Simulizi: Harakati za Jason Sizya

Simulizi: Harakati za Jason Sizya

narudi buzwagi.jpeg

79

Kabla sijajua nifanye nini mara nikasikia milio mingine kadhaa ya risasi ikirindima kama radi kuelekea kule tulikokuwa na hapo nikashuhudia kile kioo cha mbele cha gari letu kikitawanywa na kusambaa huku vipande vidogo vidogo mfano wa chenga chenga vikitumwagikia mwilini na kuendelea kuzua hali ya taharuki.

Kwa nukta chache nilihisi kama vile moyo wangu ulisahau mapigo yake, nilichoweza kusikia muda ule ilikuwa ni yowe dogo la hofu kutoka kwa yule dereva wa gari letu kisha nikamwona akiangukia kwa mbele kwenye usukani wa lile gari na kutulia kimya huku kifo kikiwa tayari kimemchukua. Waswahili wangeweza kusema kuwa “wala hakuomba maji”.

Muda ule ule abiria wenzangu ndani ya lile gari walianza kupiga mayowe ya hofu, hata hivyo ule haukuwa muda wa kushauriana kwani nilijua fika ni nini ambacho kingefuatia baada ya pale. Niliweza kushuhudia zile risasi zilizorindima zikiwa zimekifumua kichwa cha yule dereva wa gari letu na kutoboa bodi la lile gari.

Risasi nyingine zilikuwa zimeacha matundu mawili yakivuja damu katika sehemu ya kifua cha abiria mtu wa makamo aliyekuwa ameketi siti ya mbele upande wa kushoto kwa dereva na nyingine ilipita hadi kwa abiria mwingine aliyekuwa ameketi nyuma ya yule abiria wa mbele katika ile siti ya katikati.

Kwa kweli sikuwahi kuingia na hofu kubwa maishani mwangu kama hofu iliyonipata siku ile, hata hivyo, katikati ya hofu ile sikuona namna nyingine yoyote ya kujiokoa haraka katika mkasa ule, hivyo nilichokifanya ilikuwa ni kuvuta haraka kabali ya ule mlango wa nyuma ambako tulikuwa tumeketi.

Niliivuta ile kabali ya mlango na kuinyonga huku nikijaribu kuusukuma ule mlango kwa nguvu, lakini haukufunguka kwa kuwa ulikuwa umepinda kidogo na kubonyea kwa ndani kutokana na gari lile kugonga ule mti mkubwa, hivyo nikaamua kuufungua kwa teke moja la nguvu.

Ule mlango ulisalimu amri na kufunguka, lakini kabla sijashuka kutoka ndani ya lile gari nikajiwa na wazo la kumwokoa yule mrembo ambaye muda ule alionekana kama aliyekuwa amepigwa bumbuwazi na presha ilikuwa imepanda na hivyo kumfanya asijue la kufanya.

Sikuona sababu ya kujiokoa mwenyewe huku nikimwacha yule mrembo auawe kinyama katika mazingira ambayo nilidhani ninawajibika kufanya hivyo. Bila kuchelewa nikamshika mkono na kumsukumia nje ili ashuke, lakini alionekana kuendelea kushangaa.

Nilipotupa macho yangu kule barabarani muda ule nikawaona majambazi wawili kati ya wale watatu waliokuwa wameruka kutoka ndani ya lile Land Cruiser Pick-up wakikimbilia kuja kule tulikokuwa huku wakiwa wameshika vyema bunduki zao mikononi. Sikutaka kuendelea kushangaa, nikamnyanyua yule msichana mrembo kutoka kwenye siti yake kisha nikaruka naye nje ya lile gari na kutua chini kwa miguu yangu kama paka.

Kutokana na kiza kilichokuwa kimetanda katika eneo lile nilishindwa kuona vizuri sehemu niliyorukia na kujikuta nikitua kwenye bonde dogo na hivyo mguu wangu wa kushoto ukashtuka na hapo nikasikia maumivu makali sana kwenye kifundo cha mguu wangu wa kushoto yaliyopanda hadi juu ya goti.

Hata hivyo, sikujali yale maumivu makali ya mguu wangu niliyoyahisi, nilimbeba juu juu yule msichana mrembo na kujitahidi kuondoka haraka kutoka eneo lile huku nikikimbilia kichakani. Sikuweza kufika mbali kwani nilihisi kama mguu wangu ukipinda kidogo, kisha nikaanguka huku nikiwa bado nimembeba yule msichana mrembo. Hata hivyo, kwa namna ya ajabu nilijikuta nikimwinua juu yule mrembo huku nikijipinda na kulalia mgongo huku yule mrembo akiangukia juu ya kifua changu.

Kitendo kile cha kuanguka chini na yule mrembo kunilalia juu kikamzindua kutoka kwenye lile bumbuwazi, na hapo nikamwona akiangalia huku na kule kwa hofu kubwa na kutaka kupiga kelele. Niliwahi kumziba mdomo wake huku nikimsukuma haraka kumwondoa eneo lile.

“Kimbilia kichakani kabla hawajafika,” nilimnong’oneza sikioni yule mrembo huku nikimsukuma aondoke haraka eneo lile na kwenda kwenye kichaka kikubwa ambacho hakikuwa mbali kutoka pale chini tulipokuwa tumeangukia. Yule msichana alionekana kuganda juu yangu kama sanamu akiwa ameanza kuchanganyikiwa na hivyo kumfanya asijue lipi la kufanya na kwa wakati gani.

Muda ule abiria wengine walikuwa wametaharuki na kuanza kutimua mbio ovyo wakikimbilia barabarani huku wakipiga kelele ovyo kwa hofu. na hapo milio mingine kadhaa ya risasi ikavuma tena hewani, kufumba na kufumbua nikawaona watu watatu miongoni mwa wale abiria wakitupwa hewani na kupiga mayowe ya uchungu.

Wale watu walipoanguka chini walitulia kimya huku uhai ukiwa mbali na nafsi zao, kwani zile risasi zilizofyatuliwa zilikuwa zimepenya kwenye maeneo nyeti na kuacha matundu makubwa yaliyokuwa yanavuja damu.

Milio ile ya risasi ikamzindua tena yule msichana mrembo, nami nikazidi kumsisitiza kwa sauti yenye kusihi na kushawishi sana kuwa akimbilie kichakani kabla wale majambazi hawajafika pale na kutuona tukiwa katika hali ile. Maneno yangu yakamfanya anitazame kwa makini kama vile alikuwa amesikia habari mpya kabisa masikioni mwake.

Nikamsukuma kwa nguvu nikimtaka aondoke haraka eneo lile, safari hii aliinuka haraka pasipo upinzani wowote, nikamwona akitimua mbio huku akiwa ameinamisha mgongo wake kuelekea kwenye kichaka.

Nikiwa bado nimelala pale kwenye majani, nilimtazama yule msichana mrembo namna alivyokuwa akipotelea kwenye kile kichaka hadi alipotoweka kabisa machoni kwangu, nami nikaubana mguu wangu wa kushoto uliokuwa na maumivu makali na kuanza kutambaa kama nyoka, haraka nikapotelea gizani huku nikielekea kwenye kile kichaka.

Muda ule abiria wengine wanne waliobaki walisambaratika kwa hofu kila mmoja na njia yake wakikimbilia porini na hivyo kusalimisha roho zao. Nilifanikiwa kufika pale kwenye kichaka japo kwa taabu nikamkuta yule mrembo akiwa kajikunyata kwa hofu kubwa huku akilia kwa uchungu kilio cha kwikwi.

Sikuwa na shaka kabisa kuwa alikuwa amechanganyikiwa kutokana na hali ile ya taharuki aliyokuwa ameishuhudia na kuna wakati alitaka kupiga yowe la hofu lakini niliwahi kumziba mdomo wake baada ya kuhisi hatari ambayo ingetukabili pindi wale wauaji wangelisikia yowe lake.

Wale wauaji wawili waliisogelea ile gari yetu kwa tahadhari wakati yule jambazi wa tatu alikuwa amesimama kwa mbali kule barabarani akionekana kulinda eneo lile pamoja na kuwalinda wale wawili endapo hatari yoyote ingetokea.

Mara nikamwona mmoja kati ya wale wauaji wawili waliokuwa wamesimama kwenye lile gari akianza kusogea taratibu kuelekea pale kwenye kile kichaka tulipokuwa tumejificha mimi na yule msichana mrembo huku akielekeza mtutu wa bunduki yake pale kichakani.

Yule mrembo akaingiwa na kiwewe na kutaka kutoka ili akimbie lakini niliwahi kumdaka na kumzuia kwa mikono yangu yenye nguvu ili asikimbie, kisha nikamziba mdomo wake kwa nguvu ili asipige kelele. Ni wazi kabisa kuwa kwa muda ule alikuwa amechanganyikiwa na hakujua hatari ambayo ingempata endapo angejaribu kukimbia.

Wakati nikiwa nimemziba mdomo yule mrembo nikaamwona yule muuaji akizidi kusogea pale kwenye kichaka kwa kupitia uwazi wa matawi na majani katika kile kichaka, niliweza kumwona vizuri yule mtu wakati akitembea kwa tahadhari kusogea pale.

Kiza kilichokuwepo katika eneo lile hakikunizuia kumtambua yule muuaji kutokana na umbile lake na hata utembeaji wake, alikuwa ni yule jamaa aliyeshuka kwenye lile Land Cruiser Pick-up pale jirani na kituo cha kujazia mafuta cha Masumbwe na kuja kwenye gari letu kuulizia usafiri wa kwenda Kahama.

Nilimtazama kwa mshangao akiwa ameishika vyema bunduki yake huku misuli ya shingo na mikono yake ikiwa imetuna kwa ukomavu. Mwonekano wake ukanitanabaisha kuwa alikuwa ni mtu hatari sana na aliyependa matata.

Yule muuaji akaendelea kutembea kwa tahadhari akikikaribia kile kichaka na wakati huo yule mwenzake alikwenda moja kwa moja hadi kwenye siti ya mbele kushoto kwa dereva alipokuwa ameketi yule mzee wa makamo mwenye suti maridadi, nikamwona akiuchukua ule mkoba kutoka kwenye mikono ya yule marehemu.

Itaendelea...
 
narudi buzwagi.jpeg

80

Yule muuaji aliyekuwa akisogea pale kwenye kichaka tulichokuwa tumejibanza mimi na yule mrembo alisimama ghafla, kama aliyekuwa amehisi kitu nikamwona akijaribu kunusanusa kama mbwa mwindaji aliyejaribu kubaini windo lake lilipo.

Kuona vile hofu ikazidi kutambaa kwenye mwili wangu, ikabidi nimzibe macho yule msichana mrembo ili asione kilichokuwa kikitokea, kwani bila kufanya vile angeweza hata kukurupuka ili kukimbia na hivyo kusababisha balaa zaidi.

Pamoja na kumziba yule mrembo lakini nilihisi ujasiri ulikuwa ukinipotea taratibu na moyo wangu ulizidi kupoteza utulivu huku kijasho chepesi kilikuwa kikinitoka sehemu zote za mwili wangu.

Yule muuaji aliinua ile bunduki yake na kuelekeza pale kichakani tulipokuwa tumejificha mimi na yule mrembo, kisha nikamshuhudia akiikoki tayari kwa lolote.

Kuona vile nami nikafumba macho yangu huku nikipoteza kabisa matumaini ya kuokoka katika tukio lile, mara nikamsikia yule muuaji mwenzake aliyekuwa amesimama kule kwenye lile gari akimwita huku akimwambia kuwa walipaswa waondoke haraka kabla jambo baya halijatokea na hawakutakiwa kupoteza muda wao katika eneo lile.

Kitendo kile kikamfanya muuaji ambaye alikuwa tayari kufyatua risasi katika kile kichaka tulichokuwa tumejificha asite kufyatua risasi na badala yake akakitazama kile kichaka kwa makini kama vile mtu aliyehisi kitu fulani ndani ya kile kichaka.

Hata hivyo nilimwona akishusha pumzi huku akibana taya zake akionekana kuwa hakuwa na namna nyingine ya kufanya. Alionekana kama aliyekuwa akijishauri iwapo aondoke au aendelee na dhamira yake, mara akashusha bunduki yake na kugeuka kurudi haraka kule kwa mwenzake.

Yule muuaji mwenzake muda ule alikuwa ameshika mkononi ile brifukesi ya yule mzee abiria aliyekuwa ameketi siti ya mbele kushoto kwa dereva. Nilishusha pumzi za ndani kwa ndani huku nikishuhudia gari la wale wauaji likianza kuondoka taratibu kutoka eneo lile huku wale wauaji wakilikimbilia na kurukia nyuma, kisha liliondoka kwa mwendo wa kasi kutoka eneo lile kama lilivyokuja. Yote hayo yalikuwa yamefanyika ndani ya dakika tano tu.

Baada ya sekunde chache hali ya mahala pale ikawa ya ukimya mno uliotisha katika eneo lote. Kwa sekunde kadhaa nikiwa bado nimemziba uso yule msichana mrembo nilijikuta nikiduwaa huku nikishindwa kabisa kuamini kuwa tulikuwa tumesalimika na mkasa ule hatari ulioyakatisha maisha ya abiria wenzetu wanne pamoja na dereva wa lile gari letu.

Niliweza kuyashuhudia mambo yote ambayo yalikuwa yametokea ndani ya muda wa dakika zisizozidi tano. Sasa tulikuwa tumebaki wawili tu katika eneo lile, mimi na yule msichana mrembo. Mara kukaibuka hali ya utulivu mkubwa sana katika ile barabara na eneo lile lote kwa ujumla.

Sauti pekee zilizokuwa zikisika katika eneo lile zilikuwa ni sauti za wadudu wa porini na kwa mbali niliweza kusikia sauti za mbwa waliokuwa wakibweka kutoka makazi ya watu walioishi katika vijiji vilivyokuwa jirani na eneo lile.

Kwa hali ile niliweza kugundua kuwa kumbe hatukuwa mbali na eneo la makazi ya watu pale porini. Hata hivyo, sikuthubutu kabisa kuinuka na kutoka pale kwenye kichaka tulipokuwa tumejibanza bali niliendelea kujibanza kwenye kile kichaka huku nikiwa nimemshika yule mrembo kwa muda usiopungua dakika ishirini, wote tukiwa hatuamini kama tulikuwa salama.

Nilimeza funda kubwa la mate na kumshukuru Mungu kimoyomoyo kwa kutuepusha na ile mitutu ya bunduki kutoka kwa wale wauaji. Tukiwa bado tupo pale kichakani nilimtazama kwa makini yule mrembo ambaye muda huo alikuwa amejikunyata kifuani kwangu kwa hofu huku akitetemeka.

Nilijikuta nikimhurumia sana, nikazidi kumkumbatia katika namna ya kumfariji, na mara nikamwona akijilaza kwenye kifua changu huku akinikumbatia kwa hofu, alikuwa analia kilio cha kwikwi akiwa bado anatetemeka.

Japokuwa tulikuwa kwenye taharuki la aina yake na hali yangu ilikuwa inazidi kuwa mbaya kadiri sekunde zilivyokuwa zikiyoyoma lakini nilijikuta nikijisikia faraja kubwa sana kukumbatiwa na msichana mrembo kama yule. Mwili wangu wote ulikuwa unauma sana kama kidonda, na mguu wangu wa kushoto ulikuwa umepinda kidogo na kuvimba na nilipojaribu kuuinua ulikuwa mzito mno mfano wa kipande kizito cha chuma.

Nilitamani kumwambia yule msichana mrembo jinsi nilivyokuwa nikijisikia muda ule ili atafute msaada lakini nilisita kusema chochote kwa kuhofia kuwa endapo angegundua kuwa hali yangu ilikuwa mbaya angeingiwa na hofu kubwa zaidi. Nikiwa bado katika hali ile mara nikasikia muungurumo wa gari lililokuwa likija eneo lile likitokea kule nyuma tulipotoka.

Sauti ya muungurumo ule uliashiria kuwa mwendo wa lile gari ulikuwa wa kasi mno kiasi cha kunitahadharisha kuwa mambo bado hayakuwa shwari. Moyo wangu ukashikwa na mfadhaiko huku ukianza kwenda mbio isivyo kawaida.

Kwa sekunde chache nilijikuta nikiyasahau maumivu yangu na jasho jepesi likaanza kunitoka sehemu mbalimbali za mwili wangu. Wakati huo yule msichana mrembo alikuwa akizidi kujigandamiza kwenye mwili wangu akionekana kuogopa sana.

Nikalishuhudia lile gari likikaribia kabisa eneo lile na kupunguza mwendo, na kitendo cha kupunguza mwendo kikawafanya watu watatu waliokuwa wamevaa kombati za kiaskari waruke kutoka nyuma ya lile gari na urukaji wao ulionesha kuwa walikuwa tayari kukabiliana na jambo lolote la hatari huku wakiwa wameshika vyema bunduki zao tayari kwa lolote.

Mara nikaliona lile gari likiongeza tena mwendo wake na kutupita kwa kasi, na mara tu lilipotupita nikagundua kuwa lilikuwa ni gari aina ya Nissan Patrol la rangi nyeusi lililokuwa na maandishi makubwa ya ‘POLISI’ ubavuni na nyuma yake kulikuwa na askari wengine watatu ambao mikononi walikuwa wameshika bunduki za kivita.

Lilikwenda umbali wa takriban mita ishirini au therathini mbele yetu kisha nikaliona likipunguza tena mwendo wake. Na hapo askari wale wengine watatu waliokuwa kule nyuma wakaruka kutoka nyuma ya lile gari wakiwa tayari kukabiliana na jambo lolote la hatari huku wakiwa wameshika bunduki zao tayari kwa lolote.

Niliwatazama wale askari huku nikianza kupata matumaini mapya ya kuokolewa. Hata hivyo, maumivu makali ya mwili wangu na mguu wa kushoto yalizidi kunitesa na mguu wangu ulikuwa mzito mno kama uliokuwa umefungwa chuma kizito. Niliwatazama wale askari wakati wakitawanyika haraka katika eneo lile nikatamani kufungua mdomo wangu ili nipige yowe la kuomba msaada kutoka kwao lakini nilipofungua mdomo sauti ikagoma kabisa kutoka.

Sikuona sababu ya kuendelea kujificha pale kwenye kichaka, hivyo niliamua kuinuka na kuanza kupiga hatua kuwafuata wale askari lakini maumivu makali sana ya mwili na kwenye mguu wangu wa kushoto yalinifanya nishindwe kutimiza azma yangu. Niliishiwa nguvu mwilini na kuanguka chini huku nikipiga kichwa changu kwenye kisiki cha mti mkubwa uliokuwa umekatwa na kutoa yowe dogo kwa sauti dhaifu.

Sasa moyo wangu ulikuwa unakwenda mbio isivyo kawaida na uliunguruma sana kama uliokuwa ukipambana na kazi isiyo ya kiasi chake, macho yangu nayo taratibu yakaanza kupoteza nguvu ya kuona. Hatimaye shughuli mbalimbali za mwili wangu nazo nikazihisi kuwa zilikuwa mbioni kusitisha utendaji wake.

Yule msichana mrembo alisimama akaniangalia kwa wasiwasi mkubwa, hakuweza kuvumilia akapiga kelele kubwa za hofu kuomba msaada. Muda ule ule nikasikia sauti za vishindo vya miguu za wale askari wakija mbio katika eneo lile tulilokuwepo.

Kufumba na kufumbua lile eneo lote likawa limezingirwa na wale askari wenye silaha. Muda huo nikatamani sana kuinuka au kufumbua macho yangu ili nione kilichokuwa kinaendelea katika eneo lile, na ikibidi kuongea nao ili niwaelezee kuhusu mkasa mzima ulivyokuwa lakini hilo halikuwezekana kabisa, kwani macho yangu yalizidi kuwa mazito sana na akili yangu ilianza kushindwa kufanya kazi.

Kwa mbali niliweza kusikia sauti za wale askari wakijaribu kumuuliza yule msichana mrembo kuhusu kilichotokea, lakini yule mrembo muda wote alikuwa analia kwa uchungu. Nikataka nijiinue na kusimama lakini sikuweza, nikajikakamua kuinua lakini sikuweza na mara nikahisi fahamu zangu zikinitoka taratibu.

Muda mfupi uliofuatia sikuweza tena kufahamu kilichoendelea pale. Nilianza kujiona nikitumbukia kwa kasi ya ajabu kwenye shimo refu sana lilikokuwa na kiza kilichotisha. Kabla sijafika chini kuna ndege mkubwa alininyakua na kuanza kupaa juu kwa kasi ile ile ya ajabu hadi tulipotoka ndani ya lile shimo.

Na mara giza zito likatanda kwenye mboni zangu za macho huku taratibu nguvu zikianza kuniishia na mwili wangu ukilegea, mapigo yangu ya moyo nayo yakaanza kudorora, hata hivyo yule ndege alizidi kwenda juu zaidi na kuzifanya pumzi zangu zipae na kunifanya kuhema kwa shida. Nilijaribu kupiga kelele za kuomba msaada lakini sauti yangu ilikuwa haitoki na badala yake niliisikia ikitengenezwa mwangwi ndani ya kichwa changu.

* * *

Endelea kufuatilia, hakika hutojutia muda wako...
 
narudi buzwagi.jpeg

81

The Most Wanted.


Saa 4:20 asubuhi…

NILIYATEGA masikio yangu kwa umakini huku nikijaribu kutafakari kuwa pale nilikuwa wapi. Nilikuwa nimerudiwa na fahamu, na sikujua pale nilikuwa wapi ila nilikuwa nimelala kitandani kwenye foronya laini na mto wa kuegemeza kichwa. Niliyazungusha macho yangu taratibu kuyatazama mazingira na nikagundua kuwa nipo kwenye chumba kikubwa chenye vitanda viwili vya chuma.

Ndani ya chumba kile kulikuwa na hewa safi iliyokuwa ikipita kwenye madirisha makubwa ya vioo. Sikujua nilikuwepo hapo tangu lini na kwa nini nilipoteza fahamu zangu. Sikuwa na uhakika kama nililetwa pale kwa gari, mkokoteni, machela au nilifikaje! Nikashangaa sana! Ilikuwaje hadi nikafikishwa katika chumba kile!

Nilianza kuwaza, nini kilikuwa kimenipata lakini sikuweza kukumbuka lolote. Jasho jepesi likaanza kunitoka. Sikuweza kufahamu nini kilinitokea hadi nikapoteza fahamu zangu! Hata hivyo, jambo hilo halikuwa la muhimu sana kwangu. Jambo lililokuwa la muhimu ni kwamba nilikuwa bado nipo hai, na hivyo nikataka kujua nilikuwa wapi.

Niliyatega masikio yangu kwa makini huku nikijaribu kutafakari kuwa pale nilikuwa wapi lakini sikufahamu. Nilijaribu kujiinua kutoka pale kitandani nikahisi maumivu makali yakisambaa mwilini sambamba na kichwa kuuma huku nikihisi kizunguzungu na mwili wangu ulikuwa umedhoofika sana mithili ya mlevi aliyeamka na uchovu wa pombe, kichwa changu kilikuwa kizito mno.

Nilitulia kidogo huku nikishusha pumzi zangu kwa nguvu kisha nikataka niinuke tena ili nikae, nilipojivuta nikauhisi mguu wangu wa kushoto ukiwa mzito sana kama kipande cha chuma na uliambatana na maumivu makali. Hapo nikashawishika kufunua shuka nililokuwa nimefunikwa na kuutazama kwa makini ule mguu na ndipo nilipogundua kuwa ulikuwa umefungwa bandeji ngumu (P.O.P.), nikashtuka sana.

Nikaliangalia shuka nililofunikwa na kugundua kuwa nilikuwa nimefunikwa kwa shuka safi la rangi ya samawati lililokuwa na maandishi “Hospitali ya Wilaya ya Kahama” nikashtuka. Niligeuza shingo yangu kuyatazama vizuri mandhari ya kile chumba na kugundua kuwa kilikuwa chumba maalumu kilichoonekana kama ni wodi maalumu ya watu maalumu (VIP) kikiwa na vifaa vya tiba.

Niliona kulikuwa na meza ndogo iliyokuwa katikati ya vitanda upande wa ukutani na juu ya ile meza kulikuwa na trei ndogo ya aluminium iliyokuwa na vifaa muhimu vya tiba kama kifaa cha kupimia presha ya damu (Sphygmomanometer), mikasi, bandeji, plasta, dawa ya kukaushia vidonda, mabomba ya sindano, glovu, chupa ya maji, bilauri na dawa za vidonge ambazo sikuzifahamu. Baadhi ya vile vifaa vilikuwa vimefunguliwa na kuachwa wazi kitendo kilichoashiria kuwa tayari vilikuwa vimekwisha tumika.

Kando yangu kulikuwa na stendi ndefu ya chuma ya kitabibu iliyokuwa imetundikiwa chupa mbili, moja ilikuwa chupa ya maji aina ya Dextrose 5% yaliyokuwa yamechanganywa na dawa, na nyingine ilikuwa ni chupa ya damu.

Macho yangu yakapata uhai kidogo na nilipochunguza kwa makini nikagundua kuwa mrija wa chupa ya damu ulishuka hadi kwenye mkono wangu wa kulia na mwishoni kulikuwa na sindano iliyochomekwa kwenye ule mkono na kupeleka damu kwenye mshipa wangu ya damu. Ile chupa ya maji ilikuwa imeisha na mrija ulikuwa umetundikwa juu. Niliziangalia zile chupa kwa umakini, nikashusha pumzi na kufumba macho yangu nikijaribu kutafakari.

Nilifumbua tena macho yangu nikageuza shingo yangu kuutazama mlango wa kile chumba kwa umakini, nikauona ukiwa umefungwa ingawa sikufahamu kama ulikuwa umefungwa kwa funguo au ulikuwa umerudishiwa tu. Hata hivyo, nilishindwa kuthibitisha kwani afya yangu ilikuwa dhaifu sana kiasi cha kushindwa hata kunyanyuka na kuketi pale kitandani.

Nikiwa bado nautazama ule mlango mawazo mengi yalikuwa yakipita kichwani mwangu na kunifanya nijihisi kama kiumbe kigeni katika sayari mpya. Mara picha nzima ya tukio la mauaji kule porini wakati tukitoka Masumbwe kueleka Kahama likanijia, nikakumbuka kila kitu tangu tulipokuwa ndani ya Prado hadi tulipovamiwa na majambazi yaliyoua abiria wenzetu kadhaa, nilivyomwokoa msichana mrembo ambaye sikujua alikuwa wapi muda huo.

Nilikumbuka pia jinsi nilivyohisi maumivu makali ya mguu baada ya kuruka kutoka kwenye lile gari aina ya Prado huku nikiwa nimembeba yule mrembo baada ya mguu huo kutua kwenye shimo dogo. Nikakumbuka niliinuka baada ya kuwaona polisi wakifika na kulizingira eneo lile lakini nikaanguka na kupiga kichwa changu, kisha nilianza kupoteza fahamu zangu huku yule mrembo akilia kwa uchungu.

Sura ya yule mrembo ikajaa akilini kwangu, nilikumbuka vema nilivyokuwa nimemlkumbatia pale kwenye kichaka, na hapo nikahisi maumivu ya mwili wangu yakipungua, na sasa nikapatwa na hamu ya kutaka kufahamu ni wapi alikokuwa yule mrembo na mambo mengi yaliyotokea baada ya mimi kupoteza fahamu.

Lakini sikuwa na mtu wa kumuuliza maswali yale kwani katika ile wodi sikumwona mtu yeyote niliyedhani angeweza kufahamu kile kilichonitokea, japo hata kunijuza nilikuwa nimefikaje pale hospitali. Niliamini kuwa kwa vyovyote yule mrembo aliniokoa akishirikiana na wale polisi wa Masumbwe.

Niliamini kuwa ni yeye aliyetoa maelezo kuhusu tukio lile la kutisha. Ni yeye aliyesaidia kunifikisha pale Hospitali ya Wilaya ya Kahama, na pia ni yeye ambaye angeweza kunieleza vizuri nini kilichotokea wakati nilipokuwa nimepoteza fahamu zangu. Lakini sikujua ningempata wapi na sikuwa na namna nyingine yoyote ya kupata majibu isipokua kuvuta subira.

Nilifumba macho na taratibu usingizi ukaanza kuninyemelea, mara nikashtuka baada ya kuhisi nyayo za mtu zikisogea pale mlangoni, nikageuka na kuona kitasa cha ule mlango kikizungushwa taratibu kisha ule mlango ukasukumwa na kufunguka, moyo wangu ukapoteza utulivu.

Akaingia muuguzi mwanadada mrembo, mrefu wa wastani, mweupe kiasi kwa rangi ya ngozi yake na aliyekadiriwa kutozidi miaka 30. Alikuwa na umbo kubwa lililovutia mno na mashavu yake yalikuwa mfano wa chungwa. Nywele zake zilikuwa nyingi. Alikuwa amevaa sare ya kazi, gauni jeupe zuri na pana kiasi lakini lililokuwa limeushika vema mwili wake na kulichora umbo lake zuri lenye tumbo bapa na kiuno chembamba lakini imara kilichoshikilia minofu ya mapaja yake yaliyonona.

“Bwana Sizya, unajisikiaje sasa?” yule muuguzi aliniuliza huku akiachia tabasamu pana usoni kwake.

“Ah, kwa kweli hata sielewi, nahisi kizunguzungu na mwili wangu umechoka sana kama niliyekunywa sana pombe,” nilimwambia huku nikikunja uso wangu na kupeleka mkono wangu kichwani.

“Usijali, utapona…” yule muuguzi aliniambia huku akiachia tabasamu, kisha akanitaka radhi na kuchukua kile kifaa cha kupimia presha ya damu na kukifunga kwenye mkono wangu wa kushoto kisha akaanza kukipampu kwa muda na mara presha (pressure gauge) ikaanza kupanda juu.

Niliyafumba macho yangu huku nikibana pumzi kutokana na ile mashine kuanza kubana kwenye mkono wangu na kusababisha maumivu kidogo. Baada ya kitambo fulani yule daktari alianza kulegeza taratibu skrubu fulani ndogo iliyokuwa pembeni, mara nikasikika kikitoa sauti ya ‘hisssiii’ huku pressure gauge ikishuka taratibu, na wakati huo namba zilikuwa zikijiandika kwenye kioo kidogo juu ya ile mashine.

Nilikuwa makini kutazama pale kwenye namba lakini niliishia kuona maandishi SYS 110 na chini yake kukiwa na maandishi DIA 60, huku chini zaidi kukiwa na maandishi PULSE 72. Hata hivyo, sikujua maana yake ila nilihisi kuwa zile namba zilimaanisha presha ya damu yangu na mapigo ya moyo. Kisha nikamwona akiandika taarifa kwenye faili alilokuja nalo na kuniangalia kwa tabasamu pana la kunifariji, “Pole sana, kaka…”

Kisha akaanza kupiga hatua taratibu kuondoka eneo lile lakini sikutaka aondoke bila kunitegulia kitendawili changu.

Itaendelea...
 
narudi buzwagi.jpeg

82

“Samahani dada, nimefikaje hapa hospitali na nani aliyenileta?” nilimuuliza yule muuguzi kwa sauti tulivu, nikamwona akigeuza shingo yake na kuniangalia kwa kitambo fulani pasipo kusema neno. Alikuwa kama anayefikiria jibu la kunipa.

“Kwa kweli sifahamu kwa kuwa mimi sikuwepo wakati ukiletwa, ila ninachojua uliletwa na Polisi wa Masumbwe,” yule muuguzi aliniambia huku akiniangalia kwa utulivu.

“Nimeletwa lini?” nilimuuliza tena huku nikimwangalia usoni.

“Uliletwa jana usiku…”

“Ni Polisi pekee au waliambatana na msichana fulani hivi?” niliuliza tena kwa shauku huku moyo wangu ukiwa umekosa utulivu.

“Kama nilivyokwambia, sina jibu sahihi la kukupa kwa kuwa nimeingia hapa leo asubuhi na taarifa pekee nilizo nazo kuhusu wewe ni za kitabibu zaidi,” yule muuguzi aliniambia huku akitaka kuondoka.

“Umelijuaje jina langu?” nilimuuliza tena lakini nikamuona akiniangalia kwa mshangao kana kwamba nilikuwa nimegeuka kichekesho, kwani nilikuwa nauliza swali ambalo jibu lake lilikuwa wazi kabisa.

“Si limeandikwa kwenye faili lako! Polisi ndio waliosema kuwa unaitwa Jason Sizya… au si jina lako?” yule muuguzi aliniuliza huku akiendelea kuniangalia kwa mshangao.

“Ndiyo jina langu, lakini…” nilisema lakini nikasita baada ya kugundua kuwa huenda polisi walikuwa wameona kwenye vitambulisho vyangu, cha kazi na cha taifa, ambavyo nilikuwa na kawaida ya kutembea navyo, na siku ile nilikuwa navyo kwenye begi langu la mgongoni.

Yule muuguzi aliendelea kuniangalia kwa umakini kwa kitambo kidogo kisha akashusha pumzi na kuachia tabasamu laini lililonipagawisha kwa muda, nikasahau kama nilikuwa nahitaji kupata taarifa muhimu.

“Na wewe unaitwa nani daktari wangu?” nilijikuta nikimuulza jina lake.

“Naitwa Hilda Mwendapole,” alijibu huku akiendelea kutabasamu.

“Nashukuru kukufahamu, Hilda,” nilimwambia huku nami nikitabasamu. Akaniaga na kuondoka. Mara tu Hilda alipoondoka nikaupisha utulivu kichwani mwangu huku nikigeuza tena shingo yangu kuangalia huku na kule.

Sikujua ilikuwa imetimia saa ngapi kwa kuwa sikuwa na saa yangu ya mkononi ingawa nilihisi kuwa ilikuwa inaelekea majira ya mchana kutokana na miale ya jua kuwa juu zaidi, na hapo fikra zangu zikahamia kutafakari juu ya Rehema na jamaa zangu. Sikujua kama walikuwa wanazo taarifa kuhusu mkasa ulionitokea kule porini Masumbwe, hata hivyo nilimuomba Mungu anipe unafuu haraka ili nitoke pale hospitali na kuendelea na kazi zangu.

Niligundua kuwa sikuwa na simu yangu na sikujua ilikuwa wapi, na kwa kuwaza hilo nikaanza kujiuliza iwapo Rehema alikuwa amenitafuta kwenye simu bila mafanikio na pengine aliamua kumpigia Eddy ambaye pia hakujua niko wapi! Hapo nikaanza kufikiria kuhus hali ya Rehema baada ya kutokuwa na taarifa zangu, hasa ikizingatiwa kuwa alishakuwa na hisia mbaya kabla hata sijaondoka Ushirombo. Je, alikuwa amepata taarifa za yale mauaji kule porini Masumbwe?

Mawazo mengi sasa yalianza kupita kichwani kwangu, nilijiuliza masweali mengi yaliyokosa majibu.

______

Sikuweza kufahamu ni wakati gani nilipitiwa na usingizi ulioziteka fikra zangu pale kitandani wakati nilipokuwa nikiendelea kuwaza hili na lile, nilikuja kushtuka kutoka usingizini baada ya kuhisi mkono ukinigusa kwenye paji langu la uso.

Hivyo nikafumbua macho yangu na kugeuza taratibu shingo yangu huku nikitabasamu na kuyapeleka macho yangu kumtazama yule mtu aliyekuwa amenigusa kwenye paji langu la uso, akilini kwangu nilitarajia kumwona Rehema, Eddy au yule msichana mrembo niliyekuwa naye safarini kule Masumbwe wakati tukivamiwa na wale wauaji.

Hata hivyo, hilo halikutokea na badala yake mbele yangu nilijikuta nikikabiliana na wanaume watatu waliokuwa wamesimama huku wakiniangalia kwa makini. Wanaume wawili niliwatambua mara moja kuwa walikuwa ni maofisa wa Polisi kutokana na mavazi yao.

Kati yao, mmoja alikuwa na cheo cha Mkaguzi wa Polisi kutokana na alama mbili za nyota kwenye mabega yake, nikamtambua mara moja kwani niliwahi kukutana naye mara kadhaa na alikuwa rafiki wa Eddy. Yule ofisa wa Polisi aliitwa Inspekta John. Yule mwenzake alikuwa na cheo cha Koplo kutokana na alama mbili za “V” eneo la chini ya bega lake la kulia.

Yule mwanamume wa tatu alikuwa ni daktari kutokana na mwonekano wa mavazi yake, kwani alikuwa amevaa shati la samawati, suruali ya bluu na koti refu jeupe la kidaktari, na shingoni kwake alikuwa amening’iniza kifaa cheusi cha kupimia mapigo ya moyo kinachoitwa ‘Stethoscope’.

“Pole sana Jason, unajisikiaje?” yule daktari aliniuliza huku akiendelea kunigusa kwenye paji la uso wangu kwa kiganja chake cha mkono.

“Nasikia maumivu makali sana ya mguu na kichwa changu ni kizito,” nilisema kwa utulivu huku nikiwaangalia wote daktari kwa zamu, wale maofisa wa polisi walikuwa kimya wakiniangalia kwa umakini mkubwa.

“Usijali utapona. Shukuru Mungu uliwahishwa hospitali kabla hali haijawa mbaya zaidi maana ulipoteza damu nyingi,” aliniambia yule daktari huku akigeuza shingo yake kuwaangalia wale maofisa wa Polisi aliokuwa ameongozana nao.

“Hawa ni maofisa wa Polisi wamekuja kukujulia hali na wangependa wapate maelezo kidogo kisha wakuache upumzike na ukishapata nafuu kidogo wanaweza kukuhoji tena kama itahitajika,” alisema yule daktari kwa utulivu.

“Nawafahamu, tumeshakutana mara kadhaa kwenye shughuli zetu,” nilisema kwa sauti tulivu huku macho yangu nikiwa nimeyatuliza kwenye uso wa Inspekta John.

“Ni kweli tunafahamiana. Sasa ningependa kupata maelezo kidogo kuhusu tukio,” Inspekta John aliniambia huku akijiweka sawa.

Niliwaelezea yote niliyoyafahamu na niliyoyakumbuka, kuanzia nilivyoliona gari aina ya Toyota Land Cruiser Pick-up kule katika kituo cha kujazia mafuta cha Masumbwe na kuhusu mwanamume aliyeshushwa pale kwenye kile kituo cha kujazia mafuta, jinsi nilivyopatwa na hisia mbaya juu yake pale alipokuja pale kwenye gari letu na kuonekana kama aliyekuwa anatuchunguza abiria tuliokuwa mle ndani ya gari.

Inspekta John alikuwa anaandika maelezo, nikamweleza jinsi tulivyolipita lile gari likiwa limeegeshwa kando ya barabara huku boneti la gari likiwa wazi, hadi walivyotufuata kule porini na kutuzuia kwa mbele. Kisha nikawaeleza nilivyoushuhudia mchezo mzima jinsi dereva wetu alivyorudi nyuma na kukaribisha mvua ya risasi.

Kisha nikawaeleza nilivyoweza kumwokoa binti mmoja na hadi walipofika Polisi kisha nikapoteza fahamu…

Waliandika maelezo yangu yote na kunipongeza sana kwa ujasiri wangu huku wakinipa pole, kisha wakanishukuru kwa amelezo ambayo waliamini yangewasaidia sana.

“Kwa sasa hupaswi kuhofia chochote kwani uko kwenye mikono salama,” Inspekta John aliniambia huku akiachia tabasamu la kunifariji.

“Nashukuru sana afande, lakini… mna taarifa zozote kuhusu wauaji?” nilimuuliza Inspekta John kwa shauku ya kutaka kujua, ingawa ukweli nilihitaji sana kupata taarifa za yule msichana mrembo.

“Upelelezi unaendelea, tayari tumekwisha pata maelezo ya awali kutoka kwa watu watatu walionusurika ambao ulikuwa nao kwenye gari na walishuhudia tukio lile, na sisi tunajaribu kuangalia sababu za mauaji yale, ingawa kwa harakaharaka ni kama vile kuna viashiria vya ulipizaji kisasi…” alisema Inspekta John huku akishusha pumzi.

“Kwa sasa tusingependa kuchosha, na kama alivyoshauri daktari, pumzika kwanza na kila kitu kitakuwa sawa. Nimeshawasiliana na kaka yako Eddy kumweleza yaliyokusibu. Nadhani muda wowote atafika hapa,” Inspekta John aliniambia huku akiachia tabasamu.

“Vipi kuhusu vitu vyangu, mmebahatisha kuviona?”

“Vitu vyako vipo, tumepata begi dogo la mgongoni na simu yako ya mkononi aina ya Samsung, sijui kama ulikuwa na mizigo mingine?” Inspekta John aliniuliza, nikatingisha kichwa kukataa.

“Nashukuru sana, sijui ni watu wangapi waliokufa katika tukio lile?” niliuliza tena kwa udadisi.

“Taarifa rasmi tulizonazo ni watu sita ndio waliokufa,” aliniambia huku akianza kupiga hataua kuondoka.

Itaendelea...
 
narudi buzwagi.jpeg

83

Maelezo yake yakanifanya nivute kumbukumbu zangu kujaribu kukumbuka kilichotokea katika lile tukio. Taarifa zile zikasababisha jasho jepesi lianze kunitoka mwilini!

“Naomba kujua jambo moja la mwisho… yule msichana niliyemwokoa yuko wapi?” nilimuuliza tena Inspekta John wakati akifungua mlango atoke.

“Amechukuliwa na mzazi wake mara baada ya kufika hapa Kahama, ni yeye aliyetusaidia sana kufahamu mengi kuhusu lile tukio, na hongera sana maana umeokoa maisha yake,” Inspekta John alinijibu huku akiniangalia kwa tabasamu.

By the way, vitu vyako vimehifadhiwa mahala salama, utaletewa wakati wowote,” Inspekta John alisema na kugeuka kuwatazama wengine kisha wakaondoka zao.

Nilifarijika kidogo kusikia kuwa alikuwa salama na kwamba aliwaeleza Polisi jinsi nilivyomwokoa nikaamini kuwa kwa namna fulani alikuwa ameguswa na mimi, ila sikuwa na raha kwa kuwa hata jina lake sikulijua na hivyo nikaamua kumpachika jina la ‘the most wanted’.

Dakika chache tu tangu walipoondoka wale maofisa wa polisi na daktari nikashuhudia tena kitasa cha mlango wa kile chumba kikizungushwa taratibu kisha ule mlango ukasukumwa ndani na kufunguka. Hilda akachungulia ndani kisha akageuza shingo yake kutazama nyuma yake akionekana kungong’ona jambo, akaingia akiongozana na Eddy, Swedi na Rehema.

Moyo wangu ulilipuka kwa furaha baada ya kuwaona. Rehema alikuwa amevaa suti nadhifu ya kike ya rangi ya kijivu iliyomkaa vema na kumpendeza sana. Eddy alivaa suti nyeusi na Swedi alivaa shati la pundamilia la mikono mirefu na suruali nyeusi.

Eddy alikuwa amebeba begi langu dogo nililokuwa nalo siku ya tukio pamoja na simu yangu, Swedi alibeba maua mazuri na Rehema alikuwa amebeba kikapu mkono mmoja na mkono mwingine alibeba maua mazuri, yalikuwa ni kwa ajili kunitakia uponaji.

“Mungu wangu! Kumbe ni kweli jambo hili limekutokea?” Eddy aliniongea huku akiniangalia kwa mshangao.

Rehema alisimama akaniangalia akiwa haamini, machozi yakaanza kumtoka. Alitaka kuongea neno lakini akashindwa na kuanza kulia kilio cha kwikwi, huku Eddy na Swedi wakibaki kimya wanamtumbulia macho huku machozi yakiwalenga.

“Inspekta John aliponipigia simu jambo la kwanza kujiuliza lilikuwa leo ni tarehe ngapi, maana nilidhani ni siku ya wajinga. Baadaye shemeji Rehema naye akanipigia simu kuniuliza kama umefika salama maana alikuwa amepata taarifa za gari moja aina ya Prado kuvamiwa na ilisemekana abiria karibu wote wameuawa,” Eddy aliongeza huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Ndiyo hivyo tena, kama mlivyosikia. Yaani ilikuwa ni zaidi ya hatari. Ni bora usimuliwe tu!” niliwaambia kwa taabu huku nikiminya sura yangu kwa maumivu.

Niligeuza shingo yangu kumwangalia Rehema ambaye aliendelea kusimama kama sanamu huku machozi yakimtiririka machoni.

“Rehema!” nikamwita kwa sauti ya chini yenye kuashiria maumivu.

“Jason!” hatimaye Rehema alionekana kuzinduka, akaniita kwa sauti tulivu lakini ya mshangao kisha akiharakisha kuja pale kitandani nilipolala, akaliweka chini lile kapu na maua aliyobeba na kunikumbatia kwa nguvu bila kujali majeraha yangu, alikuwa akilia kwa furaha.

Na mimi pia nikajikuta nalia. Tulibaki tukiwa tumekumbatiana kwa dakika kadhaa huku tukiendelea kulia, kilio chetu kikaamsha simanzi kwa wengine. Sasa chumba chote kilichachatika simanzi na nyuso zetu zikafiringiswa katika viganja vya mikono.

Baada ya kitambo kidogo tulinyamaza na hali ndani ya kile chumba ikarudi katika hali yake ya kawaida. Swedi aliyachukua yale maua akayaweka kwenye meza ndugo iliyokuwemo mle chumbani.

“Hivi nini hasa kilitokea?” Rehema aliniuliza kwa shauku huku akiniangalia kwa umakini.

“Dah, ni hadithi ndefu…” nilijibu huku nikishusha pumzi ndefu.

Anyway, unapaswa kula kwanza ili upate nguvu,” Rehema aliniambia huku akikichukua kile kikapu. Nikaweza kuona kilichokuwemo ndani, kulikuwa na hotpot kubwa la chakula, mabakuli mawili yaliyokuwa na mfuniko, sahani, kijiko kikubwa cha kupakulia na kingine cha kulia chakula, na bilauri pamoja na chupa kubwa ya maji ya kunywa.

Alitoa lile hotpot kisha akalifunua. Nilipotupa jicho langu kuangalia nikagundua kulikuwa na mchemsho wa ndizi na samaki aina ya sato. Akachukua sahani na kijiko kikubwa na kunipakulia chakula kidogo kisha akayafunua yale mabakuli mawili yaliyokuwa na mifuniko, bakuli moja lilikuwa na mboga za majani na saladi na jingine lilikuwa na matunda mchanganyiko.

Alipakua kisha akaonja kidogo huku akionekana kukifurahia sana kile chakula. Kwa msaada wa Eddy na Swedi nilifanikiwa kunyanyuka kidogo na kukiegemeza kichwa changu kwenye mto ulioegemezwa ukutani pembeni mwa kitanda. Wakati huu nilisikia kichwa changu kikipwita kwa maumivu kana kwamba nilikuwa nimebebeshwa mzigo mzito sana.

Rehema akaanza kunilisha kile chakula. Sikujivunga, nilikila bila kujali maumivu ya mwili niliyokuwa nayo wakati huo. Wakati naendelea kula Rehema alikuwa ananiangalia kwa uyakinifu sana. Nilimaliza kula kile chakula ambacho kiukweli kilikuwa kitamu sana, kisha Rehema akavitoa vile vyombo na kuvisogeza kando.

Kikapita tena kitambo kifupi cha ukimya, hakuna aliyesema neno kati yetu. Rehema alikuwa akiniangalia kwa umaakini akiwa haamini, kuna wakati alitingisha kichwa chake taratibu na kumeza mate kutowesha koo lake lililokuwa limekauka.

Katika muda huo niliwasimulia mambo yaliyotokea katika tukio lile la porini wakati tukitoka Masumbwe. Tangu nilivyomshtukia jamaa mmoja aliyeshuka kwenye lile Land Cruiser Pick-up pale jirani na kituo cha kujazia mafuta cha Masumbwe na kuja kwenye gari letu kuulizia usafiri wa kwenda Kahama hadi tulipovamiwa porini na nilivyoweza kujiokoa na kumuokoa abiria mmoja, ila nilikuwa makini kuongea habari za yule msichana mrembo ili nisije nikamkwaza Rehema. Muda wote wakati nasimulia Rehema alikuwa anatokwa na machozi.

“Unakumbuka nilikwambia kuhusu hisia mbaya zilizonijia? Yaani roho yangu ilikuwa nzito sana kukuruhusu uondoke lakini kwa sababu uling’ang’ania sikuwa na namna ya kukuzuia,” Rehema alisema kwa huzuni huku akifuta machozi kwa mgongo wa kiganja chake, kisha akaketi kwenye ukingo wa kitanda.

“Hata mimi, kuna wakati nilitamani kuahirisha safari… lakini ndiyo hivyo tena yameshatokea!” nilisema na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Yaani hadi unanipigia simu kuwa upo Masumbwe bado nilitamani kukwambia urudi Ushirombo. Na niliposikia kuna gari limevamiwa na majambazi na abiria wameuawa katika pori la Mkweni moja kwa moja akili yangu ikanituma wewe ulikuwemo kwenye gari hilo, kwa kweli niliogopa sana. Nilipopiga simu yako ikawa haipatikani. Nilihisi haja kubwa na ndogo zinataka kutoka kwa pamoja!” Rehema alisema na wote tukajikuta tukicheka.

“Ulisikia wapi?” nilimuuliza Rehema huku nikishangaa kidogo.

“Mbona wametangaza kwenye vyombo vya habari! Lakini kwanza nilianza kusoma kwenye mitandao ya kijamii, bahati mbaya hawakuweza kutoa majina ya waliokufa wala waliopona.”

“Unajisikiaje kwa sasa?” Swedi aliniuliza baada ya kukaa kimya muda mrefu.

“Nasikia maumivu makali katika mguu wa kushoto uliovunjika, mwili pia unaniuma na kichwa kizito,” niliongea kwa utulivu huku nikipiga mwayo hafifu.

“Mungu atakusaidia… Kwa kweli siamini macho yangu kuwa upo hai,” Swedi aliniambia.

“Ni vigumu sana kuamini lakini Mungu ndiye aliyeniokoa, maana ilikuwa inatisha! Ni kama unaangalia sinema,” nilimwambia Swdei kwa utulivu huku nikitabasamu.

Itaendelea...
 
narudi buzwagi.jpeg

84

“Shemeji Eddy aliponiambia kuwa amepigiwa simu na rafiki yake Inspekta John na kuelezwa kuwa umelazwa hapa sikuamini, nilitamani nipae nije nikuone…” Rehema alisemana kushusha pumzi za ndani kwa ndani. Sasa alikuwa amechangamka.

Tuliendelea na maongezi, hata hivyo nikiwa pale kitandani mara kwa mara fikra zangu ziliendelea kusumbuliwa na yule msichana mrembo ‘the most wanted’, kuna wakati sura yake ilinijia na sikujua kwa nini. Nilitamani japo nimuone tur oho yangu iridhike.

Baadaye jamaa, marafiki na wafanyakazi wenzangu wa mgodi wa Buzwagi waliendelea kuwasili wakiwa na nyuso zilizoshindwa kuficha huzuni wakiwa hawaamini kilichotokea. Wote waliokuja kunijulia hali walikuwa wakinitakia uponaji wa haraka. Kila aliyeniona alishindwa kujizuia, machozi yaliwatoka.

Muda wote Rehema alikuwa akiniangalia akiwa haamini macho yake, kuna wakati tulitazamana usoni kwa kitambo huku kila mmoja akitokwa machozi. Kwa kweli Rehema alinipenda sana.

* * *



Nilikuwa nimemaliza wiki moja tangu nilazwe pale hospitali. Kwa siku zote nilikuwa nimetembelewa na watu wengi, hata Mama alifika toka Tabora kwa ajili ya kuniona mtoto wake. Licha ya umri wake wa miaka hamsini na tano lakini Mama alionekana bado kijana. Alikuwa mnene wa wastani, mrefu na ngozi yake ilikuwa ya rangi ya maji ya kunde.

Wengi waliofika kuniona walibeba maua na kadi za kunitakia uponaji wa haraka. Hata hivyo, kuna kitu bado kilikuwa kinaniumiza kichwa changu, katika watu wote waliofika kuniona yule mrembo ‘the most wanted’ sikumwona hata siku moja.

Siku ambayo Mama alifika ndiyo siku ambayo Rehema alikuwa anaaga ili kurudi Ushirombo. Rehema alikuwa nami kwa siku tatu akishinda pale hospitali muda wote kuanzia asubuhi hadi usiku na aliruhusiwa kulala nami pale hospitali kuniuguza. Na siku alipokuwa akiniaga kuwa alitakiwa kurudi kazini baada ya ruhusa yake ya siku tatu kuisha, muda wote alikuwa akitokwa machozi, hakupenda kuniacha. Ilibidi Mama amtie moyo ndipo alipokubali kuondoka.

Katika wiki hiyo, chumba changu kiliendelea kujaa maua na kadi nyingi za kunitakia uponaji wa haraka toka kwa watu mbalimbali waliofika kunitembelea.

Katika wiki ile Selemani Abeid alifika kunijulia hali baada ya kupata taarifa kupitia vyombo vya habari. Alioneshwa kuguswa sana na lile tukio la mauaji ya watu sita kule porini. Pia alinifikishia salamu kutoka kwa Mama yake na ndugu zake na kunieleza jinsi walivyoshtushwa na taarifa zile, kisha akaniambia kuwa wote walikuwa wananiombea kwa Mungu ili nipone haraka na niendelee na majukumu yangu kama kawaida.

Tuliongea mengi na muda wote wa maongezi yetu nilitamani sana kusikia habari za Jamila lakini sikuthubutu kuulizia, kwani sikutaka kugombana na Selemani maana alifahamu kuhusu tabia yangu ya ukware. Aliondoka akiahidi kunitembelea tena baada ya siku mbili.

Siku ile baada ya Selemani kuondoka, Dk. Camilla Mpogolo, dada wa Rehema, na mumewe walifika kunijulia hali baada ya siku kadhaa za kuwa nje ya Wilaya ya Kahama. Walibeba maua na kadi maalumu za kunijulia hali. Walikutana na Mama na tulipata wasaa mzuri wa kuongea mengi, nikawaeleza kuwa nilikuwa kwenye mkakati wa kukutana na kaka Eddy kwa ajili ya mchakato wa kupeleka washenga ili tukamilishe suala langu na Rehema lakini ndiyo yakatokea yaliyotokea.

Wakati tukiendelea kuongea Inspekta John akaingia na kutusalimia. Alikuja kunijulia hali na pia kunipa taarifa za walipofikia kwenye upelelezi wao. Alisema kuwa melezo yangu yaliwasaidia kuwakamata watu watatu, na lile Land Cruiser Pick-up lililotumika kwenye lile tukio lilikuwa linashikiliwa kituo cha polisi, baada ya watu kulitambua.

Pia alisema kwamba bado walikuwa wanaendelea na msako mkali wa kuwatafuta wahusika wengine ambao waliamini wamekimbilia Bukoba na pengine wakiwa na mpango wa kukimbilia nchi jirani ya Uganda.

“Hata hivyo, hatuwezi kusema zaidi jinsi tunavyopata taarifa zetu kwa sababu ni mambo ya ndani sana ya kiuchunguzi na kutokana na matukio yenyewe kuwa nyeti sana. Lakini pia tumegundua kulikuwa na ajenda fulani nyuma ya mauaji haya,” aliniambia Inspekta John.

“Kwa kifupi, tunataka kila shambulio la umwagaji damu ya mtu yeyote uchunguzi wake uwe ni mkubwa zaidi kuliko matukio mengine tunayoyafanya kikawaida,” aliongeza Inspekta John.

Nilibetua kichwa changu kukubaliana naye bila kuongeza neno lolote, kisha nilishusha pumzi za ndani kwa ndani huku nikiegemeza kichwa changu vizuri kwenye mto. Hata hivyo nilitamani sana kumuuliza kama alikuwa ana taarifa zozote za yule mrembo ‘the most wanted’ lakini niliogopa kwa kuwa mle ndani sikuwa peke yangu bali pia walikuwemo Mama, Dk. Mpogolo na mumewe.

Kilichonisikitisha zaidi ni kwamba muda wote tangu nilipolazwa pale hospitali sikuwahi kumtia machoni ‘the most wanted’, hata siku moja, ingawa nilikuwa nimejitolea maisha yangu kumwokoa katika tukio lile baya la mauaji. Inamaana alikuwa amenisahau kabisa au labda hakuona umuhimu wa kujua afya yangu!

* * *

Itaendelea...
 
narudi buzwagi.jpeg

85

Dah… Amenasa!


Saa 4:30 asubuhi…

NILISHTUKA toka usingizini baada ya kitasa cha mlango wa chumba changu kuzungushwa taratibu na mlango kufunguliwa kisha ukasukumwa taratibu kwa ndani. Nilikuwa nimeanza kunyemelewa na usingizi muda mfupi tu baada ya jamaa zangu kunijulia hali na kuelekea kwenye shughuli zao.

Kitendo cha mlango kufunguliwa kikanifanya nihisi huenda alikuwa nesi Hilda alikuwa anaingia zamu ya asubuhi, na hivyo alikuja kunisalimia. Niligeuza shingo yangu taratibu kuangalia mlangoni huku nikitabasamu kumuona Hilda kwani kwa wiki nzima niliyolazwa pale hospitali tulijikuta tukizoeana sana, alikuwa hakosi kuja chumbani kwangu kupiga stori. Hata hivyo, hilo halikutokea na badala yake mbele yangu nikajikuta nikikabiliana na mshtuko usioelezeka.

Nilimwona Amanda akiingia taratibu mle ndani huku akiwa mwenye wasiwasi. Kwa sekunde kadhaa macho yangu yalikataa kabisa kuamini kuwa taswira ya mrembo niliyekuwa nikimwona mbele yangu alikuwa Amanda. Alikuwa katika mwonekano tofauti kabisa wa kupendeza ulioichanganya akili yangu na kuamsha hisia zisizoelezeka.

Amanda alikuwa amevaa fulana nyepesi ya rangi ya maruni iliyoyahifadhi matiti yake ya wastani yenye chuchu nyeusi imara zilizosimama kikamilifu zikitishia kuitoboa, na chini alivaa sketi fupi ya rangi ya maruni iliyoifichua hazina ya kupendeza ya mapaja yake maang’avu yenye mvuto wa ajabu. Miguuni alivaa raba nzuri nyeusi za kike.

Kichwani alikuwa amevaa kofia ya rangi ya maruni aina ya kapelo na kubeba mkoba mzuri wa rangi nyeusi, nyusi na kope zake alikuwa amezitinda vizuri na kuzipaka rangi nyeusi ya wanja iliyoyafanya macho yake makubwa na legevu yazidi kupendeza.

Amanda alisimama mlangoni akiniangalia kwa wasiwasi, nikataka kumwambia asogee pale kitandani nilipolala lakini nilipokumbuka kile alichonifanyia kule Ushirombo ghafla nilijikuta nikipandwa na hasira.

“Amanda, umesahau nini kwangu?” nilimuuliza kwa hasira. Amanda alibaki kimya kisha akainamisha uso wake chini, machozi yalikuwa yanamlengalenga machoni.

“Nakuuliza, umesahau nini kwangu? Unalialia nini, hebu nitolee unafiki wako hapa! Rudi kwa huyohuyo mwanamume wako,” nilifoka huku nikitaka kuinuka nimzabe makofi.

“Jason, najua hufurahishwi na ujio wangu hapa, naomba uniruhusu nikujulie hali tu kisha nitaondoka…” Amanda alisema kwa sauti tulivu yenye kitetemeshi huku akifuta machozi. “Hata hivyo, bado nakupenda na ninatamani kuendelea kuona tabasamu lako tena. Kwa nini unanifanyia hivi?”

“Nakuomba uondoke, kwa sasa mimi si yule Jason uliyemfahamu. Mimi ni mpya na unajua kila kitu… unafahamu tulikuwa na malengo gani, unajua tulikubaliana nini. Sasa angalia… kila kitu kimebadilika! Kila kitu kimeharibika! Unawezaje kuja hapa na kudai eti bado unanipenda?” niliendelea kufoka huku nikijiinua toka pale kitandani na kuketi.

“Najua sina tena thamani kwako. Hata nikikueleza vipi bado huwezi kuniamini ila elewa tu kuwa nimeshindwa kuendelea kuigiza kwa yule mwanamume. Nimemwambia ukweli kuwa wewe ndiye chaguo langu na sasa maisha yangu yamebadilika kabisa tangu siku ile,” Amanda alisema kwa sauti iliyojaa uchungu moyoni. Kisha akanisogelea pale kitandani na kupiga magoti mbele yangu.

“Jason, nakosa hata neno la kusema. Nashindwa nikwambie kitu gani cha kuweza kulifuta doa nililoliweka moyoni mwako kwa tamaa zangu. Najua nimekuumiza sana Jason, na sistahili hata huruma yako. Lakini pamoja na hayo yote naomba ufahamu kitu kimoja, toka ndani ya moyo wangu bado nakupenda sana na ninaomba msamaha wako. Mimi sitajali kama una wanawake wengine, nitakuvumilia na kukupenda kwa dhati, naahidi sitafanya tena kosa kama lile katika maisha yangu…” Amanda alisema kwa uchungu kisha akaanza kulia kilio cha kwikwi.

Nilitamani kumsukuma lakini nikasita, nilijikuta nashikwa na huruma. Hata hivvyo, nilijiuliza mara mbili mbili kama ni kweli nilipaswa kumsamehe! Amanda aliendelea kulia kama mtoto mdogo. Machozi yalitiririka masavuni kwake. Niliweza kuyaona vizuri machozi yake. Alikuwa analilia mapenzi na alionekana hakuwa tayari kuishi bila mimi.

Nikajiuliza kama nilikuwa tayari kumsamehe na kurudia uhusiano, na vipi kuhusu Rehema? Nikajikuta nikichanganyikiwa sana. Nilikuwa njia panda nikiwa sijui nifanye nini, sikutaka kumuumiza zaidi Amanda kwa kuwa alikuwa amekiri kosa lake, lakini pia sikuwa tayari kuumiza hisia za Rehema, mwanamke aliyenivumilia kwa mengi licha ya kujua kuwa nilikuwa na uhusiano na Amanda. Hata hivyo moyo wangu uliniambia kwamba nilitakiwa kuwa makini nisije nikafanya tena kosa.

“Jason, mpenzi wangu…” Amanda aliniita.

“Mimi si mpenzi wako tena na wala maneno yako hayatakuwa na maana yoyote kwa sasa,” nilimwambia Amanda huku nikijitahidi kuyazuia machozi yangu.

“Sawa lakini naomba nisikilize kwanza, mpenzi…” Amanda alisema huku akivuta kamasi zilizotokana na kulia.

“Amanda, najua unaweza sana kuongea. Najua ulivyo na maneno matamu ya ushawishi. Ninachokuomba kama kweli unanipenda, basi niache nipumzike. Sitaki tena kuumizwa kihisia,” nilimwambia Amanda kwa sauti tulivu.

“Ujue unaniachia mateso makubwa sana ya moyo kama hautanisamehe. Nimejaribu kukutoa moyoni mwangu sijui kwa nini nimeshindwa! Sina amani hata kidogo. Nisamehe na ninakuahidi sitakusaliti tena,” Amanda alisema kwa huzuni huku akipangusa machozi kwa kitambaa laini.

“Siwezi na sifikirii tena kuwa na uhusiano na wewe kwa sababu hivi karibuni nitaoa…” nilimwambia Amanda huku nikishusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Unasema kweli?” Amanda aliuliza kama aliyepungukiwa na akili.

“Kweli kabisa! Wala sikutanii.”

“Hata kama unaoa, kwa nini hutaki kunisamehe?”

“Nimekusamehe lakini siwezi tena kuwa na wewe. Nafanya hivi kwa sababu nzuri kabisa ili tusije kuumizana baadaye.” Nilimwambia kwa sauti tulivu. “Naomba uondoke kabla Mama yangu hajakukuta humu ndani maana nitakosa majibu ya kumpa.”

Amanda alinyamaza kwa muda na kuinamisha kichwa chake, akawa anatafakari huku machozi yakiendelea kumtoka. Sikujua alikuwa anawaza nini. Pamoja na yote, bado nilijikuta naguswa sana na machozi yake. Ni kweli nilikuwa nimemsamehe lakini moyo wangu ulisita sana kurudiana naye, hasa baada ya maongezi yangu na Rehema. Kisha Amanda aliinua uso wake kuniangalia.

“Jason!” Amanda aliniita.

“Unasemaje?” nilimuuliza huku nikimwangalia kwa umakini.

“Sikiliza maneno yangu.”

“Nakusikiliza.”

“Tazama macho yangu…”

“Nayaona.”

“Unaona nini?”

“Machozi.”

“Machozi yapo kweli, hakuna kingine unachokiona zaidi ya machozi?”

“Sioni kingine zaidi ya machozi.”

“Angalia kwa makini Jason,” Amanda akasisitiza.

Nilijua anamaanisha nini lakini nikajifanya naangalia kwa umakini huku nikiwa sioni kitu! Nikatingisha kichwa changu taratibu.

“Bado hujaona tu?” Amanda akaniuliza tena huku akiniangalia usoni.

“Sioni kitu labda uniambie kuna nini!” nilimwambia huku nikiminya midomo yangu.

“Najua ni jinsi gani umeumia moyoni baada ya kile kilichotokea Ushirombo. Hata mimi nimeumia pia. Najua sikupaswa kuusogeza tena uso wangu mbele yako lakini kinachonifanya niwe hapa karibu yako ni moyo wangu ambao hauna furaha bila ya kukuona… Jason, nakupenda sana… nakupenda kuliko unavyoweza kufikiria. Kwa moyo wangu wote… naomba uniruhusu nikuoneshe ni kwa kiasi gani nakupenda,” Amanda alisema kwa uchungu, machozi yalikuwa yanamtiririka.

Itaendelea...
 
narudi buzwagi.jpeg

86

Nilitulia kwa muda nikawa namwangalia kwa umakini, nikajikuta katika lindi fupi la mawazo nikizikumbuka nyakati za furaha kati yangu na Amanda hadi siku nilipomkuta Migombani Club akiwa na mwanamume mwingine.

Nikiwa bado katika mawazo Amanda aliinuka taratibu, akaniinamia pale kitandani nilipoketi, akanibusu mdomoni na kupenyeza ulimi wake kinywani mwangu, sasa tukajikuta tukikutanisha ndimi zetu. Kwa kasi ya ajabu, nilihisi msisimko wa ajabu nikamvutia kifuani kwangu pasipo kujali maumivu ya mguu wangu, akaja mzimamzima! Tukajibwaga juu ya kitanda.

Sikuwa tena na uwezo wa kuendelea kupingana na hisia zangu ila nilitaka kuona kitakachofanywa na Amanda. Mwanamke huyo alikuwa na busu za ajabu zilizosisimua mno. Mwili wangu ulikuwa unazizima kwa ashki. Hata hivyo sauti fulani ilinikumbusha kuhusu nadhiri yangu kwa Rehema, nikataka kumtoa Amanda kifuani kwangu, akanidhibiti. Haikuwa rahisi kabisa kumtoa.

“Usinikatili mpenzi,” Amanda alilalama.

“Lakini si hapa, watu wanaweza kuingia wakati wowote. Pia kumbuka bado naumwa,” nilimtahadharisha lakini hakutaka kunielewa.

“Nimekuelewa Jason lakini naomba uelewe kuwa siwezi kukuacha. Tafadhali naomba uthibitishe kuwa hutaniacha.”

“Hata mimi siwezi kukuacha,” nilijikuta naropoka. Hata hivyo nilihisi moyo wangu ukiingiwa na ubaridi kama wa maji ya barafu. Sikutegemea kama ningeuruhusu tena moyo wangu kumkubali Amanda. Mapenzi yake yalianza kunichanganya.

Tukiwa bado katika hali ile mikono yangu ilianza kutambaa kwenye mwili wake, mara tukahisi kama nyayo za mtu zilikuwa zinakuja kwenye mlango wa chumba chetu, tukashtuka! Amanda akajitoa haraka juu yangu na kusimama kando, macho yalikuwa yametuwiva na kuwa mekundu kwa ashki.

Sekunde zilizofuatia mlango wa chumba changu ukafunguliwa. Selemani aliingia ndani na alionekana kama mtu aliyekuwa na haraka. Alipomwona Amanda akashtuka kidogo, aliniangalia kwa macho ya tabasamu huku akinikonyeza.

“Karibu?” nilimkaribisha Selemani baada ya kumwona amezubaa akimtupia jicho la wizi Amanda.

Selemani alijishtukia akamsalimia Amanda kisha akasogea pale kitandani kwangu na kuketi juu ya kitanda kando yangu.

“Nadhani tumeshamalizana, unaweza kwenda na uwasalimie Ushirombo,” nilimwambia Amanda huku nikimwangalia usoni.

“Siendi tena Ushirombo. Nitakwenda sehemu ambayo sitaki mtu yeyote afahamu na huko nitajaribu kusahau yote ingawa sijui kama nitaweza,” Amanda alisema na kumtupia jicho la wizi Selemani kisha akalazimisha tabasamu. Taratibu aligeuka na kufungua mlango, akatoka na kwenda zake.

Selemani alimsindikiza kwa macho hadi alipotoka kisha akayahamishia macho yake kwangu huku akiachia tabasamu, nami nilitabasamu ila sikusema neno. Kikapita kitambo kifupi cha ukimya, kila mmoja wetu akionekana kutafakari.

“Naona mambo yako. Vipi ndo shemeji yetu nini!” Selemani alivunja ukimya. Nilitingisha kichwa changu taratibu kukataa.

“Alikuwa shemeji yenu lakini kwa sasa hatupo pamoja baada ya jamaa fulani kuingilia kati, na mimi tayari nina mtu wangu,” nilimwambia kwa sauti tulivu.

“Kwa hiyo alikuja kufanya nini?”

“Alikuja kunijulia hali baada ya kupata taarifa, si unajua hatujaachana kwa uhasama!”

“Dah, ila ndugu yangu unajua kulenga… mwanamke wa ukweli, unaweza hata kujikuta unatelekeza familia!” Selemani alisema huku akiachia kicheko hafifu. Nilitabasamu pasipo kusema neno.

“Enhe, unaendeleaje?” Selemani aliuliza huku akiniuangalia mguu wangu kwa makini.

“Naendelea vizuri, madaktari wanaangalia uwezekano wa kuniruhusu kesho ili nikaugulie nyumbani, maana yale maumivu makali ya mguu yamepungua tofauti na ulivyonikuta juzi,” nilimwambia Selemani huku nikijiweka vizuri pale kitandani.

“Nashukuru kama unaendelea vyema, leo mimi si mkaaji, nimeruhusiwa na nesi kukuona mara moja tu kwani nakwenda kushughulikia hati yangu ya kusafiria, na kama Mungu akinijaalia nitasafiri mwezi ujao kwenda Omani,” Selemani alisema huku akiinuka.

Okay!” nilisema kwa utulivu.

“Hivi una gari?” Selemani aliniuliza huku akiniangalia usoni.

“Sina.”

“Hujawahi kufikiria kumiliki gari?” Selemani aliniuliza tena.

“Hakuna asiyependa kumiliki gari, ila wakati mwingine unajikuta ukiwa na mambo mengi ya kufanya na kushindwa uanze na kipi kwanza. Lakini Mungu akinijaalia mwakani nitakuwa na gari,” nilimwambia Selemani huku tabasamu likiumbika vizuri usoni mwangu.

“Kama mambo yangu yatakwenda vizuri nadhani nitakuletea zawadi ya gari. Sijui utapenda gari aina gani?” Selemani aliniuliza swali lililonifanya kupigwa butwaa kidogo.

“Zawadi ni zawadi tu, yoyote utakayoona inanifaa nitapokea,” nilimwambia huku moyo wangu ukiingiwa na furaha.

“Basi tuombe uzima,” Selemani alisema kisha aliitazama saa yake na kushtuka. “Ngoja nikuache, tutawasiliana.”

“Ahsante sana kwa kuja kunijulia hali. Wasalimie wote nyumbani,” nilimshukuru Selemani huku nikinyoosha mkono wangu kumpa, “Nakutakia kila la kheri ufanikiwe katika mipango yako yote.”

“Ahsante sana, na wewe Mungu akuponye haraka. Tutaonana panapo majaaliwa,” Selemani alisema na kunyoosha mkono wake kunipa, kisha akanishika begani katika namna ya kunitoa hofu juu yake na kuanza kuzitupa hatua zake kwa utulivu kuelekea mlangoni.

Aliufungua mlango na kabla hajatoka aligeuza shingo yake kuniangalia kisha akaachia tabasamu la kunifariji na kisha akatoka. Nilibakia nikiwa natafakari kuhusu lile tukio la mauaji kule porini. Nilijiuliza ni nini kilichokuwa nyuma ya yale mauaji. Je, ni kweli yalikuwa mauaji yaliyobeba kisasi? Ujambazi? Na kama si ya kisasi wala ujambazi basi yalibeba ajenda gani?

Nilikosa majibu nikaamua kuachana na mawazo yale, na hapo mawazo yangu yakahamia kwenye kuifikiria zawadi ya gari niliyoahidiwa na kisha Selemani. Nilikuwa nimepanga kununua gari lakini kwa kuwa Selemani aliahidi kuniletea nilitakiwa kusubiri kwanza.

Wakati nikitafakari mara nikahisi mlango wa chumba changu ukifunguliwa tena, akaingia nesi Hilda akiwa ameongozana na dada mmoja mrefu kiasi, si mnene wala mwembamba na alikuwa amevaa baibui la ninja lililombakisha macho tu, na miguuni alivaa sendoz nzuri za kike za ngozi halisi.

Kwa mwonekano wa harakaharaka tu nilitambua kuwa alikuwa binti wa Kiarabu. Nikajikuta nikipatwa na mshtuko mkubwa. Akili yangu ikanituma kuwa huyo ni Rahma, mwanamke wa Kiarabu ambaye habari zake ziliandikwa kwenye mkasa uliopewa jina la ‘Safari ya Buzwagi’. Ni mwanamke niliyemchukua siku moja Tabora nikiwa nimelewa na nisitambue nini kiliendelea baada ya kwenda naye nyumbani kwangu, wakati huo nilikuwa naishi Ng’ambo, Tabora.

Nikahisi ubaridi wa aina yake ukinitambaa mwilini na mapigo ya moyo wangu yakaanza kwenda mbio isivyo kawaida! Nilibaki mdomo wazi nikimkodolea macho yule dada wa Kiarabu aliyevaa baibui, yeye alisimama akiniangalia kama ambaye hakuamini macho yake. Nilihisi machozi yalikuwa yakimtoka.

Itaendelea...
 
narudi buzwagi.jpeg

87

“Shikamoo, kaka Jason!” yule msichana wa Kiarabu aliniamkia kwa sauti nyororo ya chini lakini iliyopenya vyema kwenye ngoma za masikio yangu. Hata hivyo, sauti yake ilikuwa ya huzuni yenye mtetemo.

Nikapigwa na butwaa. Ilikuwa ni sauti niliyoijua vyema lakini haikuwa ya Rahma! Ni nani? Nikashindwa kubashiri na hapo nikahisi pumzi zikinipaa taratibu.

“Marhaba… karibu!” nilimjibu huku nikiwa na mashaka kidogo. “Za nyumbani?” niliongeza nikitaka nimsikie tena.

“Salama tu, hofu ni kwako,” alinijibu huku akilifungua lile baibui na kunifanya niingiwe na mshtuko mkubwa zaidi. “Naona unajiuliza huyu ni nani?” Jamila alisema baada ya kugundua kuwa sikuwa nimemfahamu hadi muda huo.

“Jamila!” nilijikuta nikiita kwa sauti ya chini sana iliyojaa mshangao mkubwa. Jamila alikuwa katika mwonekano wa kupendeza mno ulioichanganya zaidi akili yangu na kuamsha hisia zisizoelezeka mwilini mwangu na kunifanya kuyasahau kabisa maumivu niliyokuwa nayo. Nilimkodolea macho huku nikibabaishwa na harufu nzuri ya manukato aliyojipulizia mwilini mwake.

Nilimwangalia Jamila kwa makini nikiwa siamini macho yangu, nilihisi yote niliyokuwa nikiyaona yalikuwa yakitendeka wakati nikiwa nipo ndotoni. Tuliendelea kutazamana kwa kitambo kirefu huku kila mmoja akionesha hisia za furaha kwa mwenzake. Macho yake yalishindwa kuficha furaha kubwa aliyokuwa nayo. Huku machozi yakiendelewa kumtoka, alitoa kitambaa laini na kuyafuta machozi.

Alitaka kusema neno lakini akasita na kumtupia jicho Hilda kabla hajayarudisha macho yake kwangu, tukaendeelea kuangaliana kwa kitambo huku nikihishi shughuli za mwili wangu zikisimama kwa muda na macho yangu yakikataa kabisa kuamini kama taswira ya mrombo aliyesimama mbele yangu alikuwa Jamila.

Nesi Hilda alimtupia jicho Jamila kisha akaniangalia na kuachia tabasamu.

“Binti, una dakika tano tu za kusalimia maana muda huu si wa kuona wagonjwa,” Hilda alimwambia Jamila kisha akanikonyeza na kuondoka akituacha wawili.

“Jamila!” nilimwita kwa sauti ya chini huku nikishindwa kuificha furaha yangu. Nilitamani kuinuka kutoka pale kitandani ili nimkumbatie.

“Jason!” Jamila naye aliniita kisha alipiga hatua zake za ki-miss kwa madaha na taratibu hadi pale kitandani nilipokuwa nimejilaza, huku mtikisiko wa umbo lake zuri la kike ukizimeza haraka hisia zangu. Alifika pale kitandani na kuinama, akanibusu kwenye paji langu la uso huku akitokwa na machozi ya furaha.

Kisha aliketi pale kitandani kando yangu akaniangalia kwa tabasamu jepesi la matumaini huku akinipa pole. “Pole sana, Jason…” alisema na kushusha pumzi ndefu. “Nilipooneshwa picha za watu waliouawa kwa kweli sikuamini kabisa kama wewe ulisalimika…” Jamila aliniuliza kwa shauku baada ya kitambo huku tukiangaliana kwa hisia.

Nilishusha pumzi za ndani kwa ndani kisha nikafumba macho yangu kujaribu kulifikiria lile tukio la mauaji kule porini.

“We acha tu, kwa kweli ulikuwa unyama wa kutisha ambao sijawahi kuushuhudia katika maisha yangu, siamini kama bado nipo hai!” nilimwambia Jamila huku nikivishikashika taratibu vidole vyake vya mkononi, hali iliyomfanya azidi kutabasamu na kufuta machozi ya furaha kwa mgongo wa kiganja chake.

“Kaka Sele ametusimulia, kwa nilivyosikia ni vigumu sana kuamini kama uliokoka, Mungu tu ndiye wa kumshukuru,” Jamila alisema kwa utulivu huku akitabasamu.

Ukimya kidogo ukapita huku kila mmoja akizama kwenye tafakuri, Jamila alionekana kuwaza mbali na mimi nilikuwa nawaza juu ya mambo yote yaliyotokea tangu nilipoondoka kule Ushirombo kisha nikakutana na Selemani na kupewa lifti, hadi tulipoachana pale Masumbwe.

“Unajisikiaje kwa sasa?” Jamila akavunja ule ukimya.

“Kwa sasa najisikia nafuu zaidi hasa nilipokuona. Natamani waniruhusu twende nyumbani,” nilimwambia Jamila kwa utani kisha nikaachia kicheko hafifu.

“Usikonde, nipo kwa ajili yako, naamini sasa utapona kabisa!” Jamila naye alisema kwa utani huku akiachia kicheko hafifu.

“Halafu, muda mfupi tu uliopita kaka yako alikuwa hapa,” nilimwambia Jamila huku nikimwangalia usoni. Jamila alivuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu huku akiachia tabasamu.

“Najua,” Jamila alinijibu kwa kifupi. Jibu lake lilinifanya nishangae kidogo.

“Na yeye anajua kuwa umekuja kunitembelea?” nilimuuliza huku nikiwa bado namtazama kwa mshangao.

Jamila alitingisha kichwa chake kukataa kisha akasema jambo lililozidisha mshangao wangu. “Hajui chochote kuhusu uwepo wangu hapa na wala sitaki ajue.”

“Sasa umeaga vipi nyumbani?” nilizidi kumdodosa Jamila kwa mshangao.

“Mmh! Mbona maswali mengi kama polisi?” Jamila aliniuliza huku akikunja ndita usoni kwake.

“Kwani kuna ubaya wowote kutaka kujua?” nilimuuliza huku nikitabasamu. “Nina uhakika kaka yako hawezi kukuruhusu kuja kuniona, hata kwa dawa…”

“Umejuaje?” Jamila alidakia huku akiniangalia kwa mshangao.

“Mimi ni mtu mzima, nilichokishuhudia siku ile ndani ya gari pale Masumbwe kilitosha kabisa kunionesha ni kwa kiwango gani Selemani hapendi uwe huru kuongea mwanamume yeyote,” nilimwambia Jamila huku nikijiweka vyema pale kitandani.

Jamila aliniangalia kwa kitambo pasipo kusema neno, alionekana kuwaza jambo, ilionekana maneno yangu yalikuwa na ukweli fulani.

“Ni kweli. Kaka Sele hawezi kuniruhusu lakini kwa sasa mimi nipo hapa Kahama, eneo la Nyasubi kwa shangazi,” Jamila alisema na kunifanya nizidi kushangaa.

“Upo Nyasubi! Umekuja kufanya nini wakati unatakiwa ukae ndani kusubiri ndoa?” nilimuuliza nikizidi kushangaa.

“Kwani hujui kuwa Shangazi ndiyo somo wangu? Shangazi ndiyo kungwi wangu aliyekabidhiwa kunifunda. Unadhani nilipoomba namba yako ilikuwa ni kwa ajili ya nini?” Jamila aliniuliza huku akiachia tabasamu.

“Nilijua kuwa sitamaliza siku mbili lazima nije Kahama na nilipanga nikifika tu nikutafute. Ila sikujua kama haya yangetokea. Nilipopata taarifa za mauaji nilichanganyikiwa sana, sikuweza kula siku mbili na kila nilipokupigia simu ulikuwa hupatikani,” Jamila alisema kwa huzuni. Niliendelea kushangaa.

“Namshukuru sana Shangazi, alinitia moyo na bahati nzuri, yeye ni tofauti na mama au kaka Sele, anathamini hisia zangu na ndiye ameniruhusu kwa siri kuja kukuona,” Jamila alimaliza na kushusha pumzi ndefu.

“Sasa umejuaje kuwa nipo hapa?” nilimuuliza Jamila huku mshangao ukiwa bado haujanitoka.

“Kaka Sele alipita kwa Shangazi akamweleza kuwa anakwenda kumwona rafiki yake kalazwa wodi maalumu ya VIP namba mbili katika Hospitali ya Wilaya. Nilimfuata kwa siri na alipokuwa humu nilikuwa nimejificha hapo nje nikisubiri atoke na mimi niingie,” Jamila alisema huku akitabasamu.

Nilishangazwa sana na maneno ya Jamila, eti alishindwa kula kwa sabau yangu! Kitambo kifupi cha ukimya kikapita ndani ya kile chumba kila mmoja akiwaza lake kisha Jamila akakohoa kidogo kurekebisha sauti yake.

Itaendelea...
 
narudi buzwagi.jpeg

88

“Jason, kuna jambo nataka kuongea nawe, sijui unaniruhusu?” Jamila aliniuliza huku akionesha wasiwasi kidogo.

Yeah! Unaweza kuongea. Kuna nini?” nilimuuliza Jamila huku nikiachia tabasamu pana ambalo niliamini lilimchanganya sana Jamila, maana aliduwaa kwa sekunde kadhaa.

“Sina namna isipokuwa kuongea nawe, leo hii,” Jamila aliniambia huku akiminya midomo yake.

“Kuongea na mimi! Kuhusu nini?” nilimuuliza huku nikianza kushangaa.

“Mahusiano,” Jamila alinijibu huku kwa mbali nikikiona kijasho chembamba cha uoga kikianza kumtoka na kilionekana usoni kwake. Nilishtuka kidogo lakini nikajikausha.

“Mahusiano gani?” niliuliza nikijifanya sielewi alichokimaanisha.

Jamila aliinamisha uso wake kuangalia chini kwa aibu, akakaa kimya kwa muda, swali ambalo nilikuwa nimemuuliza lilikuwa jepesi sana kujibika lakini, kwa mtoto wa kike, kulitoa jibu lake lilihitaji ujasiri wa hali ya juu. Niliiona hali ya uoga ikizidi kumwingia zaidi. Sikujua kuhusu mapigo yake ya moyo, nilihisi kuwa pia yalikuwa yanadunda kwa kasi zaidi, na ujasiri wote ambao alikuja nao ukaanza kupotea.

“Jamila” nilimwita baada ya kuona yupo kimya kwa kitambo kirefu.

“Abee!” Jamila aliitika huku akiniangalia kwa jicho la wizi, aliogopa kukutanisha macho yake na yangu.

“Mbona hauongei tena?” nilimuuliza huku nikiyatuliza macho yangu usoni kwake. Tabasamu liliupamba uso wangu.

“Najaribu kukufikiria kidogo,” Jamila alinijibu kwa sauti ya chini yenye kitetemeshi.

“Kunifikiria?” nilimuuliza kwa udadisi. Japo nilishajua Jamila alitaka kusema nini lakini niliamua kumchimba ili nione kama angekuwa na ujasiri wa kutamka.

“Ndiyo.”

“Kunifikiria kuhusu nini?”

“Uwezo wako wa kusoma hisia za mtu,” Jamila alijibu huku akiangalia chini kwa aibu aliendelea kuyakwepa macho yangu.

“Ah… au nitakwambia siku nyingine, muda niliopewa umeisha,” Jamila aliniambia huku akiinuka toka pale kitandani kisha akaanza kupiga zake taratibu kwa mwendo wa madaha.

“Jamila!” nilimwita, akageuka kunitazama. “Niambie leo kwani linalowezekana leo lisingoje kesho.”

“Jason! Kiukweli nashindwa hata nikuambieje!” Jamila alianza kujieleza huku akijitahidi kutabasamu.

“We sema tu, n’taelewa!” nilimwambia kwa sauti tulivu nikimpa moyo. Aliniangalia kwa kitambo kasha alianza kupepesa macho yake pembeni huku akitabasamu kwa aibu.

“Jason, unaona nini kwenye macho yangu?” Jamila aliniuliza swali lililonifanya nishtuke sana, nikajiuliza kama yeye na Amanda walipanga kuja kuniuliza swali lile!

“Sioni kitu!” nilijibu kwa kifupi.

Jamila aliinamisha kichwa chake chini huku akionekana kukosa raha, tabasamu lake lilififia na kupotea. Nilidhani alihisi ugumu wa kutamka alichokusudia. Niligundua lakini bado nilijifanya sielewi.

“Kwani wewe unaona nini kwenye macho yangu?” nilimuuliza Jamila baada ya kuona kimya kwa muda mrefu.

Jamila alinitazama bila kuzungumza chochote. Sikuiona tashwishwi yoyote usoni kwake, bila shaka alikuwa ameshachukia au amekwazika na majibu yangu na hivyo aliona bora anyamaze huenda ingemsaidia.

“Niambie tu Jamila, naona kama unazungukazunguka tu, sikuelewi!” nilivunja ukimya huku nikiachia tabasamu.

“Jason! Unanikatisha tamaa!” Jamila alizungumza kwa sauti iliyojaa hisia lakini iliyoonesha kukata tamaa baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu.

“Nakukatisha tamaa kivipi?”

“Wewe huoni?”

Nilitabasamu kidogo kisha nikaachia kicheko hafifu. Sikujua kuwa kicheko kile kilimwongezea hasira Jamila. Alishika kitasa cha mlango akitaka kuondoka lakini alipokuwa katika kuufungua ule mlango nikamuwahi tena.

“Jamila, tafadhali usiondoke. Naomba basi unidokezee tu kama hauko tayari kuniambia!” nilisisitiza.

“Jason moyo wangu umekuchagua wewe,” Jamila alisema kwa sauti ya chini ya kunong’ona huku akiyakwepa macho yangu kwa aibu.

“Umee… sijasikia vizuri! Moyo wako umefanya nini?” nilimuuliza kana kwamba sijasikia vizuri.

“Kwa kifupi, nakupenda Jason,” Jamila aliongea tena kwa sauti ya chini ya kunong’ona.

Nilibaki kimya nikiwa siamini kama kweli Jamila aliamua kujilipua. Nilijiuliza ningefanyaje kwani nilishaamua kubadilisha mwenendo wa maisha yangu? Ni kweli Jamila alikuwa msichana mzuri sana na kila mwanamume angetamani kummiliki lakini alikuwa dada wa rafiki yangu na pia alikuwa mbioni kuolewa.

“Mbona uko kimya?” Jamila aliniuliza na kunizindua toka katika mawazo.

“Nashindwa nikujibu vipi Jamila!” nilimwambia kwa sauti tulivu.

“Kama huna jibu basi!” Jamila alisema na kufungua mlango, akachungulia nje na kuyarudisha macho yake ndani kuniangalia. Nikayaona macho yake yalikuwa yanalengwa na machozi. Hata hivyo, katikati ya machozi yale aliachia tabasamu lililobeba uchungu na kunipiga busu la hewani, kisha akatoka haraka na kuufunga mlango na kuniacha nikiwa na mshangao.

Maneno na vitendo vyake yalinibainishia kuwa alikuwa amenasa na yu mapenzini. Nilimhurumia sana na sikutegemea kabisa kwa msichana yule kutamka maneno kama yale. Niliyafikiria kwa muda wa zaidi ya dakika mbili, nikakumbuka jicho alilokuwa akiniangalia na kauli yake siku ile nilipopewa lifti na kaka yake.

“Dah… amenasa!” nilijisemea huku uso wangu ukiunda tabasamu pana.

* * *

Itaendelea...
 
narudi buzwagi.jpeg

89

Uwe Mwaminifu.


Saa 5:00 asubuhi…

Ilikuwa ni zaidi ya mwezi tangu lile tukio la mauaji kule porini. Na ilikuwa siku ya tano tu tangu nitoke hospitali kuondolewa ile bandeji ngumu mguuni kwangu, maarufu kama P.O.P. Mguu ulikuwa umepona ingawa bado nilikuwa natembea kwa kuchechemea kidogo, na madaktari walikuwa wamenishauri nisifanye kazi ngumu angalau kwa muda wa miezi mitatu.

Siku hii nilikuwa nimepanga kushinda ndani tu nikifanya kazi zangu na kutizama movie kwenye runinga pana iliyotundikwa ukutani. Ilikuwa ni Jumamosi na nilikuwa nimeketi sebuleni, nyumbani kwangu nikiwa nimevaa bukta na fulana nyepesi tu. Mama alikwisha ondoka kurudi Tabora na niliambiwa kuwa walishaanza mchakato wa kupeleka mahari nyumbani kwa wazazi wa Rehema. Nilishaamua kumuoa Rehema.

Nyumba niliyoishi ilikuwa katika eneo la Mbulu, ilikuwa kubwa ya kuweza kuchukua familia. Ilikuwa ni nyumba kubwa yenye vyumba yenye vitatu, jiko na sebule kubwa yenye kila samani za kisasa yakiwemo makochi mazuri ya ngozi ya sofa, runinga pana kutani na madirisha makubwa yenye kupitisha hewa safi. Mbele ya sebule ile kulikuwa na ukumbi wa chakula wenye meza moja iliyozungukwa na viti sita.

Nyumba hiyo ilikuwa moja kati ya nyumba sita za kisasa zilizokuwa zimejengwa kwa mtindo wa kota zikiwa ndani ya uzio mmoja mpana, si mbali sana kutoka katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi. Nyumba hizo zilikaliwa na wafanyakazi wa daraja la mameneja wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi.

Pale sebuleni nilikuwa natazama filamu ya Nairobi Half Life iliyotengenezwa nchini Kenya, ni filamu ya kwanza ya Kenya kuingizwa kwenye Tuzo za 85 za Oscar ingawa haikufanikiwa kupenya katika filamu 5 za mwisho zilizoingia kwenye kinyang’anyiro.

Filamu ile ilikuwa imenivutia sana, nilimfuatilia kijana tineja, Mwas, kielelezo cha vijana wanaohangaika huku na kule kutafuta maisha mazuri, wakiondoka vijijini kwenda mjini kutafuta kazi. Mwas anajikuta akiingia jijini Nairobi, ambako anagundua kuna mengi zaidi ya kujifunza kuliko fursa na uzuri alioutarajia. Siku ya kwanza tu tangu aingie jijini humo, anapoteza kila kitu na kuishia mahabusu, na huo unakuwa mwanzo wa safari yake ngumu ya kuisaka shilingi…

Nikiwa nimetekwa na stori ya filamu ile nikashtushwa na simu yangu ya mkononi iliyoanza kuita kwa fujo, niliinyanyua na kuitazama kwa makini. Alikuwa Rehema. Niliipokea haraka.

Hi, baby!” nilisema kwa sauti ya mahaba mara tu nilipoiweka kwenye sikio langu.

Hi, uko wapi sweetie?” Rehema aliniuliza kwa sauti iliyoonesha wasiwasi kidogo.

“Nipo home, baby. Kwani vipi?” nilimuuliza kwa mshangao. “Si unajua mguu bado unasumbua, n’takwenda wapi saa hizi!”

“N’tajuaje, maana huaminiki wewe?” Rehema aliongea kwa utani huku akiachia kicheko hafifu.

“Wasiwasi wako tu, mke wangu! Mimi sasa hivi nimeshakua, sitaki tena ujinga.”

“Basi nakuja, nipo njiani. Najua utakuwa umeshapata habari…” Rehema alisema kwa sauti tulivu lakini iliyobeba kitu fulani ndani yake. Nilipomuuliza habari zipi nikagundua kuwa simu ilishakatwa.

Nikabaki na mshangao mkubwa. Sikujua Rehema alikuwa anaongelea habari zipi! Hata hivyo, sikutaka kuumiza kichwa changu kwa kuwa alisema yupo njiani anakuja nyumbani. Nikaamua kusubiri.

Nusu saa baadaye nilisikia muungurumo wa gari huko nje, uliokomea mbele ya nyumba yangu. Nikiwa bado nimeketi pale sebuleni, Rehema aliingia sebuleni huku uso wake ukiwa una mashaka kidogo. Alikuwa amevaa suruali nyeupe ya dengrizi na blauzi nyeusi ya mikono mirefu. Nguo zilikuwa zimempendeza sana kutokana na umbo lake refu lenye kiuno chembamba na tumbo flati.

Miguuni alivaa viatu vyenye vikanyagio virefu vya mchuchumio, bangili nyingi za pembe mkononi na begani alikuwa amening’iniza mkoba mzuri wa nguo ya pundamilia ambao uligharimu fedha nyingi. Alipoingia tu mafuta mazuri aliyojimwagia yalisambaa sebuleni nzima.

Alisimama akaniangalia kwa utulivu mkubwa huku uso wake ukiwa umepambwa na mashaka, kisha alipiga hatua zake taratibu hadi pale kwenye sofa nilipoketi, akaketi kando yangu huku akiendelea kuniangalia kwa mashaka. Mara nyingi Rehema alionekana mwenye furaha sana kila alipokuwa na mimi lakini siku hiyo hali yake ilinichanganya kidogo.

Nilishindwa kuelewa kama alikuwa na furaha au huzuni, au vyote pamoja! Nilichoweza kugundua ni kwamba alionekana kuwa na jambo serious sana alilotaka kunishirikisha. Sikujua ni jambo gani.

“Najua umeshasikia habari…” Rehema alianza kuongea lakini nikamkatisha.

“Habari zipi?” nilimuuliza haraka kwa mshangao huku nikimwangalia usoni.

“Una uhakika hujasikia habari zozote?” Rehema aliniuliza huku akiniangalia kwa umakini machoni akijaribu kuyasoma mawazo yangu.

“Wala! Kwani kuna nini?” nilimuuliza huku mapigo ya moyo wangu yakianza kwenda mbio isivyo kawaida.

Rehema akabaki kimya akiniangalia kwa umakini kwa kitambo kirefu, mara hii niliyaona macho yake yakilengwalengwa na machozi. Kwa kitambo fulani ukimya ulitawala pale sebuleni huku Rehema akionekana kusongwa na mawazo, na mara kwa mara alikuwa anasonya, na sikujua kilichomfanya asonye ni nini! Nikaingia na hofu na moyo wangu ukapiga mshindo mkubwa!

Nilijikuta nikiishiwa nguvu, nikahisi kuwa jambo baya lilikuwa limetokea. Nilimwangalia Rehema kwa umakini zaidi, sasa uvumilivu ulionekana kumshinda na machozi yalianza kumdondoka. Nikamwona akimeza funda la mate. Sikuvumilia tena.

“Baby, kuna nini? Mbona sikuelewi!” nilimuuliza Rehema huku nikimwangalia kwa umakini. “Tangu umekuja husemi kitu, unasonya tu! Naona leo umebadilika kwa kiasi fulani tofauti na kawaida yako,” nilisema huku nikianza kukerwa na hali ile. Rehema aliendelea kuniangalia pasipo kusema neno.

“Unajua nakupenda sana na wewe ni shahidi yangu… ni kweli mwanzo sikuwa serious na uhusiano wetu lakini baadaye nikaitambua thamani yako kwangu na kuachana na mambo yote ya kijinga ili tujenge familia. Unajua kabisa mchakato wa ndoa yetu kwa sasa unakwenda vizuri na ninaahidi kuwa mume bora, usifikiri labda nitageuka…” nilisema kwa sauti iliyoonesha kutetemeka kwa kuingiwa na simanzi.

“Sipendi hali hii na sipendi kukuona katika hali hiyo. Najisikia kuumia sana unapokuwa hivi. Jana tu nimewasiliana na Baba na ameniahidi kuwa kila kitu kipo sawa, labda kama unaona hupendezwi na mambo fulani ni vyema ukayaweka wazi ili…”

“Baby, umefika mbali jamani. Wala mimi sijaja kwa ajili ya hilo na kamwe sitaki tena kukuwazia vibaya,” Rehema alinikata kauli kwa upole kabisa, kisha akaweka kiganja chake shavuni pangu huku akinitazama kwa ukaribu.

“Jason, najua habari hii inaweza kukushtua kidogo, sijui utahuzunika au ndiyo utafurahi… ila nakuomba uelewe, mpezi wangu, sijapenda iwe hivi lakini ndo n’tafanaye!” Rehema aliendelea kusema kwa sauti ya upole kabisa. Nilibaki kimya nikimtumbulia macho.

“Nimeteuliwa kuwa DC… Mkuu wa Wilaya…” Rehema alisema kwa sauti tulivu na kusita kidogo huku akiniangalia kwa wasiwasi kidogo.

“Hongera sana, mke wangu. Sasa hii habari ndiyo inihuzunishe?” nilimuuliza Rehema kwa mshangao lakini sikuiona tashwishwi yoyote usoni kwake. Nikahisi kulikuwa na jambo ambalo hakuwa ameniambia.

“Au kuna jingine zaidi ya habari hii?” nikamuuliza huku nikimkazia macho.

“Ndiyo. Napelekwa kuwa DC wa Misungwi. Nitakuwa mbali zaidi na wewe, mume wangu,” Rehema aliongea huku akiyatuliza macho yake usoni kwangu.

“Dah! Misungwi? Hii sasa si habari nzuri, sijui kama nitapata hata hamu ya kufanya kazi!” nilisema huku nikiwa nimekata tamaa.

Itaendelea...
 
narudi buzwagi.jpeg

90

“Halafu naondoka kesho mapema sana maana Jumatatu ninatakiwa kuapishwa rasmi. Hapa nimechanganyikiwa, sijui kama nifurahie kupandishwa cheo au nihuzunike kuwa mbali na wewe. Unajua hata hatujafika mbali kwenye jambo letu!”

“Mimi nadhani… cha msingi kwanza ni kumshukuru Mungu kakuinua hadi mheshimiwa Rais amekuona. Mambo mengine yapo tu. Mungu ndiye anajua kwani ndiye aliyepanga!” nilimweleza Rehema kwa sauti tulivu baada ya kutafakari kidogo.

“Ahsante, baby kwa maneno yako ya faraja,” Rehema alisema huku akiachia tabasamu. Nami nikatabasamu, lilikuwa tabasamu dogo lililomtia hamu ya kunibusu limwingie akiwa katika mawazo magumu.

Taratibu mkono ulionishika shavu ukatambaa mgongoni kwangu nikahisi kwa mbali joto la vidole vyake, alijisogeza karibu nami tukawa kama mwili mmoja, nilijigeuza nikakutanisha mikono yangu nyuma ya shingo yake na kuisogeza midomo yangu karibu na yake tukakutanisha. Tulibaki hivyo kwa muda nisioweza kukumbuka, mioyo yetu ikidunda na jasho likianza kututoka. Kisha akaniachia.

“Mpenzi!” Rehema alisema, sauti yake ilikuwa ndogo, “Nakuomba usiache kufuatilia jambo letu na uwe mwaminifu. Niahidi hivyo tafadhali.”

“Baby!” niliita, sauti yangu ilikuwa ndogo zaidi na macho yalifunguka nusu tu, “Bila ya wewe sina la kufanya miye. Nakuahidi kuwa mwaminifu. Nakuahidi hivyo, mke wangu,” nilimwambia Rehema, akanibusu tena mdomoni na kuinuka.

“Nashukuru kusikia hivyo, basi naomba uniruhusu niende nikajiandae, nikisha apishwa tu n’tarudi kwanza huku kuweka vitu vyangu sawa kisha tuongee kwa kirefu zaidi,” Rehema alisema kwa sauti tulivu. “Ila kwa lolote lile naomba usinisaliti.”

Moyo wangu ukawa mzito lakini sikuwa na namna. Niliinuka huku nikichechemea kidogo nikamsindikiza kuelekea nje. Pale nje nililikuta gari la dada yake, aina ya Toyota Prado alilopenda kulitumia mara kwa mara alipokuwa Kahama.

Nilisimama pale barazani nikimsindikiza kwa macho huku nikiyatazama maungo yake kwa nyuma. Nikatikisa kichwa changu na kujiaminisha kwamba nilikuwa nimepata mwanamke mzuri aliyenipenda kwa dhati.

Rehema alifika kwenye gari, akafungua mlango lakini kabla hajapanda aligeuza shingo yake kunitazama. Macho yetu yakakutana. Nikayaona matone ya machozi yaliyoanza kuchuruzika ghafla huku macho yake yakibeba ujumbe ambao ulinisisitiza nisiivunje ahadi yetu.

Pale niliposimama nilipumua kwa nguvu kisha nikajiegemeza kichovu kwenye kibaraza nikijaribu kutathmini hali halisi ya maisha yangu na Rehema yalikotoka, yalipo na yalikoelekea, ama kwenye heri au shari.

Mawazo yaliniteka na kunirudisha miaka kadhaa nyuma namna tulivyoanza kufahamiana na hatimaye kuangukia kwenye uhusiano wa kimapenzi. Niliyakumbuka yote, hasa maisha yangu ya ufuska yaliyokuwa yakimuuza zaidi Rehema lakini akawa akinivumilia…

Rehema alikuwa mwanamke wa ajabu kabisa, mwanamke mwenye moyo wa kusamehe hata pale nilipomfanyia kosa kubwa la makusudi, alikasirika lakini hakuchelewea kusamehe na wala hakuweka kisasi rohoni mwake. Tabia yake ya upole, ucheshi na kusamehe ilinifundisha jambo kubwa sana maishani kwangu na safari hii sikutaka kurudia makosa.

Nilikiri kufanya makosa makubwa kudhani kuwa duniani hakukuwa na mapenzi ya kweli. Sikupaswa kumfanyia vile. Rehema alikuwa mwanamke aliyenipenda kwa moyo wake wote na siku zote alikuwa tayari kwa lolote kwa ajili yangu. Kuna wakati nilijitia pambani nikayapuuza yote, nikaupuuza upendo wake kwangu na kuamini kwamba yale yalikuwa maigizo tu na hakukuwa na penzi la kweli… Kumbe duniani kulikuwa na watu wenye upendo wa kweli. Hata hivyo nilikuwa sijachelewa kuyapanga na kuyajenga upya maisha yangu…

Nilipozinduka kutoka kwenye lindi la mawazo sikuliona gari, Rehema alikuwa ameshaondoka na wala sikujua ni muda gani niliutumia nikiwa nimesimama pale kibarazani. Niliingia ndani taratibu na kuketi kwenye sofa huku nikihisi akili yangu imekuwa nzito, nilianza kushindwa hata kufikiri.

* * *

Endelea kufuatilia hadi mwisho...
 
narudi buzwagi.jpeg

92

Nilishindwa kuvumilia, nikamshika mikono yake na kumvutia kifuani kwangu lakini nikakumbuka kitu na kumwachia, nikayaendea madirisha makubwa ya pale sebuleni na kuyashusha pazia kisha nikageuka kumtazama bila ya kusema lolote. Mle ndani kukawa na mwanga hafifu sana. Nilihisi Jamila alikuwa akiniona kama kivuli tu pale nilipokuwa nimesimama.

Taratibu niliivua ile fulana nyepesi niliyovaa nikaitupia kwenye sofa, nikaenda kuketi karibu yake huku nikihisi kijasho chembamba kikinitoka mwilini. Nilimshika na kugandisha midomo yangu kwenye midomo yake. Na hapo nikamuona akiyafumba macho yake na kukunja uso wake kama mtu aliyekuwa anahisi kizunguzungu na kuanza kutokwa na jasho kupita kiasi.

Mara simu yake ikaanza kuita na kutushtua. Jamila alikunja sura yake akionesha kuchukizwa, akanyanyuka na kwenda kuichuka, akaiangalia kwa makini na kukunja sura yake huku akiipokea.

“Eh, Shangazi!” Jamila aliongea akiwa amekunja sura. “Bado nipo hapa hapa ila sitachelewa…”

Alinitupia jicho la mahaba huku akimng’ong’a mtu aliyepo upande wa pili wa ile simu. Alisikiliza kidogo kabla hajakata simu na kuiweka kando na kisha akarudi nilipokuwa nimeketi.

“Shangazi naye!” Jamila alisema huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani. Alikuwa amenuna.

“Kwani anasemaje?”

“Ananitaka nirudi nyumbani haraka kwa kuwa kuna sehemu anataka twende!" Jamila alisema huku akianza kunipapasa kifuani.

“Kwani shangazi yako anajua kuwa upo kwangu?” nilimuuliza Jamila huku moyo wangu ukipiga kite kwa nguvu.

“Ndiyo anajua. Ni yeye aliyenileta hadi hapo nje ya uzio kisha akaondoka,” Jamila aliongea kwa sauti ya chini huku akiangua kicheko kisha akaupeleka ulimi wake kwenye chuchu zangu.

Nilifinya macho yangu kwa raha niliyoisikia, mara nikaanza kuisikia sauti fulani ikinisema. Ilikuwa ni ile sauti niliyoisikia kwa mara ya kwanza Ushirombo nyumbani kwa Rehema, ilikuwa sauti tulivu sana na ya kirafiki lakini iliyoonya. Ilipenya vema masikioni mwangu, ikaanza kuujaza ganzi mwili wangu wote. Mwanzoni ilikuwa ni sauti nisiyoijua lakini taratibu ikaanza kubadilika na sasa nilimsikia Rehema. Sauti yake ilikuwa ndogo yenye kusihi, “Ila kwa lolote lile naomba usinisaliti.”

Nikajikuta nikiwa njia panda. Ni saa chache tu zilizopita Rehema alikuwepo pale nyumbani kwangu na aliyatamka maneno hayo, hata kabla hajaondoka kwenda Misungwi tayari nimeshaingiza mwanamke na kupoteza uaminifu! Je, nilichotaka kukifanya kilikuwa sahihi? Hilo lilikuwa swali la kwanza.

Nikabaki nimekaa kama sanamu pale kwenye sofa huku nikihema kwa nguvu kama simba aliyemkimbiza swala na kumkosa. Jasho lilikuwa linanitoka. Jamila akaniangalia kwa mshangao.

“Jason, kuna tatizo? Mbona kama umenywea ghafla?” Jamila aliniuliza kwa utulivu huku akiniangalia usoni kwa mshangao.

Bila shaka aligundua kuwa kuna niliingiwa na uoga. Hivyo akaona bora afanye kazi ya ziada, aliipitisha mikono yake nyuma ya shingo yangu na kufanya chuchu za matiti yake kukitekenya kifua changu. Joto kali la mwili wake likanifanya nianze kujisikia faraja ya aina yake. Nilipomtazama machoni nikayaona machozi ya furaha yakianza kumtoka.

Jamila alikuwa na kiu ya penzi langu na sikutaka kuamini kuwa nilikuwa mwanamume wake wa kwanza. Kufumba na kufumbua ndimi zetu zikakutana, mkono wake mmoja akaupeleka ikulu na kuanza kunichua taratibu.

Nilitaka kuleta pingamizi kwa vile sauti ya Rehema iliendelea kunisihi nisimsaliti na ilikataa kuondoka akilini kwangu, hata hivyo sikufanikiwa. Kama mtu aliyepandwa na wazimu wa mapenzi Jamila alifanya jambo ambalo sikulitarajia, nilibaki mdomo wazi! Muda mfupi uliofuata tulikuwa kwenye kochi kubwa la sofa pale sebuleni huku kila mmoja akiwa amepandwa na wazimu, tulihama kutoka dunia hii na kwenda katika sayari ya mbali kabisa, sayari ya huba.

Jamila alikuwa mtundu mno na aliyamudu vyema mapenzi na kunifanya nijihisi kama mwanafunzi wa shule ya msingi. Pamoja na ufundi wangu wote bado sikuweza kufua dafu kabisa, alinidhibiti kwa kila idara. Sikudhani kama kungekuwapo mwanamke mwingine ambaye angeweza kumfikia Rehema. Lakini sasa niligundua kosa langu haraka nilipokutana na Jamila.

Jamila alikuwa wa aina ya pekee, mtundu mno na alikuwa amenionesha ulimwengu mpya ambao sikuwa mjuzi kabisa, na aliniachia maswali kibao kuliko majibu, nikijiuliza ni wapi alijifunzia mambo hayo! Kama kungefanyika mashindano kati yake na Rehema, sidhani kama Rehema angefua dafu. Sikuutilia mashaka ukweli huo. Si kwamba Rehema hakuwa mjuzi, alikuwa mjuzi kweli kweli lakini kulikuwa na upekee fulani kwa Jamila kama ungejaribu kuwalinganisha watu hao wawili.

Muda huo tulikuwa tunahema kwa uchovu tukiwa tumekwenda mizunguko mitatu pasipo kupumzika. Nilimtazama Jamila nikiwa siamini kabisa. Nilimshangaa, mambo aliyoyafanya hayakuendana na mwonekano wake na sura yake ya upole ambayo si rahisi kabisa kumdhania. Sasa vidole vyake vilikuwa vinatambaa juu ya kifua changu na ukimya ulikuwa umetawala mle.

“Jason!” Jamila alivunja ukimya.

“Naam Jamila.”

“Nashukuru kwa raha ulizonipa. Nakupenda hadi najihisi kuchanganyikiwa!” Jamila alisema kwa sauti ya kunong’ona. “Na kama ungenikatalia nadhani leo ningekufa kwa kihoro.”

Sikusema kitu, akili yangu ilikuwa haijatulia. Bado sauti ya Rehema ilisikika akilini kwangu ikinilaumu. Nilianza kujilaumu, hata hivyo nilijua kuwa isingesaidia kwani maji yalikwishamwagika na yasingeweza kuzoleka, na hivyo nikaamua kukubaliana na matokeo.

“Tafadhali usiniache mpenzi wangu. Natamani kutoroka nyumbani, tutafute sehemu yoyote duniani ambako watu hawatujui tukaishi…” Jamila alisema huku akinibusu mdomoni.

“Dah… sidhani kama ni jambo zuri…” nilijionya mwenyewe. “Rehema ndiye mwanamke wa maisha yangu, huyu ni mke mtarajiwa wa mtu mwingine na pia ni dada wa rafiki yangu. Yaweza ikawa si vibaya kufanya mapenzi na Jamila lakini si kama anavyotaka…”

Ni kama aliyekuwa akiyasoma mawazo yangu, Jamila aliachia tabasamu pana huku akiniangalia machoni.

“Najua una mtu wako na huenda mko mbioni kuoana. Mimi pia hivi karibuni nitaolewa. Huo ni ukweli unaoniumiza roho, ukweli ambao sina budi niuvumilie. Lakini pamoja na ukweli huo, lazima nikwambie, Jason, nakupenda sana kuliko mwanaume yeyote. Nataka niwe na uhuru wa kuchagua nipendalo kufanya kwako. Nataka nijione wako. Msahau mtu wako nami nimsahau wa kwangu. Tuwaone wote kama hawapo duniani na wasitusumbue lolote…” Jamila alisema kwa sauti ya chini lakini iliyopenya vema kwenye ngoma zangu za masikio.

Ingawa nilikuwa mwanamume jasiri lakini mbele ya Jamila nilijihisi kukosa ujasiri kabisa, nilikuwa kama mbwa muoga mbele ya chatu mwenye njaa kali.

Itaendelea...
 
narudi buzwagi.jpeg

93

“Niwie radhi kama waona nakueleza mambo usiyoyapenda, lakini bila ya hivyo hatutafika mbali na penzi letu,” Jamila aliniambia huku akiinuka kisha akanishika mkono, nami nikainuka. Tukaingia bafuni na baada ya dakika chake Jamila alivaa nguo zake kisha akajifunga ninja yake na kuniaga kwa mabusu motomoto akiahidi kuja tena.

Alifungua mlango akachungulia nje akuzungusha macho huku na kule, alipoona pako shwari akatoka na kwenda zake akiniacha nimesimama katikati ya sebule kama mtu aliyeshikwa na bumbuwazi.

Nilijilaza pale kwenye sofa nikiwa sijui nifanye nini, nilikuwa nimechoka sana. Niliulalia ubavu wa kulia kisha nikayafumba macho yangu nikijaribu kuyapotezea mawazo juu ya Jamila. Nilijidanganya! Mawazo hayakunitoka na wala akili yangu haikuweza kupata utulivu, na badala yake nilijiwa na taswira ambazo zilinifanya nijione nikiwa njia panda, upande mmoja amesimama Rehema na upande wa pili kasimama Jamila, na kila mmoja akiniangalia kwa namna ya kutaka niende kwake.

Taswira hizo zilinichukua mpaka kwenye lindi la mawazo yaliyonifanya niingie katika tafakuri nzito juu ya hatma ya maisha yangu, “Hivi nitaendelea kuwa mtumwa wa ngono mpaka lini?” niliwaza.

Mawazo hayo ndiyo yaliyonifanya nianze kuyafikiria upya maisha yangu, maisha ya kubadilibadili wanawake kila kukicha niliyaona ni kama vile yaliudhihaki umri wangu. Wakati wowote ningetimiza miaka therathini nikiwa sina familia. Mawazo yalizidi kunitafuna zaidi na nilipokuja kushtuka ilikuwa imeshatimia saa 8:30 mchana. Sasa nilianza kuhisi njaa.

Taratibu akili yangu ikaanza kuyasahau yote yaliyotokea na kufikiria kuhusu chakula maana njaa ilikuwa inauma kama kidonda. Pasipo kutafakari mara mbili nikapanga kutoka kwenda kutafuta chakula kizuri na kisha nishushie na mvinyo au bia mbili ili kupoteza mawazo yaliyonisonga.

Nilitoka nje nikaufunga mlango wangu kisha nikaita teksi na kumtaka dereva anipeleke Chattle Restaurant. Huu ulikuwa mgahawa wa kisasa kabisa wenye kila aina ya vionjo vya daraja la kimataifa. Ulikuwa na mandhari yenye ubora yaliyowafanya wageni wengi waliofika Kahama kufika hapo. Ulikuwa kumbi mbili maalumu, mmoja wa vyakula vya watu wa mataifa tofauti na mwingine wa kisasa uliotumika kwa ajili ya burudani au mikutano mbalimbali, bila kusahau huduma ya bure ya mtandao wa intaneti ya Wi-Fi (Wireless Fidelity).

Nilipofika pale Chattle Restaurant nilichagua meza moja iliyojitenga na watu na mhudumu alipokuja nikamwomba kwanza aniletee supu ya samaki nikapasha tumbo joto na ilipoletwa niliifakamia kwa kasi ya ajabu kutokana na njaa niliyokuwa nayo na muda mfupi baadaye lile bakuli lilikuwa tupu. Nikasubiri dakika chache ule mlo ushuke vizuri tumboni nikaagiza ugali wa dona, samaki wa kupakwa na saladi ya matunda. Halafu nikaomba niletewe mvinyo mwekundu aina ya Dompo.

Nilikula kile chakula kisha nikashushia taratibu ule mvinyo mwekundu taratibu kooni mwangu na muda huo akili yangu nayo ikaanza kuchangamka na kuanza kufikiria ni wapi ningeenda kuimalizia siku yangu. Mara nikakumbuka kuwa Jumamosi hiyo kulikuwa na mechi ya Ligi Kuu katika Uwanja wa Taifa.

Saa yangu ya mkononi ilionesha kuwa ilikuwa ikielekea kutimia saa 10:30 jioni wakati nilipokuwa nikitoka nje ya ule mgahawa na kuelekea kando ya eneo lile sehemu kulipokuwa na maegesho ya teksi. Hata hivyo nilisita kuchukua teksi kwa kuwa sikuona tena haja ya kwenda Uwanja wa Taifa, nikaanza kutembea taratibu nikiifuata barabara ya lami iliyotokea katika mgahawa ule kuelekea eneo la Nyasubi.

Sikujua nilikuwa naelekea wapi lakini kuna sauti fulani ilinitaka kuifuata barabara ile. Nikazitii hisia zangu. Sikufika mbali, wakati natembea macho yangu yakavutwa kumtazama msichana mmoja mrembo aliyekuwa akikatiza mbele yangu kuelekea kwenye duka moja upande wa pili wa ile barabara. Nilisimama ghafla na kumkodolea macho yule mrembo wakati akifika pale dukani na kuanza kununua bidhaa.

Nilikuwa najiuliza kama niliwahi kumwona sehemu na mara nikakumbuka, alikuwa ni yule mrembo ‘the most wanted’ tuliyesafiri pamoja kutoka Masumbwe kabla ya lile tukio la mauaji kule porini. Nilipogundua hivyo nikajikuta naanza kuchanganya miguu yangu kuelekea pale dukani, na nilimpofikia yule mrembo ‘the most wanted’ nikamsalimia huku nikiagiza maji madogo.

Yule mrembo ‘the most wanted’ aliitikia salamu yangu pasipo hata kugeuza shingo yake kunitazama usoni, na wakati yule muuzaji alipokuwa ananipatia chupa ya maji na kuendelea kumhudumia yule mrembo, nikapata wasaa mzuri wa kumchunguza kwa umakini, hivyo nikawa nakunywa maji yangu taratibu huku nikiendelea kumchunguza nikiwa siamini macho yangu.

Yule mrembo yule ‘the most wanted’ alifungasha bidhaa zake pasipo kuniangalia wala kunijali na hivyo nikaamua kujikohoza kidogo na kumfanya ageuze shingo yake kunitazama usoni kwa umakini, macho yetu yalipokutana nikaachia tabasamu kaabambe lakini sikuona tashwishwi yoyote usoni kwake, na wala hakuonesha kabisa kunikumbuka.

“Samahani bi mdogo, nimegundua kuwa nilikuwa sijakukaribisha japo soda. Chukua soda nitalipa,” niliongea kwa sauti tulivu ya chini huku nikimwangalia usoni kwa tabasamu.

Aliniangalia mara moja tu na kutingisha kichwa chake kukataa huku akiendelea kukusanya vitu vyake. “Asante sana, lakini samahani mimi sinywi soda!”

Japokuwa alikataa ofa yangu nilijikuta nikifarijika kidogo kwani alinijibu pasipo kuonesha maringo yoyote kama walivyo wasichana wengine waliojiona warembo. Nikamchombeza tena. “Sasa, sijui nikununulie nini ambacho unakunywa, bi mdogo?”

“Hakuna chochote uwezacho kuninunulia, bwana mkubwa…” alisema tena yule mrembo bila hata kunitazama.

Okay! Naitwa Jason Sizya… sijui unanikumbuka?” nilimuuliza tena, safari hii niliongea kwa msisitizo.

Yule mrembo alinitupia jicho mara moja tu na kutingisha kichwa chake huku akimalizia kufungasha vitu vyake na kuanza kupiga hatua zake taratibu, “Wala sikufahamu. Hata hivyo kwa heri, Mr Jason Sizya!” alisema kwa sauti tulivu huku akiondoka eneo lile.

Nilitaka kusema neno lakini nikasita na kubaki kimya nikimsindikiza kwa macho huku nikiwa nimekata tamaa. Nilimtazama huku nikipeleka chupa ya maji mdomoni na kunywa maji yote yaliyobakia kwa mkupuo mmoja tu. Kisha nikatoa noti ya shilingi 1,000 kwenye pochi yangu na kumpa yule muuzaji pale dukani. “Samahani ndugu, hivi huyu binti anaitwa nani?” nilimdodosa yule muuzaji, alikuwa kijana wa umri wangu.

“Anaitwa Asia,” alinijibu yule muuzaji wa dukani pasipo kuwa na wasiwasi wowote na mimi.

“Ooh, Asia! Na anakaa mtaa gani kwa hapa?”

“Anakaa kwenye ile pale nyumba kubwa ya kisasa. Kwa Bi Aisha,” aliniambia yule muuzaji wa dukani huku akinielekeza kwa kidole.

Nilibetua kichwa changu huku nikiitazama ile nyumba kwa makini kisha nikamtazama yule muuzaji kwa tabasamu. Moyoni nilimshukuru sana yule muuzaji wa dukani kwa kunipa taarifa ambazo hakujua kuwa zilikuwa muhimu sana kwangu na nilikuwa nimehangaika kwa takriban mwezi mmoja na ushee kuzitafuta.

Niliondoka pale dukani na kutembea taratibu hadi kwenye kituo cha teksi, sikuona tena haja ya kutembea. Sasa hamu yangu juu ya mrembo ‘the most wanted’ ambaye niliambiwa anaitwa Asia iliibuka upya.

* * *

Itaendelea...
 
narudi buzwagi.jpeg

94

Kwani Unatakaje!


Saa 6:30 usiku…

USIKU wa siku ile ulikuwa mmoja kati ya siku zilizokuwa ngumu zaidi kwangu. Fikra zangu zilizunguka mara mbili, nilikuwa na maswali mengi ya kujiuliza yaliyoonekana kukosa majibu sahihi. Hata hivyo niliazimia kupata majibu kwani ndiyo jambo la maana na la lazima. Majibu lazima yapatikane. Niligaagaa pale kitandani kwangu usiku kucha nikiwaza. Ni kutokana na maswali yaliyonizinga kichwani na majibu yake ndipo ningeweza kuamua kumtafuta Asia au kuachana naye.

Je, ni kweli kwamba nilihitaji kuonana na Asia katika wakati ambao nilishaamua kuachana na maisha ya uchafu na kuanza maisha mapya na Rehema? Hilo lilikuwa swali langu la kwanza nilipokuwa nimejilaza pale kitandani, nilifikiria sana swali hilo. Kwa kweli, sikudhani kama ingekuwa busara kufanya hivyo, na sikuwa na sababu hata moja ya kumsaliti Rehema.

Wanawake si wa kuwaamini sana na hasa wanapopata madaraka! Rehema alipandishwa cheo na alikuwa anahamia Misungwi, mbali zaidi nami na sasa angekuwa anakutana na watu wakubwa na wenye ushawishi zaidi na hata kunisaliti, je nilipaswa kufanya au kuendeleza kumsaliti kwa kuwa sikuwa na uhakika naye huko aliko? Hilo lilikuwa swali la pili. La isingeleta maana yoyote kufanya hivyo. Makosa mawili yasingeleta sahihisho.

Hata hivyo, baada ya kutafakari sana niliamua kumtafuta Asia japo nijiridhishe kwa nini alishindwa kunitembelea pale hospitali kisha ningeamua nifanye nini. Sikudhani kama nilimhitaji tena. Na kama ningeona ipo sababu ya kutoka naye ningefanya hivyo mara moja tu kisha ningeacha upuuzi wote na kusahau kabisa kama nilitoka na nani, wapi, au lini!

Hivyo nikaamua kukutana na Asia, iwapo mipango yenyewe ingeniridhisha. Kama mpumbavu, nilicheka peke yangu pale kitandani. Nilifurahia uamuzi wangu nikavuta mto na kuulalia huku nikijiuliza maswali madogo madogo kama Asia angeweza kunipa penzi kama la Rehema au ilivyotokea kwa Jamila? Mabusu yake yangekuwa matamu kama ya Rehema au ilivyotokea kwa Jamila? Nikajikuta nikiingiwa na hamu ya kumkumbatia Asia. Nilitamani kuche haraka. Laiti ningeijua namba yake ya simu ningempigia usiku huohuo niisikie sauti yake nyembamba yenye kushawishi.

Ningemwomba aje nyumbani kwangu, angefika ningemkumbatia na nisingejali kama nilikuwa nimemuahidi Rehema ahadi ya uaminifu! Nisingejali kama Jamila pia alikuwa ameingia kwenye mlolongo wa wanawake walioisumbua akili yangu! Nisingejali!

Niliweka vema kichwa changu juu ya mto nikaelekeza macho yangu darini! Niliangalia dari kwa dakika kadhaa kisha nikayageuza macho kutazama saa. Zilibaki dakika tatu tu kutimu saa 9:15 usiku.

Nilinyoosha mkono na kushika swichi ya taa iliyokuwa ukutani pembeni mwa kitanda. Nikazima taa! Niliendeelea kugaagaa pale kitandani na sikuwa na habari ilipogonga saa 11:00 alfajiri!

Niliamka saa 2:30 asubuhi na sikuwa na haraka ya kuondoka kitandani. Ningeharakisha kwenda wapi wakati ilikuwa ni Jumapili na sikuwa na mpango wa kwenda kanisani? Hata hivyo sikupenda kuendelea kulala wakati kulishakucha, nilipiga mwayo nikalitupa shuka kando na kuinuka, nikaelekea chooni.

Nilipotoka huko kitu cha kwanza nilichokifanya ilikuwa ni kuingia jikoni, nikawasha jiko la gesi na kutengeneza mayai na soseji kisha nikachemsha kahawa. Nilipomaliza nikafanya usafi katika nyumba yangu. Muda huo nilijisikia njaa kali sana, na ilipotimu saa 4:15 asubuhi nilikuwa nimekwisha maliza kazi zangu zote. Nikaketi mezani katika ukumbi wa chakula, nikaanza kunywa taratibu kahawa huku mezani pia kukiwa na mayai na soseji, na mkate wa Ata nilioununua jioni ya siku iliyotangulia.

Wakati nikiendelea kupata kifungua kinywa nilianza kujiuliza lipi la kufanya nimalizapo kunywa hiyo kahawa. Nishinde nyumbani nikifanya kazi zangu? Niende nyumbani kwa Eddy tukaongee kuhusu suala la Rehema? Niende Nyasubi kwa Asia? Niwapigie simu wazee kuwaambia wawaandae washenga wa kwenda kwa wazazi wa Rehema? Nimpigie simu Rehema? Au nifanye nini?

Muda huo akili yangu haikuwa imetulia kabisa. Mara kwa mara katikati ya mawazo yangu nilijikuta namuwaza Asia. Nilidhani kuwa endapo ningempata na kuongea naye basi angetosha kabisa kuifanya siku yangu kuwa ya furaha. Nilijilaumu kwa kutogundua mapema kuwa alikuwa akiishi jirani na mgahawa wa Chattle, eneo ambalo nilipenda kwenda mara kwa mara kupata msosi.

Na laiti ningejua mapema wala nisingekuwa nakosa usingizi kumfikiria. Ukiwaacha Rehema, Amanda na sasa Jamila sikuona mwanamke mwingine ambaye ningeweza kumfananisha na Asia hadi wakati huo. Asia ndiye angebakia kuwa mwokozi wangu baada ya mchumba wangu Rehema kuhamia Misungwi, mbali nami.

Amanda alikuwa ameanza maisha mapya na yule mfanyabiashara wa madini, na Jamila alikuwa mbioni kuolewa na kwenda kuishi Omani. Hata kama Jamila angeendelea kuwepo bado nisingeweza kuendelea naye kwani sikutaka kugombana na rafiki yangu, Selemani.

Sikujua kwa nini nilikuwa napata msukumo mkubwa sana ndani yangu wa kumtafuta Asia! Hata hivyo, ndani yangu kulikuwa na sauti fulani iliyonionya niachane na Asia kwa kuwa nisingeweza kumuoa bali nilitaka kuonja vilivyomo ndani na baadaye kumuumiza kihisia. Kwa kifupi nilimtamani tu, yaani nilitaka anivulie nguo zake tushiriki tendo na hamu yangu iishe kisha niachane naye.

Ndiyo nisingeweza kuwa naye kwa sababu tayari nilikwisha ingia agano na Rehema. Wakati naendelea kuwaza nikasikia sauti ya mtu akibisha hodi, na kabla sijafanya chochote mlango ukafunguliwa, Jamila aliingia akanikuta nikiwa mezani naendelea kunywa kahawa. Nilishtuka sana lakini sikutaka kuonesha mshtuko wangu.

Jamila alisimama akaniangalia kwa umakini huku akiachia tabasamu pana lililovinjari usoni pake. Kwa sekunde kadhaa niliusahau mshtuko wangu na macho yangu yalijikuta yakipumbazwa na uzuri wake. Jamila alikuwa msichana mrembo sana japokuwa alikuwa amevaa hijabu iliyokuwa imefunika mwili wake wote kasoro sehemu ndogo ya uso wake, lakini bado uzuri wake haukujificha kabisa.

Mdomo wake laini wenye kingo pana kiasi ulikuwa umepakwa rangi ya mdomo ya chokoleti. Huku akiendelea kutabasamu, alilivua lile hijabu na kunisogelea taratibu. Nywele zake nyeusi za Kiarabu alikuwa amezisuka mtindo wa mkiwa wa pweza. Ndani alikuwa amevaa fulana nyepesi nyeusi iliyoyaficha vyema matiti yake imara na hapohapo nikakiona kidani cha dhahabu chenye herufi “J” kikiwa kimenasa vyema kwenye shingo yake ndefu na kupotelea katikati ya kichochoro hafifu katikati ya matiti yake. Chini alivaa pensi fupi na nyepesi ya rangi nyekundu iliyoonesha minofu ya mapaja yake yaliyonona.

“Karibu Jamila,” niliinuka kumkaribisha Jamila mara tu aliponisogelea karibu kabisa na kusimama mbele yangu. “Una mguu mzuri, umewahi stafstahi,” nilimwambia huku nikimkumbatia na kumbusu kwenye paji la uso wake.

“Ahsante mpenzi, lakini ungesubiri nije nikupikie,” Jamila alisema huku akiketi kwenye kiti kwa kifungua kinywa.

Itaendelea...
 
narudi buzwagi.jpeg

95

Jumapili ile ilikuwa ngumu sana kwangu kwani sikuweza kutoka kabisa na ule mpango wa kumtafuta Asia ulikuwa umeingia doa kwani Jamila alikuja nyumbani kwangu kushinda na hatimaye kulala palepale, baada ya kuruhusiwa na shangazi yake na kutakiwa kuamka mapema siku iliyofuata kwa safari ya Masumbwe.

Jumapili ile tulishinda ndani tu tukicheza kila aina ya mchezo kila tulipohitajiana. Jamila alionesha kunipania siku hiyo. Ilipofika saa nane mchana nilikuwa nahisi njaa.

“Nahisi njaa, ngoja nikanunue chakula. Au mwenzangu huhisi njaa?” nilimuuliza Jamila huku nikianza kuinuka.

“Leo nataka nikupikie. Nataka tuandae pamoja chakula maana ni muda mrefu nimetamani kukupikia,” Jamila aliniambia huku naye akiinuka.

Wow! That’s great. Leo nataka nionje mapishi yako,” nilimwambia Jamila huku nikiachia kicheko hafifu.

“Unapenda tupike nini kwa ajili ya siku ya leo?” Jamila aliniuliza huku akiniangalia kwa macho ya huba.

“Kitu chochote utakachopenda tupike, mimi niko tayari,” nilimjibu na kumfanya atabasamu.

“Kuna nini humu ndani au ndiyo mpaka tukanunue?”

“Vitu vyote vipo, twende nikuoneshe jikoni!” niliongea huku nikimshika mkono Jamila, nikampeleka jikoni.

Kulikuwa na kila kitu kama mchele, unga wa dona, unga wa ngano, sukari, mafuta, viungo mbalimbali na vitu vingine vingi ambavyo hata sikujua matumizi yake, ilimradi vilinunuliwa na kuhifadhiwa mle ndani. Vitu hivyo vilikuwa vikinunuliwa na Rehema kwa kuwa ndiye aliyekuwa mpishi wakati alipokuwa Kahama, na baada ya kwenda Ushirombo Amanda aliendelea kununua na kunipikia.

“Nakuahidi leo itakuwa siku maalumu kwetu. Nitahakikisha siku ya leo inabaki kuwa ya kukumbukwa,” Jamila alisema baada ya kuona vile vitu.

Jamila aliniomba nikanunue kuku na baadhi ya vitu ambavyo sikuvijua ila aliniandikia kwenye karatasi. Nikatoka na kuchukua pikipiki kwenda soko la jirani ambapo vitu vyote vilikuwa vinapatikana na baada ya muda nilirudi nikakuta amekwisha andaa mchele na baadhi ya viungo, kisha tukaanza maandalizi kwa pamoja. Kitendo cha kushirikiana kuandaa chakula kilionekana kumpa Jamila furaha ya ajabu sana. Muda wote uso wake ulipambwa na tabasamu.

Baada ya saa moja chakula kilikuwa tayari na tulipakua tukaketi mezani kwa chakula. Kilikuwa chakula kitamu sana, biriani la kuku. Tukala, tukalishana na kuifurahia Jumapili hiyo. Nilijikuta nikiwa na furaha kubwa na kuusahau wasiwasi niliokuwa nao mwanzo maana nilihisi kama vile nipo na Rehema ambaye mara nyingi nilimsaidia kupika.

Tulipomaliza kula tuliosha vyombo na kisha tukaketi kwenye kochi kubwa la sofa tukiifurahia Jumapili yetu, mara simu yangu ilianza kuita na nilipoangalia nikaliona jina la Rehema, nikaipokea huku kidole changu kimoja kikiwa mdomoni nikimuashiria Jamila asizungumze kitu chochote. Sikutaka Rehema ahisi chochote kibaya.

“Mambo, baby!” nilisema kwa sauti ya mahaba huku niking’onga. Nikamwona Jamila akiniangalia kwa jicho baya lililojaa wivu.

“Safi baby, nimefika salama Misungwi na nipo katika maandalizi ya kuapishwa kesho Jumatatu.”

Okay, nakutakia mafanikio mema, mke wangu.”

“Ahsante sana mpenzi wangu, ila kwa nini unanisaliti?” Rehema alisema na mara moyo wangu ukanipasuka. Nilijikuta mwili mzima ukianza kunitetemeka na nikaanza kujiuliza alijuwaje kuwa nilikuwa namsaliti. Nikapatwa na kigugumizi cha gafla.

“Nakusaliti… vipi ba…by?”

“Hata sijui ila hisia zangu zinaniambia kuwa hali si shwari huko!”

“Wasiwasi wako tu, mke wangu. Inamaana bado huniamini?”

“Nakuamini ingawa tahadhari ni muhimu.”

“Kwani unakuja lini?”

“Ijumaa nitakuwa hapo, baada ya makabidhiano ya ofisi,” Rehema alisema kisha tuliongea mengi yaliyohusu mustakabali wetu na baada ya muda akakata simu. Muda wote Jamila alikuwa kimya kabisa akiniangalia kwa jicho kali. Sikumjali.

Baadaye Jamila aliondoka lakini akiahidi kuwa angerudi jioni na kuniomba nisiondoke. Hakuniambia alikuwa anakwenda wapi. Alirudi saa 12:30 jioni wakati huo nilikuwa chumbani kwangu nimepumzika baada ya kutafakari mambo mengi kuhusu maisha yangu.

Sikujua kuwa alikuwa amefikia jikoni kuandaa maakuli na kuufanya usiku wa siku hiyo kuwa maalumu kwa ajili yetu. Baada ya kumaliza kuandaa chakula alipamba pale sebuleni kabla hajaniita, na nilipotoka nikapigwa na mshangao kwa nilichokikuta. Alikuwa amevaa gauni fupi jepesi lililoishia juu ya magoti yake na liliyaonesha maungo yake na nguo yake.

Sebule ilikuwa imebadilika sana na kuwa na mandhari ya kuvutia mno. Taa zote zilikuwa zimezimwa na kilichokuwa kinawaka ni mishumaa iliyopapendezesha mahala pale na kupafanya pa pekee kabisa. Muda huo kulikuwa na sauti ya chini ya muziki laini toka kwenye redio kubwa iliyokuwepo pale sebuleni.

Wow! It’s amazing!” nilijikuta nikiropoka huku nikimwangalia Jamila kwa tabasamu.

“Karibu mpenzi,” Jamila aliniambia kwa sauti laini iliyojaa mahaba huku akinishika mkono akaniongoza kuelekea katika meza ya chakula iliyosheheni mapochopocho ya kila aina.

Mapigo ya moyo wangu yalikuwa yanaenda kasi sana. Tulikuwa tunaangaliana kwa tabasamu huku tukielekea katika meza ya chakula. Niligundua kuwa maongezi yangu na Rehema yalikuwa yamemuumiza sana na pengine aliamua kumalizia hasira zake katika usiku ule kwa kunifanyia jambo ambalo aliamini lingenifanya nimsahau Rehema.

“Karibu chakula mume wangu, hiki ni chakula maalumu kwa ajili yetu kitakachoufanya usiku wa leo kuwa wa kukumbukwa zaidi,” Jamila alisema kwa sauti ya chini iliyoonesha kuhemkwa na mahaba.

Duh! Mume wake tena! Nilihisi kuchanganyikiwa, hata hivyo niliamua kukaa kimya. Tulikula taratibu huku tukisindikizwa na muziki laini.

Tulilishana kwa mahaba na kila nilipomtazama Jamila akiwa ndani ya lile vazi jepesi lililoyaonesha maungo yake nilihisi kusisimkwa mno mwili wangu. Nilizishuhudia chuchu zake za kuvutia na zilikuwa zinaonekana kwa urahisi kutokana na vazi lile. Taratibu nikaanza kuhisi mtafaruku katika sehemu za ikulu.

Muda wote nilijikuta katika wakati mgumu sana na baada ya kumaliza kula Jamila aliondoa vyombo na kusafisha meza kasha akaniomba tuelekee katika sofa kubwa hapo nikakuta chupa kubwa mbili za mvinyo ghali mwekundu wa Kifaransa aina ya Navette de Marseille pamoja na bilauri mbili. Nilihisi kuanza kuchanganyikiwa, Rehema alikuwa amenifanya niache pombe na sasa Jamila alitaka kunirudisha kwenye ulimwengu huo!

“Leo nataka tunywe kwa ajili ya furaha yetu na maisha marefu ya penzi letu,” Jamila alisema huku akimimina kwenye mvinyo kwenye zile bilauri kisha tukagonganisha bilauri.

Jamila akagida funda kubwa huku akisisimkwa mwili wake. Ukweli alizidi kunishangaza, sikutegemea kama alikuwa anakunywa pombe, tena pombe kali. Tulikunywa huku moyo mapigo ya wangu yakienda mbio kutokana na wasiwasi na kadiri muda ulivyozidi kusonga ndivyo wasiwasi ulivyopungua na maongezi na vicheko vikazidi. Ulikuwa wakati wa furaha mno kwetu sote. Maongezi yalikolea na kulikuwa na kila dalili kwamba tulianza kulemewa na kilevi.

Jamila akainuka pale alipokuwa amekaa na kuelekea katika redio akaongeza sauti ya muziki, ulikuwa muziki laini, halafu akanifuata.

Jason, can we dance?” Jamila aliongea kwa mbwembwe akinitaka tucheze huku akirembua macho yake.

Itaendelea...
 
Back
Top Bottom