta kadhaa akinikodolea macho. Nilihisi kama vile alikuwa akijiuliza maswali ambayo hayakuwa na majibu, mwisho alimudu kutamka, “Hapana, usiwe na wasiwasi, kaka!”

“Naitwa Mgeni… Mgeni Mwema,” nilisema huku nikiketi kwenye benchi jirani na alipokuwa ameketi mwanadada huyo. Na hapo macho yangu yakaangukia kwenye gazeti aliloshika.

“Gazeti gani hilo?” nilimuuliza huku nikimtazama usoni.

Hakunijibu bali alinyoosha mkono wake kunipa lile gazeti huku akinitazama kwa umakini zaidi. Nililipokea lile gazeti na kulitupia jicho mara moja tu, macho yangu yakatua kwenye jina la gazeti hilo lililoandikwa kwa maandishi makubwa mekundu: HabariLeo.

Hata hivyo sikuwa na nia ya kulisoma bali niliendelea kumporomoshea maswali mfululizo. “Umelinunua hapa hapa hospitali?”

“Kwa nini?” yule mwanadada aliniuliza kwa mshangao. Sauti yake ilikuwa ya upole kila alipoongea.

“Aah… nimeuliza tu! Kwani kuna ubaya?” nami niliuliza kwa upole huku nikiendelea kumtazama usoni.

“Hapana! Nililinunua mjini wakati nakuja hapa. Lakini kama unalihitaji naweza kukuachia nitanunua jingine,” yule mwanadada alijibu kwa upole huku akiachia tabasamu.

“Usijali,” nilisema huku nikiligeuza geuza lile gazeti, nilifungua na kutupia macho kurasa mbili tatu, nikalifunga na kumkazia macho yule mwanadada.

“Hivi nimekutambulisha jina langu, eh?” nilimuuliza.

“Mgeni Mwema, au sivyo?” yule mwanadada alijibu kwa kunisaili.

“Ndiyo, na wewe unaitwa nani?” nilimtandika swali jingine huku nikiendelea kutabasamu.

“Mmh! Kwani una shida gani, kaka?” yule mwanadada aliguna na kunitupia jicho la udadisi zaidi akionekana kuwa makini zaidi.

Nilisita kidogo na kuangalia kando kwa kitambo, nilitamani sana kumpata mtu wa kunifumbulia fumbo ambalo lilikuwa likinitesha kwa miezi saba, fumbo lililokuwa likinitatiza sana na kunifanya nisijue nianzie wapi!

“Samahani, naomba nikuulize jambo…” hatimaye nilimudu kusema baada ya kushusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Ruksa, niulize!” yule msichana alijibu huku akiendelea kunitazama kwa udadisi. Tukabaki tumetazamana kwa kitambo fulani.

“Kwa kweli nashindwa hata nianzie wapi maana…” nilisema nikiwa nimekata tamaa na kusita, moyo wangu uligwaya na kunienda mbio isivyo kawaida, na mdomo wangu ukawa mzito kusema nilichotaka kuuliza!

“Kama nimekukwaza kwa njia yoyote ile naomba uniwie radhi, kwa kweli ninayo maswali mengi ninayohitaji majibu lakini huenda wewe unaweza usiwe na majibu hayo…” nilisema kwa huzuni na kuongeza, “Samahani sana, dada.”

Kisha nilikohoa kidogo kusafisha koo langu halafu nikanyanyua mabega yangu juu na kubetua midomo yangu kama ishara ya kusalimu amri, nikainuka taratibu na kumtaka radhi tena yule dada, nikaondoka zangu nikimwacha anashangaa.

Wakati natembea nilikuwa na uhakika kuwa macho yake yalikuwa yakinitazama kwa umakini, huenda alikuwa akijiuliza kama nilikuwa sawa kiakili au nilikuwa na tatizo kubwa lililohitaji msaada wa kisaikolojia.

Sikujali. Niliendelea na safari yangu na kutokea mbele ya jengo la Hospitali ya Benjamin Mkapa, hapo nikajikuta nikikabiliana na macho ya watu kadhaa wakiwemo madereva wa teksi waliosubiri watu wenye mahitaji ya usafiri wa kwenda sehemu mbalimbali za mji. Niliwapita bila kuwatilia maanani.

Inaendelea...
 
Mgeni mwema.jpg

166

Eneo lile la mbele ya Hospitali ya Benjamain Mkapa lilikuwa pana lililopandwa miti mizuri mirefu ya kivuli iliyolifanya kupendeza. Pia kulipandwa nyasi nzuri laini katikati ya bustani nzuri ya maua baina ya sehemu moja ya maegesho ya magari na sehemu nyingine.

Nilitembea taratibu katika barabara ya lami huku nikiyatazama kwa umakini mandhari ya eneo lile nikielekea kwenye mghahawa wa chakula. Wakati nikitembea niliwapita wahudumu wa huduma za usafi wa kampuni moja ya usafi waliohemewa na kazi kuhakikisha mazingira ya eneo lile yanakuwa safi.

Mara moyo wangu ukapiga kite kwa nguvu baada ya kuliona gari moja la wagonjwa likija upande wangu kwa mwendo wa kasi na kunipita kisha likakata kona na kwenda moja kwa moja kusimama mbele kabisa ya lango kuu la kuingilia kwenye ile hospitali.

Sikujua kwa nini moyo wangu ulishtuka kiasi kile na kuvutwa kulitazama lile gari la wagonjwa, hata hivyo nilijikuta nikipatwa tu na shauku kubwa ya kutaka kumfahamu mgonjwa aliyeletwa na lile gari la wagonjwa. Nilikuwa kama mtu aliyetarajia kumwona mtu fulani aliyemfahamu akitoka ndani ya lile gari la wagonjwa.

Nililitazama kwa umakini mkubwa huku macho yangu yakivutwa kumtazama mwanadada mmoja mrefu na mrembo aliyeshuka kutoka ndani ya lile gari akiwa ameinamisha kichwa chake kwa huzuni huku akiongea na simu. Kimwonekano alikuwa na umri wa kati ya miaka ishirini na sita na therathini.

Alikuwa amevaa suruali ya bluu ya dengrizi na blauzi nyekundu. Kichwani alikuwa amevaa kofia ya kapelo ya rangi ya bluu na miguuni alivaa raba nyekundu.

Nilipomtazama vizuri niliuona uso wake wenye nyusi nyingi na kope zake zilikuwa zimechongwa kwa ustadi mkubwa na kupakwa wanja uliomfanya kupendeza mno na hivyo kuyafanya macho yake yawe wazi nusu. Pua yake ndogo iliiacha midomo yake ijidai kwa kuhifadhi meno meupe yaliyojipanga vizuri, huku yakiachia uwazi mdogo kwa mbele yaani mwanya. Kwa rangi mwanadada huyo alikuwa maji ya kunde.

Nguo zake zilizombana kiasi zililichora vyema umbo lake refu la kuvutia lenye kiuno chembamba lakini imara kilichoshikilia minofu ya mapaja yake iliyokaza. Kwenye bega alikuwa amening’iniza mkoba mzuri wa bluu ambao thamani yake ilitosha kabisa kumpa mwananchi wa kipato cha chini uhakika wa mlo kwa wiki kadhaa.

Wakati nikiuajabia uzuri wa yule mwanadada nikawaona wafanyakazi wa ile hospitali wakifika kwenye lile gari la wagonjwa wakiwa na kitanda cha magurudumu na muda mfupi baadaye walikuwa wamemtoa mgonjwa na kumlaza kwenye kile kitanda. Mgonjwa huyo alikuwa mwanadada ambaye rika lake halikuonekana kutofautiana na yule mwanadada mrefu na mrembo alishuka toka ndani ya lile gari la wagonjwa.

Mkono wa kulia wa yule mgonjwa ulikuwa umechomekwa sindano yenye mrija ambao ulipeleka maji yaliyokuwa na dawa ndani yake kwenye mishipa ya damu.

Haraka haraka wale wauguzi walimwondosha yule mgonjwa toka eneo lile wakikisukuma kile kitanda na kuelekea eneo la mapokezi. Yule mwanadada mrefu na mrembo aligeuka upande wangu, tukatazamana na hapo nikamwona akishtuka kidogo lakini akaitwa na muuguzi mmoja na kuondoka haraka akiwafuata wale wauguzi kwa nyuma huku akionekana mwenye wasiwasi mwingi. Alikuwa anatokwa na machozi na muda wote alionekana kuongea na simu, huenda alikuwa akiwawasiliana na ndugu na jamaa.

“Mpitisheni huku moja kwa moja,” nilimsikia mmoja wa wafanyakazi wa mapokezi akisema huku akiwaelekeza wale wauguzi sehemu ya kumpeleka yule mgonjwa.

Nilibaki nimesimama pale pale kama niliyepigiliwa misumali huku nikiwatazama kwa umakini kisha nilianza kuwafuata nikitaka kufahamu yule mgonjwa alikuwa nani na alikuwa na tatizo gani, lakini nilikuwa nimechelewa kwani walikuwa wamekwisha potelea ndani.

Nilibaki pale kwa dakika kadhaa nikiwa najishangaa, sikujua kwa nini nilivutiwa sana kutaka kujua habari za yule mgonjwa asiyenihusu. Nikashusha pumzi za ndani kwa ndani huku nikimhurumia sana yule mgonjwa ingawa sikumfahamu na sikujua ni lipi tatizo lililokuwa linamsumbua.

* * *

Endelea kufuatilia...
 
View attachment 2259080
157

Labda uniite Mgeni…


Saa 4:30 asubuhi…

NDANI ya wadi ya watoto katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, iliyojengwa katika eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) jijini humo, mtoto Mariam Mgeni mwenye umri wa miaka miwili na nusu, alikuwa amelala nusu mfu kwenye kitanda cheupe cha chuma chenye godoro nene la foronya laini na mto laini wa kuegemeza kichwa.

Hospitali ya Benjamin Mkapa ilionekana dhahiri kuwakilisha mapinduzi makubwa nchini katika sekta ya afya. Ilikuwa mojawapo ya hospitali za kisasa zenye ustaarabu, usafi na mandhari yenye kuvutia kiasi cha kutoa liwazo kwa wagonjwa hata kabla ya kupata tiba. Ilikuwa na mifumo ya kisasa kabisa ya teknolojia iliyokuwa inarahisisha utendaji kazi na utunzaji wa takwimu za hospitali ile.

Mfumo uliokuwepo ulikuwa ni ule wa kusafirisha sampuli ndani ya hospitali kwa njia ya ‘mawimbi hewa’ ambao ulisaidia sana katika kuharakisha usafirishaji wa sampuli na hivyo kuepusha ucheleweshaji wa vipimo.

Uwepo wa vifaa tiba vya kutosha na matumizi ya teknolojia katika hospitali ile uliwezesha pia utoaji wa mafunzo na huduma bora za matibabu, uchunguzi wa magonjwa na kufanya tafiti za fani za afya zilizo bora hapa nchini, lakini pia ulipunguza kwa kiasi kikubwa gharama zilizokuwa zinatumika kwa ajili ya matibabu nje ya nchi.

Pale kitandani mtoto Mariam alikuwa anapumua kwa shida sana kutokana na kusumbuliwa na tatizo la seli mundu lililokuwa likisababisha apungukiwe na damu mara kwa mara na hata kupata matatizo ya kupumua.

Kando ya kitanda chake kulikuwa na stendi ndefu ya chuma ya kitabibu iliyokuwa imetundikiwa chupa ndogo ya damu na mrija wake ukipeleka damu kwenye mshipa wa damu kichwani kwa Mariam.

Kando ya ile stendi ya chuma kulikuwa na meza ndogo na juu yake kulikuwa na trei ndogo ya chuma iliyokuwa na vifaa-tiba kama mikasi, plasta, bomba la sindano, glavu, chupa kubwa ya maji safi, bilauri, chupa ndogo ya dawa ya sindano na dawa za maji kwa ajili ya tatizo lake la seli mundu.

Baadhi ya vifaa hivyo vilikuwa vimefunguliwa na kuachwa wazi baada ya kutumika.

Mwanadada Zainabu Pembe, mama wa Mariam alikuwa ameketi ukingoni mwa kitanda alicholala Mariam akiwa mwenye huzuni. Muda wote alikuwa mtulivu sana na alikuwa anamtazama Mariam katika namna ya kukata tamaa, alionekana kuwa mbali sana kimawazo na machozi yalikuwa yanamlengalenga machoni muda wote.

Zainabu alikuwa na umri wa miaka 22 na alikuwa amejaaliwa sura nzuri na umbo, alikuwa msichana mwenye mvuto sana na uzuri wa asili uliofichwa kutokana na hali duni ya maisha na hivyo ilikuwa vigumu kuuona. Alikuwa mrefu kiasi na mweupe.

Kiuno chake chembamba kilikuwa kimefinyangwa katika namna ya kulifanya umbo lake liweze kuitaabisha kila nafsi ya mwanamume yeyote asiyekuwa na msimamo.

Asubuhi hiyo alikuwa amevalia gauni zuri la kitenge lililoshonwa kwa mtindo wa ‘Ankara midi tube dress’ na alijifunga khanga kiunoni huku nguo zake zikiushika vyema mwili wake na kulichora umbo lake maridhawa, na miguuni alivaa makubazi ya kike.

Mimi, Mgeni, nilikuwa nimesimama kando ya kitanda nikimtazama mwanetu Mariam kwa huzuni. Sikuwa na raha, muda wote nilikuwa njia panda nikiwa na wasiwasi mwingi, si kutokana tu na hali ya Mariam bali pia kutokana na ukweli ambao uliendelea kuitesa akili yangu kwa takriban miezi saba sasa.

Nikiwa na umri wa kati ya miaka therathini na therathini na tano – kwa kuwa sikuujua umri wangu – nilikuwa mrefu na mwenye mwili wa kimazoezi. Asubuhi hiyo nilivaa suruali ya dengrizi ya rangi ya bluu mpauko, shati la mikono mirefu la rangi ya samawati, raba nyeusi na miwani myeusi ya jua niliyoipandisha kichwani juu ya uso wangu.

Huku nikimtazama Mariam sikuacha kutafakari kuhusu maisha yangu na hatma yangu. Nilikuwa nawazia kitu ambacho kilikuwa kikinitatiza sana na kukaribia kunitia uwendawazimu kwa takriban miezi saba, tangu nijifahamu. Nilijiuliza sana lakini bado sikuwa napata majibu: “Hivi mimi ni nani hasa?”; “Asili yangu ni wapi?”; “Jina langu nani?” n.k.

Hata hivyo, niliamini kuwa kujiuliza maswali hayo ni kupoteza muda tu maana nisingepata majibu abadani. Lakini si mimi tu, bali hakuna mtu yeyote kati ya watu walionizunguka aliyeijua asili yangu, jina langu, kabila langu, dini yangu wala jamaa zangu.

Jambo hili lilikuwa linaniumiza sana na hata kunitia hofu; kutokuijua asili yangu wala jina langu kulinifanya niishie kujiita “Mgeni” na Zainabu aliniongezea jina la “Mwema” baada ya kumnusuru kwenye kadhia fulani. Kwa maana hiyo nikawa najulikana kwa jina la Mgeni Mwema.

Maumivu makali yalikuwa yakiutesa moyo wangu hasa pale nilipotaka kukumbuka hata jina langu halisi lakini nikashindwa, sikukumbuka kitu chochote, niliishi maisha ya tabu sana, kila kitu kwenye maisha yangu kilikuwa kipya kabisa! Sikufahamu chochote kuhusu ulimwengu, kila kitu kilikuwa ni giza ndani ya maisha yangu.

Ilitokea tu siku moja, takriban miezi saba iliyokuwa imepita, nilipopata fahamu nikajikuta nipo katika Mji wa Kilosa, sikujua nilifikaje hapo Kilosa. Rafiki zangu walikuwa wananitania wakidai kuwa “eti” nilizuka tu kama kumbikumbi!

Sasa kumbukumbu zangu zilinirudisha miezi saba iliyokuwa imepita… siku ambayo nilizinduka toka kwenye usingizi mzito sana. Kilichonizindua ni baridi kali iliyoambatana na upepo wa kipupwe ambao ulinipiga mwili na kunifanya nijikute nikitetemeka na meno yangu yakigongana. Nilikuwa nimelala kwenye baraza ya jengo moja katikati ya mji, karibu na kituo cha mabasi, peke yangu. Jogoo waliokuwa wakiwika huko na huko waliniashiria kuwa ilikuwa alfajiri.

“Niko wapi?” nilijiluliza nikiinuka na kutazama huko na huko. Vidole vyangu vilikuwa vimekufa ganzi kutokana na baridi. Hata pale nilipojaribu kutembea miguu yangu ilinijulisha kwamba damu ilikuwa imeganda na hivyo ilikaribia ganzi kwa ajili ya baridi hiyo kali.

Nilijikaza na kuiburuza wakati inazidi kunyong’onyea, nikajikongoja hadi nilipomfikia mtu mmoja ambaye alikuwa anapita eneo lile akionekana mwenye haraka. Alikuwa mtu mzima wa makamo, mrefu na mwembamba mwenye sura ya ucheshi. Rangi ya ngozi yake ilikuwa maji ya kunde na macho yake yalikuwa makubwa yenye uchovu lakini yaliyokuwa makini. Kichwani alikuwa na upara uliokuwa unawaka na usiokuwa na unywele hata mmoja.

Alikuwa amevaa suruali ya kijivu, shati jeupe na sweta jeusi juu yake, kichwani alivaa kofia nyeusi ya pama na miguuni alivaa makubazi ya ngozi.

“Samahani, mzee. Habari za asubuhi!” nilimsalimia yule mtu kwa adabu.

“Nzuri, kijana!” yule mzee alijibu huku akinitazama usoni kwa makini.

“Samahani, sijui hapa nipo wapi?” nilimuuliza yule mzee huku nikimtazama kwa wasiwasi.

“Kwani wewe umetoka wapi hata uulize hapa ni wapi?” yule mzee aliniuliza huku akinitazama kwa mshangao kidogo.

“Hata sijui!” nilijibu kwa wasiwasi huku nikiangalia chini kuyakwepa macho ya yule mzee.

“Kwani umekuja na usafiri gani?” yule mzee aliniuliza tena huku akiendelea kunitazama kwa mshangao. Sikujua alinifikiria nini.

Sikuwa na jibu, jambo ambalo lilizidi kumshangaza yule mzee. Alinitazama kwa sekunde kadhaa kisha akaniuliza tena, “Ulikuwa umelewa au una matatizo… labda ya akili?”

Inaendelea...
Askofu hii ni mpya au ni mwendelezo wa Jason😊 Bishop Hiluka
 
Back
Top Bottom