Simulizi: Harakati za Jason Sizya

Simulizi: Harakati za Jason Sizya

Will miss u all hii simulizi itanipa ulcers nimeaga mashindano witha heavy heart. Mtunzi keep the good work..
 
Will miss u all hii simulizi itanipa ulcers nimeaga mashindano witha heavy heart. Mtunzi keep the good work..
Haha! Usikate tamaa, Jumatatu itaendelea. Kuna mambo flani ya kikazi yamenibana...
 
View attachment 2169952
34

“Natamani na mimi nicheke na kushangaa,” nilimsemesha yule mwanadada kwa nia ya kutaka kuanzisha tena mazungumzo baada ya kushindwa kuvumilia.

Yule mwanadada alinigeukia na kunitazama mara moja tu bila kusema neno, kisha akayaondosha macho yake kwangu na kuyarudisha kwenye simu yake. Kitendo kile kikanifanya nianze kujilaumu kwa kuwa nilianza kuonekana kuwa najipendekeza sana na pengine ndiyo maana aliamua kunidharau.

Am sorry kama nimeanza kuwa msumbufu kwako,” nilimwambia yule mwanadada na kujiegemeza kwenye kiti changu kisha nikakikumbuka kile kitabu cha Rosa Mistika nilichokuwa nasoma kabla ya ujio wake. Yule mwanadada hakunijibu bali alinitupia jicho la wizi huku akiachia tabasamu la aibu.

Lile basi la Makenga lilikuwa linaenda mwendo wa kasi na dereva alionekana kuwa makini sana akionesha kuizoea vizuri ile barabara ya changarawe. Nilikumbuka kuwa kabla gari halijasimama pale Itobo nilikuwa nasoma riwaya ya Rosa Mistika na hivyo nikafungua kurasa mbili tatu za kile kitabu nikitafuta sehemu nilipokuwa nimeishia kisha nikajaribu kusoma aya mbili tu na kukifunga tena baada ya kugundua kuwa nilikuwa sielewi chochote, kwa kuwa akili yangu haikuwa pale kwenye kitabu.

Sasa ilionekana kuwa uwepo wa yule mwanadada mwenye umbo la namba nane karibu yangu ulikuwa umeifanya akili yangu isitulie kabisa. Muda huo nilijikuta naanza kufikiria jinsi ya kuendeleza mazungumzo kati yangu na mwanadada yule ili tufahamiane zaidi, na ikiwezekana tuwe pamoja jioni ya siku hiyo baada ya kufika katika mji wa Kahama.

Mwendo wa basi letu ulikuwa siyo wa kubabaisha, mara tulikifikia kijiji kimoja ambacho sikufahamu kiliitwaje, nilipoangalia vizuri nililiona jengo moja kubwa na zuri la kanisa lililokuwa takriban mita 100 toka pale barabarani, nikaamua kumuuliza yule mwanadada mwenye umbo la namba nane kuhusu jina la kile kijiji.

“Panaitwa Lububu,” yule mwanadada alinijibu kwa mkato bila hata kunitazama kwani macho yake yalikuwa bado yapo kwenye kioo cha simu yake aliyoshika mkononi.

Pale katika stendi ndogo ya mabasi ya Kijiji cha Lububu kulikuwa na kikundi cha watu zaidi ya kumi, wanawake kwa wanaume na watoto, waliokuwa wamesimama chini ya mti mkubwa kando ya barabara wakisubiria usafiri. Basi la Makenga lilisimama na hapo niliwashuhudia wale watu wakikumbatiana na kuagana kisha abiria wawili tu, wote wanawake, walipanda na wale wengine walibaki pale chini wakipunga mikono yao.

Basi liliondoka huku wale wanawake waliopanda garini wakiendelea kuwapungia mikono wale waliobakia pale stendi ya Lububu, na muda mfupi baadaye gari likaanza kuyaacha makazi ya watu katika kijiji kile. Baada ya mwendo wa takriban dakika tano tayari tulikuwa tumekiacha nyuma kile kijiji na hapo dereva akaongeza kasi na gari likawa linakwenda kwa mwendo wa kupaa huku tukianza kuingia katikati ya vichaka na miti mirefu katika pori dogo.

Barabara ile ilikuwa inakatisha katikati ya vichaka vile na kwa mbali niliweza kuona mashamba na nyumba moja moja zikiwa mbalimbali sana, na hapo basi letu likaanza kushuka bonde dogo kwa mwendo wa kasi huku likijitahidi kukata upepo na kutokomea mbele zaidi. Hakuna aliyekuwa anaongea wakati huo na hivyo ndani ya gari kulitawaliwa na kiasi kikubwa cha ukimya wa namna yake. Hata hivyo, safari bado ilikuwa inaendelea.

Niligeuza tena shingo yangu kuangalia nyuma, na kwa kupitia kioo cha nyuma cha madirisha niliweza kuona wingu kubwa la vumbi nyuma yetu likitimka kutokana na ule mwendo wa kasi wa lile gari.

Wakati safari ikiendelea nilikata shauri la kuanzisha tena mazungumzo ya kirafiki na yule mwanadada mwenye umbo la namba nane, lakini nilipomtazama kwa umakini usoni sikuona tashwishwi yoyote ya urafiki baina yetu katika uso wake kwani alionekana kuzama kwenye lindi la mawazo.

Muda huo tulikuwa tunaanza kushuka mteremko fulani mrefu na mbele yetu kulikuwa na kona kali iliyokuwa inapinda kuingia upande wa kushoto, mara nikahisi tena kuwa mwendo wa gari letu ukipungua kwa ghafla huku gari likianza kuyumba. Hisia mbaya zilinijia akilini na haraka nikainua kichwa changu na kuyapeleka macho yangu kule mbele yetu kuangalia kulikuwa na nini.

Nilipotazama vizuri kule mbele niligundua kuwa kulikuwa na kundi kubwa la ng’ombe waliokuwa wanakatisha barabara kutoka upande mmoja wa barabara na kuelekea upande wa pili na kijana mdogo aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 14 na 16, mchungaji wa ng’ombe, alionekana kushtuka sana baada ya kuliona basi la Makenga likija katika uelekeo wake kwa mwendo wa kasi, na hivyo alikuwa anahangaika kuwaswaga wale ng’ombe haraka haraka akijaribu kushindana na kasi ya lile basi.

Nilimshuhudia dereva wa basi letu akijitahidi kupangua gia huku akipunguza mwendo na kulifanya gari kuyumba huku na kule wakati akijaribu kuwakwepa wale ng’ombe waliokuwa wanakimbia ovyo barabarani. Kitendo kile cha gari kuyumba huku na kule kilimfanya yule mwanadada mwenye umbo la namba nane aliyekuwa amezama kwenye lindi la mawazo kushtuka na kuanza kuyumba kama aliyekuwa na mapepo.

Nilimshuhudia akijitahidi kujishikilia vyema kwenye bomba lililokuwa linapita juu katikati ya uchochoro wa basi uliotenganisha viti vya upande mmoja na mwingine lakini hakuweza, hivyo akaanguka kama mzigo akiangukia juu ya mapaja yangu.

Kwa kuwa nilikuwa nimemshuhudia tangu alipoanza kuyumba, hivyo hakuwa amenishtukiza, kwa maana nyingine nilikwisha jiandaa kwa tukio la kumdaka na aliponikalia tu nikazungusha haraka mikono yangu kumkumbatia. Akawa amenikalia juu ya mapaja yangu kitendo kilichonifanya nijisikie faraja sana kukaliwa mapajani na yule mwanadada.

“Pole sana, mrembo!” nilinong’ona sikioni kwake kwa sauti tulivu huku nikiachia tabasamu la kirafiki.

Yule mwanadada mwenye umbo la namba nane hakunijibu bali alionekana kuzuga na kuyafumba macho yake akijaribu kupambana na aibu ya kiutu uzima huku akiwa bado ameketi juu ya mapaja yangu.

I hope hujaumia!” niliongea huku nikizidi kumsaili kwa macho katika namna ya kutengeneza mazingira ya kutufanya kuwa karibu zaidi. Mwanzo yule mwanadada hakunijibu badala yake alijiinamia kwa aibu, kisha akajiinua taratibu kutoka kwenye mapaja yangu huku akiendelea kutabasamu kwa aibu.

“Usijali kaka yangu, wala sijaumia,” hatimaye alinijibu huku akiendelea kuyakwepa macho yangu. Hata hivyo, harufu nzuri ya manukato aliyojipulizia ikazidi kuzipa uhai pua zangu wakati akiinuka kutoka pale kwenye mapaja yangu.

Eddy alinitazama kwa umakini akataka kucheka kisha akayahamisha macho yake kumtazama yule mwanadada mwenye umbo la namba nane na kutabasamu huku akiachia mguno uliomfanya yule mwanadada ageuke kumtazama huku akiachia tabasamu la aibu.

Muda wote dereva wa lile gari alikuwa akiwakwepa wale ng’ombe walioonekana kuwa wengi huku gari likiwa bado linaserereka, kisha nikamwona akimkosakosa yule kijana mdogo aliyekuwa anajitahidi kuwaswaga ng’ombe wa mwisho.

Utingo wa gari letu ambaye muda wote alikuwa ananing’inia mlangoni alimpigia kelele ya kumlaani yule kijana mchungaji wa mifugo. Baada ya kuwavuka wale ng’ombe gari letu halikwenda mbali sana mara kishindo kikubwa kilichoambatana na mtikisiko wa gari kikasikika na kutushtua abiria wote tuliokuwemo ndani ya lile gari.

Baadhi ya mizigo ilidondoka kutoka kwenye sehemu maalumu ya juu ya kuwekea mizigo na kuwaponda abiria vichwani huku hali ile ikizua taharuki. Nilishuhudia abiria wengi hususan wanawake, akiwemo yule mwanadada mwenye umbo la namba nane wakipiga yowe kubwa la hofu kutokana na tukio lile.

Yule mwanadada alijikunyata kwa hofu huku akiyatoa macho yake na wakati huo huo alinitupia jicho, na macho yetu yalipokutana niliweza kuiona hofu kubwa iliyokuwa imejengeka usoni kwake. Nilimshika mkono wake taratibu huku macho yangu yakimweleza nini alichopaswa kufanya muda ule. Nilikuwa nimedhamiria kumketisha juu ya mapaja yangu, kwa madai kuwa huo ndiyo ulikuwa usalama wake.

Itaendelea...
kitabi cha rosa mistica ninacho na nimeisha kukisoma zaidi ya mara nne ni kitabu kizuri pia katafute kitabu kingine cha huyo profesa kezilahabi kinaitwa dunia uwanja wa fujo
 
ufukweni mombasa.JPG

206

Wito Maalumu




Saa 3:30 usiku…

UPEPO wa kipupwe ulikuwa unavuma na kutengeneza sauti ya mvumo wa kustaajabisha kwenye matawi ya miti mikubwa ya kivuli iliyozunguka nyumba yetu. Kadiri matawi ya miti yalivyocheza huku na kule kwa utulivu ndivyo mvumo ule ulivyosikika na kutengeneza sauti kama ya chatu mkali aliyehisi hatari kichakani.

Upepo huo ulivuma ukayasonga songa mapazia marefu yaliyokuwa yamefunika madirisha makubwa mle chumbani nilimokuwa, ndani ya nyumba yetu kubwa ya kisasa iliyojengwa katika eneo tulivu la Mwime, nje kidogo ya Mji wa Kahama.

Muda huo wa saa tatu usiku nilikuwa katika harakati za kufungasha vitu muhimu na kuviweka ndani ya begi langu la safari kwa ajili ya safari ya kwenda Jijini Dar es Salaam, safari ambayo ilikuwa niondoke usiku huo huo. Zoezi hilo la kufungasha vitu muhimu vya kuondoka navyo kwa kweli lilinipa changamoto kubwa sana kwa vile ilikuwa inaniwia vigumu mno kuamua ni kitu gani nikiache na kipi nichukue!

Zilikuwa zimepita wiki tatu tu tangu mimi na Rehema turejee Mjini Kahama tukitokea Jijini Dodoma kwa mjomba Mchungaji Ngelela nilikokaa kwa wiki kadhaa baada ya kurudiwa na kumbukumbu zangu nikitoka kwenye tatizo lililojulikana kitaalamu kama retrograde amnesia yaani kupoteza kabisa uwezo wa kukumbuka taarifa zozote, tatizo lililojitokeza baada ya kupata ajali eneo la Makutupora, kama ambavyo iliandikwa kwenye kisa kilichopewa jina la “Mgeni Mwema”.

Kwa kweli mkasa huo, kwangu, bado niliuona kama masimulizi fulani ya kufikirika au pengine sinema ya kusisimua. Kuna wakati nilishindwa kuamini kama ni kweli hali hiyo ilikuwa imenitokea mimi na si mtu mwingine.

Mchana wa siku hii nikiwa kwenye pilika pilika zangu nilifuatwa na mtu mmoja, kijana mtanashati sana tuliyeelekeana kwa umri, alijitambulisha kwangu kwa jina moja tu la Lister, na kwamba alikuwa ana ujumbe wangu maalumu kutoka Dar es Salaam.

Kimwonekano kijana huyo alikuwa mrefu, kama mimi, mwenye mwili wa kimazoezi na mweupe mwenye sura ya tabasamu muda wote ingawa macho yake yalikuwa makini sana kama simba awindaye. Mtu huyo alikuwa mcheshi sana ingawa kwa mtazamo wa haraka haraka ungeweza kudhani hakuwa mzungumzaji.

Alikuwa amevaa shati zuri jeusi la mistari myeupe la mikono mirefu, suruali nyeusi, tai nyeusi shingoni na viatu ghali vyeusi vya ngozi halisi. Mkononi alivaa saa ghali aina ya Cartier yenye nakshi ya madini ya dhahabu na alikuwa amejipulizia manukato ghali aina ya Dolce & Gabbana.

Tukiwa tumeketi sehemu fulani tulivu Lister aliniambia kuwa nilikuwa nahitajika kwenda Jijini Dar es Salaam siku hiyo hiyo ili kuonana na wakuu wa taasisi mpya ya SPACE iliyokuwa imeanzishwa miezi michache iliyokuwa imepita ili kushughulika na masuala ya ujasusi wa mtandaoni.

Eti nilihitajika kwenda kuwatengenezea mfumo maalumu wa kufuatilia masuala ya uhalifu wa kimtandao ili kwamba kila ujumbe ambao ungetumwa mtandaoni wenye dalili za vitisho au shambulio la kimtandao dhidi ya serikali ungepaswa kujulikana ni wapi ulikotoka.

Wakati akinieleza habari zile nilionesha shaka sana, kwanza sikumwamini ingawa sikuwambia waziwazi, nilichoweza kusema ni kuwa kazi hiyo ilikuwa ngumu sana kwangu, lakini Lister alicheka sana na kuniambia kuwa alikuwa na uhakika wa asilimia mia moja kuwa nilikuwa na uwezo, tena uwezo mkubwa, wa kuifanya kazi hiyo kwa kutokana na sifa zangu.

Aliniambia kuwa walikuwa na taarifa zote kunihusu na walifahamu kuwa nilishawahi kutengeneza mfumo wa aina hiyo ingawa ulitofautiana kidogo, huo ulikuwa mfumo maalumu wa kutunza data nyeti kwenye ‘vault’ ya mgodi wa Buzwagi wakati nilipokuwa nafanya kazi hapo mgodini. Ule mfumo ulikuwa salama zaidi uliofanya isiwe rahisi kwa mtu yeyote, hata kama ni mtaalamu wa kiwango gani, kuingia kwenye mtandao wa mgodi na kuchukua taarifa.

Na hapo nikakumbuka kuwa ni kweli nilikuwa nimetengeneza mfumo maalumu wa kutunza data nyeti kwenye ‘vault’ ya mgodi wa Buzwagi na baada ya kuutengeneza mfumo huo niliuwekea code maalumu nne ambapo ili mtu yeyote akitaka kufungua vault na kuingia kwenye mfumo huo angehitaji kupata code hizo na alama za vidole gumba vya wahusika wote wakuu wa mgodi, code ambazo ni watu wawili tu, ndio walizifahamu.

Lister pia aliniambia kuwa walikuwa wanafahamu kuhusu kile nilichokifanya kule Pretoria Technikon – Institute of Technology nchini Afrika Kusini nilikohitimu Shahada yangu ya Computer System Analysis na kuweka rekodi ambayo hadi leo haijavunjwa. Kwa hali hiyo hakuwa na shaka kuwa nilikuwa chaguo sahihi kwa ajili ya kazi ya kuuandaa mfumo huo.

Na hapo akili yangu nikaihamishia Afrika Kusini nilipokwenda kusoma masuala ya teknolojia kwa miaka mitatu. Nikakumbuka kuwa kwenye mtihani wangu wa mwisho nilitengeneza mfumo fulani wa utambuzi nilioupa jila la Tracer uliotumia GPS na kuonekana unafaa sana kwa watu wanaofanya kazi za kipelelezi na nyingine nyingi zenye manufaa. Ili kufuatilia kitu mfumo huo ulihitaji kifaa maalumu kama simu au saa ambacho kingetumika kuchomekea kitu kama memory card na kisha kukiingiza kifaa hicho kwenye tarakilishi ambapo mtumiaji angehitaji kuzijua code maalumu tatu ili kufatilia yanayoendelea duniani.

Kazi hiyo ya kubuni mfumo huo na kisha kifaa maalumu cha kusaidia kufuatilia mambo ililifanya Shirika la Kijasusi la Afrika Kusini kuanza kunitazama kwa macho ya tahadhari kubwa. Nilipoondoka hapo chuoni nikaja kusikia baadaye kuwa shirika hilo la kijasusi kwa kutumia mawakala wake lilijaribu kuunda mfumo wa aina ile lakini walichemka…

“Nadhani sasa umetambua kuwa wewe ni mtu muhimu sana,” sauti ya Lister ilinizindua na kuyakatiza mawazo yangu. Kwa vyovyote alikuwa ameyasoma mawazo yangu.

Daah… ghafla nilijikuta jasho jepesi likianza kunitoka sehemu mbalimbali za mwili wangu huku nikihisi ubaridi fulani wa woga wa aina yake ukinitambaa mwilini na mapigo ya moyo wangu yakabadili mwendo wake na kwenda mbio isivyo kawaida! Niliogopa mno kusikia kuwa alikuwa anazo taarifa zangu nyingi hata zile ambazo nilizifanya kuwa siri.

“Unaweza kuniambia… wewe ni nani hasa hadi uyajue yote haya?” nilimuuliza Lister huku nikimkazia macho. Koo langu lilikuwa limekauka ghafla na nywele zangu zilinisimama kichwani kwa hofu.

Lister alicheka kidogo kisha akanitoa shaka kuwa yeye si mtu mbaya. Aliniambia kuwa yeye ni Luteni wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Komando wa daraja la pili, lakini pia ni Ofisa Usalama aliyekuwa anatokea Idara ya Usalama wa Taifa.

Nilibaki hoi nisijue la kufanya! Kwa sekunde chache nilibaki nimemkodolea macho Luteni Lister nikiwa nimepigwa butwaa. Jambo moja lilinijia haraka akilini mwangu kuwa; huenda ile ilikuwa ndoto tu kama zingine na mara tu ningeamka kutoka usingizini ningekuta kila kitu kikiwa cha kawaida. Lakini… hapana haikuwa ndoto.

Luteni Lister aligundua kuwa nilikuwa katika mkanganyiko wa kimawazo, kwa kitaalamu huitwa interpersonal conflict na pia nilikuwa na mashaka juu ya maelezo yake. Alinitoa wasiwasi kwa kuniambia kuwa hata Meja Jenerali Benard Mpogolo, baba mzazi wa mke wangu Rehema, alikuwa anafahamu kuwa yeye alikuja Kahama kunifuata kwa kuwa ni bosi wake. Ili kunihakikisha jambo hilo ilimbidi ampigie simu na kunipa nizungumze naye kama njia ya kunithibitishia kwamba asemayo ni kweli.

Inaendelea...
 
ufukweni mombasa.JPG

207

Baada ya Meja Jenerali Mpogolo kunihakikishia kuwa taarifa hizo zilikuwa sahihi na kwamba jina langu lilikuwa limependekezwa miongoni mwa wataalamu watatu wa teknolojia ya habari na mawasiliano nchini baada ya kuzingatiwa kuwa nilikuwa nimebobea kwenye utaalamu adimu wa teknolojia ya habari na mawasiliano, nilikubali mwito huo.

Ni ukweli usiopingika kuwa nilikuwa nao ujuzi adimu wa teknolojia ya habari na mawasiliano, nikikaa nyuma ya tarakilishi na kubofya kicharazio ili kuifanya dunia kuwa sawa na kijiji.

Luteni Lister aliendelea kunifahamisha kuwa wakuu wa taasisi ya ujasusi nchini walikuwa wamejiridhisha kwamba nilikuwa mjuzi sana kwenye mambo ya teknolojia, na kwamba walikubaliana na wale watu walioniita computer wizard. Luteni Lister alinisisitiza kuwa, hata hivyo, suala la mimi kwenda kuifanya kazi hiyo lilipaswa kuwa la siri sana, hakuna mtu aliyepaswa kujua, hata mke wangu Rehema hakutakiwa kujua kazi niliyokuwa nakwenda kuifanya jijini Dar es Salaam.

Japo Luteni Lister hakuwa amenieleza njia zipi walizokuwa wametumia kupata habari zangu na kisha kujiridhisha kuwa nilikuwa nafaa kuifanya kazi hiyo lakini sikuwa mbumbumbu kwani nilikuwa na ufahamu mkubwa kuhusu masuala ya ‘vetting’.

Kwa mujibu wa utaratibu, nilifahamu kuwa kwa vyovyote walikuwa wamefuatilia taarifa zangu kupitia watu wangu wa karibu, majirani, wafanyakazi wenzangu niliowahi kufanya nao kazi mgodini Buzwagi, walimu waliowahi kunifundisha kwenye shule mbalimbali nilizosoma na hata kule chuoni Pretoria Technikon – Institute of Technology nchini Afrika Kusini nilikosoma mambo ya Computer System Analysis.

Chambilecho “mzigo mzito mtwishe Mnyamwezi”, sasa mimi Mnyamwezi nilikuwa nimepewa jukumu hilo zito na nyeti mno la kuwa miongoni mwa watu watatu tu waliotakiwa kuandaa mfumo maalumu wa kufuatilia masuala ya uhalifu wa kimtandao. Kwangu, nafasi hiyo ya kuandaa mfumo huo ilikuwa ni ufahari mkubwa sana kuaminiwa kwenye taifa lenye vichwa zaidi ya milioni 50 wakiwemo wataalamu waliobobea kwenye masuala hayo ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

Baada ya maongezi ya kina mchana huo kuhusu safari ya kwenda Dar es Salaam, Luteni Lister hakunificha, alinidokeza kuwa taasisi ya SPACE ilikuwa imetokana na kilichokuwa kitengo maalumu cha Usalama wa Taifa cha kushughulika na mambo ya mtandaoni, kama sehemu ya ulinzi wa kimtandao dhidi ya serikali.

Taasisi hii ilianzishwa baada ya kikao maalumu kilichowahusisha wakuu wa Idara zote za Ulinzi na Usalama kufuatia udukuzi wa taarifa uliokuwa unafanywa na watu wasiojulikana kwa kuiba taarifa nyeti za kiusalama toka Ofisi ya Rais. Pia watu hao hawakuishia kudukua tu taarifa bali pia Ofisi ya Rais ilipokea vitisho vya kigaidi na jumbe mbalimbali zenye kuonesha dalili ya shambulio la kutaka kumdhuru Rais.

Kikao hicho maalumu kilichoongozwa na Mkuu wa Idara ya Ujasusi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (Millitary Intelligence - MI), Meja Jenerali Gozbert Bundala kama Mwenyekiti; na Mkurugenzi wa Operesheni za Ndani wa Usalama wa Taifa (Director Of Internal operations - DOI), Ismail Banda kama Katibu.

Wakuu wengine wa Idara za Ulinzi na Usalama waliohudhuria kikao hicho ni Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Zuberi Koba; Kamishna wa Intelijensia kutoka Polisi, Paul Mwita; na Mkurugenzi wa Habari na Teknolojia wa Idara ya Usalama wa Taifa, David Mshana.

Kikao hicho kiliunda kikosi kazi (task force) ili kushughulikia suala hilo na muda maalumu ulikuwa umewekwa kukamilisha kazi hiyo, na kwamba mfumo huo ukikamilika kazi ya ufuatiliaji taarifa mtandaoni ingeanza rasmi ingawa si kila ujumbe ungechunguzwa na maofisa maalumu ambao wana uwezo mkubwa wa kujua kama ujumbe fulani ni ‘serious and sensitive’ ama sivyo.

Lakini endapo mtu yeyote angechapisha au kutuma chochote kwenye mtandao ambacho maofisa hao wakiona ni hatarishi kwa usalama wa taifa basi mara moja kila taarifa kuhusu mtu huyo zingeanza kuchunguzwa kwa kuwahoji watu wake wa karibu, majirani, wafanyakazi wenziwe, hata walimu waliowahi kumfundisha na baada ya hapo hatua sahihi zingefuata iwapo mtu huyo apewe onyo, achukuliwe kwa mahojiano zaidi au ahukumiwe kwa kosa hilo…

_____

Mawazo yangu yalikatishwa ghafla na sauti ya mlango wa chumbani uliofunguliwa wakati nikiendelea na harakati za kufungasha vitu muhimu na kuviweka ndani ya begi langu la safari. Nilipotazama mlangoni nikamwona mke wangu Rehema akiingia mle chumbani na kusimama kando yangu huku akinitazama kwa umakini. Rehema alikuwa anafahamu kuwa nilikuwa nimepata safari ya ghafla kwenda Jijini Dar es Salaam na nilitakiwa kusafiri usiku huo, jambo lililompata mshangao mkubwa.

Mwanzoni ilikuwa ngumu sana kumshawishi kuwa nilitakiwa nisafiri kwenda Dar es Salaam hadi pale alipopigiwa simu na baba yake, Meja Jenerali Mpogolo na kuambiwa kuwa nilikuwa nahitajika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya kwenda kuwatengenezea mfumo maalumu ambao ungetumika kwenye vyuo vya teknolojia ya habari na mawasiliano, kazi ambayo ingechukua takriban wiki tatu.

Usiku huo, Rehema alikuwa amevaa gauni jepesi la kulalia la rangi ya pinki la kukata mikono lililolichora vyema umbo lake na kuishia sentimita chache juu ya magoti yake, na kichwani alikuwa amevaa kofia maalumu laini kwa ajili ya kukinga nywele zake.

Nikiwa napanga vitu kwenye begi langu mara macho yangu yakafanya ziara makini nikimtazama Rehema kuanzia juu na hapo nikakutana na tabasamu laini usoni mwake. Macho yake meupe na legevu yakafanikiwa kuichangamsha akili yangu. Tabasamu lake maridhawa likazisogeza kingo pana za mdomo wake juu na chini na hivyo kuyafichua meno yake meupe yaliyopangika vizuri.

Kisha macho yangu yalihama toka kwenye uso wake na kuanza kutambaa na shingo yake nzuri hadi kifuani. Kifua kilichotanuka na kubeba matiti ya wastani yaliyoachiana nafasi ya kutosha huku chuchu zake zikiwa zimesimama kana kwamba hakuwa akinyonyesha.

Hamu ya kumtazama haikuishia hapo, macho yangu yalielekea kwenye tumbo lake, na hapo nikakutana na tumbo la ubapa ambalo lilikana kuwa lilikuwa limetoka kubeba kiumbe kwa muda wa miezi tisa, kisha macho yangu yalifunga tena safari kuelekea kiunoni na hapo yakakutana na kiuno kilichobonyea na kuacha fursa ya nyonga kuchanua zilivyotaka, nyonga ambazo zilikuwa zimefinyangwa barabara. Hapo tena macho hayakukaa sana yakahamia kwenye mapaja yaliyonona. Sasa macho yangu yalituwama katikati ya mapaja yake kwa muda.

Hamu ya mapenzi ikanijaa juu ya Rehema lakini sikuweza kufanya chochote kwa kuwa nilifahamu kuwa alikuwa ametoka kwenye operesheni ya uzazi miezi miwili tu iliyokuwa imepita. Wakati wote huo Rehema alikuwa ananitazama kwa umakini na kuniacha niustaajabie uzuri wake kwa mara nyingine tena. Yeye mwenyewe alijifahamu kuwa ni mzuri sana.

Inaendelea...
 
ufukweni mombasa.JPG

208

Hata hivyo niliporudia kumtazama vizuri usoni jambo moja likanitatiza. Kulikuwa na kila dalili kuwa alikuwa ametoka kulia muda mfupi uliokuwa umepita kwani michirizi ya machozi yake mashavuni ilikuwa bado kufutika vizuri pamoja na jitihada za kuifuta zilizofanyika. Niligundua kuwa Rehema alikuwa anafanya jitihada za kuificha hali ile lakini hakufanikiwa.

Dah! Moyo wangu uliingiwa na ganzi, nikajiuliza kulikuwa na tatizo gani? Ni nini kilikuwa kimemtokea Rehema hadi atokwe na machozi? Na kwa nini hakutaka nijue kama alikuwa analia? Nilijiuliza maswali hayo pasipo kupata majibu, hatimaye nikaacha kupanga vitu vyangu na kumshika mkono kisha nikamkalisha kitandani kwa upole.

Bila upinzani wowote Rehema aliketi pale juu ya kitanda huku sauti ya kilio cha kwikwi ikianza kuhanikiza mle chumbani. Sasa hakuweza tena kuyazuia machozi yake. Mara hii machozi yalimbubujika upya kama chemchem ya kijito cha kondeni. Nikawahi kumkumbatia mikononi mwangu kisha nikamtazama usoni kwa upole, kabla ya kumuuliza huku nikiwa nimeyatuliza macho yangu usoni kwake. “Nini kimetokea, mke wangu?”

Nilimuuliza huku nikimtazama kwa umakini lakini hakunijibu, na badala yake aliangua kilio huku kingo za midomo yake zikimcheza cheza kama mtoto mdogo.

“Niambie basi, Mama Junior, kwani kumetokea nini?” nilimuuliza tena kwa sauti iliyoonesha wazi kuwa nilikuwa na wasiwasi. Safari hii swali langu lilimfanya anitazame kwa uso wa huzuni huku macho yake yakiwa yamezingirwa na machozi.

“Hakuna kilichotokea,” Rehema alijibu, sauti yake ilikuwa laini lakini yenye uchungu mwingi.

“Sasa nini kinachokuliza!” nilimuuliza huku nikishindwa kuuficha mshangao wangu.

“Ni wewe,” Rehema alinijibu na kushusha pumzi. Jibu lake lilinishtua sana na hapo nikamkazia macho kumtazama kama ambaye sikuwa nimemsikia vizuri.

“Mimi? Ninakuliza ki vipi!” nilimuuliza kwa mshangao.

“Basi tu! Hata sijui kwa nini sitaki kukuona ukiondoka hapa nyumbani!” Rehema alinijibu huku akiendelea kulia kama mtoto anayedeka.

“Usijali… najua utakuwa mkiwa nikiondoka kwa kuwa ni muda mfupi tu umepita tangu Mungu anirejeshe tena kwako na sijawahi kuwa mbali na wewe… itabidi uvumilie tu. Kama ujuavyo, hii ni safari ya muhimu sana kwangu na kwako pia. Ni safari ya maana kwa maisha yetu na ya watoto wetu. Wiki tatu si muda mrefu sana, mke wangu,” nilimsihi Rehema huku nikiwa nimeyatuliza macho yangu kwenye uso wake.

Rehema alibaki amejiinamia pasipo kusema neno, na hapo nikaongeza, “Usilie kiasi hicho, kwani hata mimi nisingelia hivyo kama ningekuwa wewe. Sipendi nirudipo nikukute umedhoofika kwa kuwaza. Napenda nikukukute wewe na mtoto mkiwa buheri wa afya, sawa?”

Rehema aliinua uso wake uliosheheni maumivu, akanitazama usoni. “Baba Junior,” aliita kwa sauti ndogo na tulivu kisha akaendelea, “Unajua tangu ule mkasa utokee nimekuwa nasita sana kukuruhusu uende mbali nami. Unadhani nitaishije wiki tatu bila wewe! Wiki tatu ni muda mrefu sana kuwa mbali na wewe. Zitakuwa ni wiki za tabu maishani mwangu,” Rehema alisema kwa majonzi.

Sasa alishindwa kuendelea kunitazama. Sikujua kwa nini alikuwa na majonzi kiasi hicho! Jambo hilo lilianza kunitisha hasa nilipokumbuka kuwa hata siku tuliyokuwa tunatoka Arusha kwenye fungate kabla ya kupata ajali iliyonisababishia kupoteza kumbukumbu Rehema alionekana kama mtu mwenye wasiwasi hivi! Ni kama alijua kuwa jambo baya lingetutokea ingawa hakusema.

Vidole vyangu vikabonyeza bega lake taratibu kisha nikasema, “Najua… najua, lakini tabu hiyo si kwako tu hata kwangu. Lichukue jambo hili kirahisi… Fikiria zaidi hali yako na ya mtoto wetu kuliko kutokuwako kwangu karibu nawe, najua kuna mengi ya kufanya ya kujipotezea mawazo.”

Rehema alinitazama kwa namna ambayo sikuweza kupata tafsiri kabisa kisha akaachia tabasamu. Lilikuwa tabasamu dogo lililonitia hamu ya kumbusu. Taratibu mkono wangu ulioshika bega lake ukatambaa mgongoni mwake, na hapo nikahisi Rehema alilihisi kwa mbali joto la vidole vyangu, maana aliyafunga macho yake na kuanza kuvuta pumzi kwa tabu.

* * *



Saa 5:50 usiku…

Zilikuwa zimebaki dakika kumi tu kabla ya muda wa safari yangu kwenda Dar es Salaam kuanza. Nilitoka chumbani nikiwa nimevaa suruali nyeusi ya dengrizi, shati la bluu la mikono mirefu na juu yake nilivalia jaketi jeusi la mtindo wa kizibao na raba nyeusi miguuni. Mkononi nilikuwa nimeshika begi langu la safari na kwenda sebuleni ambako nilimkuta Rehema akiwa amesimama kajiegemeza na ukuta.

Bado alikuwa ndani ya nguo za kulalia ila aliongezea kwa kujifunga kanga juu yake. Mikono yake aliichomeka ndani ya kanga kwa mbele na alikuwa akitafakari. Muda wote alikuwa akilengwalengwa na machozi.

Japo nilikuwa nimemsihi sana apumzike lakini hakuwa amepata usingizi hadi muda huo. Nilimtazama kwa umakini kwa kitambo kidogo kisha nilikwenda kusimama karibu yake, nikamwekea mkono taratibu begani. Mara mlio wa gari ukasikika na gari lenyewe lilikuwa likija hapo kwetu na kusimama nje ya uzio wa nyumba, kisha dereva wa gari hilo akapiga honi mara moja ya kuniashiria kuwa alikuwa amefika kunichukua.

Mara moja nilitambua kuwa hilo ndilo gari nililopaswa kuondoka nalo, na hapo nikamwona Rehema akishindwa kujizuia, machozi ya uchungu yalimtoka kimya kimya pasipo kilio cha kelele. Haraka sana alijiziba uso kwa kanga.

“Rehema!” niliita nikiongea kwa sauti tulivu karibu na sikio lake. Rehema alinitazama tu pasipo kusema neno, kisha alipitisha kipande cha kanga yake machoni kufuta machozi.

Nilimsogeza karibu yangu akawa kama sehemu ya mwili wangu. Kisha alijigeuza akakutanisha mikono yake nyuma ya shingo yangu na kuisogeza midomo yake karibu na midomo yangu, tukaikutanisha. Tulibaki hivyo kwa muda nisioweza kuukumbuka, mioyo yetu ilidunda kwa kasi na jasho jepesi lilikuwa linatutoka. Kisha nikamwachia.

Mara nikaona mlango wa kuelekea vyumbani ukifunguliwa taratibu na kisha Pendo, msichana wetu wa kazi akijitokeza na kututazama kwa wasiwasi mkubwa. Nilimtazama Pendo mara moja tu kisha nikayarudisha macho yangu kwa Rehema.

“Rehema…” niliita tena, sauti yangu ilikuwa ndogo, “nakuomba usiwaze sana nikiondoka, utasababisha maziwa yashindwe kutoka na hatimaye mtoto anaweza kudhoofika. Niahidi hivyo tafadhali,” nilisema huku nikimtazama kwa umakini.

“Baba Junior…” Neema aliita, sauti yake ilikuwa ndogo zaidi na macho yake yalifunguka nusu tu, “ninakuahidi kuwa nitazingatia yote hadi utakaporudi. Naahidi hivyo, mume wangu,” alisema huku akinikumbatia na kunibusu shavuni.

Inaendelea...
 
ufukweni mombasa.JPG

209

“Sawa, muda unaenda,” nilimwambia Rehema huku nikiangalia saa yangu ya mkononi. “Napaswa kuondoka kwani tumekubaliana kuondoka saa sita kamili usiku huu huu na hivyo yafaa niharakishe, sijui utapenda kunisindikiza hadi hapo nje?”

Rehema alitingisha kichwa chake kwa huzuni huku akinitazama usoni kisha aliniacha na kuelekea chumbani huku akifuta machozi. Pendo alimtazama Rehema kwa mshangao kisha akayarudisha macho yake kwangu, hata hivyo hakusema neno. Sikuelewa kwa nini Rehema alikuwa na huzuni kubwa kiasi hicho.

Kwa mara nyingine tena nilitamani niahirishe safari yangu lakini sikuwa na namna yoyote ya kufanya kwani taifa lilikuwa muhimu zaidi na liliniamini kwenda kuifanya kazi hiyo ngumu ya kuandaa mfumo, na hivyo nisingeweza kukataa.

“Pendo, njoo ufunge geti na mlango,” nilimwambia Pendo kisha sikungoja, nikachukua begi langu la safari lililokuwa na magurudumu na kutoka haraka.

Huko nje nililikuta gari maalumu aina ya Nissan Patrol la rangi ya jeshi, lenye vioo vya giza visivyoruhusu mtu kuona waliomo ndani likiwa limeegeshwa usawa wa geti kubwa la kuingilia kwenye uzio wa nyumba. Gari hilo lilikuwa linaunguruma taratibu kuonesha kuwa halikuwa limezimwa.

Dereva wa gari lile alikuwa Luteni Lister na aliponiona nikitokea kwenye geti dogo la nyumba alishuka haraka toka kwenye lile gari na kunipa mkono wa makaribisho huku tabasamu pana likichanua usoni kwake kisha akalichukua begi langu na kufungua mlango wa nyuma, akaliweka vizuri, na wakati huo mimi nilizunguka na kufungua mlango wa mbele. Nikaingia na kuketi kwa utulivu huku nikifunga mkanda.

Luteni Lister alikuwa amevaa suruali ya dengrizi ya rangi ya samawati, fulana nyepesi nyeusi na juu yake alivaa shati zito la dengrizi la rangi ya samawati la mikono mirefu. Mkononi alivaa saa na kichwani alivaa kofia ya bluu ya kapelo na miwani mikubwa myeusi ingawa muda huo hakukuwa na jua.

Luteni Lister, Komando na Ofisa Usalama wa Taifa, alipoingia ndani ya gari na kuketi nyuma ya usukani aligeuza shingo yake kunitazama usoni kwa namna ya kunisaili, “Hujasahau kitu chochote, Boss?”

“Sidhani… tunaweza kuondoka,” nilimwambia kwa sauti tulivu kisha nikashusha pumzi ndefu.

Kama ilivyokuwa kwangu, Luteni Lister pia hakuonekana mtu wa maneno mengi na hivyo haraka akatumbukiza gia na kukanyaga pedeli ya mafuta, na hapo gari likaanza kuondoka taratibu na kuingia barabarani kisha Luteni Lister alikata kushoto na kuingia katika barabara nyingine na hapo akaongeza mwendo hadi tulipofika katika eneo la Nyihogo akakata na kuingia upande wa kulia akiifuata barabara kuu ya lami inayotoka katika nchi za Rwanda, Uganda na Burundi.

Muda huo wa usiku Mji wa Kahama ulikuwa umemezwa na utulivu wa aina yake. Magari machache sana yalionekana barabarani wakati safari yetu ilipokuwa ikianza na hivyo ikawa rahisi kwetu kwenda kwa mwendo tulioutaka. Nilimtupia jicho Luteni Lister nikamwona akizipangua gia, nikashusha pumzi za ndani kwa ndani na kujiweka sawa kwenye kiti changu, sasa safari rasmi ya kuelekea Jijini Dar es Salaam kwenye kazi maalumu ya kiintelijensia ikawa imeanza.

Hata hivyo akili yangu bado ilikuwa ikisumbuka katika namna ya kutaka kufahamu kama ni kweli nilikuwa kwenye gari la Taasisi ya Usalama wa Taifa nikiendeshwa na Ofisa Usalama ambaye pia alikuwa Komando wa daraja la pili, na nilitakiwa kwenda Jijini Dar es Salaam kutengeneza mfumo maalumu wa kufuatilia masuala ya uhalifu wa kimtandao! Bado akili yangu ilikuwa katika mpumbao fulani hivi na mara kwa mara sikuacha kujiuliza ikiwa ile safari ilikuwa ni ndoto au lilikuwa tukio halisi lililokuwa likitokea maishani mwangu!

Nilimtupia jicho Luteni Lister nikamwona akiwa yupo makini kwenye usukani macho akiwa kayakaza kutazama barabarani. Sasa akili yangu ikawa kama vile imefunguka, nikaanza kupoteza utulivu wa kiakili huku mitupo ya mapigo ya moyo wangu ikiongezeka mara dufu.

Nikiwa nimeanza kuzama kwenye tafakuri mawazo yangu yakahamia kwa mke wangu Rehema, nilikumbuka jinsi nilivyopata shida kujieleza wakati nikimwambia kuwa nilihitajika Jijini Dar es Salaam kwenye mradi maalumu wa kuandaa mfumo maalumu ambao ungetumika kwenye vyuo vya teknolojia ya habari na mawasiliano, mradi ambao ungechukua takriban wiki tatu.

Ndiyo, safari ya wiki tatu lakini ingeweza kuwa ya muda wa mwezi, miezi au hata mwaka kutegemeana na matakwa na wakuu wa usalama kwa yale ambayo yangejiri kwenye kazi yenyewe. Kwangu, safari hiyo haikuwa na shida yoyote tatizo lilikuwa kwenye namna ya kazi yenyewe hususan pale ambapo wakuu hao wa usalama wangeonesha kuridhishwa na kazi husika.

Hata hivyo, kwa kuwa nilikuwa nimepitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria baada ya masomo yangu pale Mzumbe, nilifahamu fika kuhusu tafsiri sahihi ya uzalendo kwa nchi yangu ni kutii, na sasa sikuwa na namna yoyote ya kufanya zaidi ya kutii amri kama uzalendo unavyotaka.

Na nilipokuwa katika harakati za kuupisha utulivu kichwani mwangu katika namna ya kutafakari zaidi kwa nini Rehema hakutaka niondoke mara nikashtushwa na myumbo wa ghafla wa gari letu huku nikimshuhudia Luteni Lister akikanyaga breki kwa nguvu na kulifanya gari lisote na kuyumba kwenye barabara hiyo pana, bahati nzuri gari halikutoka nje ya barabara.

Kisha Luteni Lister aliyekuwa ametahayari kidogo aliachia tusi zito la nguoni na kusonya kwa hasira huku akikanyaga pedeli ya mafuta, gari likajivuta na kufanya magurudumu yake kuchimba lami, kisha likaondoka kwa mwendo wa kasi.

Niligeuza shingo yangu kutazama kando na hapo nikaishuhudia pikipiki aina ya Boxer iliyokuwa imebeba watu wawili ikiserereka barabarani kabla ya dereva wa pikipiki hiyo kuiweka sawa na kisha akaongeza mwendo pasipo kusimama. Na hapo nikatambua kuwa dereva wa ile pikipiki hakuwa makini kwani alikuwa ameingia upande wetu akiwa katika mwendo wa kasi na kumfanya Luteni Lister alazimike kumkwepa, vinginevyo tungezungumza mengine.

Nilipotazama vizuri nje nikagundua kuwa tulikuwa tunavuka eneo la mgodi wa dhahabu wa Buzwagi. Nikashusha pumzi ndefu na kujiegemeza kwenye kiti changu huku nikiyasikilizia mapigo ya moyo wangu yaliyokuwa yakienda kasi isivyo kawaida.

* * *

Mambo yanazidi kunoga, endelea kufuatilia...
 
View attachment 2310709
209

“Sawa, muda unaenda,” nilimwambia Rehema huku nikiangalia saa yangu ya mkononi. “Napaswa kuondoka kwani tumekubaliana kuondoka saa sita kamili usiku huu huu na hivyo yafaa niharakishe, sijui utapenda kunisindikiza hadi hapo nje?”

Rehema alitingisha kichwa chake kwa huzuni huku akinitazama usoni kisha aliniacha na kuelekea chumbani huku akifuta machozi. Pendo alimtazama Rehema kwa mshangao kisha akayarudisha macho yake kwangu, hata hivyo hakusema neno. Sikuelewa kwa nini Rehema alikuwa na huzuni kubwa kiasi hicho.

Kwa mara nyingine tena nilitamani niahirishe safari yangu lakini sikuwa na namna yoyote ya kufanya kwani taifa lilikuwa muhimu zaidi na liliniamini kwenda kuifanya kazi hiyo ngumu ya kuandaa mfumo, na hivyo nisingeweza kukataa.

“Pendo, njoo ufunge geti na mlango,” nilimwambia Pendo kisha sikungoja, nikachukua begi langu la safari lililokuwa na magurudumu na kutoka haraka.

Huko nje nililikuta gari maalumu aina ya Nissan Patrol la rangi ya jeshi, lenye vioo vya giza visivyoruhusu mtu kuona waliomo ndani likiwa limeegeshwa usawa wa geti kubwa la kuingilia kwenye uzio wa nyumba. Gari hilo lilikuwa linaunguruma taratibu kuonesha kuwa halikuwa limezimwa.

Dereva wa gari lile alikuwa Luteni Lister na aliponiona nikitokea kwenye geti dogo la nyumba alishuka haraka toka kwenye lile gari na kunipa mkono wa makaribisho huku tabasamu pana likichanua usoni kwake kisha akalichukua begi langu na kufungua mlango wa nyuma, akaliweka vizuri, na wakati huo mimi nilizunguka na kufungua mlango wa mbele. Nikaingia na kuketi kwa utulivu huku nikifunga mkanda.

Luteni Lister alikuwa amevaa suruali ya dengrizi ya rangi ya samawati, fulana nyepesi nyeusi na juu yake alivaa shati zito la dengrizi la rangi ya samawati la mikono mirefu. Mkononi alivaa saa na kichwani alivaa kofia ya bluu ya kapelo na miwani mikubwa myeusi ingawa muda huo hakukuwa na jua.

Luteni Lister, Komando na Ofisa Usalama wa Taifa, alipoingia ndani ya gari na kuketi nyuma ya usukani aligeuza shingo yake kunitazama usoni kwa namna ya kunisaili, “Hujasahau kitu chochote, Boss?”

“Sidhani… tunaweza kuondoka,” nilimwambia kwa sauti tulivu kisha nikashusha pumzi ndefu.

Kama ilivyokuwa kwangu, Luteni Lister pia hakuonekana mtu wa maneno mengi na hivyo haraka akatumbukiza gia na kukanyaga pedeli ya mafuta, na hapo gari likaanza kuondoka taratibu na kuingia barabarani kisha Luteni Lister alikata kushoto na kuingia katika barabara nyingine na hapo akaongeza mwendo hadi tulipofika katika eneo la Nyihogo akakata na kuingia upande wa kulia akiifuata barabara kuu ya lami inayotoka katika nchi za Rwanda, Uganda na Burundi.

Muda huo wa usiku Mji wa Kahama ulikuwa umemezwa na utulivu wa aina yake. Magari machache sana yalionekana barabarani wakati safari yetu ilipokuwa ikianza na hivyo ikawa rahisi kwetu kwenda kwa mwendo tulioutaka. Nilimtupia jicho Luteni Lister nikamwona akizipangua gia, nikashusha pumzi za ndani kwa ndani na kujiweka sawa kwenye kiti changu, sasa safari rasmi ya kuelekea Jijini Dar es Salaam kwenye kazi maalumu ya kiintelijensia ikawa imeanza.

Hata hivyo akili yangu bado ilikuwa ikisumbuka katika namna ya kutaka kufahamu kama ni kweli nilikuwa kwenye gari la Taasisi ya Usalama wa Taifa nikiendeshwa na Ofisa Usalama ambaye pia alikuwa Komando wa daraja la pili, na nilitakiwa kwenda Jijini Dar es Salaam kutengeneza mfumo maalumu wa kufuatilia masuala ya uhalifu wa kimtandao! Bado akili yangu ilikuwa katika mpumbao fulani hivi na mara kwa mara sikuacha kujiuliza ikiwa ile safari ilikuwa ni ndoto au lilikuwa tukio halisi lililokuwa likitokea maishani mwangu!

Nilimtupia jicho Luteni Lister nikamwona akiwa yupo makini kwenye usukani macho akiwa kayakaza kutazama barabarani. Sasa akili yangu ikawa kama vile imefunguka, nikaanza kupoteza utulivu wa kiakili huku mitupo ya mapigo ya moyo wangu ikiongezeka mara dufu.

Nikiwa nimeanza kuzama kwenye tafakuri mawazo yangu yakahamia kwa mke wangu Rehema, nilikumbuka jinsi nilivyopata shida kujieleza wakati nikimwambia kuwa nilihitajika Jijini Dar es Salaam kwenye mradi maalumu wa kuandaa mfumo maalumu ambao ungetumika kwenye vyuo vya teknolojia ya habari na mawasiliano, mradi ambao ungechukua takriban wiki tatu.

Ndiyo, safari ya wiki tatu lakini ingeweza kuwa ya muda wa mwezi, miezi au hata mwaka kutegemeana na matakwa na wakuu wa usalama kwa yale ambayo yangejiri kwenye kazi yenyewe. Kwangu, safari hiyo haikuwa na shida yoyote tatizo lilikuwa kwenye namna ya kazi yenyewe hususan pale ambapo wakuu hao wa usalama wangeonesha kuridhishwa na kazi husika.

Hata hivyo, kwa kuwa nilikuwa nimepitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria baada ya masomo yangu pale Mzumbe, nilifahamu fika kuhusu tafsiri sahihi ya uzalendo kwa nchi yangu ni kutii, na sasa sikuwa na namna yoyote ya kufanya zaidi ya kutii amri kama uzalendo unavyotaka.

Na nilipokuwa katika harakati za kuupisha utulivu kichwani mwangu katika namna ya kutafakari zaidi kwa nini Rehema hakutaka niondoke mara nikashtushwa na myumbo wa ghafla wa gari letu huku nikimshuhudia Luteni Lister akikanyaga breki kwa nguvu na kulifanya gari lisote na kuyumba kwenye barabara hiyo pana, bahati nzuri gari halikutoka nje ya barabara.

Kisha Luteni Lister aliyekuwa ametahayari kidogo aliachia tusi zito la nguoni na kusonya kwa hasira huku akikanyaga pedeli ya mafuta, gari likajivuta na kufanya magurudumu yake kuchimba lami, kisha likaondoka kwa mwendo wa kasi.

Niligeuza shingo yangu kutazama kando na hapo nikaishuhudia pikipiki aina ya Boxer iliyokuwa imebeba watu wawili ikiserereka barabarani kabla ya dereva wa pikipiki hiyo kuiweka sawa na kisha akaongeza mwendo pasipo kusimama. Na hapo nikatambua kuwa dereva wa ile pikipiki hakuwa makini kwani alikuwa ameingia upande wetu akiwa katika mwendo wa kasi na kumfanya Luteni Lister alazimike kumkwepa, vinginevyo tungezungumza mengine.

Nilipotazama vizuri nje nikagundua kuwa tulikuwa tunavuka eneo la mgodi wa dhahabu wa Buzwagi. Nikashusha pumzi ndefu na kujiegemeza kwenye kiti changu huku nikiyasikilizia mapigo ya moyo wangu yaliyokuwa yakienda kasi isivyo kawaida.

* * *

Mambo yanazidi kunoga, endelea kufuatilia...
Thanks Bishop, kazi iendelee
 
ufukweni mombasa.JPG

210

Ana kwa ana…




Saa 3:30 asubuhi…

ASUBUHI ya saa tatu na nusu siku ya pili, baada ya kufika Jijini Dar es Salaam, ilinikuta nikiwa kwenye lango kuu la Makao Makuu ya Taasisi ya Usalama wa Taifa (TISS) eneo la Oysterbay baada ya kuwasili nikiwa ndani ya gari aina ya Mercedes Benz jeusi lenye vioo vyeusi la Brigedia Jenerali Godwin Longinus, Mkurugenzi wa Uajiri Utafiti na Mafunzo wa Idara ya Usalama wa Taifa (Director of Recruitment Research and Training – DRRT).

Asubuhi hiyo Brigedia Jenerali Godwin Longinus, ambaye umri wake wa hamsini na mbili ulikuwa haujatosha kabisa kuzipokonya nguvu zake mwilini, alikuwa amevaa suti ghali ya kijivu ya single button na miwani mikubwa ya macho. Alikuwa mrefu aliyepanda hewani kisawasawa akiwa na urefu wa futi sita na nusu na mwenye mwili ulioshiba.

Alikuwa mweusi na mwenye sura ya mviringo iliyoonesha utulivu na macho yake yalikuwa makubwa, pamoja na misuli imara ya mikononi iliyotuna kikamilifu vilimfanya aonekane kama bondia mkongwe. Kichwani alikuwa na upara uliokuwa unawaka.

Hii ilikuwa siku ya pili baada ya kufika Jijini Dar es Salaam siku iliyokuwa imetangulia nilipokewa na Brigedia Jenerali Godwin Longinus mwenyewe na kisha nikapelekwa kwenye moja ya nyumba maalumu za watu wa usalama eneo lile la Oysterbay, jirani na Kanisa Katoliki la Mtakatifu Peter (St. Peter), nyumba iliyokuwa imeandaliwa maalumu kwa ajili yangu kama makazi ya muda. Hapo nilitakiwa kupumzika hadi kesho yake ili kupunguza uchovu wa safari ndefu ya kutoka Kahama.

Sasa wakati tukiwasili hapo makao makuu ya TISS, Maofisa wa kikosi cha ulinzi wa viongozi na vituo muhimu waliokuwa langoni walifungua geti la kuingilia hapo mara tu walipoliona gari la Brigedia Jenerali Godwin Longinus likikaribia lango hilo.

Brigedia Jenerali Godwin Longinus aliliingiza gari lake getini na kulisimamisha ili kuwapa walinzi nafasi ya kufunga geti na wakati huo huo Ofisa mwingine wa ulinzi aliyeshika bunduki aina ya SMG alisogea haraka kwenye dirisha la upande wa dereva alikokuwa amekaa Brigedia Jenerali Godwin Longinus.

“Mpatie gate pass huyu mgeni wangu ninayeingia naye. Ana kazi maalumu iliyomleta,” Brigedia Jenerali Godwin Longinus alimwambia yule Ofisa wa ulinzi kwa sauti kavu.

“Sawa mkuu,” yule Ofisa alijibu huku akinitazama usoni kwa shauku ya kutaka kunijua. Hata hivyo nilimwona akishusha pumzi za ndani kwa ndani kwani aliambulia patupu kwa kuwa mimi sikuwa mmoja wao.

“Samahani, unaitwa nani mkuu?” yule Ofisa aliniuliza kwa heshima.

“Jason Sizya,” nilimjibu yule Ofisa kwa sauti tulivu. Na yeye bila kuuliza swali la ziada aligeuka na kuliendea dirisha lililokuwa umbali wa takriban mita tatu hivi kutoka pale gari la Brigedia Jenerali Godwin Longinus lilipokuwa limesimama.

Nilimshuhudia yule Ofisa akimnong’oneza jambo Ofisa mwingine aliyekuwa ndani ya chumba cha walinzi akiikodolea macho runinga pana ambayo kwa vyovyote ilihusiana na kamera za ulinzi (CCTV monitor) iliyokuwa mbele yake. Baada ya takriban sekunde therathini yule Ofisa alirejea pale kwenye gari akiwa ameshikilia kitambulisho maalumu chenye utepe wa kuvaa shingoni na kunipatia.

“Nashukuru sana,” nilimwambia yule Ofisa wakati Brigedia Jenerali Godwin Longinus akiliondoa gari lake kuelekea kwenye jengo kuu, mahali yalipokuwepo maegesho maalumu kwa ajili ya magari ya wakuu wa usalama. Sikuwahi kuota hata siku moja kama kuna siku ningekuja kuingia katika ofisi hiyo.

Wakati akiliegesha gari lake kwenye maegesho maalumu Brigedia Jenerali Godwin Longinus alinifahamisha kuwa kulikuwa na tofauti kubwa sana kati ya ofisi hiyo ya Usalama wa Taifa na idara nyingine za serikali, kwani taasisi hiyo ilikuwa na utaratibu maalumu unaowazuia maofisa wake kwenda kwenye ofisi zisizo vituo vyao vya kazi bila sababu ya msingi. Utaratibu huo ulikuwa ukiwahusu maofisa wote bila kujali vyeo vyao, au idadi ya miaka waliyoitumikia idara hiyo ya Usalama wa Taifa.

Aliniambia kuwa hata kama ofisi ya kitengo kimoja iko kwenye jengo moja na kitengo kingine bado maofisa wa vitengo hivyo hawakuruhusiwa kutembeleana ofisini bila ruhusa maalumu au sababu za msingi. Na iwapo ingetokea ofisa alitakiwa kwenda katika ofisi nyingine kwa maana ya kuwa nje ya kituo chake cha kazi, kwa dharula au sababu nyingine yoyote, alitakiwa kuomba kibali (gate pass) cha kumruhusu kufanya hivyo. Kinyume cha hapo angelazimika kubaki kwenye ofisi ya mlinzi.

Utaratibu huo ulijulikana kama ‘compatimentation’ na uliisaidia sana taasisi hiyo kutunza siri, kuendesha operesheni zinazojitegemea na kuwazuia maadui wa taifa kujipatia taarifa muhimu kwa urahisi kama wangefanikiwa kupenyeza mtu wao ndani ya Idara. Kwa ujumla taasisi hiyo ilikuwa imeweka kanuni na taratibu hizo ili kulinda nyaraka na siri za Idara, na pia kujenga nidhamu ya maofisa wake, na kwamba kila ofisa alikuwa anajua kwamba muda wowote katika ajira yake angeweza kufuatiliwa nyendo zake kwa sababu mbalimbali.

Kutokana na utaratibu huu, Brigedia Jenerali Godwin Longinus aliniambia kuwa hakuna ofisa yeyote, wa mahali popote na au wa cheo chochote hata Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (Director General of Intelligence and Security – DGIS) wa kujisifu kuwa anajua kila kitu kinachotendeka ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa.

Hata hivyo, sikuelewa kwa nini Brigedia Jenerali Godwin Longinus alikuwa akinieleza mambo yote hayo ambayo mimi kama raia wa kawaida huenda sikutakiwa kuyajua kwani ni siri za Idara. Hata hivyo nilimsikiliza kwa umakini nikiwa mtulivu wakati mkurugenzi huyo wa uajiri utafiti na mafunzo wa usalama wa taifa akizima injini ya gari lake kisha sote wawili tukateremka na kutembea sambamba kuelekea ndani ya jengo lililokuwa mita chache mbele yetu.

Wakati tukitembea kuelekea ndani ya ofisi zile za makao makuu ya Idara ya Usalama wa Taifa nilikuwa nikiyatembeza macho yangu kutazama huku na kule nikilipeleleza jengo lile lenye ulinzi wa kuaminika saa ishirini na nne. Maofisa wote walikuwa katika hali ya tahadhari na kila ukumbi (corridor) tulioupita walinzi walikuwa imara tayari kwa lolote.

Kisha tuliingia kwenye ofisi moja nzuri na pana ikiwa na mazingira nadhifu sana yaliyovutia zaidi kwa mpangilio wa samani za kisasa, ilikuwa na zulia jekundu sakafuni na meza ndefu ya ofisini yenye viti kumi na viwili. Viti sita upande wa kushoto na viti vingine sita upande wa kulia.

Mara moja nilifahamu kuwa hiyo ndiyo ilikuwa ofisi ya Brigedia Jenerali Godwin Longinus, Mkurugenzi wa Uajiri Utafiti na Mafunzo wa Idara ya Usalama wa Taifa. Brigedia Jenerali Godwin Longinus alinikaribisha kwa sauti tulivu niketi kwenye kochi moja la sofa lililokuwa likitazamana na ile meza yake mle ndani. niliketi kwa utulivu mkubwa huku nikisubiri kusikia ni kipi alichotaka kunieleza.

Kisha yeye alizunguka akaenda kuketi nyuma ya meza yake kubwa ya ofisini mwisho wa ofisi ile upande wa kushoto na kisha akaegemea kiti chake cha ofisi na kuelekeza macho yake kwenye faili moja alilolitoa kwenye droo ya meza yake na kisha kuliweka juu ya meza yake, alilitazama kwa kitambo kisha akalifunua na kupitia haraka haraka taarifa zake.

Baada ya takriban sekunde ishirini za kulipitia lile faili aliyahamisha macho yake kutoka kwenye lile faili hadi kwenye uso wangu, na macho yetu yalipokutana nikajikuta nikipata kitete cha muda huku mapigo yangu ya moyo yakibadili mwendo na kwenda kasi. Naam! Sasa nilikuwa ana kwa ana nikitazamana na mwanausalama aliyebobea katika medani za kijasusi, Brigedia Jenerali Godwin Longinus.

Inaendelea...
 
ufukweni mombasa.JPG

211

Niliwahi kusoma mahala kuwa Brigedia Jenerali Godwin Longinus alikuwa amejikita kwenye kazi ya ujasusi kwa zaidi ya miaka 25. Hatua hiyo ni miongoni mwa sifa zilizomfikisha katika nafasi aliyopo na alikuwa amepata kulihudumia taifa katika masuala mbalimbali ya kiintelijensia aliyopangiwa.

Pia alikuwa Komando wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikosi namba 92 Ngerengere (92 KJ) na msomi wa Shahada mbili za Sheria na Shahada ya Sanaa katika Lugha na Uandishi. Alikuwa amepata mafunzo maalumu ya mapigano ya ana kwa ana ya kiwango cha juu zaidi, kutumia karibia aina zote za silaha na milipuko ya jeshi, ufuatiliaji adui, kukabiliana na hali ngumu kwenye mazingira ya kawaida na nyikani, kumkwepa, kumzuia na kumtoroka adui.

Mafunzo hayo yalimfanya kuwekwa katika kundi la Ofisa Mwenye Mbinu Maalumu (Specialized Skills Officer) na yalimsaidia sana kupata ufumbuzi wa maswali mengi yaliyowasumbua wataalamu na wakongwe wengine wa ujasusi Afrika.

Naam, sasa nilikuwa ana kwa ana na jasusi mbobevu, macho yake makali yalikuwa yananitazama kwa umakini pasipo kusema neno lolote huku akionekana kuipa utulivu akili yake. Mikono yake alikuwa ameiegemeza juu ya meza.

“Karibu sana Mr. Sizya,” Brigedia Jenerali Godwin Longinus aliniambia akivunja ukimya huku akiachia tabasamu la makaribisho.

“Nashukuru sana, mkuu,” nilimwitikia mwanausalama yule kwa utulivu huku akili yangu ikiwa bado kwenye tafakuri ya kutaka kufahamu zaidi kuhusu kazi iliyokuwa mbele yangu.

“Huwenda ukawa umeshangazwa sana kuona mimi ndiye niliyekupokea badala ya Mkurugenzi wa Habari na Teknolojia wa Idara, bwana David Mshana…” Brigedia Jenerali Godwin Longinus alisema na kuweka kituo kidogo kisha akakohoa kidogo kusafisha koo lake kabla ya kuendelea.

“Kama ambavyo sasa unafahamu, mimi ndiye mkurugenzi wa uajiri utafiti na mafunzo… hivyo nakutaarifu kuwa baada ya mchakato mrefu wa kukufuatilia yaani vetting iliyofanywa hata kabla hujapata ile ajali iliyokusababishia kupoteza kumbukumbu zako, Idara ya Usalama wa Taifa imejiridhisha kuwa unazo sifa zote zinazokuruhusu kujiunga na Idara kwa programu maalumu ya mafunzo ya kijasusi…” Brigedia Jenerali Godwin Longinus alisema na kuweka tena kituo kisha alinitazama kwa utulivu.

Nilishtuka sana kusikia kwamba nilikuwa naunganishwa kwenye programu ya mafunzo ya kijasusi, kwa kuwa sikuwa nimetegemea kabisa jambo hilo. Nilihisi labda nilikuwa ndotoni na pindi ningeamka ningekuta kila kitu kikiwa katika hali yake ya kawaida.

Kisha kilipita kitambo kifupi cha ukimya halafu nikamwona Brigedia Jenerali Godwin Longinus akinyoosha mkono wake kunipa karatasi tatu zilizobanwa pamoja alizozitoa ndani ya lile faili lililokuwa juu ya meza yake.

“Nina uhakika itakuwa rahisi sana kwako kufanya mafunzo haya ya kijasusi na kufuzu kwa kuwa una IQ kubwa, ni mtaalamu uliyebobea katika masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano, umeshapitia mafunzo ya kijeshi ya JKT kwa mujibu wa sheria na una mkanda mweusi katika karate…” Brigedia Jenerali Godwin Longinus alisema huku akinyoosha mkono wake kunikabidhi zile karatasi.

Haraka nikanyoosha mkono wangu kuzipokea zile karatasi kisha nikajiegemeza vizuri kwenye lile kochi nikayapitia haraka haraka maelezo yaliyokuwa kwenye karatasi zile.

Mara tu nilipoanza kusoma yale maelezo kwenye zile karatasi nikatambua kuwa ilikuwa ni fomu maalumu ya kujiunga na chuo maalumu cha ujasusi nchini Misri na kwamba tangu muda huo kila kitu changu kilikuwa chini ya udhibiti wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Sasa nikatambua kwa nini Brigedia Jenerali Godwin Longinus ndiye aliyenipokea badala ya David Mshana, mkurugenzi wa habari na teknolojia. Na hapo moyo wangu ukapoteza utulivu na kijasho chepesi kikaanza kunitoka sehemu mbalimbali za kwa mwili wangu.

“Idara ya Usalama wa Taifa kama zilivyo taasisi nyingi za kijasusi duniani ni Para Military Institute yaani taasisi inayoendeshwa nusu kijeshi nusu kiraia. Kwa sababu hii maofisa wetu hulazimika kubadilika kuendana na mazingira ya kazi. Pale mambo yanapokuwa shwari maofisa hufanya kazi kama raia halisi, na pale mambo yanapochachamaa ujeshi huchukua nafasi yake. Ndiyo maana unatakiwa ukapate mafunzo maalumu kwenye chuo makini nchini Misri…” Brigedia Jenerali Godwin Longinus alisema, kisha akaongeza.

“Kila kitu kipo kwenye mchakato, utatakiwa kuondoka nchini wiki ijayo kwenda Misri kwani mafunzo hayo yanaanza mara moja na yatakuwa ya miezi tisa yatakayokufanya uwe na ujuzi mkubwa wa mambo ya kiintelijensia… hivyo kuanzia sasa hutaruhusiwa kuwasiliana na jamaa zako wala kurudi nyumbani.”

“Vipi kuhusu familia yangu maana mke wangu…” nilitaka kujieleza lakini Godwin Longinus alinikata kauli.

“Usihofu, tayari kila kitu kinashughulikiwa na Idara. Mkeo atajulishwa kila kitu na jukumu la wale wote wanaokutegenea litakuwa la Idara wakati wote utakaokuwa mafunzoni. Labda tu nikwambie jambo ambalo ulikuwa hulifahamu; mkeo Rehema pia ni Ofisa wa Kificho wa Idara ya Usalama wa Taifa. Na tafadhali jambo hili libaki kuwa jambo lisilopaswa kuongelewa hadharani yaani siri… SIRI KUBWA!” Brigedia Jenerali Godwin Longinus alisema kwa msisitizo wakati akitamka neno SIRI KUBWA.

Kauli kuwa mke wangu Rehema alikuwa ofisa kificho ilinifanya nihisi mwili wangu ukisisimka na pumzi zikianza kunipaa. Nikiwa pale kwenye sofa moyo wangu ulionekana kupoteza utulivu hasa pale nilipokumbuka namna ambavyo Rehema alikuwa mwepesi sana kuyafahamu mambo yangu niliyoyafanya kuwa siri hata kabla sijafungua mdomo wangu kumwambia, na mara nyingi nilikuwa nashangazwa sana na namna alivyoweza kufahamu mambo hayo na hata kuyasoma mawazo yangu na bado akajifanya hajui chochote. Kumbe Ofisa Kificho!

Baada ya maelezo yale Godwin Longinus aliniagiza niijaze ile fomu kwa usahihi na kisha nimkabidhi hati yangu ya kusafiria (Passport) ambayo niliambiwa tangu mwanzo kuwa ni muhimu nifike nayo pale kwenye ofisi za Idara ya uslama wa Taifa. Nilimkabidhi ile hati ya kusafiria kisha nikaanza kuijaza ile fomu. Ilinichukua dakika zisizozidi tano kuijaza na kisha nikamkabidhi.

“Kwa upande wangu nadhani zoezi limekwisha maana kile ulichopaswa kufanya tayari kimefanyika, sasa unaweza kwenda ofisini kwa katibu muhtasi wangu kuendelea na mambo mengine,” Brigedia Jenerali Godwin Longinus aliniambia baada ya kuipitia ile fomu na kuridhishwa na maelezo niliyoyaandika.

Kisha nikamwona Brigedia Jenerali Godwin Longinus akivuta droo na kuchukua kitabu fulani kilichokuwa na Nembo ya Taifa na ile ya Usalama wa Taifa na kunikabidhi. “Baadaye utakapokuwa umepumzika kwenye makazi yako pitia pitia kitabu hiki ili uifahamu vizuri Idara yetu ya Usalama wa Taifa,” Brigedia Jenerali Godwin Longinus aliniambia wakati akinikabidhi kile kitabu.

Nilikipokea kwa heshima na taadhima huku nikanyanyuka toka kwenye kochi na kumuaga kwa kumpa mkono kama ilivyo ada ya Watanzania, halafu nikageuka na kutembea taratibu kuelekea chumba cha katibu muhtasi wake, mahali uliko mlango wa kutokea ukumbini.

Wakati nikitembea na kuufikia mlango wa chumba cha katibu muhtasi wake nilikuwa na uhakika kuwa macho ya Brigedia Jenerali Godwin Longinus yalikuwa nyuma yangu yakinisindikiza. Mara tu niliposhika kitasa cha mlango na kukinyonga ili kuufungua ule mlango niligeuka na kumtazama Brigedia Jenerali Godwin Longinus na nilichokiona usoni kwake lilikuwa tabasamu la kunitaka niwe tayari kwa chochote.

Nami niliachia tabasamu kisha nikaingia katika chumba cha katibu muhtasi wa Brigedia Jenerali Godwin Longinus na kuiendea meza ya mwanadada mmoja mrefu mweupe kiasi na umri wake ulionekana kuwa kati ya miaka 32 na 36. Asubuhi hiyo alikuwa amevaa suti nzuri ya kike ya rangi ya maruni na viatu vya rangi hiyo hiyo ya maruni vyenye vikanyagio virefu vya mchuchumio. Mkononi alikuwa amevaa saa ndogo ya kike na alijipaka mafuta mazuri yaliyosambaa ofisi nzima.

Macho yake yalikuwa makubwa na malegevu na umbo lake lilikuwa la namba nane ambalo kwa vyovyote lilikuwa likiwapagawisha wanaume wengi kila alikopita na kuwaacha wakimtazama kwa macho ya matamanio.

Yule mwanadada alinitazama kwa tabasamu na kunielekeza sehemu ya kuketi huku akiniambia kuwa nisubiri kwani kulikuwa na mtu angekuja kunichukua.

“Sawa,” nilimjibu huku nikikiendea kiti hicho na kukaa. Sikuwa na fununu yoyote mtu huyo alikuwa nani na alitaka kunieleza jambo gani. Nilichokuwa nafahamu muda huo ni kwamba nilikuwa nimeingizwa rasmi kwenye idara ya usalama na sasa nilikuwa nasubiri taratibu zingine zifanyike ili niondoke kwenda Misri kwa mafunzo maalumu ya kijasusi. Hata hivyo sikuwa na la kufanya ila kusubiri.

Nikiwa nimeketi pale mara simu iliyokuwa mezani pa yule mwanadada ikaanza kuita kwa sauti ya chini. Akanyoosha mkono wake wa kushoto kuinyanyua na kusikiliza kidogo, kisha akairudisha sehemu yake ya awali na kuniambia, “Mkuu amesema unaweza kuagiza kinywaji wakati unasubiri maana mtu unayemtarajia atachelewa kidogo.”

Sikujivunga, nilimwambia yule dada kuwa nahitaji Sprite ya baridi. Yule mwanadada alinyanyua simu na kumwagiza mmoja wa wahudumu aende kwenye mgahawa wa Idara kutuletea vinywaji na vitafunwa, yeye aliagiza Pepsi.

Tuliletewa soda zetu na vitafunwa, na wakati tukinywa taratibu tulitumia muda huo mfupi kufahamiana zaidi na kuzungumza mambo mbalimbali huku kila mmoja akiwa mwangalifu katika maneno yake asivuke mipaka. Na hapo ndipo nilipomfahamu mwanadada huyo kuwa aliitwa Salma Kilonzo.

Wakati tukiendelea kunywa soda zetu huku tukipiga soga mara mlango wa ofisi yake ukafunguliwa na Luteni Lister akaingia ndani. Aliponiona akaachia tabasamu pana huku akinyoosha mkono wake kunisalimia kwa bashasha kisha akamsalimia Salma na kujitambulisha jina lake.

“Nimekufuata…” Luteni Lister aliniambia huku akinipa mkono kwa mara ya pili kisha akaongeza, “Nimeagizwa nije kukuchukua unahitajika sehemu maana kuna mambo fulani ya kufanya huko.”

Niliinuka nikamuaga Salma na kufuatana na Luteni Lister. Naam! Sasa nilikuwa nimeingia rasmi kwenye kitengo cha ujasusi na nilikuwa bega kwa bega na mwanausalama.

* * *

Inaendelea...
 
ufukweni mombasa.JPG

212

Idara…




Saa 8:30 usiku…

TANGU nilipoachana na Luteni Lister usiku wa saa tatu na nusu baada ya kunifikisha pale kwenye makazi yangu ya muda sikuweza kabisa kupata usingizi! Usiku kucha nilikuwa nahangaika kitandani kwangu kujaribu kuutafuta usingizi bila mafanikio. Usiku wote mawazo juu ya mafunzo maalumu ya ujasusi yalikuwa yananijia kichwani. Nilijaribu kujenga picha kichwani kwangu kuhusu mazingira ya chuo nilichokuwa nakwenda kusoma na namna ambavyo mafunzo hayo yangefanyika.

Kumbukumbu juu ya maongezi yangu na Brigedia Jenerali Godwin Longinus ilikuwa bado inazunguka kichwani kwangu na maneno yote ya mkurugenzi huyo wa uajiri utafiti na mafunzo yalikuwa yanajirudia kichwani kwangu na kunifanya muda wote nisisimkwe mwili wangu. Maneno yake yalizunguka akilini kwangu kwa kasi ya ajabu sana na kunifanya nishindwe hata kupata usingizi.

Hadi wakati huo sikujua kama nilitakiwa kufurahia fursa ile ya kujiunga na mafunzo maalumu ya kijasusi au pengine nilipaswa kuogopa. Katika umri wangu wa miaka therathini niliyoishi hapakuwa na hata siku moja niliwazia kuwa ningekuja kupewa habari za aina ile… Hata siku moja!

Kabla sijapanda kitandani niliutumia muda wangu kukisoma kile kitabu nilichokuwa nimepewa na Brigedia Jenerali Godwin Longinus na kugundua kuwa zilikuwa nyaraka maalumu kuihusu Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) iliyoanza na changamoto za kila namna chini ya mkurugenzi wa kwanza, Emilio Mzena.

Sikujua kwa nini Brigedia Jenerali Godwin Longinus alinipatia kile kitabu ila hisia zangu ziliniambiwa kuwa alitaka niifahamu vyema Idara hiyo ya Usalama wa Taifa kwa kuwa tayari nilikwisha ingizwa kwenye System.

Wakati nikiendelea kukisoma kile kitabu nilifahamu kuwa baadhi ya changamoto zilizosemwa kuibuka wakati wa uongozi wa mkurugenzi Emilio Mzena zilitokana na uchanga wa taifa, wakati huo, kisiasa na kiuchumi.

Ikumbukwe kuwa Tanzania (wakati huo ikiitwa Tanganyika) ilikuwa imeshuhudia unyonyaji, ukandamizaji na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu uliokuwepo wakati wa utawala wa kikoloni, na kwa sababu hiyo, tulipopata uhuru nchi ililazimika kujipanga upya kwa kujenga misingi imara ya siasa, uchumi na utamaduni wake.

Changamoto nyingine ilikuwa vita baridi iliyokuwa ikiendelea kati ya mataifa ya Magharibi (NATO) na yale ya Mashariki (WARSAW). Katika kipindi hicho mataifa ya Mashariki (Urusi, China, Korea, Poland, Ujerumani Mashariki n.k.) yalikuwa yakifuata siasa na uchumi wa Kikomunisti/ Kisoshalisti unaotia msukumo kwa serikali (umma) kumiliki njia kuu za uchumi na kuzitumia kwa manufaa ya wote.

Siasa hizo zilipingwa vikali na mataifa ya Magharibi (Marekani, Uingereza, Ujerumani Magharibi n.k.) yaliyokuwa yakifuata siasa za kibepari (Capitalism / Market economy) zinazotia msukumo kwa sekta binafsi yaani mtu mmoja mmoja kumiliki njia kuu za uchumi.

Sasa ili kupanua dola zao kiuchumi na kiulinzi, kutafuta kuungwa mkono, na kusambaza siasa zake ulimwenguni, mataifa ya Mashariki yalijenga urafiki na kuzisaidia nchi changa (zilizopata uhuru wake karibuni), vyama vikubwa vya siasa vyenye mwelekeo wa kuchukua dola, na vikundi vya wapigania uhuru katika nchi za Afrika, Asia, na Mashariki ya Kati. Mkakati huo ulisaidia siasa za Kisoshalisti kusambaa duniani kwa kasi kama moto wa gesi.

Ili kukabiliana na hali hiyo, mataifa ya Magharibi chini ya usimamizi wa Marekani yalianzisha mpango maalumu wa kuzuia kuenea kwa ukomunisti duniani. Mpango huo uliojulikana kama Sera ya Udhibiti (Policy of Containment) ulilenga kuudumaza ukomunisti kwa kuhakikisha hauvuki mipaka au kusambaa katika nchi mpya; bali unabaki ndani ya nchi ambazo tayari zimeshaupokea.

Katika kufanikisha sera hiyo, Marekani ilitumia taasisi yake ya ujasusi (CIA) kuhujumu uchumi wa nchi changa zilizoukaribisha ukomunisti, kuwaondoa madarakani viongozi wenye msimamo wa kikomunisti na kisha kuweka vibaraka wao. CIA pia ilitumia vibaraka wake na kusambaza propaganda kwa wananchi kuchochea wachukie na kupinga sera za kikomunisti.

Kwa hiyo, Tanzania ilijikuta ikiwa mwathirika (victim) wa vita baridi mara tu baada ya kutangaza kufuata mfumo wa siasa ya ujamaa na kujitegemea, chini ya mwongozo wa Azimio la Arusha lililoanzishwa mwaka 1967. Mataifa makubwa ya Marekani, Uingereza na Ujerumani Magharibi yalianzisha mikakati mbalimbali ya siri iliyokuwa na lengo la kuiyumbisha Tanzania kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni, ili iweze kusalimu amri na kutupilia mbali siasa ya ujamaa na kujitegemea.

Kufuatia hali hiyo mwaka 1975 ulifanywa uteuzi wa mkurugenzi mpya wa Idara ya Usalama wa Taifa na nafasi kuchukuliwa na Dk. Lawrence Gama, huku malengo ya idara hiyo chini ya uongozi wake yakijikita zaidi katika kupiga vita mfumo wa siasa na uchumi wa kibepari ambao kwa nchi yetu ulifahamika kama unyonyaji, kuzuia hujuma na uzandiki uliochochewa na vita baridi, na kuweka mikakati ya kufuta ujinga ili kuimarisha umoja.

Pia Idara ya Usalama wa Taifa ilishiriki vyema katika kusaidia vita vya ukombozi wa Kusini mwa Afrika. Kwa kutumia maofisa na vyanzo vyake muhimu Idara ilihusika moja kwa moja katika kupanga mikakati ya vita, kukusanya habari za kiusalama dhidi ya adui na kutoa mafunzo ya kijeshi kwa wapiganaji wa nchi za Afrika ya Kusini, Msumbiji, Zimbabwe na Namibia.

Mwaka 1978 hali ilikuwa tete zaidi baada ya majeshi ya nduli Iddi Amin Dada wa Uganda kuvamia upande wa Kaskazini wa Mto Kagera na kuikalia ardhi yetu kimabavu. Uvamizi huo ulisababisha Tanzania iingie kwenye vita kali ili kuyaondoa majeshi hayo katika ardhi ya Tanzania na kuwakomboa Waganda kutoka utawala wa Iddi Amin Dada, aliyekuwa amejipa urais wa maisha.

Japo vita hiyo ilidumu kwa muda wa mwaka mmoja tu lakini madhara yake kisiasa na kiuchumi yaliendelea kuitesa nchi ya Tanzania kwa zaidi ya miaka therathini. Uchumi wetu uliyumba na kufanya hali ya maisha ya Watanzania kuwa ngumu mno.

Ni katika kipindi hicho Idara ya Usalama wa Taifa, chini ya uongozi wa Dk. Hassy Kitine aliyeteuliwa mwaka 1978, ililazimika kuendelea na mikakati yake ya kuwasaidia wapigania uhuru wa nchi za Zimbabwe, Namibia na Afrika ya Kusini kwa kutoa mafunzo, na kushiriki katika operesheni mbalimbali.

Kisha kati ya mwaka 1980 hadi 1983 Idara ya Usalama wa Taifa chini ya uongozi wa Dk. Augustine Mahiga ililazimika kuelekeza nguvu kubwa zaidi katika kulinda uchumi, kwa kupambana na uhujumu uchumi. Hali hiyo ilisababishwa na uhaba mkubwa wa bidhaa muhimu uliojitokeza baada ya vita vya kuikomboa Uganda.

Wakati huo wafanyabiashara wakubwa na baadhi ya watu wenye mamlaka walikuwa wameanzisha utaratibu haramu wa kununua bidhaa kwa wingi na kuzificha katika maghala ili kusababisha mfumuko wa mahitaji. Baada ya kusababisha taharuki ndipo walipozitoa na kuziuza kwa siri na kwa bei ya juu kuliko kawaida. Hali hii ilisababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi na kuzidi kuyumbisha uchumi wa taifa uliokuwa ukichechemea.

Katika kipindi hicho Idara ya Usalama wa Taifa ilifanya kazi kubwa ya kudhibiti vuguvugu la mapinduzi ya kijeshi yaliyokuwa yameshamiri katika nchi nyingi za Kiafrika, na kujipenyeza hadi Tanzania. Vuguvugu hilo kwa kiasi kikubwa lilichochewa na hali ngumu ya maisha iliyofanya wengi wasiyaone matunda ya uhuru.

Ilikuwa katika miaka ya 1982 na 83 wakati Idara ya Usalama wa Taifa ilipofanikiwa kuzima jaribio la mapinduzi ya kijeshi lililopangwa na maofisa wachache wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiongozwa na Thomas Lugangila (Uncle Tom). Wengine walikuwa Kapteni Zacharia Hanspope, Kapteni Kadego, Kapteni Hatibu Ghandi (Hatty McGee), Kapteni Eugene Maganga, Luteni Vitalis Mapunda, Luteni Pius Lugangila na Luteni Kajaji Badru, huku ofisa mwingine wa JWTZ, Komando Tamimu akiuawa kwa kupigwa risasi na Ofisa Usalama wa Taifa, Radi Simba, wakati wa jaribio la kumkamata lililofanyika maeneo ya Kinondoni Mkwajuni, Jijini Dar es Salaam.

Inaendelea...
 
ufukweni mombasa.JPG

213

Maofisa hao wa JWTZ walikamatwa na kufunguliwa kesi ya uhaini iliyosikilizwa mwaka 1985.

Kama hiyo haitoshi, mnamo Aprili 12, 1984, Idara ya Usalama wa Taifa ilipata pigo kubwa baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine kufariki dunia katika ajari ya gari iliyotokea eneo la Wami - Dakawa, nje kidogo ya Mji wa Morogoro baada ya gari aina ya Land Cruiser lililokuwa linaendeshwa na Dumisan Dube, mkimbizi wa kutoka Afrika ya Kusini aliyekuwa akiishi kwenye kambi ya wakimbizi ya Mazimbu kugongana uso kwa uso na gari la Waziri Mkuu.

Msafara wa Waziri Mkuu uliokuwa ukilindwa na maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa ulipata ajali hiyo ukitokea Dodoma alikokuwa amekwenda kuhudhuria kikao cha Bunge. Kifo hicho kilizua mtafaruku mkubwa miongoni mwa wananchi na hasusan wanasiasa ambao waliituhumu Idara ya Usalama wa Taifa kwa kutumiwa na baadhi ya wanasiasa kupanga mauaji hayo, kwa lengo la kuteka nafasi ya urais iliyoonekana kumwangukia Edward Sokoine.

Wapo pia waliowatuhumu baadhi viongozi wa juu hususan waliokuwa mawaziri wakuu wastaafu kuwa walitumia nguvu za giza kumuua kiongozi huyo. Lakini pia wapo waliovumisha kuwa mauaji hayo yalipangwa na kiongozi mkuu mwenyewe baada ya kuona Edward Sokoine angeipeleka nchi pabaya.

Hata hivyo, kadri muda ulivyokwenda tuhuma hizo zilipuuzwa na kuthibitika kuwa zilikuwa uzushi usiokuwa na ushahidi, huku Idara ya Usalama wa Taifa ikifanya kazi kubwa ya kujisafisha na kuzuia kifo hicho kisisababishe machafuko nchini.

Katika miaka ya 1983 hadi 1995, Idara ya Usalama wa Taifa ilifanya kazi chini ya Meja Jenerali Imran Kombe na kupata mafanikio makubwa kutokana na ushirikiano kutoka kwa wananchi.

Idara iliwatumia vyema vijana waliopitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria, na wazee waliopitia mafunzo ya mgambo katika kukusanya na kutoa taarifa kwa hiari (informers), na wakati mwingine bila wao kujua. Kimsingi mawazo, misingi na itikadi za ujamaa na kujitegemea vilikuwa vikiwasukuma Watanzania wengi kujivunia utaifa wao, na kuonesha uzalendo kwa kujitolea kulitumikia taifa kwa hali na mali.

Hali ilianza kubadilika baada ya Mzee Ali Hassan Mwinyi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwani alifanya kazi kubwa ya kubadilisha mfumo wa siasa na uchumi kutoka ujamaa asilia na kwenda kwenye mfumo wa biashara huria, kupitia Azimio la Zanzibar (ruksa).

Sasa Tanzania ikafungua mipaka yake, wafanyabiashara wakaruhusiwa kuingiza bidhaa za nje nchini na kuuza bidhaa za Tanzania katika masoko ya kimataifa chini ya usimamizi wa Board of External Trade (BET). Uamuzi huu ulisaidia sana kupunguza ugumu wa maisha ya Watanzania uliotokana na kukosekana kwa bidhaa muhimu.

Mwaka 1989 Idara ya Usalama wa Taifa ikakumbwa na jinamizi lingine baada ya magaidi wa The Mozambican National Resistance (MNR) wa Msumbiji kuvamia maeneo ya Kusini mwa Tanzania. Magaidi hao ambao pia hujulikana kwa jina la RENAMO (Resistência Nacional Moçambicana) au BANDITO walianza kukipinga chama tawala cha Msumbiji, FRELIMO, miaka ya 1970 kabla hata nchi hiyo haijapata uhuru.

Magaidi hao walipata nguvu zaidi mwaka 1975 baada ya kuungwa mkono na idara ya ujasusi ya makaburu wa Rhodesia (sasa Zimbabwe) iliyojulikana kwa jina la Rhodesian Central Intelligence Organization (CIO) ambayo ilikuwa na lengo la kutokomeza ukomunisti Afrika. Rhodesian Central Intelligence Organization ilifanya kazi zake kwa maelekezo na kwa kushirikiana na Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) lililokuwa likitekeleza sera za kudhibiti kuenea kwa ukomunisti.

Hivyo, uvamizi wa RENAMO ndani ya ardhi ya Tanzania hakikuwa kitu kilichotarajiwa. Kwa muda mrefu magaidi hawa walikuwa wakipigana na majeshi ya FRELIMO ndani ya nchi ya Msumbiji bila kusababisha madhara kwa Watanzania. Mambo yaligeuka baada ya magaidi hao kupokea kipigo kikubwa kutoka kwa majeshi ya Serikali ya Msumbiji, na kukosa sehemu ya kukimbilia ndani ya nchi yao.

Ndipo walipovuka mpaka na kuingia Tanzania wakiwa na uhakika kuwa majeshi ya Msumbiji hayawezi kufanya vita ndani ya nchi nyingine. Wakiwa ndani ya ardhi ya Tanzania, magaidi wa RENAMO walijikuta wakiishiwa chakula, dawa, sigara, na vitu vingine muhimu walivyokuwa wakihitaji kuweza kuishi, ndipo walipoamua kuvamia vijiji vya mipakani na kupora chakula, dawa hospitalini, mavazi ya kiraia, na kisha kubaka wanawake kabla ya kurudi msituni kujificha.

Hali hii ilisababisha taharuki kwa wananchi wa maeneo hayo. Wengi wao waliamua kukimbia makazi yao na wengine kukubali kuishi na baadhi ya magaidi hao waliojivika kofia ya ufanyabiashara au uvuvi.

Ili kudhibiti hali hiyo Idara ya Usalama wa Taifa ilifanya kazi kubwa na kwa ushirikiano wa karibu na Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika operesheni iliyofanywa sambamba na nyingine (Operesheni Uhai) ikihusisha makomando wa Idara ya Usalama wa Taifa na makomando wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania toka 92KJ Ngerengere.

Baada ya kazi ngumu iliyodumu kwa zaidi ya miezi tisa makomando hao walifanikiwa kuwatokomeza kabisa magaidi wa RENAMO na kurejesha amani katika Mikoa ya Kusini mwa Tanzania.

Baadaye Idara ya Usalama wa Taifa ilijikuta ikiwa katika ‘sintofahamu’ baada ya kufumuka kwa mageuzi makubwa ya kisiasa na kiuchumi duniani. Mageuzi haya yaliyochochewa na ‘perestroika’ yalisababisha kuvunjwa kwa ukuta wa Berlin (mwaka 1989), kusambaratika kwa dola ya Urusi (United Soviet Socialist Republic – USSR) mwaka 1991, na kumalizika kwa vita baridi kati ya Ulaya Magharibi na Ulaya Mashariki.

Pamoja na kutotajwa sana katika historia ya Tanzania, mageuzi haya kiuhalisia ndiyo yaliyochangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya jumla ya mfumo wa siasa na uchumi wa Tanzania, ikiwa pamoja na mfumo, muundo na utendaji wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Miaka mingi kabla ya mageuzi, Idara ya Usalama wa Taifa ilikuwa inafanya kazi katika mlengo wa kijamaa, kwa kufuata mfumo wa siasa wa chama kimoja, chini ya mwamvuli wa Ofisi ya Rais. Baada ya mageuzi Idara ya Usalama wa Taifa ilijikuta ikilazimika kubadilisha mfumo na malengo yake ili kwenda sambamba na mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi, na kutengeneza muundo wa kuiwezesha kufanya kazi zake kwa kujitegemea.

Miezi michache baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini, Idara ya Usalama wa Taifa ilipeleka mapendekezo ya marekebisho ya mfumo na muundo wa Idara kwa Rais Ali Hassan Mwinyi. Hata hivyo mapendekezo hayo yalikataliwa.

Mwaka 1995 Rais Benjamin Mkapa alimteua Cornel Apson Mwang’onda kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa badala ya Meja Jenerali Imran Kombe aliyestaafu. Cornel Apson Mwang’onda alitumia nafasi ya ukaribu wake na Rais Mkapa kupendekeza kwa mara ya pili mabadiliko ya mfumo na muundo wa Idara ya Usalama wa Taifa. Rais Mkapa aliridhia mapendekezo hayo na kuagiza uandaliwe muswada ili uweze kupelekwa bungeni.

Miezi michache baadaye muswada wa Sheria ya Usalama wa Taifa (Tanzania Intelligence and Security Service Act No. 15 of 1996) ulipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusainiwa na Rais Benjamin Mkapa mnamo Januari 20, 1997.

Kupitishwa kwa sheria hiyo ndiko kunatajwa kuwa mojawapo ya mafanikio makubwa ya Cornel Apson Mwang’onda, ambaye wakati wa uongozi wake Idara ya Usalama wa Taifa ilikumbwa na misukosuko mingi, ikiwa pamoja na kulipuliwa kwa ubalozi wa Marekani.

Kuanzia Agosti 20, 2006 hadi Agosti 19, 2016, Idara ya Usalama wa Taifa ilikuwa chini ya Othman Rashid (OR) kama mkurugenzi wake mkuu baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuchukua nafasi iliyoachwa na Cornel Apson Mwang’onda. Kabla ya uteuzi huo Othman Rashid alikuwa Mkuu wa Utawala na Utumishi wa Idara hiyo ya Usalama wa Taifa (Director of Administration and Personnel – DAP) baada ya kufanya kazi nzuri iliyomwezesha kuteuliwa kushika nafasi hiyo.

Katika kipindi hiki yalianza kujitokeza malalamiko kutoka kwa wabunge kuwa Idara ilishindwa kuzuia uhujumu uchumi na badala yake ikaanza kujikita kwenye siasa za kukipendelea chama tawala.

Ni kipindi hiki kulijitokeza matukio kadhaa ya ufisadi wa kutisha ikiwemo wizi wa zaidi ya Shilingi bilioni 133 katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ununuzi wa rada ya kijeshi na ufisadi uliodaiwa kufanywa katika kampuni za Meremeta, Tangold na Deep Green Finance. Na bila kusahau ufisadi wa Tegeta Escrow.

Pia nchi ilishuhudia kushamiri kwa biashara ya dawa za kulevya, ujangili, rushwa na hata uvujaji wa siri za serikali. Mwaka 2013 Othman Rashid alikuwa astaafu kwa mujibu wa sheria lakini aliongezewa mkataba wa mwaka mmoja na kisha nafasi yake ikakaimiwa na Mkurugenzi wa Operesheni za Ndani wa Usalama wa Taifa (Director Of Internal operations - DOI), George Madafa.

Kati ya Novemba 24, 2016 hadi Septemba 2019 Idara ya Usalama wa Taifa iliongozwa na Dk. Modestus Kipilimba, mtaalamu wa masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano aliyeteuliwa na Rais John Pombe Magufuli kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Othman Rashid.

Katika kipindi chake Idara ya Usalama wa Taifa iliendelea kushutumiwa na vyama vya upinzani kuwa ilikuwa ikikipendelea chama tawala, na kwa mara ya kwanza, liliibuka lindi la uhalifu wa kutisha uliofanywa na kundi la watu waliopewa jina la “wasiojulikana” ambapo watu kadhaa walipotea katika mazingira ya kutatanisha huku maiti zikiokotwa kwenye viroba kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi.

Pia ziliibuka tuhuma kuhusu mfumo wa ajira kwamba zilitolewa kwa upendeleo kwa ndugu na jamaa wa vigogo na kusababisha kuathiri sana ufanisi wa kazi huku baadhi ya maofisa usalama “wakijiumbua” kwa makusudi kwa kutaka sifa ili waogopwe mtaani. Na hapa ndiyo ile kauli ya “Unanijua mimi nani?” ilipokuwa maarufu mtaani.

Ni katika kipindi hiki pia nchi ilishuhudia kushamiri kwa matukio ya mauaji ambayo wengine waliyahusisha na ugaidi huko Mkuranga, Kibiti na Rufiji katika Mkoa wa Pwani, ambapo watu 40 wakiwemo askari polisi 15 waliripotiwa kuuawa kwenye kadhia hiyo.

Hata hivyo Idara ilifanya kazi kubwa sana na kubaini kuwa waliokuwa wakifanya mauaji hayo walikuwa wameingia kwenye maeneo hayo miaka nane kabla ya kuanza mauaji hayo, wakijipenyeza kwa njia ya kuendesha mafunzo ya dini kumbe walikuwa na mambo tofauti; wakifundisha karate, judo na namna ya kutumia silaha.

Kwa kushirikia na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kama Polisi na JWTZ, Idara ya Usalama wa Taifa ilipata mafanikio makubwa baada ya operesheni iliyofanywa maeneo husika kufanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa kadhaa wa mauaji hayo na wengine kukimbilia nchi jirani ya Msumbiji.

Halafu, Septemba 12, 2019 kulitokea mabadiliko ya uteuzi wa mkurugenzi mpya wa Idara ya Usalama wa Taifa na nafasi kuchukuliwa na Diwani Athuman Msuya. Ni katika kipindi hiki Idara ya Usalama wa Taifa ilipata pigo jingine kubwa kitaifa baada ya kifo cha Rais John Magufuli aliyekufa akiwa madarakani mnamo Machi 17, 2021 katika hospitali ya Mzena. Kifo cha Rais Magufuli kilisababisha Idara ya Usalama wa Taifa kulaumiwa kwamba ilikuwa inaficha taarifa za afya ya Rais…

Dah! Nilijikuta kichwa changu kikianza kuwa Kizito, mambo yalikuwa mengi sana na ndiyo kwanza nilikuwa nimesoma utangulizi tu wa Idara. Bado kulikuwa na mambo mengi mno ya kusisimua na hata kuogofya kuhusu mazingira ya ufanyaji kazi kwa wausalama na mengineyo.

Kufika hapo nilijikuta nikishindwa kuendelea kusoma kwani nilihisi akili yangu ikishindwa kufanya kazi sawa sawa, nikaamua kuachana kwanza na kitabu hicho na sasa mawazo yangu yakahamia kwenye mambo mengine huku hisia fulani zikinijia, hisia zilizonifanya kuanza kujenga picha fulani kichwani kwangu, picha ambayo nisingeweza kuielezea vizuri kutokana na mshawasha niliokuwa nao…

Hata hivyo, nilikuwa na matumaini makubwa juu ya kile kilichokuwa kikinisubiri mbele ya safari.

* * *

Inaendelea...
 
ufukweni mombasa.JPG

214

Bro, Kazi unayo!




Saa 3:15 asubuhi…

IKAWA asubuhi ikawa jioni… siku zilipita na hatimaye wiki moja ilifika na sasa nilikuwa ndani ya gari la Idara ya Usalama wa Taifa aina ya Nissan Patrol lililokuwa likiendeshwa na Luteni Lister nikiitazama mitaa ya Jiji la Dar es Salaam huku kichwani nikijiambia kuwa siku nyingine, baada ya kurudi toka mafunzoni, ningeipita tena mitaa ile nikiwa mtu tofauti kabisa. Ofisa Usalama wa Taifa mwenye mbinu maalumu (Specialized Skills Officer).

Ndani ya lile gari lililoendeshwa na Luteni Lister pia alikuwemo mwanadada mrembo Pamela Mkosamali, Ofisa Usalama mwenye mbinu maalumu, alikuwa ameketi kiti cha nyuma akiwa mtulivu sana. Pamela alikuwa na umri wa miaka 27, alikuwa mrefu wa wastani, mweupe kwa rangi na mwenye umbo lililovutia mno.

Asubuhi ile alikuwa amevaa gauni zuri la pundamilia la mikono mirefu lililoshonwa kwa mtindo wa ‘Ankara midi tube’ likiishia juu kidogo ya magoti yake, lilikuwa limeushika vyema mwili wake wenye umbo zuri. Miguuni alivaa viatu vyeusi vyenye vikanyagio virefu vya mchuchumio.

Nilifahamiana na Pamela miaka kadhaa nyuma kwa kuwa sote tulikuwa tumesoma katika chuo kimoja cha Pretoria Technikon nchini Afrika Kusini, ingawa nilikuwa nimemtangulia miaka miwili. Yeye alikuwa anachukua Shahada ya Sayansi ya Jamii (B.A in Social Science).

Pamela alikuwa amepata nafasi ya kusoma pale Pretoria Technikon kwa kuwa baba yake, Balozi Damian Mkosamali, wakati huo alikuwa Mwambata wa Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini kabla ya baadaye kuwa Balozi wa Nigeria na India. Pamela alikuwa mtoto wa tatu na wa mwisho wa Damian Mkosamali.

Hata hivyo, katika miaka yote niliyomfahamu Pamela sikuwahi kutambua kuwa alikuwa Ofisa Usalama wa Kificho (Covert Operative), mmoja wa waliokuwa wamepenyezwa katika sekta mbalimbali na kwamba alishawahi kushiriki kwenye operesheni kadhaa tata.

Katika siku tatu tulizokutana hapo Dar es Salaam wakati akinisaidia kukamilisha baadhi ya mambo kabla ya safari yangu, niligundua kuwa yeye alikuwa amejiunga na Idara ya Usalama wa Taifa akiwa na umri wa miaka 23 tu, mara tu alipohitimu Shahada ya Sayansi ya Jamii nchini Afrika Kusini na kisha kujiunga na programu maalumu ya kijasusi nchini Ufaransa kwa kupata mafunzo maalumu ya mapigano ya ana kwa ana ya kiwango cha juu zaidi, kutumia karibia aina zote za silaha na milipuko ya jeshi, ufuatiliaji adui, kukabiliana na hali ngumu kwenye mazingira ya kawaida na nyikani, na kumkwepa, kumzuia na kumtoroka adui.

Pamela alikuwa mzuri sana kwenye karate na judo, na kwa ujumla alikuwa mwanadada jasiri na hofu kwake ilikuwa mbali na moyo wake. Yeye na Luteni Lister ndio waliokuwa wamepewa jukumu la kuhakikisha nasafiri pasipo usumbufu wowote.

Nikiwa ndani ya lile gari hisia zangu ziliniambia kuwa katika safari yangu kuelekea nchini Misri nilikuwa naelekea kukabiliana na jambo kubwa sana maishani kwangu ambalo sikuwahi kuliota, na kwamba kila hatua niliyopiga nilikuwa naingia kwenye mlolongo wa matukio ya hatari ambayo yangenifanya kukikaribia kifo changu mwenyewe.

Hali hiyo ilianza kuniogopesha mno kiasi kwamba nilianza kuzikumbuka ndoto zangu za utotoni, nilikuwa na ndoto ya kuja kuwa mwanasayansi mkubwa duniani na si kazi ya ujasusi. Nilipenda sana kuwa mwanasayansi na niliyamudu vilivyo masomo ya sayansi kiasi kwamba wengi walifikiri huenda ningekuja kuwa daktari bingwa wa tiba ya binadamu.

Lakini dunia ikanichagulia kazi ya kuwa mtaalamu wa teknolojia ya habari na mawasiliano. Sasa, baada ya miaka mingi hatimaye nikajikuta nikitakiwa kuwa jasusi, kazi ambayo licha ya kupenda kusoma hadithi za kijasusi na kufuatilia filamu za kijasusi sikuwahi kuifikiria kabisa.

Hii haikuwa ndoto yangu, hadithi za kijasusi nilizokuwa nikizisoma na mambo ya kijasusi niliyokuwa nikiyaona kwenye filamu za kijasusi vilinifanya nione kuwa kazi ya ujasusi ilikuwa ni kazi ya roho mkononi, na hivyo nikaanza kutafakari mara mbili mbili kuhusu uamuzi wangu wa kukubali kwenda kwenye mafunzo ya kijasusi nchini Misri. Hata hivyo haikuwa hiyari yangu kukubali au kukataa. Sikuwa na namna nyingine ya kulikwepa jukumu hili.

Ni ukweli usiofichika wala kupingika kuwa watu wengi sana wanapenda kazi ya ushushushu. Hii si kwa Tanzania tu bali sehemu nyingi duniani. Ukiingia mtandaoni utakuta watu wengi wanaizungumzia taaluma ya ujasusi au hata kutamani sana waifahamu taaluma hii nyeti. Si hivyo tu wapo wengine wamefikia hatua ya kujitangazia mtaani kuwa wao ni maofisa usalama wa taifa ingawa ukweli hawafanyi kazi hii.

Niliwafahamu watu wengi waliokuwa wakiililia kazi ya ushushushu lakini hawakuwa na vigezo au kubahatika kuwa na taaluma hii… ila mimi ambaye sikuwa na mzuka na kazi hii ndiyo nimejikuta nikiaminiwa na kuingizwa kwenye taaluma hii jambo ambalo lilinifanya niingiwe na mzuka kabla hata sijafuzu mafunzo yenyewe ya ujasusi. Nilijikuta nikianza kuuweka uoga pembeni na kuazimia kufuzu mafunzo hayo na baadaye kuifanya kazi husika kwa weledi wa hali ya juu na jitihada za aina zote.

Nilitambua kuwa sikuwa peke yangu katika programu hiyo ya mafunzo ya kijasusi, tulikuwa vijana watano. Wawili walikuwa wanakwenda nchini Afrika Kusini, mmoja alikuwa anapelekwa China na mwingine Ufaransa.

Nikiwa bado nimezama kwenye tafakuri ile nikajikuta namkumbuka mke wangu Rehema na mtoto wetu Jason Sizya Junior. Sikuwa na shaka kuwa sasa Rehema alikuwa anafahamu ukweli kuwa nilikuwa safarini kwenda nchini Misri kwenye mafunzo ya kijasusi ingawa sikuwa na uhakika kama alilifahamu jambo hilo kabla sijaondoka Kahama.

Licha ya majukumu yake kama ofisa kificho wa usalama wa taifa, bado Rehema alibaki kuwa mwanamke mzuri sana mwenye sifa zote za kuwa mke. Alikuwa mwanamke jasiri na makini mno, mwenye uwezo mkubwa wa kuyasoma mawazo ya mtu na aliyajua mambo mengi ila alipenda kubaki kimya na siri yake moyoni kiasi cha kunifanya wakati fulani nitahayari kama mtoto aliyekutwa akiopoa nyama jikoni baada ya kugundua kuwa aliyajua mambo yangu ambayo sikutaka ayajue.

Siku zote nilijiuliza na sikuwa na majibu lakini sasa nilitambua kuwa uwezo huo haukuwa kipaji pekee bali pia ulitokana na mafunzo maalumu ya kijasusi aliyopitia.

Kisha mawazo yangu yalihamia kwa Zainabu, msichana mkimya, mpole na mwenye upendo lakini asiyetabirika. Nilijua kuwa yeye pia alishaambiwa kuwa nilikuwa na safari ya kwenda nje ya nchi kimasomo, kusomea masuala ya upigaji picha (photo journalism). Yeye hakutakiwa kuujua ukweli kuwa nilikuwa nakwenda kuchukua mafunzo ya kijasusi, japo alitarajiwa kuwa mama wa mtoto wangu.

Mawazo yangu yaliporudi tena mle ndani ya gari nikashtuka kuwa tayari tulikuwa tumefika katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA). Mara baada ya kuvuka geti la kuingilia kiwanjani pale Luteni Lister aliendesha gari taratibu huku akiyatembeza macho yake huku na kule akitafuta sehemu nzuri ya maegesho na baada ya muda mfupi hatimaye akawa amepata sehemu nzuri ya maegesho na kusimama.

Nilikuwa bado nina muda kwa mujibu wa ratiba iliyokuwa kwenye tiketi ile ya ndege niliyopewa na Brigedia Jenerali Godwin Longinus. Tulikuwa tumefika pale Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere mnamo saa nne kasoro dakika chache, ikiwa ni zaidi ya saa moja kabla ndege yetu aina ya Airbus A340-600 ya shirika la ndege la Misri, EgyptAir, niliyotarajia kusafiria nayo haijaruka mnamo saa tano kamili asubuhi ile.

Baada ya gari kuegeshwa na kisha injini kuzimwa nilifyatua kabari ya mkanda wa kiti changu kisha nikashuka na kuchukua mabegi yangu ya safari kutoka kwenye kiti cha nyuma. Luteni Lister na Pamela pia walishuka, Pamela akanisaidia begi moja kisha wakanisindikiza hadi ndani ya jengo la kituo nambari tatu cha kiwanja cha ndege, jengo maarufu kama ‘Terminal 3’ lililokuwa na uwezo wa kuruhusu ndege kubwa 24 kwa wakati mmoja na abiria milioni 6 kwa mwaka.

Jengo lile la kituo nambari tatu lilikuwa kubwa na refu zaidi kuliko yale majengo mengine ya Terminal 1 na Terminal 2, na lilikuwa lina migahawa na maduka ya kisasa, na ofisi mbalimbali za utawala zikiwemo ofisi za uhamiaji kwa ajili ya wageni waliokuwa wakifika nchini kupitia kile kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere.

Tulipoingia ndani ya lile jengo la Terminal 3 nilianza mchakato wa kukamilisha taratibu zote za uhamiaji pale kiwanjani kabla ya kuondoka. Niliwaacha Luteni Lister na Pamela wakilinda mizigo yangu, nikapanga foleni kwenye dirisha la ofisi ya uhamiaji pale kiwanjani kisha nikapenyeza vibali vyangu vyote vya kusafiria kwenye dirisha dogo la kioo la chumba kilichomhifadhi msichana mmoja mlimbwende aliyekuwa na sura ya uchangamfu.

Msichana yule, ofisa uhamiaji, alivipokea vibali vyangu vya kusafiria huku akiliachia tabasamu lake maridhawa na kulifanya lizisumbue fikra zangu. Ama kweli jasiri haachi asili, nilijikuta nikisuuzika moyoni kwani bado nilikuwa mgonjwa kwa walimbwende kama huyu.

Mambo yote yalikuwa chap chap kwani yule ofisa uhamiaji alimaliza haraka kuingiza taarifa zangu kwenye tarakilishi yake kisha akagonga mhuri kwenye hati yangu ya kusafiria na hivyo safari yangu kuelekea Misri ikawa imeidhinishwa rasmi. Bila kupoteza muda niliipokea ile pasi yangu ya kusafiria na kuitia mfukoni huku tabasamu langu la kichokozi likichomoza na kuzisumbua vibaya hisia za yule ofisa uhamiaji.

Kisha nilinyoosha mkono wangu kumpa, wakati tukipeana mkono wa kuagana na yule ofisa uhamiaji nikapitisha kidole changu cha shahada katikati ya kiganja chake kumtekenya, kitendo kile kikamfanya yule ofisa uhamiaji ashtuke na kuutoa haraka mkono wake kutoka kwenye kiganja changu. Sikuishia hapo, nikamkonyeza kidogo kumchombeza.

Wakati yule ofisa uhamiaji akiwa bado ana mshangao usoni kwake nikamnong’oneza kuwa siku nikirudi Jijini Dar es Salaam ningemtafuta, kisha nikanza kuzitupa hatua zangu kwa utulivu kuliacha eneo lile. Yule ofisa wa uhamiaji hakujibu bali alibaki ameduwaa huku macho yake yakinisindikiza nyuma yangu hadi pale nilipopotea mbele ya macho yake.

Kisha kwa kusaidiwa na Pamela tulichukua mizigo yangu na kwenda kupanga foleni kwa ajili ya ukaguzi wa mizigo. Baada ya hapo niliwashukuru akina Pamela na Luteni Lister na kuwataka wasipoteze muda wao kuendelea kusubiri kwani kila kitu kilishakuwa tayari na sasa nilikuwa naelekea kwenye ukumbi maalumu wa kusubiria tayari kwa safari yangu ya kuelekea Misri. Hivyo tukaagana.

Walinitakia safari njema yenye mafanikio katika mafunzo yangu. Nikawashukuru kwa msaada wao huku nikiliacha tabasamu langu lijivinjari usoni mwangu ingawaje moyoni nilihisi kuwa ni kama vile Pamela alikuwa ananiambia “Bro, kazi unayo!”

* * *

Endelea kuifuatilia simulizi hii ya kusisimua kujua nini kitajili huko nchini Misri...
 
Back
Top Bottom