Litro
JF-Expert Member
- Nov 18, 2018
- 1,080
- 2,248
tafta ela mkuu wangu hivi vitu vidogo haviitaji hasira mwaaah wewe utaendelea kungojea wenye pesa zetu itabidi tukuache nyuma kidogo.Acha unaa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
tafta ela mkuu wangu hivi vitu vidogo haviitaji hasira mwaaah wewe utaendelea kungojea wenye pesa zetu itabidi tukuache nyuma kidogo.Acha unaa
Haha! Usikate tamaa, Jumatatu itaendelea. Kuna mambo flani ya kikazi yamenibana...Will miss u all hii simulizi itanipa ulcers nimeaga mashindano witha heavy heart. Mtunzi keep the good work..
kitabi cha rosa mistica ninacho na nimeisha kukisoma zaidi ya mara nne ni kitabu kizuri pia katafute kitabu kingine cha huyo profesa kezilahabi kinaitwa dunia uwanja wa fujoView attachment 2169952
34
“Natamani na mimi nicheke na kushangaa,” nilimsemesha yule mwanadada kwa nia ya kutaka kuanzisha tena mazungumzo baada ya kushindwa kuvumilia.
Yule mwanadada alinigeukia na kunitazama mara moja tu bila kusema neno, kisha akayaondosha macho yake kwangu na kuyarudisha kwenye simu yake. Kitendo kile kikanifanya nianze kujilaumu kwa kuwa nilianza kuonekana kuwa najipendekeza sana na pengine ndiyo maana aliamua kunidharau.
“Am sorry kama nimeanza kuwa msumbufu kwako,” nilimwambia yule mwanadada na kujiegemeza kwenye kiti changu kisha nikakikumbuka kile kitabu cha Rosa Mistika nilichokuwa nasoma kabla ya ujio wake. Yule mwanadada hakunijibu bali alinitupia jicho la wizi huku akiachia tabasamu la aibu.
Lile basi la Makenga lilikuwa linaenda mwendo wa kasi na dereva alionekana kuwa makini sana akionesha kuizoea vizuri ile barabara ya changarawe. Nilikumbuka kuwa kabla gari halijasimama pale Itobo nilikuwa nasoma riwaya ya Rosa Mistika na hivyo nikafungua kurasa mbili tatu za kile kitabu nikitafuta sehemu nilipokuwa nimeishia kisha nikajaribu kusoma aya mbili tu na kukifunga tena baada ya kugundua kuwa nilikuwa sielewi chochote, kwa kuwa akili yangu haikuwa pale kwenye kitabu.
Sasa ilionekana kuwa uwepo wa yule mwanadada mwenye umbo la namba nane karibu yangu ulikuwa umeifanya akili yangu isitulie kabisa. Muda huo nilijikuta naanza kufikiria jinsi ya kuendeleza mazungumzo kati yangu na mwanadada yule ili tufahamiane zaidi, na ikiwezekana tuwe pamoja jioni ya siku hiyo baada ya kufika katika mji wa Kahama.
Mwendo wa basi letu ulikuwa siyo wa kubabaisha, mara tulikifikia kijiji kimoja ambacho sikufahamu kiliitwaje, nilipoangalia vizuri nililiona jengo moja kubwa na zuri la kanisa lililokuwa takriban mita 100 toka pale barabarani, nikaamua kumuuliza yule mwanadada mwenye umbo la namba nane kuhusu jina la kile kijiji.
“Panaitwa Lububu,” yule mwanadada alinijibu kwa mkato bila hata kunitazama kwani macho yake yalikuwa bado yapo kwenye kioo cha simu yake aliyoshika mkononi.
Pale katika stendi ndogo ya mabasi ya Kijiji cha Lububu kulikuwa na kikundi cha watu zaidi ya kumi, wanawake kwa wanaume na watoto, waliokuwa wamesimama chini ya mti mkubwa kando ya barabara wakisubiria usafiri. Basi la Makenga lilisimama na hapo niliwashuhudia wale watu wakikumbatiana na kuagana kisha abiria wawili tu, wote wanawake, walipanda na wale wengine walibaki pale chini wakipunga mikono yao.
Basi liliondoka huku wale wanawake waliopanda garini wakiendelea kuwapungia mikono wale waliobakia pale stendi ya Lububu, na muda mfupi baadaye gari likaanza kuyaacha makazi ya watu katika kijiji kile. Baada ya mwendo wa takriban dakika tano tayari tulikuwa tumekiacha nyuma kile kijiji na hapo dereva akaongeza kasi na gari likawa linakwenda kwa mwendo wa kupaa huku tukianza kuingia katikati ya vichaka na miti mirefu katika pori dogo.
Barabara ile ilikuwa inakatisha katikati ya vichaka vile na kwa mbali niliweza kuona mashamba na nyumba moja moja zikiwa mbalimbali sana, na hapo basi letu likaanza kushuka bonde dogo kwa mwendo wa kasi huku likijitahidi kukata upepo na kutokomea mbele zaidi. Hakuna aliyekuwa anaongea wakati huo na hivyo ndani ya gari kulitawaliwa na kiasi kikubwa cha ukimya wa namna yake. Hata hivyo, safari bado ilikuwa inaendelea.
Niligeuza tena shingo yangu kuangalia nyuma, na kwa kupitia kioo cha nyuma cha madirisha niliweza kuona wingu kubwa la vumbi nyuma yetu likitimka kutokana na ule mwendo wa kasi wa lile gari.
Wakati safari ikiendelea nilikata shauri la kuanzisha tena mazungumzo ya kirafiki na yule mwanadada mwenye umbo la namba nane, lakini nilipomtazama kwa umakini usoni sikuona tashwishwi yoyote ya urafiki baina yetu katika uso wake kwani alionekana kuzama kwenye lindi la mawazo.
Muda huo tulikuwa tunaanza kushuka mteremko fulani mrefu na mbele yetu kulikuwa na kona kali iliyokuwa inapinda kuingia upande wa kushoto, mara nikahisi tena kuwa mwendo wa gari letu ukipungua kwa ghafla huku gari likianza kuyumba. Hisia mbaya zilinijia akilini na haraka nikainua kichwa changu na kuyapeleka macho yangu kule mbele yetu kuangalia kulikuwa na nini.
Nilipotazama vizuri kule mbele niligundua kuwa kulikuwa na kundi kubwa la ng’ombe waliokuwa wanakatisha barabara kutoka upande mmoja wa barabara na kuelekea upande wa pili na kijana mdogo aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 14 na 16, mchungaji wa ng’ombe, alionekana kushtuka sana baada ya kuliona basi la Makenga likija katika uelekeo wake kwa mwendo wa kasi, na hivyo alikuwa anahangaika kuwaswaga wale ng’ombe haraka haraka akijaribu kushindana na kasi ya lile basi.
Nilimshuhudia dereva wa basi letu akijitahidi kupangua gia huku akipunguza mwendo na kulifanya gari kuyumba huku na kule wakati akijaribu kuwakwepa wale ng’ombe waliokuwa wanakimbia ovyo barabarani. Kitendo kile cha gari kuyumba huku na kule kilimfanya yule mwanadada mwenye umbo la namba nane aliyekuwa amezama kwenye lindi la mawazo kushtuka na kuanza kuyumba kama aliyekuwa na mapepo.
Nilimshuhudia akijitahidi kujishikilia vyema kwenye bomba lililokuwa linapita juu katikati ya uchochoro wa basi uliotenganisha viti vya upande mmoja na mwingine lakini hakuweza, hivyo akaanguka kama mzigo akiangukia juu ya mapaja yangu.
Kwa kuwa nilikuwa nimemshuhudia tangu alipoanza kuyumba, hivyo hakuwa amenishtukiza, kwa maana nyingine nilikwisha jiandaa kwa tukio la kumdaka na aliponikalia tu nikazungusha haraka mikono yangu kumkumbatia. Akawa amenikalia juu ya mapaja yangu kitendo kilichonifanya nijisikie faraja sana kukaliwa mapajani na yule mwanadada.
“Pole sana, mrembo!” nilinong’ona sikioni kwake kwa sauti tulivu huku nikiachia tabasamu la kirafiki.
Yule mwanadada mwenye umbo la namba nane hakunijibu bali alionekana kuzuga na kuyafumba macho yake akijaribu kupambana na aibu ya kiutu uzima huku akiwa bado ameketi juu ya mapaja yangu.
“I hope hujaumia!” niliongea huku nikizidi kumsaili kwa macho katika namna ya kutengeneza mazingira ya kutufanya kuwa karibu zaidi. Mwanzo yule mwanadada hakunijibu badala yake alijiinamia kwa aibu, kisha akajiinua taratibu kutoka kwenye mapaja yangu huku akiendelea kutabasamu kwa aibu.
“Usijali kaka yangu, wala sijaumia,” hatimaye alinijibu huku akiendelea kuyakwepa macho yangu. Hata hivyo, harufu nzuri ya manukato aliyojipulizia ikazidi kuzipa uhai pua zangu wakati akiinuka kutoka pale kwenye mapaja yangu.
Eddy alinitazama kwa umakini akataka kucheka kisha akayahamisha macho yake kumtazama yule mwanadada mwenye umbo la namba nane na kutabasamu huku akiachia mguno uliomfanya yule mwanadada ageuke kumtazama huku akiachia tabasamu la aibu.
Muda wote dereva wa lile gari alikuwa akiwakwepa wale ng’ombe walioonekana kuwa wengi huku gari likiwa bado linaserereka, kisha nikamwona akimkosakosa yule kijana mdogo aliyekuwa anajitahidi kuwaswaga ng’ombe wa mwisho.
Utingo wa gari letu ambaye muda wote alikuwa ananing’inia mlangoni alimpigia kelele ya kumlaani yule kijana mchungaji wa mifugo. Baada ya kuwavuka wale ng’ombe gari letu halikwenda mbali sana mara kishindo kikubwa kilichoambatana na mtikisiko wa gari kikasikika na kutushtua abiria wote tuliokuwemo ndani ya lile gari.
Baadhi ya mizigo ilidondoka kutoka kwenye sehemu maalumu ya juu ya kuwekea mizigo na kuwaponda abiria vichwani huku hali ile ikizua taharuki. Nilishuhudia abiria wengi hususan wanawake, akiwemo yule mwanadada mwenye umbo la namba nane wakipiga yowe kubwa la hofu kutokana na tukio lile.
Yule mwanadada alijikunyata kwa hofu huku akiyatoa macho yake na wakati huo huo alinitupia jicho, na macho yetu yalipokutana niliweza kuiona hofu kubwa iliyokuwa imejengeka usoni kwake. Nilimshika mkono wake taratibu huku macho yangu yakimweleza nini alichopaswa kufanya muda ule. Nilikuwa nimedhamiria kumketisha juu ya mapaja yangu, kwa madai kuwa huo ndiyo ulikuwa usalama wake.
Itaendelea...
Vyote nimevisoma...kitabi cha rosa mistica ninacho na nimeisha kukisoma zaidi ya mara nne ni kitabu kizuri pia katafute kitabu kingine cha huyo profesa kezilahabi kinaitwa dunia uwanja wa fujo
Thanks Bishop, kazi iendeleeView attachment 2310709
209
“Sawa, muda unaenda,” nilimwambia Rehema huku nikiangalia saa yangu ya mkononi. “Napaswa kuondoka kwani tumekubaliana kuondoka saa sita kamili usiku huu huu na hivyo yafaa niharakishe, sijui utapenda kunisindikiza hadi hapo nje?”
Rehema alitingisha kichwa chake kwa huzuni huku akinitazama usoni kisha aliniacha na kuelekea chumbani huku akifuta machozi. Pendo alimtazama Rehema kwa mshangao kisha akayarudisha macho yake kwangu, hata hivyo hakusema neno. Sikuelewa kwa nini Rehema alikuwa na huzuni kubwa kiasi hicho.
Kwa mara nyingine tena nilitamani niahirishe safari yangu lakini sikuwa na namna yoyote ya kufanya kwani taifa lilikuwa muhimu zaidi na liliniamini kwenda kuifanya kazi hiyo ngumu ya kuandaa mfumo, na hivyo nisingeweza kukataa.
“Pendo, njoo ufunge geti na mlango,” nilimwambia Pendo kisha sikungoja, nikachukua begi langu la safari lililokuwa na magurudumu na kutoka haraka.
Huko nje nililikuta gari maalumu aina ya Nissan Patrol la rangi ya jeshi, lenye vioo vya giza visivyoruhusu mtu kuona waliomo ndani likiwa limeegeshwa usawa wa geti kubwa la kuingilia kwenye uzio wa nyumba. Gari hilo lilikuwa linaunguruma taratibu kuonesha kuwa halikuwa limezimwa.
Dereva wa gari lile alikuwa Luteni Lister na aliponiona nikitokea kwenye geti dogo la nyumba alishuka haraka toka kwenye lile gari na kunipa mkono wa makaribisho huku tabasamu pana likichanua usoni kwake kisha akalichukua begi langu na kufungua mlango wa nyuma, akaliweka vizuri, na wakati huo mimi nilizunguka na kufungua mlango wa mbele. Nikaingia na kuketi kwa utulivu huku nikifunga mkanda.
Luteni Lister alikuwa amevaa suruali ya dengrizi ya rangi ya samawati, fulana nyepesi nyeusi na juu yake alivaa shati zito la dengrizi la rangi ya samawati la mikono mirefu. Mkononi alivaa saa na kichwani alivaa kofia ya bluu ya kapelo na miwani mikubwa myeusi ingawa muda huo hakukuwa na jua.
Luteni Lister, Komando na Ofisa Usalama wa Taifa, alipoingia ndani ya gari na kuketi nyuma ya usukani aligeuza shingo yake kunitazama usoni kwa namna ya kunisaili, “Hujasahau kitu chochote, Boss?”
“Sidhani… tunaweza kuondoka,” nilimwambia kwa sauti tulivu kisha nikashusha pumzi ndefu.
Kama ilivyokuwa kwangu, Luteni Lister pia hakuonekana mtu wa maneno mengi na hivyo haraka akatumbukiza gia na kukanyaga pedeli ya mafuta, na hapo gari likaanza kuondoka taratibu na kuingia barabarani kisha Luteni Lister alikata kushoto na kuingia katika barabara nyingine na hapo akaongeza mwendo hadi tulipofika katika eneo la Nyihogo akakata na kuingia upande wa kulia akiifuata barabara kuu ya lami inayotoka katika nchi za Rwanda, Uganda na Burundi.
Muda huo wa usiku Mji wa Kahama ulikuwa umemezwa na utulivu wa aina yake. Magari machache sana yalionekana barabarani wakati safari yetu ilipokuwa ikianza na hivyo ikawa rahisi kwetu kwenda kwa mwendo tulioutaka. Nilimtupia jicho Luteni Lister nikamwona akizipangua gia, nikashusha pumzi za ndani kwa ndani na kujiweka sawa kwenye kiti changu, sasa safari rasmi ya kuelekea Jijini Dar es Salaam kwenye kazi maalumu ya kiintelijensia ikawa imeanza.
Hata hivyo akili yangu bado ilikuwa ikisumbuka katika namna ya kutaka kufahamu kama ni kweli nilikuwa kwenye gari la Taasisi ya Usalama wa Taifa nikiendeshwa na Ofisa Usalama ambaye pia alikuwa Komando wa daraja la pili, na nilitakiwa kwenda Jijini Dar es Salaam kutengeneza mfumo maalumu wa kufuatilia masuala ya uhalifu wa kimtandao! Bado akili yangu ilikuwa katika mpumbao fulani hivi na mara kwa mara sikuacha kujiuliza ikiwa ile safari ilikuwa ni ndoto au lilikuwa tukio halisi lililokuwa likitokea maishani mwangu!
Nilimtupia jicho Luteni Lister nikamwona akiwa yupo makini kwenye usukani macho akiwa kayakaza kutazama barabarani. Sasa akili yangu ikawa kama vile imefunguka, nikaanza kupoteza utulivu wa kiakili huku mitupo ya mapigo ya moyo wangu ikiongezeka mara dufu.
Nikiwa nimeanza kuzama kwenye tafakuri mawazo yangu yakahamia kwa mke wangu Rehema, nilikumbuka jinsi nilivyopata shida kujieleza wakati nikimwambia kuwa nilihitajika Jijini Dar es Salaam kwenye mradi maalumu wa kuandaa mfumo maalumu ambao ungetumika kwenye vyuo vya teknolojia ya habari na mawasiliano, mradi ambao ungechukua takriban wiki tatu.
Ndiyo, safari ya wiki tatu lakini ingeweza kuwa ya muda wa mwezi, miezi au hata mwaka kutegemeana na matakwa na wakuu wa usalama kwa yale ambayo yangejiri kwenye kazi yenyewe. Kwangu, safari hiyo haikuwa na shida yoyote tatizo lilikuwa kwenye namna ya kazi yenyewe hususan pale ambapo wakuu hao wa usalama wangeonesha kuridhishwa na kazi husika.
Hata hivyo, kwa kuwa nilikuwa nimepitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria baada ya masomo yangu pale Mzumbe, nilifahamu fika kuhusu tafsiri sahihi ya uzalendo kwa nchi yangu ni kutii, na sasa sikuwa na namna yoyote ya kufanya zaidi ya kutii amri kama uzalendo unavyotaka.
Na nilipokuwa katika harakati za kuupisha utulivu kichwani mwangu katika namna ya kutafakari zaidi kwa nini Rehema hakutaka niondoke mara nikashtushwa na myumbo wa ghafla wa gari letu huku nikimshuhudia Luteni Lister akikanyaga breki kwa nguvu na kulifanya gari lisote na kuyumba kwenye barabara hiyo pana, bahati nzuri gari halikutoka nje ya barabara.
Kisha Luteni Lister aliyekuwa ametahayari kidogo aliachia tusi zito la nguoni na kusonya kwa hasira huku akikanyaga pedeli ya mafuta, gari likajivuta na kufanya magurudumu yake kuchimba lami, kisha likaondoka kwa mwendo wa kasi.
Niligeuza shingo yangu kutazama kando na hapo nikaishuhudia pikipiki aina ya Boxer iliyokuwa imebeba watu wawili ikiserereka barabarani kabla ya dereva wa pikipiki hiyo kuiweka sawa na kisha akaongeza mwendo pasipo kusimama. Na hapo nikatambua kuwa dereva wa ile pikipiki hakuwa makini kwani alikuwa ameingia upande wetu akiwa katika mwendo wa kasi na kumfanya Luteni Lister alazimike kumkwepa, vinginevyo tungezungumza mengine.
Nilipotazama vizuri nje nikagundua kuwa tulikuwa tunavuka eneo la mgodi wa dhahabu wa Buzwagi. Nikashusha pumzi ndefu na kujiegemeza kwenye kiti changu huku nikiyasikilizia mapigo ya moyo wangu yaliyokuwa yakienda kasi isivyo kawaida.
* * *
Mambo yanazidi kunoga, endelea kufuatilia...
Tuvumiliane tu, mkuu... Nitashusha tena mzigo wa maana Ijumaa ya wiki hii. Tuombe Mungu atupe uzima...mzigo unazidi kunoga sema bamjoli unachelewa sana kushusha mamb
inshalah bamjol tuombe uzimaTuvumiliane tu, mkuu... Nitashusha tena mzigo wa maana Ijumaa ya wiki hii. Tuombe Mungu atupe uzima...